Kikwete Mzee wetu, mbona bashasha imepotea ghafla?

Hakuna mzazi anekuwa na furaha mwanae anapo huzunika, tangu mirija ya kina Riz moko imekatwa familia nzima imekuwa kama imepata ugonjwa wa kupooza, yule doo aliekuwa anatoa kashfa kwa vyama vya upinzani sasa hivi kazama kabisa hajitokezi hata kumpa pongezi Magufuli kwa kazi ILIYOTUKUKA ya kuwapoteza waliokuwa wanaishi kama malaika. Lazima baba awe mnyonge tu.
Sure hata mm nawaza hivi sasa hivi riz anaishije? Maana kiila kitu tuliambiwa cha riz 1..anzia masheli..magari ya mafuta...mahotel...nk
 
Kati ya vitu ambavyo JK alijipotezea heshima ni kuingia kikao cha CC na majina yake mfukoni

Pili aliyemtegemea kama atamrithi akapigwa mweleka

Tatu ni usaliti mkubwa aliyomfanyia rafiki yake wa muda mrefu Na aliyemsaidia kwa hali na mali kuingia magogoni 2005, kitu hiki hasa ndo kinachomtesa

Nne ni tumbua tumbua ya kipenzi cha wananchi Mh JPM

kwa mkutadha huu lazima anyauke na kusinyaa
Ukweli ni kwamba Kikwete hakutakiwa awe raisi 2005. Nafasi ya Uraisi ilikuwa ni Dr Salim Ahmed Salim. Lowassa, Membe, Kikwete, Mwang'onda, Mkapa, Rostam, Sitta, Pengo na genge zima LA mtandao walioaminisha watu Kikwete ni chaguo la Mungu lazima ile kwao.

Na hiyo Lowassa wenu hii dhambi ya kumbagua na kumchafua, kumbagua Dr Salim na kutuhujumu Watanzania kutopata raisi bora lazima hadi vizazi vyake. Na uraisi ataendelea kuusikia tu na kuuota wala haji kupata.

Wewe huwezi kuwa mbaguzi wa rangi na mzandiki halafu upate uraisi tu hivi hivi. Na bado tutaona mengi sana kwa hilo limtandao lao.
 
WATANZANIA BUANA,SASA WEWE ULITAKA ASIZEEKE KWANI YEYE NI JIWE? HATA JIWE NALO LINAZEEKAGA JAMANI LIKIPIGWA NA JUA SANA LINAPASUKA LENYEWE,ACHENI MAMBO YA AJABU AJABU HAPA,WE ULITAKA AWEJE SASA,JUA JK SASA ANAKIMBILIA 70 YRS MUDA SI MREFU PENGINE AKAFIKISHA MIAKA YA AHADI YA BINADAMU YA KUISHI MIAKA 70
hatujasema kazeeka,mbona akina mwinyi wazee lakini hawajachoka kama yeye?
 
JK atakumbukwa kuwa alikuwa mzee wa vicheko na bashasha hata pale aliposhambuliwa kwa maneno ya kuudhi.

Kwa waliomuona Jana akifungua KK kwa hakika sio yule tunayemjua. Kwanza anaonekana mgonjwa na mzee kuliko hata mzee Mwinyi.

Nini kimemsibu mzee wetu hata katika siku aliyopaswa kuonyesha furaha? Siku ya kustaafu kabisa uongozi.

Kwa muonekano wa Jana jinsi alivyo choka na ukimuangalia kwa sasa rafiki yake Edward na ukiwasimamisha pamoja waweza kudhani Jakaya ni baba na Edo ni mwanae au mdogo wake wa mbali.

Kuna nini hii sudden change?
Acha uongo,ngoja uone kesho atakavyocheka
 
Malcom Lumumba! Nakubaliana na wewe japo umechepuka mada

Naomba tukubaliane tu kwamba mchakato wa kutafta wagombea hasa kwenye nafasi ya juu unakuwa Na figisu nyingi sana duniani

Mfano Obama na Hillary Clinton
 
Jamani wana jamii. Kama mnafuatilia huu mkutano wa ccm, wakati huu anapoongea Kikwete, naona kabisa Raisi kwa sura hana raha. Watu wake wa karibu wanaweza kutujuza nini tatizo!
 
JK atakumbukwa kuwa alikuwa mzee wa vicheko na bashasha hata pale aliposhambuliwa kwa maneno ya kuudhi.

Kwa waliomuona Jana akifungua KK kwa hakika sio yule tunayemjua. Kwanza anaonekana mgonjwa na mzee kuliko hata mzee Mwinyi.

Nini kimemsibu mzee wetu hata katika siku aliyopaswa kuonyesha furaha? Siku ya kustaafu kabisa uongozi.

Kwa muonekano wa Jana jinsi alivyo choka na ukimuangalia kwa sasa rafiki yake Edward na ukiwasimamisha pamoja waweza kudhani Jakaya ni baba na Edo ni mwanae au mdogo wake wa mbali.

Kuna nini hii sudden change?
Yakiiva pakua ule kisha kakojoe ukalale..
Maana unaonekana mtaalamu wa kuyapika Majungu..

Ukiwa huna la kuandika pumzika.. si lazima kujitanabaisha ufinyu wa akili yako kiasi hiki katika jamii..

Sura ya bashasha ya JK inahusiana nini na mustakabali wa maendeleo ya Taifa??

Au kwa vile ww umezoea kushinda kwenye kioo unajipodoa, ndio unajiona mwingi wa bashasha??
 
Hizi kejeli za JK kwenye kipindi cha uraisi wa bwana Magu naona zitakuwa za mtandaoni tu, ukijipendekeza kwenye majukwaa Magufuli ananunua ugomvi unakuwa wake. Leo ndio nimeelewa kwanini Gwajima aliingia mitini ugomvi na JK utashukiw mzima mzima na nguvu zake zote.
 
Kwani Kikwete yupo Ikulu?
Au kutokua na furaha mpk mtu aumwe?
Unajua yamemsibu yapi mpk awe moodless?
What if ni family matter, business matter, etc.

Usimlinganishe Kikwete na huyo mgonjwa wa makorokocho plz.
Tena mumuache Kikwete wetu apumue.
Bila Shaka umeingia mwezini ghafla bila maandalizi.
 
Bila Shaka umeingia mwezini ghafla bila maandalizi.
Stick na michango ya bongo celebrities uwezo wa ku interpret message na emphasize inayowekwa sio mambo ya size yako; kuona psychology na umuhimu wa hilo swala kwa muongeaji.

Usione vinaelea; vimeundwa
 
Back
Top Bottom