Kikwete kutembelea wizara tena

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,163
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Januari 15, 2009, anaanza awamu ya pili ya mikutano muhimu na wizara mbalimbali kufuatilia utendaji wa wizara hizo, utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, pamoja na maagizo aliyoyatoa kwa wizara hizo wakati anaingia madarakani.

Katika mikutano ya mwanzo, Rais Kikwete ataanza na wizara zinazohusika na masuala ya uchumi, ambayo ni sekta kuu lengwa katika utekelezaji wa Serikali ya Rais Kikwete kwa mwaka huu, 2009.

Leo katika mkutano wake wa kwanza ataanza na Wizara ya Miundombinu pamoja na uongozi wa Bandari ya Dar es Salaam na Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL).

Kesho, Ijumaa, Januari 16, 2009, ataendelea na Wizara ya Miundombinu kwa kukutana na viongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Wizara yenyewe, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Wakala wa Majengo ya Serikali, TANROADS na SUMATRA.

Jumatatu ijayo, Januari 19, 2009, Rais atakutana na viongozi wa Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA), Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Wizara ya Fedha na Uchumi pamoja na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG).

Jumatatu ya Februari 9, 2009, Rais atakutana na viongozi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko; Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) pamoja na Bodi ya Biashara ya Nje (BET).

Jumanne, Februari 10, 2009, Rais atakutana na uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Kusambaza Umeme Vijijini (REA), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA).

Februari 11, 2009, Rais atakutana na uongozi wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika. Siku hiyo hiyo mchana, Rais atakutana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia; Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano (TCRA) na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

Alhamisi ya Februari 12, 2009, Rais atafanya kikao na Wizara ya Elimu, Mafunzo na Ufundi; Baraza la Mitihani, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu, TAHLISO na viongozi wa vyuo vikuu vya umma nchini.

Ijumaa ya Februari 13, 2009, Rais atakutana na uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA).

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

14 Januari, 2008
 
wandungu,

..huu ni usanii mtupu.

..ujue hapo he is laying the ground kwa safari ya muda mrefu nje nchi.

..anakutana na TRA,BOT,CAG, hawajatajwa watu wa CMSA lakini na wenyewe wanahusika, etc etc. kesho yake anadamkia wizara nyingine yenye taasisi lukuki chini yake. muda wa kutafakari na kufanyia kazi issues zitakazojitokeza uko wapi?

..nasema Raisi Kikwete hana tofauti na Richmond. yeye pia alidanganya[kwa kununua magazeti,rushwa,..] kwamba anaiweza kazi ya Uraisi. ukweli unadhihirika sasa hivi kwamba hana uwezo wa kuongoza.

NB:

..are going to have Ngurdoto II ???
 
yawezekana ni hivyo lakini hawakuiweka hiyo ya yahoo kwenye barua yao ya leo siyo?

Kwenye taarifa yao of course haikuwapo hiyo ya yahoo lakini taarifa yenyewe imesambazwa kupitia: "Salvator Rweyemamu" <salvatorweyemamu@yahoo.co.uk>
 
...but question is, does this new email actually work? like, can you shoot an email and get a response?
...i guess there is only one way to find out...

We, wala uspoteze muda wako, wako busy sana hawana muda wa kujibu
 
Hivi ile tabia ya kupaka rangi mpya majengo ya serikali wakati wa ziara ya Prez bado ipo?
 
Hivi ile tabia ya kupaka rangi mpya majengo ya serikali wakati wa ziara ya Prez bado ipo?

Kichwa cha habari kinazungumzia "kutembelea" wizara lakini kwenye details wanazungumzia "kukutana" na viongozi.

Natumaini viongozi wanaotakiwa wataitwa Ikulu wazungumze na Rais, na Rais hatakwenda sehemu mbali mbali wizarani.

Rais akitembelea Wizara, barabara zinafungwa na Wizara haifanyi kazi yoyote siku hiyo. Nilijionea mwenyewe wakati alipotembelea Wizara ya Mambo ya Ndani mara ya kwanza.

Ni murua kabisa Rais kukutana na watendaji wake, ofisini kwake. Iwapo atakosea aende yeye maofisini kwao, basi ataharibu usafiri na utendaji kazi Dar es Salaam kwa siku zote hizo za ziara.
 
...........swine...,anapenda sifa kuliko kazi na kampeni ndani yake....kuna haja gani ya kutembelea wizara wakati angeweza kukalisha ****** ofisini na kuagiza kila taarifa anayotaka na kumuita kila anayetaka na akafanya kazi kimya kimya.....unajuwa kuna madhara makubwa sana kufanya kazi kwa kupiga filimbi..filimbi...unawapa watu matumaini ambayo hayapo....
 
