Elections 2010 Kikwete kavutwa naye amevutika

mama yangu weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.maneno haya yametoka mdomoni mwake kweli?Yaani jamani afadhali mungu akunyime utajiri akupe akili...Wapi palipohubiriwa umwagaji wa damu?kweli kikwete umeishiwa ,khaaa this is very low for you...wewe si ndo unatuma majeshi yatishe watu wewe,synovate na REDET na tafiti zao za makengeza..mbona una hofu sana mwanakwetu...kaa utulie kushindwa ni kawaida TZ ya leo sio ya 2005....wewe watu hawakupendi na hawakutaki kwa kuwa serikali yako longolongo au nalo hulielewi
Binafsi nimeshitushwa sana rais kuanza kutaja taja neno DAMU tena mbele ya hadhara asifikiri Somalia na kwingineko wanakouana wanapenda kitu hicho. Nilitegemea atakemea wanaosambaza badala yake anakemea watu wengine wasiohusika. Namtahadharisha kuwa endapo DAMU DAMU DAMU itagika hata kama imeanzishwa na mtu mwingine provided yeye anao uwezo wa kuizuia kama rais itamulilia hadi anakwenda kaburini.
 
Kumbe ndiyo maana yule wa majeshi alikuwa na ubavu wa kusema yale........ulimi huu utatuponza na kwa kweli utatuponza...
 
Kikwete ameanza kuchanganyikiwa chochote atakachokiokota anafikiri kitamsaidia mfa maji hata akiona jani linaelea atafikiri gogo, haya maneno si mazuri kinywani mwa kiongozi kama yeye asifikiri atayakwepa.
 
huyu huwa hawezagi kuchuja mambo..yaani hapa ndo ninapomkumbukaga mkapa mimi
 
huyu huwa hawezagi kuchuja mambo..yaani hapa ndo ninapomkumbukaga mkapa mimi
Kikwete kanasa kwenye uchafu wa damu ambao kujisafisha kwake kunahitaji damu, amuulize Charles Taylor wa Liberia, ukianza kuongelea mambo ya damu lazima unawe damu na ukishanawa damu utaendelea kunuka damu na Tanzania hatuko mbali na huko.
 
nasema hivi huko tunakoelekea tunahitaji kuwapima akili wagombea wetu wanafasi ya juu hizi katika Taifa, maana afya ya akili ya mgombea wa ccm inanitia shaka, sijui kama hii shaka naipata peke yangu, namuona kama anamapungufu fulani.
Bado nawaza sana juu ya afya yake ya akili, simuelewi mgombea Urais wa ccm, maana maneno yake hayawiani na umri na uzoefu wake katika siasa.
 
Kikwete kuanza kuzungumzia maneno ya uchochezi ya kumwaga damu siku moja baada ya kusambazwa inaashiria kitu gani? Lini kafanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa si maneno ya kubuni. Je tukisema anahusika na kuyaandaa ili aje kuyatumia kisiasa tutakuwa tunamwonea?

Inaonyesha amemaliza ahadi zote na kuanza kujiingiza kwenye siasa za maji taka kama katibu wake Mkuu. Ndugu wana jamvi mimi nina wasiwasi na Kikwete kuwa ni mmojawapo wa walioandaa maneno hayo kwa jinsi alivyoyachukulia upesi upesi na kuanza kuyatumia majukwaani.

The problem with political jokes is that they get elected.
 
Kikwete ni kumuonea huruma kwa kweli manake mpaka sasa maji yamemfika shingoni, mwache tu atapetape!
 
Sishangai maneno ya JK. Nimewasikia makada wa CCM wakiongea hayo hayo mara nyingi hasa wakati huu wa kampeni. Siasa za kudanganya, uchonganishi na vitisho ndio msingi wa ushindi wa CCM. JK ni sehemu yao anaongoza genge hilo na kamwe hawezi kukemea chochote.
At last kati ya wale vijana 630 waliofunzwa kusigina demokrasia ya Tanzania nimekutana na wawili. Hakuna ubishi wamepanga kunyonga demokrasia
 
Hata mimi nimesikia amezungumzia hilo kwenye kampeni zake huko Songea.

Jamaa ana matatizo kweli.

Hivi mtu kama huyo utamtofautishaje na watu wa taarabu? Akisikia umbea anaugeuza kuwa kweli na kuuhubiri.

Au anaangalia na hadhira wanaomsikiliza?

Hebu akaseme maneno hayo Mbeya, Moshi au hata Iringa kama hajapigwa mawe.

