Kikwete kuwa Gorbachev wetu?

Hiyo siyo nadharia yako ila mwl nyerere..alisema hayo kwenye maongezi yake...kama amekuwa yahaya na yeye sijui!

Hata ikiwa hivyo wewe mtanganyika inakuhusu nini? ombeni na nyinyi kusitokee mwanza zone and kilimanjaro zone damn!


Kidole kimoja hakivunji chawa.Umoja ni Nguvu na Utengano ni dhaifu. Wazanzibari wanashangilia kufa kwa muungano lakini hawajui baada ya hilo fungate ni mateso. Yani hawa jamaa wananifananisha na wakati wa Musa na Waisraeli kule jangwani. Kwamba bora usultani kuliko kwenda nchi ya maziwa na asali. Tumaini naona unajiandaa kurudi kwenye zama za makuli na kufuta dhana ya Shafi Adamu Shari kwenye kitabu chake cha KULI.
 
Kidole kimoja hakivunji chawa.Umoja ni Nguvu na Utengano ni dhaifu. Wazanzibari wanashangilia kufa kwa muungano lakini hawajui baada ya hilo fungate ni mateso. Yani hawa jamaa wananifananisha na wakati wa Musa na Waisraeli kule jangwani. Kwamba bora usultani kuliko kwenda nchi ya maziwa na asali. Tumaini naona unajiandaa kurudi kwenye zama za makuli na kufuta dhana ya Shafi Adamu Shari kwenye kitabu chake cha KULI.

Wahurumie watanganyika walioko shinyanga hawajaona maji tangu uhuru kuliko wazanzibar?

Wahurumie watanganyika walioko kigoma ambao hawana njia nyingine zaidi reli ya kati tangu uhuru (na haiko salama) kuliko wazenj?

Mimi siyo mzenj lakini watanganyika ni wanafiki to highest standard...waacheni wakirudi kwenye ukuli inawauma nini? mnajifanya mna wahurumia wazenj kuliko watanganyika au mna ajenda zenu chafu
 
Muungano ulipigiwa kura na Bunge la Tanganyika na Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar. Pande zote mbili zilijadili (najua wengi hawajui historia hiyo). Nyerere alileta hoja Bungeni na kuwaelewa wabunge wetu kwanini mataifa mawili haya yataungana. Wabunge wakaridhia na ni baada ya hapo ndio Muungano ukafanyika.

Hivyo ni Muungano halali na ni jukumu la kila Mtanzania kuulinda. Katika kuulinda huko ni jukumu letu kuwapinga pasipo kuwapepesea macho wale wote wanaotaka Muungano uvunjike kwa sababu hawataki kufanya maamuzi magumu au kuzungumzia mambo yanayoleta utata katika Muungano. Wapo watu wa bara ambao kwa kawaida hatupendi sana migongano, tunapenda vitu lelemama kiasi kwamba tumekuwa kama tumedekezwa hivi!

Serikali ikisema "hawa wanaleta mgawanyiko katika jamii" basi kama watoto tunakubali na kuwakimbia wenzetu kwa sababu "serikali imesema"; Serikali ikija na kusema wapinzani wanataka kuligawa taifa basi tunakimbia kama watoto huku tumenyanyua mikono tubebwe huku tunaonesha vidole "yule anataka kuligawa taifa mama!".

Hatutaki kugonganisha mawazo na matokeo yake hata kwenye vikao vya kazi tumekuwa hivi hivi tu. Mtu anayebisha sana anaonekana "mbishi tu"; mtu anayetaka maelezo zaidi anaonekana kama anataka kujipendekeza. Tunataka mambo ya upole upole na taratibu.

Ndio maana utaona watu wengi wa bara wanaotaka Muungano uvunjike wanafanya hivyo kwa sababu utaondoa "migongano" na kubishana bishana. Tunataka "utulivu, amani, na mshikamano" wa uongo. Ndio maana watu wa bara wanaona kama Zanzibar ni wakorofi kweli kumbe kule Zanzibar wao wameshazoea zile siasa za kujibizana, kubishana na serikali, na kutunishiana misuli.

Ninaamini athari kubwa sana ya ukoloni katika psyche ya watu wa bara ni unchecked docility ya ajabu sana. Na watawala wetu wanatumia sana hii kuwatuliza watu wa bara.

Muungano tutaulinda na tutaudumisha na kuuboresha. Tutawapinga watu wa bara wanaotaka kuuvunja kwa sababu hawataki kubishana na kulumbana na kugongana kifikra na tutawapinga watu wa visiwani wanaotaka kuuvunja kwa sababu wanaogopa kukubali ukweli wa umuhimu wa muungano.

Tutawaunga mkono wale wote majasiri ambao watasimama na kutoa hoja za jinsi ya kuudumisha, watakaokuwa tayari kutoa mapendekezo ya jinsi ya kuuboresha na wale watakaonesha uongozi wa kuboresha muungano wetu kwa uwazi na ukweli na ujasiri usio kikomo.

Natumaini hatutawafumbia macho wala kuwaonea haya kuwashughulikia pasipo kuwabembeleza watu wanaofanya njama za kuuvunja muungano wetu.

Muungano daima!

Mkuu Mwanakijiji,

Kama ni kweli kuwa "muungano ulijadiliwa na kuridhiwa na bunge" kuna ugumu gani wa kuleta hili swala kwa public tukubaliane?

Why is it that linapokuja swala la muungano inakuwa siri siri tuu?

Nakubaliana nawewe kuwa bara tunapenda utulivu na amani ki uwongo!! Hivi inamaana hao wakubwa hawaelewi ni muhimu wananchi wakashirikishwa in full kujadili mustakabali wa muungano?

Kwa kweli mimi nawa-support wazanzibar walivyoamua kukubaliana kivyao na kuamua kusinga mbele!!!

Sisi tutabaki kufuata upepo tu...
 
of course hana; lakini ana uwezo wa kuwazuia wengine wasivunje?

JK hatufai!! my take ni kuwa, kama hawezi kuunusuru huu muungano alioapa kuulinda, lakini kuwa tayari kutumia mabavu kuuzuia!!!

Tutaingia katika machafuko makubwa... I htink it is the beginning of the failure...
 
Si ndio wanafuata wanatumia kikao cha wawakilishi kilicho halali kikatiba kuomba kibadilishwe ili kiwafae watu na mahitaji yao...

tatizo kwanini watu wa bara wanataka kuwahadaa wazenj wasitumie fursa hiyo kubadilisha katiba?
Sometimes men are masters of their own fate! Nafikiri Zenj wameshafanya due diligence ya kutosha ya consequences za kuuvunja muungano.
Pamoja na makosa kadhaa ndani ya muungano, pia muungano huu umeyasitiri mengi. Ngoja tuone nini kitajiri baada ya kujivua nguo hii ya muungano.
Lakini wakati huo huo, uongozi imara hauonekani wakati wa kushangilia stars ikicheza na Msumbiji au Ghana...unaonekana katika umahili wa kutatua matatizo yaliyopo mezani wakati huo. All the best kwenu leaders!!!
 
of course hana; lakini ana uwezo wa kuwazuia wengine wasivunje?

Wewe unaunga muungano kwasababu gani? au kwa vile kasema nyerere?

Huwa napata shida na watu wanaoshadidia muungano usivunjwe utafikiri kijiti agh! wekeni hadharani tujadili kipengele kwa kipengele faida na hasara zake kwa mwaka mzima halafu tupige kura Watetezi vs Wapingaji hoja kwa hoja..hatuwezi kuendelea ku-rely kwa nyerere na karume time is over!

Kama hatupendani kuna haja gani ya kugan'angania muungano au agenda gani zaidi ya watu na uchumi? kwa ajili ya watu?