Kama nawanona watu wa RAILWAY, ATC wanavyohaha kujipanga. Nadhani hizi ziara zinasadia sana maana huwa wakifuka ofisini huwa chai nusu saa, maongezi ya mpira lisaa limoja, sms za bure nusu saa, lunch masaa mawili then wanatoka mikutano hewa ya nje siku imeisha.

HONGERA JK
 
- Hivi kazi ya Pinda ni nini hasa? Muungwana punguza safari mkuu I mean hata hizi nazo ni safari ati! mwe!
sio safari yuko ndani ya nchi ni eneo lake la kazi, kama vile wee unavyotoka hapo chumbani kwako, unaingia bafuni, sebeleni nakadhalika
 
wandungu,

..huu ni usanii mtupu.

..ujue hapo he is laying the ground kwa safari ya muda mrefu nje nchi.

..anakutana na TRA,BOT,CAG, hawajatajwa watu wa CMSA lakini na wenyewe wanahusika, etc etc. kesho yake anadamkia wizara nyingine yenye taasisi lukuki chini yake. muda wa kutafakari na kufanyia kazi issues zitakazojitokeza uko wapi?

..nasema Raisi Kikwete hana tofauti na Richmond. yeye pia alidanganya[kwa kununua magazeti,rushwa,..] kwamba anaiweza kazi ya Uraisi. ukweli unadhihirika sasa hivi kwamba hana uwezo wa kuongoza.

NB:

..are going to have Ngurdoto II ???[/QUOTE

Kazi kweli kweli
 
- Hivi kazi ya Pinda ni nini hasa? Muungwana punguza safari mkuu I mean hata hizi nazo ni safari ati! mwe!

Wandugu,

Mchango wangu!!! mimi ninavyoielewa katiba ya Jamhuri

Hiki anachokifanya Rais sasa ni moja ya kazi za Waziri mkuu!!!

Hata hivyo Rais kufanya hivyo mara mbili kwa uongozi wake sio tatizo.... Sio tatizo Rais kwenda kwenye maofisi moja kwa moja;

Kwa taarifa yenu... anaona mengi anapoenda huko moja kwa moja... viongozi wetu watendaji wana uwezo mkubwa wa kuandaa taarifa kiasi kwamba utaona kila kitu kinaenda vizuri na hakuna issue yoyote.

Mfano mmoja wa mafanikio ya kutembelea kwake sehemu mbalimbali mfano mzuri kwangu ... maboresho ya magereza na usafiri wa wafungwa na mahabusu.

Lakini tukumbuke jambo kwamba Waziri mkuu ana mamlaka makubwa kwenye usimamizi wa TAMISEMI zaidi na wizara chache, kama kilimo etc... lakini usimamizi wa Vizara kama za Fedha na Uchumi, MiondoMbinu... Katiba na Sheria, etc na nyingine muhimu bado ziko chini ya Rais zaidi kuliko kwa Waziri Mkuu...

Kwa ujumla sina tatizo na ziara zake... kama atatumia vizuri... kuliko kutumia muda mwingi kuelezea jambo moja... it is an opportunity... awe msikilizaji zaidi... na awajibu akirudi ofisini... asije kuwa mwongeaji zaidi.
 
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Januari 15, 2009 ameanza mikutano yake ya kufuatilia utendaji wa Serikali yake kwa kufanya mkutano wa kwanza na uongozi wa Wizara ya Miundombinu na mashirika yake muhimu.

Mkutano huo wa kwanza uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam, umezungumzia utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam na umehudhuriwa na viongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), wale wa Bandari yenyewe ya Dar es Salaam pamoja na maofisa waandamizi wa Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA).

Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ni Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein; Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo na Waziri mwenyewe wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa.

Katika mkutano wake wa pili, Rais Kikwete anatarajiwa kukutana baadaye leo jioni na uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), na ule wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).

Mikutano hiyo ya kwanza ni mwanzo wa mfululizo wa mikutano ambayo Rais Kikwete atafanya na viongozi wa wizara mbali mbali za Serikali yake kutaka kujua utendaji wa wizara hizo, kutathmini utelekezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2005 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa wakati alipotembelea wizara zake mwanzoni mwa uongozi wake mwaka 2006.

Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa na kukubaliwa katika mkutano wa kwanza ni kama ifuatavyo:

(a) Kuitaka Kampuni ya Kupakia na Kupakua Makontena (TICTS) katika Bandari ya Dar es Salaam kutekeleza wajibu wake ipasavyo kwa mujibu wa mkataba wake kwa kuongeza ufanisi na kuboresha kiwango chake cha utendaji kwa lengo la kupunguza mlundikano wa meli katika Bandari ya Dar es Salaam.

(b) Kuchukua hatua nyingine za kupunguza mlundikano wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam kwa kuchukua mfululizo wa hatua ikiwa ni pamoja na:

(i) Kuhakikisha kuwa mizigo inaondolewa haraka kwa kadri inavyowezekana katika Bandari, kwa kutumia taratibu muhimu zilizopo, ikiwa ni pamoja na kontena kupigwa mnada baada ya kuwa zimekaa bandarini kwa siku 21 kwa mujibu wa sheria.

