Elections 2010 Kikwete Kuzomewa na Kupigwa mawe?

ni mstari gani vile unaosema usipojisaidia hatokusaidia? Nadhani shy hapa umetudanganya hakuna mahali katika biblia au quran ambapo mungu amesema tujisaidie na yeye atusaidie. Kama upo tunaomba mtuwekee hapa.

Watanzania wametimiza wajibu wao kwa kiasi kikubwa. Wamejenga shule ambazo serikali imeshindwa hata kupeleka walimu, wala vifaa vya maabara. Wamejenga zahanati kwa mikono yao, lakini serikali imeshindwa kupeleka madaktari. Unaposema watanzania wajisaidie, unamaanisha waanzishe vyuo vya ualimu na udaktari wenyewe? Hii ni mifano tu kwamba wananchi wametimiza wajibu wao lakini serikali imeshindwa kutimiza sehemu yake.

Si uungwana kabisa kufikiria kumpiga mawe jk, lakini ni busara kuangalia ni kwa kiasi gani amefanikia kutimiza ndoto za watanzania wengi kwa kutekeleza wajibu halali aliokabidhiwa kuutekeleza. Na tufanye maamuzi yetu kwenye sanduku la kura tar 31/10. Binafsi naona tofauti kubwa sana kati ya uongozi wa mkapa na kikwete katika suala la kujenga nchi. Tafakari.

ndugu yangu unafikiri kila mtu ni muisilamu au mkristo tu kuna dini nyingi duniani ona mbali sio lazima neno au msitari huo uwe ndani ya upeo wako
 
mtaozea segerea/keko!

Dont try this anywhere!

halafu huyu ni raisi wetu wote unapofanya fujo unaharibu nchi yako unaharibu amani ya wananchi wenzako wapenda amani na mshikamano - haya maneno tusiseme seme tu kama yanaathari kubwa sana katika jamii tuwe makini

nazani tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu ni vizuri moderator wafanye mpango wa mifuta baadhi ya mada
 
Watanzania wamechoka na maisha kuwa magumu hawaoni direction ya maisha yao
mbeya walishaonesha ukomavu wao wakampiga JK mawe. Je watanzania katika kuelekea uchaguzi watamzomea na kupiga mawe baada ya kuchoshwa na maisha haya??

Hakuna sababu ya Kumpiga Mawe,hasira zetu ziwe Kuhamasishana wote sisi wenye hati za kupigia kura,kupanga foleni
,kupida kura,kulinda baada ya kuhesabiwa na kukataa matokeo bandikizi,muache aondoke kwa usalama akapumzke vizuri na kuendelea na kazi ya kuendeleza shamba lake
 
Watanganyika hamuwezi kuikataa CCM katika masanduku ya kura ,hilo kamwe halitasaidia kitu ,mbinu za kuishinda CCM ni mbinu zilezile zilizotumika Pemba ,mbinu ambazo ziliwafanya usa;lama wa Taifa wasipate usingizi mbinu ambazo ziliwafanya FFU wakimbie na masanduku ya kura mchana kweupe,mbinu ambazo zilivifanya vikosi vya SMZ na Polisi wa Muungano kufanya unyama usiosahaulika ,mbinu ambazo zimeilazimisha Serikali ya CCM Zanzibar kuamua na kukubali serikali ya umoja wa Kitaifa ,ni baada ya October kwisha kwa Uchaguzi mkuu ndipo hapo CUF itakapoingia kwenye serikali hio ,mawili ama awe ndio mshindi na CCM kuingia au awe ameshindwa na hivyo pia atakuwemo kwenye serikali tena kwa nafasi nyeti.

WaTanganyika walio wengi bado wanawaogopa polisi ufikapo uchaguzi hawawezi kuwaekea ngumu na kuhakikisha asiehusika hapigi kura ,na maboxi ya kura yanaisabiwa na kila mmoja anaona ,zaidi ni hawa mawakala wa vyama ambao roho zao bado hazijatosheka na kuweza kuibeba dhamana waliopewa kwa lolote litakalo kuwa ,akiekea hela ndogo kama milioni moja tu anawacha mawakala na watume wafanye na kupanga watakavyo. Hilo sio jambo dogo.

Jengine ni kuwa WaTanganyika hawawezi kuungana na kupinga matokeo kwa pamoja na kujumuisha wananchi ,mara utasikia akina Chadema hawaungi mkono wala mguu na si ajabu wakatoa pongezi ,kusema kweli hamuna musimamo ni mahodari wa kusema na kulipuwa mabomu pale bungeni lakini ukweli unapodhihiri huwa mnajitenga.
 
Una uhakika wamechoka na maisha umefanya utafiti wako lini mkuu ? hao ni watanzania wa maeneo gani haswa wenye kukata tamaa kihivyo - wanaofikiri mitaa yao isafishwe na kikwete , watoto wao wasomeshwe na kikwete , yeye ndio awafanyie na kutekeleza majukumu yao kila siku ni watanzania gani hao naomba kujua .

Hata mungu alisema usipojisaidia hatoweza kukusaidia so as kikwete usipojisaidia na kuonyesha njia yeye hatoweza kusaidia
Asante kwa kunena vizuri. Unajua hawa watu wanataka jk awabebe mpaka hata kwenda kwenye nyumba za ibada badala watembee kwa miguu yao. Mshindwe. Sasa mnataka kuharibu hata amani ya nchi yetu, mshindwe kabisa.
 
Hata yeye mwenyewe KKikwete amejichokea ndio maana anasema hana haja wala shida za kura zenu WAFANYAKAZI
Watanzania wamechoka na maisha kuwa magumu hawaoni direction ya maisha yao
mbeya walishaonesha ukomavu wao wakampiga JK mawe. Je watanzania katika kuelekea uchaguzi watamzomea na kupiga mawe baada ya kuchoshwa na maisha haya??
 
Watanzania wamechoka na maisha kuwa magumu hawaoni direction ya maisha yao
mbeya walishaonesha ukomavu wao wakampiga JK mawe. Je watanzania katika kuelekea uchaguzi watamzomea na kupiga mawe baada ya kuchoshwa na maisha haya??
1.Jeshi la Polisi ni lake
2.Uhasama wa taifa ooooh am sore namaanisha Usalama wa Taifa wapo chini yake.
3.Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni yake
4.Zekomedi (Augustine Mrema et al) ni wakwake
5.Waongo,wanafiki,wazushi, wambea na wababaishaji(Muhingo Rweyemamu aliyezusha eti Dakta Slaa katumwa na Mzee Ratzinger) nae anaripoti kwake
6.Yeye ni kiongozi wa Chama cha watu waliofuzu digrii za juu zaidi za WIZI WA KURA
Kwahiyo hata akipigwa mawe au akizomewa haisaidii kitu
 
Kwa mtindo huu hatutajenga ndugu zangu - huyu ni raisi wetu tumshukuru kwa yale aliyoyafanya mpaka sasa hivi hayo mengine ni ya kawaida kila kiongozi anashindwa katika baadhi ya mambo hata mwalimu nyerere aliwahi kukiri kushindwa kwake baadhi ya majukumu lakini akaamua kuchukuwa yale mazuri na kuyafanye yawe nuru ya taifa hili na mengine mengi

Kwahiyo tumheshimu raisi wetu na tumuombee mazuri kama kuna ambayo kafanya mabaya na ushahidi upo kuna vyombo vya dola vya kufanya kazi hiyo vilivyo huru kabisa na kama kuna mazuri ambayo kafanya mpaka sasa hivi apongezwe kwa hayo azidi kupewe moyo na sisi wananchi tuendele kujenga chi hii mpaka hatu ya mwisho tutakayofikia huku tukiendeleza umoja , upendo na mshikamano wetu
 
Una uhakika wamechoka na maisha umefanya utafiti wako lini mkuu ? hao ni watanzania wa maeneo gani haswa wenye kukata tamaa kihivyo - wanaofikiri mitaa yao isafishwe na kikwete , watoto wao wasomeshwe na kikwete , yeye ndio awafanyie na kutekeleza majukumu yao kila siku ni watanzania gani hao naomba kujua .

Hata mungu alisema usipojisaidia hatoweza kukusaidia so as kikwete usipojisaidia na kuonyesha njia yeye hatoweza kusaidia
Ukiisoma vizuri kauli yako, inaonyesha hata wewe unajua kuwa hakuna mtz anayetaka kusafishiwa mtaa wake na JK, kusomeshewa mtoto na JK au kutekelezewa majukumu yake na JK. Huo ni wajibu wa kila mtz kwa nafasi yake. Hata hivyo, umekwepa kusema wajibu wa JK kwa wananchi wake. Hebu tafakari mtumishi ambaye leo anapokea mshahara wa sh. 134,000 kwa mwezi, tafakari juu ya mfumuko wa bei, tafakari juu upatikanaji wa huduma za afya, tafakari juu elimu ya shule za kata, tafakari kuhusu hali ya miundombinu ya usafiri mijini na vijijini, tafakari kuhusu maisha kwa ujumla. Shusha pumzi kidogo, endelea kutafakari kuhusu hatua zinazochukuliwa na JK (Serikali)kukabiliana na hali hizo ( eti KILIMO KWANZA) endelea kutafakari juu ya hali ya vitendo vya rushwa, ufisadi na ubadhilifu wa kila namna,pima hatua zinazochukuliwa na JK (Serikali). Asiyechoshwa na haya ni mmoja wao au kuna walakini.
 
Mkuu Shy, nchi haijengwi kwa kauli mbiu
 
Najua watu wamechoka na maisha, watu hawapiti unafuu wa kuishi kuzomewa najua atazomewa wewe subri tarehe 20 mwezi huu

Wakimzomea au hata kumpiga mawe, halafu wakakamatwa na kufungwa; they have nothing to lose in fact they will be better off kwa sababu huko jela they are assured of at least one meal a day which is not the case where they live now!!
 
