Kamakabuzi
JF-Expert Member
- Dec 3, 2007
- 2,861
- 1,302
Ni kweli kutumia yahoo si sahihi. Ni wazi pia kuwa sms zote na e-mails zitafikia TBC ambao watachuja kipi rais ajibu. Lakini ukweli utabaki palepale kuwa message sent and delivered. Rais mjanja inabidi baada ya kujibu atake apewe maswali yote na sms zote ili aone maoni ya waTZ. Naamini hawezi kujibu kila kitu, hii imetumika kama njia ya kupima joto letu.
Ushauri wangu ni kwamba tutume maswali kadri tunavyoweza ili kesho tuchambue yale ambayo ameyakwepa, tusipouliza hatutakuwa na cha kulaumu maana hatutajua yapi hakuyajibu - kesho tuanzishe thread ya maswali aliyoyakwepa.
Kwa wanaoweza kutumia landline, nadhani hao ndio watauliza live, hivyo mjipange mapema, yaani mtu uwe na maswali kama matano tofauti ili utakapopenyeza simu yako usijikute unarudia swali lililokwisha ulizwa/ kujibiwa. Kama swali limeshaulizwa usirudie tena labda kama atakuwa ametoa majibu ya hovyohovyo.