Nashawishika kusema Huu muungano una sababu Chafu sana tena sana kwa wazanzibar kwasababu kila wakati wabara wanahangaika nao utafikiri unalipa kuliko issue ya maji shinyanga agh!
 
Mimi sishabikii kuvunja muungano kama unakuwa na manufaa lakini vile vile siungi mkono tubaki na muungano wa kulazimishana ambao kwa zaidi ya miaka 40 sijaona matunda yake au matunda yake ni ya kufikirika sana yanayoonekana kwa wachache hasa viongozi na si wananchi.

Maana mtu akihoji juu ya muungano utasikia oooh acha kabisa usiguse hapo waasisi wetu walisema hivi Tanganyika tulizaliwa na muungano au tumerogwa kuwa tusiguse kitu hiki siku tukigusa hakika tutakufa kwa nini tunaendelea kuusujudu kama dini

Kuna viinchi vidogo tu kama Rwanda na Burundi vinamendeleo kutuzidi na watu wake ni wa kabila moja watusi na wahutu mbona hatujasikia wanataka iwe nchi moja kwa nini tusiende kuwashauri na wao waungane kama sisi

Nimezaliwa enzi za uhuru karibu nazeeka sasa nasubiria matunda yake sijayaona zaidi ya kutishiwa nisihoji kama ni vipi bana muungano na ufe tuone kama watanganyika hatuwezi kuishi bila muungano.
 
@Kuchanganya Mchanga
Mchanga uliochanganywa ni wa Tanganyika tuu...naye ni Nyerere pekee ndie aliechanganya mchanga huo wa mikoa tofauti kutoka Bara.

Ukitizama hii picha, utaona Karume hajagusa mchanganya huo..kwasababu si mchanga wa visiwani.

@Mwanakijiji
Ukitizama nyaraka ya muungano ni saini za Nyerere tuu na Msekwa hakuna saini ya Baraza au bunge la Zanzibar.Sasa huu msimamo wako kuwa Zanzibar walipitisha na kukubali muungano ulitokea wapi?Lete ushahidi kama huna basi unazungumza pumba tupu...

Nyaraka ya muungano iliyopo kwenye public http://www.scribd.com/full/24823426?access_key=key-1dlp0tnzt4n91utuby5c
 

Attachments

  • muungano1bc.jpg
    muungano1bc.jpg
    50.4 KB · Views: 46
@Kuchanganya Mchanga
Mchanga uliochanganywa ni wa Tanganyika tuu...naye ni Nyerere pekee ndie aliechanganya mchanga huo wa mikoa tofauti kutoka Bara.

Ukitizama hii picha, utaona Karume hajagusa mchanganya huo..kwasababu si mchanga wa visiwani.

@Mwanakijiji
Ukitizama nyaraka ya muungano ni saini za Nyerere tuu na Msekwa hakuna saini ya Baraza au bunge la Zanzibar.Sasa huu msimamo wako kuwa Zanzibar walipitisha na kukubali muungano ulitokea wapi?Lete ushahidi kama huna basi unazungumza pumba tupu...

Nyaraka ya muungano iliyopo kwenye public http://www.scribd.com/full/24823426?access_key=key-1dlp0tnzt4n91utuby5c


MrFroasty angalia picha hii Karume naye alisaini, hizo nyaraka za sahihi yake ziko wapi mbona umetupa za Nyerere na Msekwa tu.

Nyerere na Karume wasaini mkataba


 
MrFroasty angalia picha hii Karume naye alisaini hizo nyaraka za sahihi yake ziko wapi mbona umetupa za Nyerere na Msekwa tu.

Nyerere na Karume wasaini mkataba



Inachanganya kidogo kwamba Karume anatia saini lakini haionekani kwenye mkataba...naona picha hii imepigwa wakiuziana kiwanja sio muungano.

