Kikwete mbona haendi mikoani?

bushman

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,411
743
Wana JF kuna jambo nimeligundua kwa mkuu wa kaya ni tofauti na awamu ya kwanza ya uongozi wake.

Toka achaguliwe ziara zake ni dodoma na bagamoyo, mkoa wa Iringa kakanyaga juzi kwenye mazishi ya mama yake spika (gamba).najiuliza kunanini?

Mzee wa kaya hata kushukuru waliokupa ulaji,au ndio tuamini maneno ya cdm kwamba ulichakachua kwa hiyo unaona soni,kukutana na wananchi?Ziara za wizarani ulitakiwa uzihamishie mikoani na wilayani ndiko walipo wananchi walalahoi,

Naomba kuwasilisha.
 
Kwani akifanya ziara dodoma na bagamoyo anakutana na nani kama si wananchi
 
Kwa hiyo tz ni bagamoyo na dodoma?umetoka shimoni nn?hujui unachocoment?
 
kwani akifanya ziara dodoma na bagamoyo anakutana na nani kama si wananchi

nimeshtukaaaaa............. huyu ni miongoni mwa wale wageni wa jamvini waliojiunga baada ya vikao vya kujivua magamba. waliishambulia jf kwenye vikao vyao,wakadai inabidi watumie mitandao vizuri na wao. daaahhh!!!!!!!!!!!!!!! mkuu hapa jf utachemka,its a home of great thinkers.
 
Hapo ndio nilikuwa napataka,anaogopa kuvuliwa gamba pamoja sana mpiganaji
 
kwa hapa arusha kama leo hii jk atafanya mkutano pale sheikh amri abed na wasiwepo wasanii basi akipata watu mia tatu nitashangaa...nasemea arusha mjini maana wengine hutoka momduli kwa mabasi anapokuwa anafanya mikutano..
 
Jamani ndugu zangu wana jamvi mbona rais wetu haendi mikoani husani mikoa ya kaskazini na mikoa ya kanda ya ziwa. Yeye anakwenda dodoma tu
 
Ashasikia alowatuma huko kibano wanachokula kwani wananchi wamechoka na analijua hilo!!!
 
Jamani ndugu zangu wana jamvi mbona rais wetu haendi mikoani husani mikoa ya kaskazini na mikoa ya kanda ya ziwa. Yeye anakwenda dodoma tu

Mkuu wakati kama huu wa zomeazomea na mawe unataka Rais naye azomewe? Hata ungekuwa wewe unamtuma katibu mkuu wako wa Chama anazomewa tena nyumbani kwao na kila akiangalia kwenye magazeti na Luninga anaona nyomi ya wapinzani unadhani afanye nini zaidi ya kukaa ikulu ama kwenda nje ya nchi? Siamini kama atafanya ziara za mikoani hivi karibuni asije akazomewa bure.
 
Jamani acheni hayo hamsomi magazeti au kusikiliza habari? Juzi tu ametoka mkoani Namibia na amefanya vizuri kweli huko; Naona hamumuoni sana Airport Sababu anasafiri usiku na Ndege yake kwahiyo hujui anamchukua nani na ni nini ndani ya ndege kupeleka Mkoani Namibia
 
Ni swali zuri sana. Lakini usijeshangaa akasema Nape anamwakilisha on his behalf!!
Mi nasubiri tu ile ahadi ya meli yetu kule ziwani Tanganyika, na ujenzi wa mji wa kisasa wa Kigoma aka Dubai ya Africa, nilitegemea ujenzi wa miundombinu ungekuwa umeshaanza
 
Ni swali zuri sana. Lakini usijeshangaa akasema Nape anamwakilisha on his behalf!!
Mi nasubiri tu ile ahadi ya meli yetu kule ziwani Tanganyika, na ujenzi wa mji wa kisasa wa Kigoma aka Dubai ya Africa, nilitegemea ujenzi wa miundombinu ungekuwa umeshaanza

hata sis huku Kagera tunasubiri ile meli mpya kuliplace ile MV BUKOBA iliyozama. Mweeee huyu jamaa hana aibu, ngoja tusubiri.
 
Anaogopa kwani ashaliwa kichwa na magamba!!


5410309.jpg
 
Shida gani itampeleka huko mikoani? Biashara zake anafanyia pale Magogoni na mara chache chache sana Dodoma. Akitaka kwenye kutembea anapanda ndege kwenye nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom