KIKWETE: Leteni Majina ya Wajumbe wa KATIBA niwateuwe!

Hatimaye Mchakato wa kuandika Katiba mpya umechukua sura mpya baada ya Rais kuitisha wadau mbali mbali kupeleka majina ya watu wenye sifa ili awateue.

Source: Chanel Ten.

Good move mheshimiwa rais..haya waosha vinywa nafasi hiyo sasa muache maneno maneno muungwana katoa nafasi tusijekulaumiana tena huko mbele ya safari kaamua kuwashirikisha kila hatua ili likiharibika liwe letu wote...

Huyu atakua shujaa sana baada ya kutoka madarani,watz tutamkumbuka sana baada kuja kugundua mambo aliyotuachia...

Mimi naanza..

Jenerali ulimwengu

Prof issa shivji

mabere marando

Prof Mwesiga Baregu

Ananilea Nkya

Edward Lowassa

Peter serukamba

Hamis Mgeja

Kingunge Ngombare mwiru

............
 
nampendekeza bi kiroboto, a.k.a vitoto vya ndege(makinda) ili posho ya wabunge isisahauliwe katika katiba mpya
 
Ngoma nzima hiyo:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Jumatano, Februari 29, 2012

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amevialika vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, jumuiya za kidini, asasi za kiraia na makundi mengine ya watu wenye malengo yanayofanana kuwasilisha kwake orodha ya majina ya watu watakaoteuliwa kuwa Wajumbe wa Tume ya Kuratibu na Kukusanya Maoni ya Wananchi kuhusu Mabadiliko ya Katiba.

Mheshimiwa Rais ametoa mwaliko huo kupitia Tangazo la Serikali Na. 66 la tarehe 24 Februari, 2012 kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 6(6) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011.

Kifungu cha 6(6) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, 2011 kinamtaka Mheshimiwa Rais kualika vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, jumuiya za dini, asasi za kiraia, jumuiya, taasisi na makundi mengine ya watu wenye malengo yanayofanana kuwsilisha kwa Rais orodha ya majina ya watu kwa ajili ya kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume.

Kwa mujibu wa Tangazo hilo la Serikali, kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu, jumuiya ya kidini, asasi ya kiraia na kila kundi lenye watu wenye malengo yanayofanana itapaswa kuwasilisha orodha ya majina yasiyozidi matatu ambayo itaonyesha umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali anapoishi kila mtu aliyemo katika orodha.

Aidha, orodha hiyo inatakiwa iwasilishwe kwa Mheshimiwa Rais kwa maandishi ama moja kwa moja kwa mkono au kwa rejista ya posta kupitia anuani ifuatayo: Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu, S.L.P. 9120, DAR ES SALAAM Au Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Ofisi ya Rais, S.L.P. 4224, ZANZIBAR.

Mwisho wa kuwasilisha orodha ni tarehe 16 Machi, 2012.

Imetolewa na: Wizara ya Katiba na Sheria, Makutano ya barabara ya Sokoine na Mkwepu, S.L.P 70069,
DAR ES SALAAM,
 
samahani...

naona hii move ni hcanga la macho tu, huwa hasikilizi watu
 
Back
Top Bottom