Kama ingelikuwa muungano basi hiyo saini ya Karume ni lazima ionekane kwenye mkataba.
 
Wacha wenda kunaani kwani yakhe. Katiba tuliyonayo haitoi fursa ya kuleta mabadiliko yanayohitajika kwa sasa. Muungano huu pia, tangu wazo hadi kusainiwa na kuwa mkataba, ulichukua muda mfupi mno. Hata mijadala ndani ya mabunge haikuwepo zaidi ya kuwa mihuri tu. Jumbe alihoji, lakini akaonekana mchafuzi wa hali ya hewa. Muungano ulisimamiwa na katiba ya muda, muda ambao ni umri wa mtu. Nyerere alisema angekuwa na uwezo angevisukumia mbali visiwa hivi, na alisisitiza kuwa hatanii. Wanaong'ang'ania muungano huu wanapuuza maono ya Nyerere aliyeona tangu zamani kuwa vitatusumbua. Tusiwe wagumu wa kukubali mabadiliko. Mke akishindwa ndoa mpe talaka ende. Mie Mtanganyika sijaona faida hata kidogo ya muungano hili. Enzi ya vita baridi imekufa kibudu, no Cuba ya Afrika wala mjukuu wake. Wapemba, vunjeni muungano, mbaki na hisbu yenu, sisi huku tupue alaaa. Na hatutaki wakimbizi mwende shimoni. Acha tuonje nyama ya mtu, tuwe wachawi kwishneee.
 
Inachanganya kidogo kwamba Karume anatia saini lakini haionekani kwenye mkataba...naona picha hii imepigwa wakiuziana kiwanja sio muungano.

Kama ingelikuwa muungano basi hiyo saini ya Karume ni lazima ionekane kwenye mkataba.
Duuh hii kali, na kiwanja chenyewe ni hicho kisiwa cha zbar!
 
@Mwanakijiji
Ukitizama nyaraka ya muungano ni saini za Nyerere tuu na Msekwa hakuna saini ya Baraza au bunge la Zanzibar.Sasa huu msimamo wako kuwa Zanzibar walipitisha na kukubali muungano ulitokea wapi?Lete ushahidi kama huna basi unazungumza pumba tupu...

Nyaraka ya muungano iliyopo kwenye public http://www.scribd.com/full/24823426?access_key=key-1dlp0tnzt4n91utuby5c

Kuna msemo unasema "usilolijua ni kama usiku wa kiza".

Ulichoambatanisha kuwa ni "nyaraka za Muungano" ukweli ni sheria iliyopitishwa na Bunge la Tanganyika kuridhia muungano; sheria kama hiyo ilipitishwa Zanzibar vile vile. Utaona kuwa ni kwa sababu hiyo unaona sahihi ya Nyerere kukubali mswada wa sheria kuwa sheria kamili; sahihi ya Katibu wa Bunge (wakati huo Msekwa) na chini kuna sahihi ya Chief Mkwawa (ambaye alikuwa ni Spika).

Wale wanaodai Muungano ulifanywa kwa siri ni wakanaji wa historia. Sheria ya Muungano iko wazi (kama ulivyoiweka hapa). Na mjadala wa Bunge la Tanganyika kuhusu Muungano unaweza kupatikana kwenye ofisi za Bunge. Hakuna cha siri ni tatizo la watu ambao hawataki kufanya uchunguzi wao wenyewe kwenda kutafuta ukweli.
 
Sioni faida ya hili dubwana muungano kwa sasa,maoni yangu huu muungano wanaoufaidi ni wanasiasa wa pande zote mbili na Wanzazibari sisi Wadanganyika wa kawaida huo muungano hautupi tija yoyote zaidi ya kutupotezea muda na raslimali zetu,waachieni Zanzibar yao na hapo ndio tuanze kuwasikia sisi wazanzibara wao Wazanzibari,sisi wapemba wao waunguja
 
Back
Top Bottom