Elections 2010 Kikwete Kuzomewa na Kupigwa mawe?

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,269
675
Watanzania wamechoka na maisha kuwa magumu hawaoni direction ya maisha yao
mbeya walishaonesha ukomavu wao wakampiga JK mawe. Je watanzania katika kuelekea uchaguzi watamzomea na kupiga mawe baada ya kuchoshwa na maisha haya??
 
Hatazomewa wala kipigwa mawe hadharani ila atafanyiwa mambo hayo siku ya kupiga kura,kumbuka ya msafara wake kupigwa mawe usiku mkoani Mbeya
 
Kwa nini wampige mawe? hakuna sababu wala ya kumzomea, wamnyime kura zao wakitaka inatosha.
 
Najua watu wamechoka na maisha, watu hawapiti unafuu wa kuishi kuzomewa najua atazomewa wewe subri tarehe 20 mwezi huu
 
Una uhakika wamechoka na maisha umefanya utafiti wako lini mkuu ? hao ni watanzania wa maeneo gani haswa wenye kukata tamaa kihivyo - wanaofikiri mitaa yao isafishwe na kikwete , watoto wao wasomeshwe na kikwete , yeye ndio awafanyie na kutekeleza majukumu yao kila siku ni watanzania gani hao naomba kujua .

Hata mungu alisema usipojisaidia hatoweza kukusaidia so as kikwete usipojisaidia na kuonyesha njia yeye hatoweza kusaidia
 
Shy umenena vizuri, lakini cha msingi anatakiwa aongoze watu katika mwelekeo wenye kukidhi haja zao. siyo kama sasa kila mtu kawa mpenda hela, watu hawafanyi kazi zao bwana, nategemea JK kama kiongozi angekuwa ameshachukua hatua za haraka na kuweka mambo sawa, mfano ni mfumuko wa bei, watu kibao wanakaa vijiweni hao watu si angebuni ( toa assignment kwa wahusika ili watu washughulishwe). Tuna ardhi, tuna vitu kibao vya kufanya lakini tunasubiri wafadhili watufanyie kila. Tatizo linajulikana lakini viongozi wetu wengi wamekuwa wabinafsi sana.
 
unaleta siasa za chuki, huna maana. kwanini unahamasisha watu wampige kikwete mawe hata kama yeye si chaguo lako?
 
Bange hizi!
 
mhhh mnataka kufungwa plasta usoni nyie....mmh mi sipo ntamoigia Dr.Slaa kimya kimya wala staki mbwembwe mie
 
Mie naona hasira zote zielekezwe kwenye sanduku la kura tu....hapo itakuwa poa.
 
Maneno matupu hayavunji mfupa.
Kumtupia mawe mkuu wa nchi siyo jambo la busara.
Tumia nafasi yako kama mtanzania kupiga kura ya amani KIKWETE YES/NO na DR SLAA YES/NO.
Hapo utakuwa umeuridhisha moyo wako kwa amani.
Hasira hasara!!!!!!!!!!
 
Watanzania wamechoka na maisha kuwa magumu hawaoni direction ya maisha yao
mbeya walishaonesha ukomavu wao wakampiga JK mawe. Je watanzania katika kuelekea uchaguzi watamzomea na kupiga mawe baada ya kuchoshwa na maisha haya??

Je ugumu wa maisha yao umeanza wakati wa kikwete? na kama siyo wakati wa kikwete walifanya nini mwaka 2005? Wambie hao wenye fikra za kuzomea na kupiga mawe kuwa wakitaka mageuzi wajitokeze kupiga kura. Vile vile hakuna rais atakaye wapelekea pesa majumbani au mifukoni kwao bila kufanya kazi. Tamaa ya pesa za haraka haraka ndiyo iliyowafanya hao jamaa wa mbeya kuishia kuchuna watu ngozi na kupigana nondo hovyo.
 
Una uhakika wamechoka na maisha umefanya utafiti wako lini mkuu ? hao ni watanzania wa maeneo gani haswa wenye kukata tamaa kihivyo - wanaofikiri mitaa yao isafishwe na kikwete , watoto wao wasomeshwe na kikwete , yeye ndio awafanyie na kutekeleza majukumu yao kila siku ni watanzania gani hao naomba kujua .

Hata mungu alisema usipojisaidia hatoweza kukusaidia so as kikwete usipojisaidia na kuonyesha njia yeye hatoweza kusaidia
Ni mstari gani vile unaosema usipojisaidia hatokusaidia? Nadhani Shy hapa umetudanganya hakuna mahali katika biblia au Quran ambapo Mungu amesema tujisaidie na yeye atusaidie. Kama upo tunaomba mtuwekee hapa.

Watanzania wametimiza wajibu wao kwa kiasi kikubwa. Wamejenga shule ambazo serikali imeshindwa hata kupeleka walimu, wala vifaa vya maabara. Wamejenga zahanati kwa mikono yao, lakini serikali imeshindwa kupeleka madaktari. Unaposema watanzania wajisaidie, unamaanisha waanzishe vyuo vya ualimu na udaktari wenyewe? Hii ni mifano tu kwamba wananchi wametimiza wajibu wao lakini serikali imeshindwa kutimiza sehemu yake.

Si uungwana kabisa kufikiria kumpiga mawe JK, lakini ni busara kuangalia ni kwa kiasi gani amefanikia kutimiza ndoto za watanzania wengi kwa kutekeleza wajibu halali aliokabidhiwa kuutekeleza. Na tufanye maamuzi yetu kwenye sanduku la kura tar 31/10. Binafsi naona tofauti kubwa sana kati ya uongozi wa Mkapa na Kikwete katika suala la kujenga nchi. Tafakari.
 
Watanzania wamechoka na maisha kuwa magumu hawaoni direction ya maisha yao
mbeya walishaonesha ukomavu wao wakampiga JK mawe. Je watanzania katika kuelekea uchaguzi watamzomea na kupiga mawe baada ya kuchoshwa na maisha haya??

huu si ukomavu ni UHALIFU.......Kikwete kachaguliwa kwa kura na mnaweza kumtoa kwa KURA........
 
Kwa nini wampige mawe? hakuna sababu wala ya kumzomea, wamnyime kura zao wakitaka inatosha.

kweli wakimpiga mawe watakuwa wamemkosea watafanya kweli kwa kuchekesha pumba na mchele

Una uhakika wamechoka na maisha umefanya utafiti wako lini mkuu ? hao ni watanzania wa maeneo gani haswa wenye kukata tamaa kihivyo - wanaofikiri mitaa yao isafishwe na kikwete , watoto wao wasomeshwe na kikwete , yeye ndio awafanyie na kutekeleza majukumu yao kila siku ni watanzania gani hao naomba kujua .

Hata mungu alisema usipojisaidia hatoweza kukusaidia so as kikwete usipojisaidia na kuonyesha njia yeye hatoweza kusaidia

Mkuu hapa hakuna haja ya kufanya utafiti labda kama wewe huishi Tanzania, Maisha yamekuwa magumu saaana

Shy umenena vizuri, lakini cha msingi anatakiwa aongoze watu katika mwelekeo wenye kukidhi haja zao. siyo kama sasa kila mtu kawa mpenda hela, watu hawafanyi kazi zao bwana, nategemea JK kama kiongozi angekuwa ameshachukua hatua za haraka na kuweka mambo sawa, mfano ni mfumuko wa bei, watu kibao wanakaa vijiweni hao watu si angebuni ( toa assignment kwa wahusika ili watu washughulishwe). Tuna ardhi, tuna vitu kibao vya kufanya lakini tunasubiri wafadhili watufanyie kila. Tatizo linajulikana lakini viongozi wetu wengi wamekuwa wabinafsi sana.

Asante mkuu mpaka sasa hatujawa na uwezo wa kuendesha rasilimali zetu

unaleta siasa za chuki, huna maana. kwanini unahamasisha watu wampige kikwete mawe hata kama yeye si chaguo lako?

Kikwete ni chaguo langu ila matendo na utendaji wake ndo unaikosesha amani

Maneno matupu hayavunji mfupa.
Kumtupia mawe mkuu wa nchi siyo jambo la busara.
Tumia nafasi yako kama mtanzania kupiga kura ya amani KIKWETE YES/NO na DR SLAA YES/NO.
Hapo utakuwa umeuridhisha moyo wako kwa amani.
Hasira hasara!!!!!!!!!!

Asante mkuu

Je ugumu wa maisha yao umeanza wakati wa kikwete? na kama siyo wakati wa kikwete walifanya nini mwaka 2005? Wambie hao wenye fikra za kuzomea na kupiga mawe kuwa wakitaka mageuzi wajitokeze kupiga kura. Vile vile hakuna rais atakaye wapelekea pesa majumbani au mifukoni kwao bila kufanya kazi. Tamaa ya pesa za haraka haraka ndiyo iliyowafanya hao jamaa wa mbeya kuishia kuchuna watu ngozi na kupigana nondo hovyo.

Umeongezeka saana kwa kipindi cha miaka 5 from 2005
 
Una uhakika wamechoka na maisha umefanya utafiti wako lini mkuu ? hao ni watanzania wa maeneo gani haswa wenye kukata tamaa kihivyo - wanaofikiri mitaa yao isafishwe na kikwete , watoto wao wasomeshwe na kikwete , yeye ndio awafanyie na kutekeleza majukumu yao kila siku ni watanzania gani hao naomba kujua .

Hata mungu alisema usipojisaidia hatoweza kukusaidia so as kikwete usipojisaidia na kuonyesha njia yeye hatoweza kusaidia

Hapa mkuu umepotea. Kuna kazi zinazo fanywa na Serikali. Hizi kazi zisipo timizwa, ndo mambo yanaonekana kombo.Hatuzungumzii mambo ya mtu binafsi, tunaongelea kazi zilizo shindwa kufanywa na Serikali.
 
Back
Top Bottom