Una uhakika wamechoka na maisha umefanya utafiti wako lini mkuu ? hao ni watanzania wa maeneo gani haswa wenye kukata tamaa kihivyo - wanaofikiri mitaa yao isafishwe na kikwete , watoto wao wasomeshwe na kikwete , yeye ndio awafanyie na kutekeleza majukumu yao kila siku ni watanzania gani hao naomba kujua .

Hata mungu alisema usipojisaidia hatoweza kukusaidia so as kikwete usipojisaidia na kuonyesha njia yeye hatoweza kusaidia

Out of curiosity, which holy book does have that highlighted statement? Ninaisikia sana hiyo statement lakini sijawahi kusomewa au kusoma kwenye kitabu chochote kitakatifu.
 
Jiwe kubwa kuliko yote la kumpondea JK ni kura yako hapo 31 october utakapo ibonyeeeee kwa Dr. wa Slaaa, kisha kujitoa kuilinda isinyakuliwe hadi itangazwe hapo hapo kituoni! Ila msisahu kwenda na digital camera matokeo yakitoka tu, picha zinapigwa hayo makaratasi ili zikibadilishwa tuna record zote!
 
Una uhakika wamechoka na maisha umefanya utafiti wako lini mkuu ? hao ni watanzania wa maeneo gani haswa wenye kukata tamaa kihivyo - wanaofikiri mitaa yao isafishwe na kikwete , watoto wao wasomeshwe na kikwete , yeye ndio awafanyie na kutekeleza majukumu yao kila siku ni watanzania gani hao naomba kujua .

Hata mungu alisema usipojisaidia hatoweza kukusaidia so as kikwete usipojisaidia na kuonyesha njia yeye hatoweza kusaidia

Shy, ni mungu yupi aliyesema maneno niliyo-bold. Tupe specifically kama ni kutoka kwenye Biblia au Quran...maandiko yametoka mistari/sura ipi?
 
Ukiisoma vizuri kauli yako, inaonyesha hata wewe unajua kuwa hakuna mtz anayetaka kusafishiwa mtaa wake na JK, kusomeshewa mtoto na JK au kutekelezewa majukumu yake na JK. Huo ni wajibu wa kila mtz kwa nafasi yake. Hata hivyo, umekwepa kusema wajibu wa JK kwa wananchi wake. Hebu tafakari mtumishi ambaye leo anapokea mshahara wa sh. 134,000 kwa mwezi, tafakari juu ya mfumuko wa bei, tafakari juu upatikanaji wa huduma za afya, tafakari juu elimu ya shule za kata, tafakari kuhusu hali ya miundombinu ya usafiri mijini na vijijini, tafakari kuhusu maisha kwa ujumla. Shusha pumzi kidogo, endelea kutafakari kuhusu hatua zinazochukuliwa na JK (Serikali)kukabiliana na hali hizo ( eti KILIMO KWANZA) endelea kutafakari juu ya hali ya vitendo vya rushwa, ufisadi na ubadhilifu wa kila namna,pima hatua zinazochukuliwa na JK (Serikali). Asiyechoshwa na haya ni mmoja wao au kuna walakini.

Asante mkuu
 
Asipigwe mawe wala kuzomewa, bali apigwe chini kwenye uchaguzi mkuu ujao aede zake hollywood kucheza sinema kwani kazi ya usanii anaiweza, au kama hollywood iko juu sana kwake ajiunge na kina joti kwenye komedi
 
Hata mungu alisema usipojisaidia hatoweza kukusaidia so as kikwete usipojisaidia na kuonyesha njia yeye hatoweza kusaidia

MUNGU ALISEMA WAPI HAYO??? NAOMBA ANDIKO PLEASE
 
Watanzania wamechoka na maisha kuwa magumu hawaoni direction ya maisha yao
mbeya walishaonesha ukomavu wao wakampiga JK mawe. Je watanzania katika kuelekea uchaguzi watamzomea na kupiga mawe baada ya kuchoshwa na maisha haya??

Nafikiri wa kumlaumu si JK, ila ni hawa watu wa karibu waliomshauri angombee tena 2010. mi sielewi kwenye kampeni zake ataongea nini kitakacholeta mvuto kwa wananchi baada ya zile ahadi lukuki za 2005 kutotelelezwa huku maisha yakizidi kuwa magumu.

Wananchi hawatampiga mawe ila atapoteza asimilia nyingi sana za kura maana majority wananchi hawana imani naye binafsi na chama chake. Upepo ushabadilika.
 
Watanzania wamechoka na maisha kuwa magumu hawaoni direction ya maisha yao
mbeya walishaonesha ukomavu wao wakampiga JK mawe. Je watanzania katika kuelekea uchaguzi watamzomea na kupiga mawe baada ya kuchoshwa na maisha haya??

Mie naona huu ni uchochezi mmbaya sana. Kwa nini apigwe mawe au azomewe? Kama wamemchoka njia ni moja tu ambayo ni kura tarehe 31.10.2010
 
Back
Top Bottom