Kikwete hana mkono kashfa ya Richmond - Ikulu

Lengeri

Senior Member
Jul 3, 2009
180
15
Kizitto Noya, Dodoma

SASA ni wazi kwamba sakata la Richmond limeingia katika hatua nyingine baada ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ofisi Rais kutangaza kwamba, Rais Jakaya Kikwete hahusiki kwa namna yoyote na kashfa hiyo ambayo inaendelea kulitikisa taifa kwa muda sasa.

Hatua ya Rais Kikwete kutotaka kuhusishwa na kashfa hiyo ya Richmond kunazidi kuibua maswali mengi kutoka kwa wananchi kwamba, ni nini hatima ya mjadala huo ambao unazidi kupamba moto kila kukicha nje na ndani ya Bunge.

Wakati Rais Kikwete akijivua kutoka katika sakata hilo, Kamati ya Nishati na Madini imetoa maazimio ya kupinga jinsi serikali inavyotekeleza maazimio ya Bunge kuhusu ripoti ya Richmond. Jana jioni Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ilitoa taarifa ikimuepusha rais na kashfa hiyo.

"Tumepata kusema huko nyuma, na tunapenda kusisitiza kwa mara nyingine kuwa, Rais hana mkono katika Richmond na hata Ripoti ya Bunge iliyotolewa kufuatia uchunguzi katika suala hilo la Richmond, haikumhusisha Rais Kikwete," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa ya Ikulu, imetolewa huku Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba akidai kwamba, Rais Kikwete anahusika na Richmond kwa kuwa maamuzi yalifanyika chini ya serikali anayoiongoza.

Habari kutoka Dodoma zinadai kuwa kutokana na kusuasua kwa utekelezaji wa maazimio ya Bunge kutaka maafisa wa serikali waliohusika kwa njia moja au nyingine na mchakato wa kampuni hiyo kupewa zabuni Tanesco, wachukuliwe hatua.

Kundi mojawapo la wabunge limeeleza kutoridhishwa na ripoti ya serikali iliyotolewa bungeni hivi karibuni kuwasafisha. Kundi hilo limepanga kumchukulia hatua kubwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye ndiye kiongozi mkuu wa serikali bungeni, kutokana na kuwanusuru maafisa waliotuhumiwa kuhusika na kashfa hiyo.

Wakati kamati hiyo ikitoa msimamo huo, wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikutana jana usiku katika Ukumbi wa Pius Msekwa kutafakari sakata hilo.

Ingawa tangazo la Mwenyekiti wa Bunge, Job Ndugai jana mchana halikueleza agenda za kikao hicho, vyanzo huru vya habari vililidokeza gazeti hili kuwa wabunge hao wangejadili ripoti ya Richmond na kuweka mkakati wa kuinusuru serikali.

Mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini ambaye hakutaka kutajwa gazetini akihofia kuvunja Kanuni za Bunge kwa kutoa siri za vikao, alisema kamati haikuridhishwa na ripoti ya serikali hasa katika suala la kuwasafisha Mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward Hoseah na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika.

"Kamati haikubaliani na ripoti hiyo hasa pale iliposema Dk Hoseah na Mwanyika hawana hatia. Tumekuwa na vikao kwa siku mbili jana (juzi), leo (jana) na bado tunaendelea kesho (leo),”alisema.

Alisema mapendekezo ya kamati ya Bunge kuhusu Richmond yalijitosheleza kimaamuzi na serikali ilitakiwa kuyatekeleza tu na sio kuendesha uchunguzi mwingine.

"Uchunguzi ulishafanywa na Bunge, serikali ilitakiwa kutekeleza tu. Ilikuaje ifanye tena uchunguzi kwa muda zaidi ya ule uliopangwa na Bunge badala ya kufanya utekelezaji?" alihoji.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, William Shelukindo na Makamu wake, Dk Harrison Mwakyembe hawakupatikana jana kuzungumzia suala hilo na simu zao za mikononi kutopatikana kabisa.

Mjumbe wa kamati iliyoundwa na Bunge kuchunguza suala la Richmond, Habib Mnyaa alikiri kuwa na taarifa ya kamati ya kisekta kukutana na kujadili ripoti hiyo, lakini akaeleza kuwa kikao hicho kilichokaa juzi na jana, kinamalizika leo.