Hii inaonyesha yeye ndo aliyoianzisha kwahiyo anachofanya ni kuiboost tu basi
 
Kikwete kuanza kuzungumzia maneno ya uchochezi ya kumwaga damu siku moja baada ya kusambazwa inaashiria kitu gani? Lini kafanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa si maneno ya kubuni. Je tukisema anahusika na kuyaandaa ili aje kuyatumia kisiasa tutakuwa tunamwonea?

Inaonyesha amemaliza ahadi zote na kuanza kujiingiza kwenye siasa za maji taka kama katibu wake Mkuu. Ndugu wana jamvi mimi nina wasiwasi na Kikwete kuwa ni mmojawapo wa walioandaa maneno hayo kwa jinsi alivyoyachukulia upesi upesi na kuanza kuyatumia majukwaani.

JAMANI EEEH The purpose of getting power is to be able to give it away.
 
The end is nigh and JK shall indeed go we are going to free at last! The date is October 31, 2010. Now less than twenty days. The end is nigh!

Go Slaa Go. Tuko pamoja Doc, all the way, come what may!
 
akihutubia mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa majimaji mjini songea jana, jumapili, oktoba 10, 2010, rais kikwete amewasuta wanasiasa ambao wamekuwa wanatishia umwagaji wa damu nchi kama hawakufanikiwa kushika nafasi za uongozi wanazozitaka.

“sisi ni ccm. Sisi ni chama kisichohubiri umwagaji damu. Sisi ni chama cha amani. Umwagaji damu hauna maslahi yoyote na wala tija kwa yoyote isipokuwa kwa wanasiasa wanaotaka kutumia maiti za watu kama ngazi ya kuingilia ikulu,” amesema rais kikwete na kuongeza:

“hawa siyo watu. Hawana maana yoyote. Achaneni nao watu wa namna hii wanaotaka kupata madaraka kwa ngazi ya maiti za wananchi wasiokuwa na hatia

amesisitiza rais kikwete: “wanachochea watu wamwage damu na wao wapande ndege kwenda zao ulaya na kuwaachia nyie mkitoana damu

my take: Haya ni maneno mazito kutamkwa na kiongozi hasa rais wa nchi. Kikwete kama rais alitakiwa akemee message hizo na wanaozisambaza kwa kuwa zinachonganisha watu badala yake yeye bila kufanya utafiti kama yaliyotamkwa ni ya kweli au la anaanza kuzitumia kama mtaji wa kisiasa. inawezekana anajua zinakotoka.

kwani kikwete huwa anfanya utafiti wa mambo anayoongea huyu jamaa raisi wetu ni incompetent jamani mwacheni hajui hata kwa nini anaongea hivyo na sijui kwa nini watanzania walimpa 80% huyu mwaka 2005, shame upon him.
 
quote_icon.png
Originally Posted by Zed
Nani anasema CCM Mgombea Urasi wa CCM hana mkono katika hizi meseji.... Ushahidi wa kimazingira huu hapa: Uki-fatilia domain 6telecoms.co.tz, iliyotumika utaona wazi share the name IP ya Kikwete2010co.tz na JK web site yake na nyingine za mafisadi wa papa ziko hosted nao.
Angalia maandishi mekundu!
"
Kikwete2010.co.tz is a domain controlled by two name servers at co.tz. Both are on different IP networks. The name server kikwete2010.co.tz stated in SOA record is not in the list of name servers. Incoming mail for kikwete2010.co.tz is handled by two mail servers also at co.tz. Both are on different IP networks. kikwete2010.co.tz has one IP number (41.77.226.253).
212.233.84.in-addr.arpa, 229.77.41.in-addr.arpa, 228.77.41.in-addr.arpa and 227.77.41.in-addr.arpa share name servers with this domain. 6telecoms.co.tz share mail servers with this domain.

Thanks Zed

Toka mwanzo mimi nilikuwa na wasiwasi na Kikwete kwamba was behind or aware of what was happening, maana haiingii akilini kiongozi mkuu tena rais kuanza kutumia ujumbe hatari wa email kwenye kampeni zake siku moja tu baada ya kusambazwa bila hata kujiridhisha kama ni wa kweli ama la.

Nafikiri JK anaelewa fika mbinu chafu kama hizi ndizo zilizotumiwa na viongozi wa Rwanda kuwachonganisha wahutu na watusi wamalizane ili wao waendelee kutawala, shame on him.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom