Kikwete: Lowassa ni msafi, alisingiziwa!

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Baada ya kumpigia kampeni BAsil Mramba Rombo, JK saa Katika kampeni zake za mkoani Arusha anaelekea Monduli atakapomnadi na kufanya mazungumzo ya faragha na Lowassa

wtcoj.jpg

"TOBIKO Kikwete, Tobiko," yalikuwa ni maneno yaliyotamkwa na maelfu ya wananchi wa mji wa Monduli mkoani Arusha jana.

Neno hilo la lugha ya Kimasai lenye maana ya juu; lilitamkwa mara nyingi na umati uliofurika kwenye Uwanja wa Polisi mjini hapa kumsikiliza Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Rais Jakaya Kikwete akiomba kura.

Wananchi hao walieleza kwamba mgombea huyo hakuwa na sababu ya kufika kwao kuomba kura kwani wameshakata shauri kuwa ndiye chaguo lao.

Mbunge wa Monduli anayewania tena kiti hicho kwa tiketi ya CCM, Edward Lowassa, alikuwa kinara katika kuwaongoza wananchi hao kueleza hisia za furaha kwa Rais Kikwete, hasa baada ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005/2010, kutekelezwa kwa asilimia 99 jimboni humo.

"Tobiko Kikwete, Tobiko…Wataweza? Watamuweza Kikwete," yalikuwa maneno yaliyotamkwa na Lowassa na umati huo kujibu, "Tobiko Kikwete, Tobiko' pamoja na ‘Hawataweza, Hawatamuweza.'

Akizungumza kabla ya kuanza kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi, Lowassa ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu, alimpongeza Rais Kikwete kwa mafanikio makubwa ya serikali yake akieleza kuwa amefanya kazi kubwa kuliko marais wote waliomtangulia, kutokana na uongozi mahiri na makini.

Aliyataja mafanikio yaliyopatikana katika Ilani jimboni Monduli kuwa ni ujenzi wa shule za sekondari za kata na kwamba mwakani watakuwa na shule tatu za elimu ya juu kwa sababu sekondari za kata zimekamilika.

Lowassa ambaye kila alipofafanua mafanikio ya Ilani, aliuliza umati na kuhoji Shukrani kwa nani na kujibiwa, ‘Kwa Kikwete,' alieleza jinsi serikali ilivyowajali na kuwapata misaada wakati wa ukame mwaka jana uliosababisha vifo vya mifugo na ukosefu wa chakula, lakini hakuna mwananchi aliyekufa.

Alieleza pia upatikanaji wa maji umeboreka ingawa kumebaki maeneo machache likiwamo la kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), lakini watapatiwa mkopo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa ajili ya huduma ya maji pamoja na mradi wa Benki ya Dunia kwa vijiji kadhaa.

Lowassa anayetumia kaulimbiu ya ‘Tulifurahi Pamoja, Tulihuzunika Pamoja na Tutasonga Mbele Pamoja na Tutashinda,' katika kuomba kura, alisema wanajiandaa kujenga kiwanda cha kisasa cha nyama mjini Makuyuni.

Akimnadi Lowassa, Rais Kikwete alisema, "huyu ni mtu anayewapenda sana, anawahangaikia sana, haya yote (mafanikio) yanayosemwa sasa yametokana na juhudi zake…hakuna mwakilishi mzuri kushinda Edward Ngoyai Lowassa.

Naye Lowassa pamoja na Diwani mteule wa Kata ya Monduli Mjini, Issack Joseph, walieleza kwamba Rais Kikwete alifika hapo kuwasalimia tu kwani Monduli wameshafanya uamuzi kwamba huyo ndiye rais wao.

SOURCE: Blogu ya Kampeni ya Kikwete 2010
Jana mkuu wa kaya akimnadi Edo kwa wakazi wa Monduli alisema kuwa Lowassa ni msafi na tuhma zinazomkabili ni za uongo na kusakiziwa.

Je ni kweli Mwakyembe alimsingizia Lowassa?

Nakumbuka akitoa ripoti yake kwa Bunge Mwakyembe alisema wana ripoti mbili, ile yennye mauchafu yote ya Lowassa anayo, sasa ni muda wa kuiachia ili wananchi waone jinsi rais wao asivyokuwa na adabu kwa wananchi waliomweka madarakani.
 
Baada ya kumpigia kampeni BAsil Mramba Rombo, JK saa Katika kampeni zake za mkoani Arusha anaelekea Monduli atakapomnadi na kufanya mazungumzo ya faragha na Lowassa

Ni bora achaguliwe tena kuwa mbunge..nafasi hiyo size yake kama chanda na pete
 
Mbona haya tuliyasema mapema jamani.. hakuna wakati wowote ambapo hawa wawili hawakuwa wamoja.. na chances ni kuwa EL atarudi kuwa Waziri Mkuu.. walianza pamoja watamaliza pamoja..si unajua tena "hawakukutana barabarani"?
 
Mkuu, hapo kwenye red bold, "you must be kidding"
 
Mwanakijiji umepinda.
Inatabiri mzee white head anarudi kwenye UKANDA?
 
mwaka huu atakufa nao...........mwache tu aendelee kuwalea na kuwadanganya watz kuwa ni ajali ya kisiasa tu....
Baada ya kumpigia kampeni BAsil Mramba Rombo, JK saa Katika kampeni zake za mkoani Arusha anaelekea Monduli atakapomnadi na kufanya mazungumzo ya faragha na Lowassa
 
Kwa JK suala la kumrudisha EL siwezi shangaa bse maamuzi yake huwa yanashangaza wengi
 
serikali ya ccm imeonyesha kuwa inaweza kupambana na ufisadi.hayo ndiyo maneno yao
Hii nikutufanya wajinga unamtuhumu mtu kuwa fisadi hata unamfungulia kesi, halafu baaado unampigia kampeni .
HAYA NI MATUSI KWA WATZ, NI SAWA NA KUWAAMBIA
1.WANA MACHO LAKINI HAWAONI , WANA MASIKIO WALA HAWASIKII , WANA UBONGO USIOWAZA NA AKILI ISIYOWEZA KUKUMBUKA NA KUCHAKUA MBIVU NA MBOVU.

pigia kampeni
 
Kwa JK suala la kumrudisha EL siwezi shangaa bse maamuzi yake huwa yanashangaza wengi

Hapana mkuu hawezi kufanya ujinga kiasi hicho anajua amechemsha ndiyo maana anafanya mikutano mitano kwa siku moja.
 
Mbona haya tuliyasema mapema jamani.. hakuna wakati wowote ambapo hawa wawili hawakuwa wamoja.. na chances ni kuwa EL atarudi kuwa Waziri Mkuu.. walianza pamoja watamaliza pamoja..si unajua tena "hawakukutana barabarani"?

MM, unaota au? nani amekuambia JK atapita kwenye kinyanganyiro hiki cha urais? kwa taarifa yako tu huyu Bw hafiki kokote, na siku ya uchaguzi hatopiga kura kwani hatakuwa nje ya nchi kwa dharura.
 
MM, unaota au? nani amekuambia JK atapita kwenye kinyanganyiro hiki cha urais? kwa taarifa yako tu huyu Bw hafiki kokote, na siku ya uchaguzi hatopiga kura kwani hatakuwa nje ya nchi kwa dharura.
Kumbe kina Yahaya Hussein mpo wengi!
 
Kwa JK suala la kumrudisha EL siwezi shangaa bse maamuzi yake huwa yanashangaza wengi

Simple saaaana kumrudisha Lowassa kwenye mstari, kwa maandalizi ya kuukwaa Urais hapo 2015.

Kama kawaida yake, huku akicheka cheka, JK atautangazia umma kwamba Lowassa alisingiziwa na kuonewa tu, na ndio maana hata kamati ya akina Mwakyembe haikumpa haki yake ya kumuhoji kabla ya kutoa hukumu yao. Hivyo basi, kwa kuwa Lowassa alisemewa uongo, yeye JK ameamua kumrudishia nafasi aliyokuwa nayo (ya Uwaziri Mkuu) au hata uwaziri wa Mambo ya Nje/Fedha - Ili mradi tu awe na chance kubwa ya kuja kuwa Rais 2015.

Usicheze na Serikali ya JK/CCM bana, kama wamekula U-turn in less than 2 months na kusema sasa Bashe ni Raia, tena wa kuzaliwa, kwa nyuso kavukavu, watashindwa nini hawa?
 
Mkuu, hapo kwenye red bold, "you must be kidding"

What's wrong with tha? Lowassa is one of the finest politicians this nation has ever produced!
Just like Netanyahu, he resigned, went to regroup and will be back again. Netanyahu did the same. Even the late Sokoine did the same:eyebrows:
Vote CCM
Go JK
 
ampigie magoti kwa lipi? wizi wake ndiyo ulimfanya apoteze dira yake na imani yake, Six alifanya lile lililo bora kwa Taifa.

Remember, the late PM Sokoine resigned, took a break and came back!
So did PM Netanyahu!
Why not Lowassa?
 
Lowassa anaandaliwa kuwa spika wa bunge na eti tayari ana kura za kutosha kumpa nafasi hiyo bungeni hapo Novemba.

Nafikiri amekata tamaa ya kuwa rais au PM.
 
Back
Top Bottom