"Kikao kimekuwapo, lakini hakijafikia maamuzi hayo unayosema," alisema Mnyaa akirejea hoja ya mwandishi wa habari aliyetaka kuthibitisha taarifa kwamba, kikao hicho kimejenga hoja ya kutokuwa na imani na serikali katika suala la Richmond.

Hata hivyo, habari nyingine zinadai kuwa kamati hiyo leo inatarajia kumweka kiti moto Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja ili awaeleze ni kwanini serikali imeshindwa kutekeleza mapendekezo ya Bunge.

Hata hivyo, mjumbe mwingine, Lucas Selelii alilieleza gazeti hili kuwa vikao vyote vilivyojadili Richmond, vimemaliza kazi na kuwasilisha hoja zake kwa spika wa Bunge Samuel Sitta ambaye leo atatoa mwongozo bungeni.

"Mjadala wa Richmond umemalizika na mambo yote kesho (leo) yako hadharani. Kamati ya kisekta imekaa na kuandaa taarifa ambayo amekabidhiwa spika wa Bunge leo (jana). Kikubwa jamii ijue kwamba, kamati iko makini, haimwonei wala kumpendelea mtu," alisema Selelii.

Alipotakiwa kuthibitisha kama amepokea hoja za kamati hiyo kuhusu Richmond na kwamba ataruhusu mjadala wake bungeni leo, Spika Sita alisema: "Haijanifikia bado".

Alifafanua kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini anatarajia kuwasilisha hoja za Kiwira na Richmond kesho, siku ambayo pia wenyeviti wa kamati za Miundombinu, Ardhi, Maliasili na Mazingira watawasilisha hoja zao.

Alibanwa zaidi aeleze kama endapo angeipata jana jioni angekuwa tayari kuiwasilisha leo kama ilivyoelezwa, alijibu:

"Hata kama nitaipata sasa, siwezi kuitable kesho (leo) kwani nahitaji muda kuisoma na kuielewa".

Awali mbung wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alisema suala la Richmond limeanza kuligawa taifa na njia pekee ya kuirudishia jamii imani na serikali, ni Rais kwa mamlaka ya kuwa mkuu wa nchi kuunda jopo la majaji kupitia upya hoja zote na kutoa maamuzi.

"Suala hili limeonekana kuigonganisha mihimili mikuu miwili ya dola, Bunge na Serikali, dawa yake sasa ili liishe, ni Rais kama mkuu wa nchi nasisitiza, mkuu wa nchi sio serikali kuunda tume ya majaji wapitie Maazimio ya Bunge, utekelezaji wa serikali na watoe maamuzi," alisema.
Alisema: "Inavyoonekana kila upande unavutia kwake, wakati Bunge likitaka serikali itekeleze mapendekezo yake ndani ya miezi mitatu, serikali imetumia karibu mwaka na nusu na bado inakuja na majibu ya kubabaisha.

source Mwananchi
 
Last edited by a moderator:
....mara baada ya jogoo kuwika, utanikana mara 3!

Lakini Petro huyohuyo alipoona mambo yamekuwa moto akasema "SIMJUI MTU HUYU"!

Asomaye na Afahamu...!

Nawasilisha!
 
ameshindwa kuwachukulia hatua AG na Hosea....ndo hapo ikatae Richmond hahusiki?
 
Kikwete anahusika moja kwa moja kwa kupitia former ambassador (Mr Daraja) ndo alimuunganishia hili dili, maana Daraja alikuwa kila week yuko Houston na hawa jamaa wa Richmond. Hila Kikwete alifikiri hawa Jamaa ni mahili kwa hii mitambo baada ya kuangalia website zao za kufoji, kumbe ni bure.

Richmond----Daraja (Barozi)-------Kikwete---------Lowasa (Msimamizi wa hiyo tender).

Hivyo Kikwete anahusika moja kwa moja, asikwepe.
 
Kikwete anahusika moja kwa moja kwa kupitia former ambassador (Mr Daraja) ndo alimuunganishia hili dili, maana Daraja alikuwa kila week yuko Houstonna hawa jamaa wa Richmond.

