Kikwete kuvuliwa Uenyekiti wa CCM 2012? Makamba awajia juu wanaojipanga

Status
Not open for further replies.
Mfa maji haishi kutapatapa.

Mwisho wa Sisiemu huoooo umewadia.

1. Hawana mgombea anayekubalika 2015
2. Hawana sera mpya
3. Wameendekeza ufisadi

Hapo ndio patakuwa patamu, wamweke Makamba kuwa mwenyekiti wao
 
Tusiandikie mate na wino upo.

Tusubiri 2015 kama Chadema ataweza kufikisha japo 10% ya kura za rais na kupata hata 5% ya idadi ya wabunge ndani ya bunge la muungano.
 
Hata gazeti likaamini upupu huu na watu wakaushabikia inaonyesha vipi Watanzania tulivyokwisha kata tamaa. Tumebaki kuishi kwa mategemeo na udaku basi!

yakitokea utaomba radhi? Au kama kawaida yenu kujifanya wajuaji katika kila jambo kumbe..
 
KATIBU MKUU wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusufu Makamba, amesema wanaofikiria kumpokonya Rais Jakaya Kikwete kiti chake cha uenyekiti wa chama hicho ni wahaini. Makamba alitoa kauli hiyo jana kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari akijibu taarifa ya gazeti hili juzi kwamba kuna kikundi ndani ya CCM kinachofikiria kutenganisha kofia ya urais na uenyekiti wa chama hicho tawala.

Huku akitumia maneno makali na ya kejeli, Makamba alisema Rais Kikwete ni mtaji wa kuaminika ndani ya chama hicho na kwamba alishinda uchaguzi mkuu uliopita kwa sababu ya umaarufu wake. “Mtaji kwa kawaida haufujwi bali unakuzwa, kwa hiyo hatuwezi kumng’oa Rais Kikwete anayependwa na wananchi baada ya ushindi huu mkubwa, alisema na kuongeza: “…kitendo chochote cha kufikiria kumng’oa katika nafasi hizo ni cha uhaini dhidi ya chama chetu na hakiwezi kukubalika,” alisema Makamba.

Alisema hata Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haina uwezo wa kumng’oa mwenyekiti huyo na wala CCM haiwezi kutenganisha kofia alizonazo Rais Kikwete.
Katika gazeti hili Jumatano wiki hii iliripotiwa taarifa iliyoeleza kuwa mambo yazidi kwenda mrama ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo mkakati unasukwa kutaka kumuengua Rais Jakaya Kikwete kwenye nafasi yake ya uenyekiti wa chama hicho taifa. “Sababu kubwa inayotajwa na waumini wa mkakati huo ni kwamba muundo wa sasa wa Rais kuwa na kofia mbili umesababisha dhambi za chama kubebwa na serikali na zile za serikali kubebwa na chama,” ilibainika.

Source: Tanzania Daima
 
Makamba na Jk ni gamba ambalo ccm inatakiwa ijivue, kama ulivyo mkakati wake kamambe wa kufanya marekebisho makubwa ya kukinusuru chama.
.
 
CCM; nyoka ni yule yule na gamba ni lile lie - hakika chama hiki ni sikio la kufa hivyo kamwe halitokaa lisikie dawa isipokua ufisadi tu!!!!!!!

Heko yenu Mzee Makamba na wala msisikilize cha mtu; go go go CCM, go hadi kaburini just go!!!!!!!!!!
 
Re: Prof. Safari ajiunga CHADEMA; akabidhiwa kadi rasmi leo

VITA DHIDI YA UFISADI NCHINI UTASHINDWA KIULAINI ZAIDI NA SISI VIJANA TUKIFANIKIWA KWANZA KUSHINDA NGUVU ZA MIGAWANYIKO KIDINI, KIKANDA, KISOMI, NA KIKABILA

Kwa kauli za kiupole, kistaarabu na kizalendo zaidi alizozitumia mwenzetu MZALENDO80 tena kwa moyo Ki-Tanzania kabisa, kama kweli bado kuna binamu mwenye ujasiri wa kubishana na hii kauli kutoka kwenye sakafu ya moyo wa huyu ngudu yetu basi naomba sana hapa niwe wa kwenza kukuombe usamehewe bure kabisa bi gharama yoyote.

Ewe Mungu wetu mkuu uliye Mungu mmoja tu na huku duniani watu tukikuabudu kwa dini na mi-dhebu zetu tofauti tofauti lakini wewe ukibakia kuwa ni Mungu yule yule Jana, Leo na Milele; nakuomba hata dakika moja usituache tuaibike, usituache tunyanyasike na wala usituache tugawanyike kama taifa kwa wakati wote tunaendelea kupigana vita vikali nchini dhidi ya UFISADI uliorasmishwa na kulazimishwa kuwa sehemu ya maisha yetu hata kama tunakufa na umasikini wa kupindukia huku wachache wakila na kusaza.

Mungu wetu fungua njia Tanzania Bara na Visiwani kote vijana tuondokane na minyororo ya chuki za kuchonga za kidini, na migawanyiko aina mbali mbali isiyokua na kichwa wala miguu ili tukalipiganie kwa pamoja taifa letu kwani sisi vijana ustawi mzuri wa taifa hili linatuhusu na vizazi vijazo kuliko kundi nyingine yoyote ya Wa-Tanzania.