(ii) Ili kutekeleza jambo hilo la kuhakikisha kuwa mizigo inaondolewa Bandari haraka, TPA na TRA zimeagizwa kuhakikisha kuwa zinapiga mnada kiasi cha asilimia 30 ya makontena yaliyokaa zaidi ya siku 21 katika bandari hiyo, kama njia ya haraka ya kupunguza mlundikano wa mizigo katika Bandari hiyo.

(iii) Kuhakikisha kuwa kuanzia sasa kontena zote zinazopakuliwa kwenye meli, zinapelekwa moja kwa moja kwenye Vituo vya Kuhifadhi Kontena Nje ya Bandari (ICD’s) na gharama za zoezi hilo zinakuwa sehemu ya kutoa mizigo katika Bandari hiyo.

(iv) Kuchukua hatua za kupunguza muda wa meli kusubiri pwani ya Bandari ya Dar es Salaam kwa kuhakikisha kuwa upakiaji na upakuaji mizigo unaharakishwa kwa TICTS kununua vifaa zaidi na pia kuhakikisha kuwa vifaa vya TPA vinatumika.

(v) Kuhakikisha kuwa maarifa yanatafutwa kuondoa magari yaliyoko Bandarini kwa sasa yakisubiri kuchukuliwa na wenyewe, ili kupatikane nafasi zaidi ndani ya eneo la Bandari hiyo kwa shughuli na mizigo mingine. Hili lifanyike kwa kutafuta eneo jingine nje ya Bandari kuhifadhi magari hayo.

(vi) Kuharakisha zoezi zima la kuondoa mizigo Bandarini kwa nyaraka muhimu za kufanikisha jambo hilo kujazwa na kupitishwa haraka iwezekanavyo na TRA.

(vii) Ili kufanikisha uharaka huo, TRA imeagizwa kuhakikisha kuwa sehemu ya kushughulikia nyaraka ya long-room inafanywa kuwa short-room kwa maofisa wa Mamlaka hayo kufanya kazi kwa saa 24, ikiwa ni pamoja na siku za Jumapili.

(viii) Kuongeza ushirikiano wa utendaji miongoni mwa taasisi mbalimbali zinazohusika na kuondoa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam, ili kuongeza ufanisi wa Bandari hiyo na kuiwezesha kupambana ipasavyo na ushindani kutoka kwa bandari nyingine katika eneo la Mashariki na Kusini mwa Afrika.

(ix) Kuchukua hatua za kuboresha ushindani wa Bandari ya Dar es Salaam kwa miaka ijayo, hasa baada ya ongezeko kubwa la mizigo litakalokuwa linapitia katika bandari hiyo baada ya Reli ya Kati kufanyiwa matengenezo makubwa ya kupanua geji yake.

15 Januari, 2009
 
- Hivi kazi ya Pinda ni nini hasa? Muungwana punguza safari mkuu I mean hata hizi nazo ni safari ati! mwe!
MMhm ......naona kama unamwonea Prez, wacha atembelee hizo wizara kwani kwa namna moja ama nyingine ni sehemu ya kazi yake. Na hasa ofisi za wizara ambazo zipo chini ya ofisi ya rais.
 
Rais JK hapa umeongezea wananchi mzigo mkubwa sana na umewapa ulaji usio wa lazima hao TICTS.

(iii) Kuhakikisha kuwa kuanzia sasa kontena zote zinazopakuliwa kwenye meli, zinapelekwa moja kwa moja kwenye Vituo vya Kuhifadhi Kontena Nje ya Bandari (ICD's) na gharama za zoezi hilo zinakuwa sehemu ya kutoa mizigo katika Bandari hiyo.

Yaani TICTS wakisema hizo gharama za kupeleka macontainer Ubungo ni $200, si wananchi wanazidi kuumizwa?? Je hii itafanya kweli Bandari ya Dar kuwa competitive ukicompare na Mombasa au hata Durban???

Halafu umeweka blanket tu kuwa macontainer yote yapelekwe Inland ports kwa gharama za waagizaji, sasa TICTS si wataacha kabisa kuweka macontainer hapo Bandarini sababu hamna faida kwao???

Mimi hata utaalamu wa haya mambo ya bandari sina lakini Trust me kesho au keshokutwa, utasikia malalamiko ya waagizaji.

Lazima TICTS then wapunguze gharama za awali ambazo walikuwa wanacharge kwenye kutoa mizigo au iwekwe limit ya maybe $10 per container na serikali kupeleka mizigo huko inland otherwise itakuwa wazimu tu.

JK kudos kwa kusema Long Room iwe 24 hrs sababu hiyo ni gharama ya serikali na italeta ufanisi bila kuwapenalize waagizaji wa mizigo
 
Back
Top Bottom