Richmond----Daraja (Barozi)-------Kikwete---------Lowasa (Msimamizi wa hiyo tender).

Ndio maana Daraja alipotakiwa kustaafu akatengenezewa cheo cha ajabu ajabu Ikulu? Eti kapewa mkataba.
 
Kikwete anahusika moja kwa moja kwa kupitia former ambassador (Mr Daraja) ndo alimuunganishia hili dili, maana Daraja alikuwa kila week yuko Houston na hawa jamaa wa Richmond. Hila Kikwete alifikiri hawa Jamaa ni mahili kwa hii mitambo baada ya kuangalia website zao za kufoji, kumbe ni bure.

Richmond----Daraja (Barozi)-------Kikwete---------Lowasa (Msimamizi wa hiyo tender).

Hivyo Kikwete anahusika moja kwa moja, asikwepe.

Embu jenga zaidi hii habari, ili nafasi ya Daraja, JK, RA na EL ziweze kueleweka vyema. Hapa sasa panaonekana Unne badala ya Utatu!
 
Kwa kweli hii inatia aibu ni lini viongozi wetu watakuwa waadilifu,hakika nafikiri wabunge wanakina sababu ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Serikali kwenye hili.Na endapo wabunge watapika kura hiyo nini itakuwa matokeo ya Serikali ya JK?Ntamani kuona hilo likitokea tumechoshwa na usanii serikanlini.
 
Kizitto Noya, Dodoma

SASA ni wazi kwamba sakata la Richmond limeingia katika hatua nyingine baada ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ofisi Rais kutangaza kwamba, Rais Jakaya Kikwete hahusiki kwa namna yoyote na kashfa hiyo ambayo inaendelea kulitikisa taifa kwa muda sasa.

Hatua ya Rais Kikwete kutotaka kuhusishwa na kashfa hiyo ya Richmond kunazidi kuibua maswali mengi kutoka kwa wananchi kwamba, ni nini hatima ya mjadala huo ambao unazidi kupamba moto kila kukicha nje na ndani ya Bunge.

Wakati Rais Kikwete akijivua kutoka katika sakata hilo, Kamati ya Nishati na Madini imetoa maazimio ya kupinga jinsi serikali inavyotekeleza maazimio ya Bunge kuhusu ripoti ya Richmond. Jana jioni Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ilitoa taarifa ikimuepusha rais na kashfa hiyo.

"Tumepata kusema huko nyuma, na tunapenda kusisitiza kwa mara nyingine kuwa, Rais hana mkono katika Richmond na hata Ripoti ya Bunge iliyotolewa kufuatia uchunguzi katika suala hilo la Richmond, haikumhusisha Rais Kikwete," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa ya Ikulu, imetolewa huku Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba akidai kwamba, Rais Kikwete anahusika na Richmond kwa kuwa maamuzi yalifanyika chini ya serikali anayoiongoza.

Habari kutoka Dodoma zinadai kuwa kutokana na kusuasua kwa utekelezaji wa maazimio ya Bunge kutaka maafisa wa serikali waliohusika kwa njia moja au nyingine na mchakato wa kampuni hiyo kupewa zabuni Tanesco, wachukuliwe hatua.

Kundi mojawapo la wabunge limeeleza kutoridhishwa na ripoti ya serikali iliyotolewa bungeni hivi karibuni kuwasafisha. Kundi hilo limepanga kumchukulia hatua kubwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye ndiye kiongozi mkuu wa serikali bungeni, kutokana na kuwanusuru maafisa waliotuhumiwa kuhusika na kashfa hiyo.

Wakati kamati hiyo ikitoa msimamo huo, wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikutana jana usiku katika Ukumbi wa Pius Msekwa kutafakari sakata hilo.

Ingawa tangazo la Mwenyekiti wa Bunge, Job Ndugai jana mchana halikueleza agenda za kikao hicho, vyanzo huru vya habari vililidokeza gazeti hili kuwa wabunge hao wangejadili ripoti ya Richmond na kuweka mkakati wa kuinusuru serikali.

Mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini ambaye hakutaka kutajwa gazetini akihofia kuvunja Kanuni za Bunge kwa kutoa siri za vikao, alisema kamati haikuridhishwa na ripoti ya serikali hasa katika suala la kuwasafisha Mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward Hoseah na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika.

"Kamati haikubaliani na ripoti hiyo hasa pale iliposema Dk Hoseah na Mwanyika hawana hatia. Tumekuwa na vikao kwa siku mbili jana (juzi), leo (jana) na bado tunaendelea kesho (leo),”alisema.

Alisema mapendekezo ya kamati ya Bunge kuhusu Richmond yalijitosheleza kimaamuzi na serikali ilitakiwa kuyatekeleza tu na sio kuendesha uchunguzi mwingine.

"Uchunguzi ulishafanywa na Bunge, serikali ilitakiwa kutekeleza tu. Ilikuaje ifanye tena uchunguzi kwa muda zaidi ya ule uliopangwa na Bunge badala ya kufanya utekelezaji?" alihoji.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, William Shelukindo na Makamu wake, Dk Harrison Mwakyembe hawakupatikana jana kuzungumzia suala hilo na simu zao za mikononi kutopatikana kabisa.

Mjumbe wa kamati iliyoundwa na Bunge kuchunguza suala la Richmond, Habib Mnyaa alikiri kuwa na taarifa ya kamati ya kisekta kukutana na kujadili ripoti hiyo, lakini akaeleza kuwa kikao hicho kilichokaa juzi na jana, kinamalizika leo.

"Kikao kimekuwapo, lakini hakijafikia maamuzi hayo unayosema," alisema Mnyaa akirejea hoja ya mwandishi wa habari aliyetaka kuthibitisha taarifa kwamba, kikao hicho kimejenga hoja ya kutokuwa na imani na serikali katika suala la Richmond.

Hata hivyo, habari nyingine zinadai kuwa kamati hiyo leo inatarajia kumweka kiti moto Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja ili awaeleze ni kwanini serikali imeshindwa kutekeleza mapendekezo ya Bunge.

Hata hivyo, mjumbe mwingine, Lucas Selelii alilieleza gazeti hili kuwa vikao vyote vilivyojadili Richmond, vimemaliza kazi na kuwasilisha hoja zake kwa spika wa Bunge Samuel Sitta ambaye leo atatoa mwongozo bungeni.

"Mjadala wa Richmond umemalizika na mambo yote kesho (leo) yako hadharani. Kamati ya kisekta imekaa na kuandaa taarifa ambayo amekabidhiwa spika wa Bunge leo (jana). Kikubwa jamii ijue kwamba, kamati iko makini, haimwonei wala kumpendelea mtu," alisema Selelii.

Alipotakiwa kuthibitisha kama amepokea hoja za kamati hiyo kuhusu Richmond na kwamba ataruhusu mjadala wake bungeni leo, Spika Sita alisema: "Haijanifikia bado".

Alifafanua kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini anatarajia kuwasilisha hoja za Kiwira na Richmond kesho, siku ambayo pia wenyeviti wa kamati za Miundombinu, Ardhi, Maliasili na Mazingira watawasilisha hoja zao.

Alibanwa zaidi aeleze kama endapo angeipata jana jioni angekuwa tayari kuiwasilisha leo kama ilivyoelezwa, alijibu:

"Hata kama nitaipata sasa, siwezi kuitable kesho (leo) kwani nahitaji muda kuisoma na kuielewa".

Awali mbung wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alisema suala la Richmond limeanza kuligawa taifa na njia pekee ya kuirudishia jamii imani na serikali, ni Rais kwa mamlaka ya kuwa mkuu wa nchi kuunda jopo la majaji kupitia upya hoja zote na kutoa maamuzi.

"Suala hili limeonekana kuigonganisha mihimili mikuu miwili ya dola, Bunge na Serikali, dawa yake sasa ili liishe, ni Rais kama mkuu wa nchi nasisitiza, mkuu wa nchi sio serikali kuunda tume ya majaji wapitie Maazimio ya Bunge, utekelezaji wa serikali na watoe maamuzi," alisema.
Alisema: "Inavyoonekana kila upande unavutia kwake, wakati Bunge likitaka serikali itekeleze mapendekezo yake ndani ya miezi mitatu, serikali imetumia karibu mwaka na nusu na bado inakuja na majibu ya kubabaisha.

source Mwananchi

Hivi ni sahihi Baba na/au Mama wa familia kusema hahusiki na wizi uliofanywa na mmoja wa wanafamilia wake?Ni sahihi kweli kwa Baba kusema hahusiki na wizi uliofanywa na mtoto wake wa kwanza?

Mkulu bana,ishu zingine ni bora ukauke tu usubiri hukumu ya wananchi kuliko kuendelea kudhihirisha uhamnazo wako.
 
Kikwete anahusika moja kwa moja kwa kupitia former ambassador (Mr Daraja) ndo alimuunganishia hili dili, maana Daraja alikuwa kila week yuko Houston na hawa jamaa wa Richmond. Hila Kikwete alifikiri hawa Jamaa ni mahili kwa hii mitambo baada ya kuangalia website zao za kufoji, kumbe ni bure.

Richmond----Daraja (Barozi)-------Kikwete---------Lowasa (Msimamizi wa hiyo tender).

Hivyo Kikwete anahusika moja kwa moja, asikwepe.

Mrugaruga!

Mpaka hapo uko sahihi!! Waligawana baada ya Ridhwan kuchemsha alichukua lowasa ile ya Megawati mia na RA alichukua ile ya Megawati 40 za Aggreco na alizifunga na zikzalisha umeme!

Mpaka hapo dili lilikwenda vizuri ila teddy Lowasa alipochemsha kwani mashine za Awamu ya kwanza ziliuza umeme hewa ndiposa wakamwomba RA awasidie na mkataba akaridhishwa na hatimaye ikazaliwa DOWANS yote haya yanatokea Kikwete tulimwambia lakini haka kajamaa ka kikwere kakabishi kuliko Nyerere !! Kwa hiyo kwa IQ yake alifikiri yataisha kumbe yakamtumbukia nyongo!!!

Piga ua kama asipowaadabisha waliobakia CCM marijo bai!!! What goes around comes around. Kikwete komaa lakini ikifika 2015 utafute pa kuficha uso wako!! Kumbuka una watoto tena bado wadogo utawaficha wapi na pindi wakwere wengi hamjaenda shule na hata pesa hamna!!

Enzi ya Mkapa hakupata kupewa hivi vidonge laivu kama wewe shauri yako soma hapa jamii!!!
 
Kikwete: Msinihusishe na kashfa ya Richmond
Kizitto Noya, Dodoma

SASA ni wazi kwamba sakata la Richmond limeingia katika hatua nyingine baada ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ofisi Rais kutangaza kwamba, Rais Jakaya Kikwete hahusiki kwa namna yoyote na kashfa hiyo ambayo inaendelea kulitikisa taifa kwa muda sasa.

Hatua ya Rais Kikwete kutotaka kuhusishwa na kashfa hiyo ya Richmond kunazidi kuibua maswali mengi kutoka kwa wananchi kwamba, ni nini hatima ya mjadala huo ambao unazidi kupamba moto kila kukicha nje na ndani ya Bunge.

Wakati Rais Kikwete akijivua kutoka katika sakata hilo, Kamati ya Nishati na Madini imetoa maazimio ya kupinga jinsi serikali inavyotekeleza maazimio ya Bunge kuhusu ripoti ya Richmond. Jana jioni Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ilitoa taarifa ikimuepusha rais na kashfa hiyo.

"Tumepata kusema huko nyuma, na tunapenda kusisitiza kwa mara nyingine kuwa, Rais hana mkono katika Richmond na hata Ripoti ya Bunge iliyotolewa kufuatia uchunguzi katika suala hilo la Richmond, haikumhusisha Rais Kikwete," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa ya Ikulu, imetolewa huku Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba akidai kwamba, Rais Kikwete anahusika na Richmond kwa kuwa maamuzi yalifanyika chini ya serikali anayoiongoza.

Habari kutoka Dodoma zinadai kuwa kutokana na kusuasua kwa utekelezaji wa maazimio ya Bunge kutaka maafisa wa serikali waliohusika kwa njia moja au nyingine na mchakato wa kampuni hiyo kupewa zabuni Tanesco, wachukuliwe hatua.

Kundi mojawapo la wabunge limeeleza kutoridhishwa na ripoti ya serikali iliyotolewa bungeni hivi karibuni kuwasafisha. Kundi hilo limepanga kumchukulia hatua kubwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye ndiye kiongozi mkuu wa serikali bungeni, kutokana na kuwanusuru maafisa waliotuhumiwa kuhusika na kashfa hiyo.

Wakati kamati hiyo ikitoa msimamo huo, wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikutana jana usiku katika Ukumbi wa Pius Msekwa kutafakari sakata hilo.

Ingawa tangazo la Mwenyekiti wa Bunge, Job Ndugai jana mchana halikueleza agenda za kikao hicho, vyanzo huru vya habari vililidokeza gazeti hili kuwa wabunge hao wangejadili ripoti ya Richmond na kuweka mkakati wa kuinusuru serikali.

Mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini ambaye hakutaka kutajwa gazetini akihofia kuvunja Kanuni za Bunge kwa kutoa siri za vikao, alisema kamati haikuridhishwa na ripoti ya serikali hasa katika suala la kuwasafisha Mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward Hoseah na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika.

"Kamati haikubaliani na ripoti hiyo hasa pale iliposema Dk Hoseah na Mwanyika hawana hatia. Tumekuwa na vikao kwa siku mbili jana (juzi), leo (jana) na bado tunaendelea kesho (leo),”alisema.

Alisema mapendekezo ya kamati ya Bunge kuhusu Richmond yalijitosheleza kimaamuzi na serikali ilitakiwa kuyatekeleza tu na sio kuendesha uchunguzi mwingine.

"Uchunguzi ulishafanywa na Bunge, serikali ilitakiwa kutekeleza tu. Ilikuaje ifanye tena uchunguzi kwa muda zaidi ya ule uliopangwa na Bunge badala ya kufanya utekelezaji?" alihoji.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, William Shelukindo na Makamu wake, Dk Harrison Mwakyembe hawakupatikana jana kuzungumzia suala hilo na simu zao za mikononi kutopatikana kabisa.

Mjumbe wa kamati iliyoundwa na Bunge kuchunguza suala la Richmond, Habib Mnyaa alikiri kuwa na taarifa ya kamati ya kisekta kukutana na kujadili ripoti hiyo, lakini akaeleza kuwa kikao hicho kilichokaa juzi na jana, kinamalizika leo.

"Kikao kimekuwapo, lakini hakijafikia maamuzi hayo unayosema," alisema Mnyaa akirejea hoja ya mwandishi wa habari aliyetaka kuthibitisha taarifa kwamba, kikao hicho kimejenga hoja ya kutokuwa na imani na serikali katika suala la Richmond.

Hata hivyo, habari nyingine zinadai kuwa kamati hiyo leo inatarajia kumweka kiti moto Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja ili awaeleze ni kwanini serikali imeshindwa kutekeleza mapendekezo ya Bunge.

Hata hivyo, mjumbe mwingine, Lucas Selelii alilieleza gazeti hili kuwa vikao vyote vilivyojadili Richmond, vimemaliza kazi na kuwasilisha hoja zake kwa spika wa Bunge Samuel Sitta ambaye leo atatoa mwongozo bungeni.

"Mjadala wa Richmond umemalizika na mambo yote kesho (leo) yako hadharani. Kamati ya kisekta imekaa na kuandaa taarifa ambayo amekabidhiwa spika wa Bunge leo (jana). Kikubwa jamii ijue kwamba, kamati iko makini, haimwonei wala kumpendelea mtu," alisema Selelii.

Alipotakiwa kuthibitisha kama amepokea hoja za kamati hiyo kuhusu Richmond na kwamba ataruhusu mjadala wake bungeni leo, Spika Sita alisema: "Haijanifikia bado".

Alifafanua kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini anatarajia kuwasilisha hoja za Kiwira na Richmond kesho, siku ambayo pia wenyeviti wa kamati za Miundombinu, Ardhi, Maliasili na Mazingira watawasilisha hoja zao.

Alibanwa zaidi aeleze kama endapo angeipata jana jioni angekuwa tayari kuiwasilisha leo kama ilivyoelezwa, alijibu:

"Hata kama nitaipata sasa, siwezi kuitable kesho (leo) kwani nahitaji muda kuisoma na kuielewa".

Awali mbung wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alisema suala la Richmond limeanza kuligawa taifa na njia pekee ya kuirudishia jamii imani na serikali, ni Rais kwa mamlaka ya kuwa mkuu wa nchi kuunda jopo la majaji kupitia upya hoja zote na kutoa maamuzi.

"Suala hili limeonekana kuigonganisha mihimili mikuu miwili ya dola, Bunge na Serikali, dawa yake sasa ili liishe, ni Rais kama mkuu wa nchi nasisitiza, mkuu wa nchi sio serikali kuunda tume ya majaji wapitie Maazimio ya Bunge, utekelezaji wa serikali na watoe maamuzi," alisema. Alisema: "Inavyoonekana kila upande unavutia kwake, wakati Bunge likitaka serikali itekeleze mapendekezo yake ndani ya miezi mitatu, serikali imetumia karibu mwaka na nusu na bado inakuja na majibu ya kubabaisha
 
Kikwete anahusika moja kwa moja kwa kupitia former ambassador (Mr Daraja) ndo alimuunganishia hili dili, maana Daraja alikuwa kila week yuko Houston na hawa jamaa wa Richmond. Hila Kikwete alifikiri hawa Jamaa ni mahili kwa hii mitambo baada ya kuangalia website zao za kufoji, kumbe ni bure.

Richmond----Daraja (Barozi)-------Kikwete---------Lowasa (Msimamizi wa hiyo tender).

Hivyo Kikwete anahusika moja kwa moja, asikwepe.
Mkuu uliposema haya watu walikuona mzushi kama leo wengine wanavyomsema Hutaki Unaacha! rudi umwage nyeti nzima mkuu umepotea kabisa!
 
wakuu comments za wadau hapo juu hatari tupu! Natamani hawa wadau warudi tena!
 
Mrugaruga!

Mpaka hapo uko sahihi!! Waligawana baada ya Ridhwan kuchemsha alichukua lowasa ile ya Megawati mia na RA alichukua ile ya Megawati 40 za Aggreco na alizifunga na zikzalisha umeme!

Mpaka hapo dili lilikwenda vizuri ila teddy Lowasa alipochemsha kwani mashine za Awamu ya kwanza ziliuza umeme hewa ndiposa wakamwomba RA awasidie na mkataba akaridhishwa na hatimaye ikazaliwa DOWANS yote haya yanatokea Kikwete tulimwambia lakini haka kajamaa ka kikwere kakabishi kuliko Nyerere !! Kwa hiyo kwa IQ yake alifikiri yataisha kumbe yakamtumbukia nyongo!!!

Piga ua kama asipowaadabisha waliobakia CCM marijo bai!!! What goes around comes around. Kikwete komaa lakini ikifika 2015 utafute pa kuficha uso wako!! Kumbuka una watoto tena bado wadogo utawaficha wapi na pindi wakwere wengi hamjaenda shule na hata pesa hamna!!

Enzi ya Mkapa hakupata kupewa hivi vidonge laivu kama wewe shauri yako soma hapa jamii!!!
Hii ya huyu bwana ndio kabisaa kafunguka! Ndio maana dogo kawa bilionea ghafla!
 
Kikwete anahusika moja kwa moja kwa kupitia former ambassador (Mr Daraja) ndo alimuunganishia hili dili, maana Daraja alikuwa kila week yuko Houston na hawa jamaa wa Richmond. Hila Kikwete alifikiri hawa Jamaa ni mahili kwa hii mitambo baada ya kuangalia website zao za kufoji, kumbe ni bure.

Richmond----Daraja (Barozi)-------Kikwete---------Lowasa (Msimamizi wa hiyo tender).

Hivyo Kikwete anahusika moja kwa moja, asikwepe.
Napenda kujua hiyo Daraja yupo wapi kwa sasa
 
Kwa speed hii ya ufukuaji wa makaburi simuoni JHMK akipona, japo nafikiri hawa wazee wangeachwa wapumzike tu na namna nzuri ya kuwaacha wapumzike ni kuyaacha makaburi yawe yalivyo!
 
Back
Top Bottom