Mungu unaju fika kwamba sisi kama vijana wa taifa hili nguvu ya fedha hatuna, dola hatuna wala makeke hatuonyeshi ila nia thabiti ndio nguzo yetu kuu tunayoitumia leo na siku zote kulikomboa taifa hili kwa manufaa ya umma wa taifa hili.

Nguvu Tunayo kupigania taifa la Tanzania, Sababu Tunayo ya kuung'oa UFISADI na mizizi yake yote nchina, na kubwa zaidi ni kwamba UWEZO TUNAO pia tutakaoutumia kukamilisha azma yetu kwa njia mbali mbali zote za amani.

Ewe Mungu tusaidie na Vijana sasa tusonge mbele zaidi kumalizili kiporo cha mfumo wa ufisadi uliobakia na tukajiletee wenyewe katiba mpya tuitakavyo sisi wenyewe wananchi.

quote_icon.png
Originally Posted by HM Hafif
ndugu yangu weeee mbona mikwara mingi sana na kujinasibu kwa sana kuwa wewe muislam.

nani aliyejinasibu au kukueleza kuwa mimi mwislam au kwa sababu za hoja zangu. Hakika mimi ni msema kweli bila kuogopa na nina uwezo mkubwa sana wa kuonesha na mara nyingi nimebainisha kuonyesha umma kuwa Chadema ni chama cha kikanda, kikabila , kiudugu na kidini. Mifano ipo mingi na takriban yoote nimeibansha lakini kwa kukusaidia na kukuzindua kuhusu hilo hebu pitia mchakato wao wa uchaguzi mkuu wa viongozi wao ngazi ya taifa na uchaguzi wenyewe na umchakato na uteuzi wa viti maalum utagundua hilo.

naomba uzinduke na kuyaona hayo na sio kujifanya mwenye chongo.

KATIBU MKUU wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusufu Makamba, amesema wanaofikiria kumpokonya Rais Jakaya Kikwete kiti chake cha uenyekiti wa chama hicho ni wahaini.

Makamba alitoa kauli hiyo jana kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari akijibu taarifa ya gazeti hili juzi kwamba kuna kikundi ndani ya CCM kinachofikiria kutenganisha kofia ya urais na uenyekiti wa chama hicho tawala.

Huku akitumia maneno makali na ya kejeli, Makamba alisema Rais Kikwete ni mtaji wa kuaminika ndani ya chama hicho na kwamba alishinda uchaguzi mkuu uliopita kwa sababu ya umaarufu wake. “Mtaji kwa kawaida haufujwi bali unakuzwa, kwa hiyo hatuwezi kumng’oa Rais Kikwete anayependwa na wananchi baada ya ushindi huu mkubwa, alisema na kuongeza: “…kitendo chochote cha kufikiria kumng’oa katika nafasi hizo ni cha uhaini dhidi ya chama chetu na hakiwezi kukubalika,” alisema Makamba.

Alisema hata Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haina uwezo wa kumng’oa mwenyekiti huyo na wala CCM haiwezi kutenganisha kofia alizonazo Rais Kikwete.
Katika gazeti hili Jumatano wiki hii iliripotiwa taarifa iliyoeleza kuwa mambo yazidi kwenda mrama ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo mkakati unasukwa kutaka kumuengua Rais Jakaya Kikwete kwenye nafasi yake ya uenyekiti wa chama hicho taifa. “Sababu kubwa inayotajwa na waumini wa mkakati huo ni kwamba muundo wa sasa wa Rais kuwa na kofia mbili umesababisha dhambi za chama kubebwa na serikali na zile za serikali kubebwa na chama,” ilibainika.
Source: Tanzania daima
 
CCM; nyoka ni yule yule na gamba ni lile lie - hakika chama hiki ni sikio la kufa hivyo kamwe halitokaa lisikie dawa isipokua ufisadi tu!!!!!!!

Heko yenu Mzee Makamba na wala msisikilize cha mtu; go go go CCM, go hadi kaburini just go!!!!!!!!!!

hata akija nani sie wapinzani wenu 'wakuu sana' CDM tunadunda tu kama jana,pee..opleeees ..!!
 
na nahisi Lowasa ataukwaa uenyekiti

Kosa lako ni kuhisi wakati yeye ndiye anayesuka mpango huu ili aweze kukimiliki chama na hatimaye kigeuke kuwa ngalawa yake ya kuvukia pwani na kuingia nyumba nyeupe. Hii stori imepitishiwa Tanzania Daima kupitia kwa sabuni yao Kibanda ili kupima upepo wa wananchi. Lakini tunasema hivi: WANAJIDANGANYA! WAKITAKA WAKAUNDE CHAMA CHAO, KAMA WATAPATA WAFUASI ZAIDI YA WAKE ZAO, WATOTO NA HAWARA ZAO!
 
kwa jinsi alivyoongea jana ,watamfukuza soon maana hana vision,mission wala sio concious wa nchi wala chama chake
 
Mkimuondoa JK kwenye uwenyekiti, labda mumweke FFU, maana sasa ndo ccm itasambaratika kabisa. maana na wasiwasi hata na nidhamu katika vikao itashuka, na makonde yatachapwa. Huyo ni raisi at least mnamuogopa.

Shauri yenu.:redfaces:
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom