Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)

natamani niipate ile part one niiunganishe aliyenayo msaada please

Hutaki Unaacha said..

JK, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)
Mr President,

Ningekuwa na muda ningekueleza mengi sana. Muda wangu ni kidogo sana ndiyo maana nashindwa hata kupost mambo mengi kuhusu taifa hili hapa JF. Ninatuma post hii si kwa lengo la kukutisha. Lengo ni kukukumbusha uwe makini ili usijefanya uamuzi wa hovyo na kuliingiza taifa katika machafuko na kuharibu timetable za watanzania. Machafuko ndiyo tunayoyakwepa lakini si wewe (I have to tell you the truth because you are not my breadwinner at all).

Mtandao

Ninachozungumzia hapa ni kundi kubwa na hatari linaloaminika kuongozwa na Edward, Rostam, Othman, Apson, Karume na Shein na Mkapa. Ninakufahamu vizuri sana na ungekuwa uwezo wako, hawa wote ungeweza kufanya uwezalo ili kumweka madarakani mtu unayemtaka kwa maana ya Asha au Nahodha. Huu ni mtandao unaofanya kazi kwa umakini wa hali ya juu sana. Ukitaka kuamini, jiulize swali la kipuuzi sana kuwa kwanini kila plans unazofanya (zisizo na faida) kwa kundi hili zote zimefail?

1. Shein ni nani?

Nataka nikukumbushe ''issue'' ya Omar Juma. Huyu alikuwa threat kubwa kwa kundi lenu kwa ajili ya 2005. Mtandao wake ukibebwa na Mkapa ulikuwa ni hatari sana. The only way ilikuwa ni ''kumwondoa'' na hilo liliwezekana. Siku nikiwa na muda nitaeleza mchezo wote ulivyofanyika. Wakati jina limeletwa tukiwa hotel moja maarufu hapa Dar, nakumbuka hukuweza kumfahamu Shein wala kulitamka jina lake vizuri. Ulikosea mara tatu kulitamka. Tukacheka wote. Hatimaye Shein akawa makamu wa rais.

Baada ya wenzako kukuweka madarakani (mgombea ndani ya CCM), kosa ambalo Shein hataweza kukusamehe katika maisha yake (Mimi sio Mungu, kwani anaweza kukusamehe vilevile) ni pale ulipo-attempt kumfanya Zakhia kuwa makamu wa rais. Asingekuwa Edward, Rostam, Mkapa na Karume, leo hii Shein angekuwa mwenyekiti wa TPDC au TANAPA!. Kitendo cha Shein kuletwa na kundi hili, kutetewa na kundi hili achilia mbali kushawishiwa na kundi hili agombee urais wa Zanzibar ili kummaliza nguvu Nahodha chaguo lako kinamfanya awe mtiifu kwao kuliko hata kwa Mwanamwema!. Unafahamu vizuri Shein alivyoshinda urais Zanzibar, rafiki zako walikuchezea akili wakikuambia kuwa wamemleta Shein ili kupunguza kura za Bilal na ulipomkubali Shein wao wakaenda kumpigia Bilal kampeni wakijua kazi ya kumweka Shein imekamilika. Baada ya hapo uliendelea kumng'ang'ania Zakhia kuwa makamu. Mkapa akishirikiana na Rostam (ambaye alikuwa akim-install Bilal kuwa makamu huku yeye akiwa South Africa kuangalia World Cup) walimweka Bilal hapo alipo.

Shein hakushinda uchaguzi Zanzibar. Kilichofanyika ni Mkapa, Rostam, Karume kumhonga pesa za kutosha sana Maalim kupitia kwa kijana wao hatari sana Jussa (kumbuka huyu aliletwa na Rosatm ili umteue awe mbunge). Today, umeshindwa kumweka mtu wako Zanzibar na makamu wa rais Muungano. Walichoweza kufanikisha ni kuiteka Zanzibar yote (Bilal na Shein). Nakukumbusha ya kwamba, ili uwe mgombea kupitia CCM, unahitaji Zanzibar na 'Lake Zone'. Kule 'Lake Zone' wamekushinda. Hilo unalifahamu vizuri. Hii ndiyo maana Wanzanzibar wamekutesa sana ndani ya CC iliyopita. Ili kukuonyesha kwamba hufai, Shein kampa udaktari wa heshima ''Baba yake'' mdogo Karume. Ninafahamu jinsi unavyojikosha kwa Anne kwa kumpa nishani ili kusiwe na vote of no confidence mwakani hasa kwa sakata la Richmond na Twiga. Napenda kumhakikishia Anne ya kwamba that's a strategy anayoitumia Mugabe ya kuwamaliza watu. JK ameiiga huko. Naomba Anne uwe makini sana. Waweza kufa kwa ''presha'' usipoangalia.

2. Karume ni nani?

Huyu alipigiwa kampeni kubwa sana na Edward na Rostam mwaka 2000 licha ya CCM Zanzibar kumkata jina lake. Kwa hili Karume hawezi kuwasahau hawa jamaa mpaka anakufa. Karume alikupinga Butiama. Yeye, Edward na Rostam wakaenda ku-design ''mwafaka'' wao wanaoujua ambao leo hii unafanya kazi Zanzibar. Nataka nikukumbushe mara ya pili kuwa Jussa aliletwa kwako na Rostam ili umpe ubunge. Think twice! Karume ndiye rais aliyeleta maendeleo makubwa Zanzibar. Shein will do more than what Karume did. Usishangae ukisikia Karume kuwa makamu wa Lowassa 2015!. Karume ana msimamo. Hayumbi na bahati mbaya sana hakuogopi.


NITAENDELA SIKU NYINGINE WAPENDWA WANA JF
 
mmm h Rostam akasomeshwa na CIA mmmmmh hii imekaaje? Mbona Rostam ni maarufu sana Iran kwa sababu kwa muda mrefu amekuwa kiungo kati ya Iran yenyewe, Wairain waliopo nchini na ubarozi wake uliopo nchini sasa unaposema anaunganishwa na Iran haitoi taswira ya kweli.
 
Si kwamba CIA wanakumbatia mafisadi au nini. Kuna wakati CIA wanatumia watu fulani ambao either watakua wamewaandaa wao au ni wafanyabiashara wakubwa kuwa "Contractor" wao kwenye various operations. Hawa watu wanakuwa si waajiliwa wa moja kwa moja wa CIA, ila wanakuwa for special au specific tasks. Ukipata muda, soma confession of an economic hitman utaelewa, au soma historia ya vita ya Balkan. Mimi sishangai kwa RA kuwa agent.

Pia, kwa nchi kama Tz ambayo ina various invaluable resources, lazima CIA watakuwa macho na nchi yetu na ndio maana wakawa wanataka mfumo wa ulinzi ubadilike.
Ni kweli,kuna operation nyingi tu wamefanikiwa,walishamtumia Osama Bin Laden itakuwa Rostam

Watu wanataka kutukoroga tu!
 
@ Hutaki Unaacha and other JF members
  • Kuanza ningependa tu kuhoji credibility ya wewe Hutaki Unaacha kuhusu hizi habari unazotuletea.....je umeamua kuwa whistle blower?we uko TISS au unapataje hizi habari...please ningependa tu kujua ukweli wa habari hizi maana zitabadili mindset ya wale wenye kupigia watu compaign za urais wa 2015 humu jf.
  • Kwa wale true patriots wa tz habari kama hizi(kama ni za kweli) zinazidi kuwaweka kwenye nafasi nzuri ya kuipigania nchi kwani habari inazidi kutufichulia ni nani mmbaya wetu wa tz.Hii habari inatakiwa isijenge hofu kwa watu(kama ambavyo nimekwisha soma humu) bali inatakiwa iwajaze watu ujasiri na kuwabadilisha wale wenye mitazamo ya kuwafagilia mafisadi humu jf....pasipo kujua kuwa hawa mafisadi mnaowataka wawe viongozi wetu wa kesho ni mawakala wa networks mbaya zaidi ambazo zinavuka mipaka ya tz......kwa maana nyingine...kwa mtu anayeipenda tz huwezi kukifagilia chama(ccm) kumtoa kiongozi atakayeleta mabadiliko ya kweli tz...kwanii wengi tunaowapigia debe humu jf ni mawakala wa mitandao ya kibapari na kinyonyaji ya magharibi ambayo siku zote wangependa nchi zenye raslimali kama tz zizidi kuwa ombaomba.
  • Tukumbuke uwakala wa viongozi wetu kwa nchi za magharibi kamwe hautatuletea mabadiliko kimaendeleo tz zaidi ya kuzidisha umaskini na hata kujenga vurugu na hata vita ili tu kujustify wao(magharibi) kuhodhi raslimali zetu...mifano tumeiona kongo na kwingineko.....
  • Habari kama hizi zinazidi kutuonyesha kuwa kuwa suluhisho pekee la kumpata kiongozi wa kweli kwa umma wa tz ...ni kwa njia ya nguvu ya umma peke yake....ndipo atapatikana kiongozi atakayaweza hata kusimamia kuwahukumu hawa mafisadi na wasaliti wa nchi. Kiongozi atakayekuwa radhi kupinga mashinikizo toka kwa hizi nchi za magharibi zenye interest na utajiri wetu wa tz.Habari hizi zinathibitisha kuwa tz kura hazitaweza kutupatia rais wa wote bali kura zitazidi kutupatia mawakala wa mitandao ya kimagharibi daima....
  • Napata shida sana kuamini kuwa kweli hivi tz hawa TISS kazi yao ni kuwatumikia wa tz au hawa mafisadi???kwanini wanaingia kwenye usaliti huu??,iko siku.........they will pay for this.......tz bado tuna uwezo wa kuwana viongozi wazalendo watakaojali raslimali na utajiri wa nchi.........tunahitaji kiongozi mifano ya kina Hugo Morales na Chaves ambao wamesimama kidete kutetea utajiri wa nchi zao pamoja na mashinikizo toka nchii za magharibi........
  • Ni wakati sasa kwa baadhi ya hawa TISS kusimama na kuhesabiwa kwani inatia simanzi kuona kuwa inafika mahali tunapata habari za utendaji wao mbovu kwa kupitia mitandao!!!!!this is unbelievable yaani.........only in tz .........
 
je lowassa ni nani.............. nadhani hiyo ndio itakuwa part three, kwanini nyerere alishtuka baada ya kupata undani juu ya lowassa na Kikwete kuwa ni mapandikizi ya ...................... . Usiogope JK yuko makini kuliko mnavyo fikiria.
 
Umeandika kama mhandisi anayesimamia matengenezo ya barabara yenye kona nyingi ambayo inamsumbua kurekebisha kwa sababu ya ukosefu wa vifaa. katafute vifaa ndio urejee tena na habari ya kweli.

Hutaki unaacha! We do not want to listen to your handbag tantrums here, please madam!
 
Mmetumwa nyie! Hamuwezi kushusha credibility ya mada!! Hutaki unaacha ala!
 
Mmetumwa nyie! Hamuwezi kushusha credibility ya mada!! Hutaki unaacha ala!



  • Changanya kidogo na akili yako...sio kuingiza kichwani kila kitu,2015 toka sasa ni mbali sana,utakiover work kichwa chako kakaangu maana yataletwa mengi humu
 
Hakika Hutaki Unaacha [HU] sasa umeunganisha dots zangu nimepata picha kamili kuwa RA ni Agent wa kanda ya East Africa,kama ndio hivyo basi ndie msimamizi wa maslahi yao kanda hii yote,ndio maana akapata Contarct kwenye Migodi yetu ya Madini. ambazo kampuni nyingine yoyote ahijapata kupata Tanzania katika migodi ya Bulyangulu na Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamonds mwanzoni mwa miaka ya 1996. Kwa wakati huo anapata tenda ya Mgodi wa Bulyangulu kwenye miaka ya 2000s kama sikosei jamaa ile deal ilikuwa na thamani ya Billioni 45.Na hiyo ni mgodi mmoja pata picha migodi kama Mitatu yote huko una tenda ya kila Mwaka na ni mpaka sasa.

Natumaini kama alikuwa recruited na CIA ni kuanzia miaka ya mwishoni ya utawala wa Mzee Mwinyi,na ndio maana HU alisema Mzee Mwinyi alitoa agizo Wanasiasa kumshika mkono Mhindi au Mwalabu mfanyabiashara.Na aikuwa ajabu kwa kuwa yuko kazini aliweza kucheza na makundi yote mawili la Mkapa na Kikwete mwaka 1995.

RA kama agent wa CIA,alijiimalisha sana wakati wa kipindi cha Mkapa,na ni katika kipindi hicho hakuna Mtanzania aliyekuwa na shaka na Jamaa huyu, ukizingatia alikuwa anasifiwa na watawala kwamba ndiye Mtanzania wa kwanza kwa kampuni yake kushinda tenda ya za kimataifa kwenye visima vya mafuta vya CASPIAN SEA uko umangani.Na kwa kuwa CIA wao kwao ni mianya ya biashara na maslahi yao, hivyo si ajabu wanahusika na kumpa support na access zote muhimu kama vile kupropose kwa Marais na viongozi wakuu kusikiliza ushauri wa wake kwenye nyanja ya Biashara na siasa kwa kumuona kama part ya Mwananchi kumbe wanafeed nini cha kuwaambia na kufanya dhidi ya marais wetu.

Nakumbuka wakati fulani Rais Kikwete alipata kulopoka nafikili alishindwa kujizuia kwa uchungu kuhusu Richmond aliona kama kawapiga bao na ndio maana akasemwa HAWALIPWI, lakini yaliyosikika akisema "SIJUI WATAKUJA KWA MBINU GANI".Hakika sasa nimeelewa kuwa alimaanisha hao waajili wa RA ambayo RA ndio Agent wao.Na kweli wakaa chini wakaona migodi yao bado inaitaji umeme hivyo wakaja na simbion Pole sana Kikwete hakika unastahiki pongezi kwa kuwa umekuwa na kigugumizi kwa mengi,kumbe nyuma yake wapo wazee wakazi wanaoitetemesha dunia.Umejitahidi sana kucheza nao.Manake kazi yao kwa sasa umangani imefanikiwa sana.

Hila huyu agent wao na hakika mambo yao na wao watamalizana nao kwa kuwa wanakanuni zao za USE AND ABUSES.Wakiona mambo kama haya mission inakuwa terminated. Ni vyema haki sytle ya usalama ilokuwa inatumiwa na Mwalimu haina budi kuludishwa yani safari hii Jamaa wameingia mpaka kwenye TISS yetu jamani Watanzania mliosomeshwa Cuba, Russia, China, Israel mlikuwa wapi mnawaacha watu aina ya RA na JM wanasogelea TISS na viongozi, wake nanyi mnakaa kimya matokeo yake mmeshikwa na woga na stahili yao ya vitisho.

Kosa kubwa sana na lawama kwa haya yote kutokea ziende kwa utawala wa awamu ya tatu.Na hakika safu za Watanzania waliosomea ujasusi Tanzania, China, Cuba, Russia , Misri na kwingineko kujiunga na kuondoa uchafu huu kwa kuwa tunajulikana hatufungamani na mtu yoyote.Tanzania ni kwa Watanzania, hakika Mwalimu ilo aliliweza na CIA wanalijua hilo walimuheshimu Mwalimu nae aliwaheshimu Marekani lakini sio hilii la kuja kututawala kisiasa na kiuchumi na soon watatuwala kiutamaduni ndio maana wanatuletea Shogaism. Yani ndio kusema tumebuluzwa na Marekani yapata miaka ishirini sasa.Ndio maana hata Mwananchi wa kawaida kesha stuka kuwa Nchi ilishauzwa

Ila hakuna Nyoka mbaya Tanzania na kwa Iran na Mataifa yote ya EA kama RA.Hivi jamani unawezaje kuwa msaliti kwa watu ambao umekuwa nao maisha yako yote hata kama si ndugu zako.Mimi mwenyewe kumsaliti classmate wangu siwezi sembuse jamaa wa karibu. Ila dawa yake wanao hao hao waliomuhajili uzuri Rais ujumbe kapata.Ndio maana nikasema wenye akili zao wanamchezesha hakuna cha King maker hapo kuna Tarishi kw kuwa agent kazi yake ni kutekeleza maigizo ya principal.Hivyo vindumbwe ndubwe vyote nchini vya Migodi,EPA, Richomond na Dowans nyuma yake kuna vigogo wa dunia aka viongozi wetu toka enzi ya Mwalimu wamezoe kuwaita "Wakubwa hawa"
 
Ndugu yetu Hutaki Unaacha, kwanza asante kwa muendelezo huu, pili naweza kukubalia yote uliyoyasema kwa sababu mengi siyajui japo baadhi niliwahi kuyasoma katika zile dossier za Mzee Mwanakijiji ambazo alizitoa kwa subscription.

.................................
Wanasema ukishikwa, shikamana na ukibebwa, bebeka!. Kijana mpaka kabebwa habebeki aingekuwa ni shukranisi angeendelea kuning'inizwa huko huko juu alikopandishwa?. Mbona sasa ameachwa akaporomoka?!. Sio shukrani ni hisani tuu!.
mkuu nimeshindwa kutofautisha shukrani na hisani kwenye medali za kisiasa
 
Hujatuambia Rostam alisoma muda gani kutoka tarehe ngapi au mwaka gani. masomo yalichukua muda gani na alikuwa anasomea nini maalum kwa umri wake?
 
Angali hitimisho la mwandishi.....Hii thread imeanza kwa ujanja sana kama vile inatuambia habari za mtandao lakini kikubwa mwandishi alikuwa anataka kutueleza nguvu ya Rostam Aziz ili tutisheke na kuogopa kumshughulikia na kashfa zake. ndio maana kamuelezea kwa kirefu sana habari zake na huyu anaweza kuwa kwenye kambi ya Hussin Bashe
 
Cha kufahamu nikwamba hawa jamaa CIA wako another level za intelijensia compared to TISS.Alafu, mipango ya CIA ni ya long run (e.g. 20 and above). Afu tukumbuke TISS, kimfumo wamechelewa kubadilika sana. Nchi yetu ilipoanza kuingia kwenye ubepari (kipindi cha mwinyi), TISS walikua wanashangaa shangaa tu. Hivi inawezekana vipi nchi inaingia kwenye mfumo wa soko huria afu mali zote zinakwapuliwa na wageni afu TISS wapo tu wanatoa macho?

Pia, mfumo wan chi unapokosewa (unapokua wrong), inachukua muda mrefu kuurekebisha, and it needs real expertsto do it with perfection, sio hawa watoto wa mafisadi waliojaa pale oyesterbayna dodoma. Afu tufahamu kuwa tupo kwenye imperialist world, kwa hiyo instrumentkama CIA ipo everywhere penye interest ya US.

Kimuundo hawa TISS bado wako nyuma. Afu usikute hata hizo computer zao plus servers walizopewa msaada kutoka kwa watu wa Marekani ziko monitored na hao CIA.
 
Mkuu kama RA ni real agent or CIA contractor, ni ngumu sana kujua previous trend ya maisha yake, kuna sehemu utaona kuna vitu vina miss. Hata Osama ilikua ni hivyo hivyo.
 
Hussein Bashe katika style nyingine ya kumsafisha Rostam na kundi lake. TISS na serikali kamateni huyu achana na maneno haya ya mtaani CIA watamkuta gerezani. haingii akilini ni mpango wa vitisho vilivyotengenezwa kwa akili ya hali ya juu ili kumpa kinga RA.
 
Back
Top Bottom