KIKWETE HAJAPATA RC WA Dar es Salaam??

bwegebwege

JF-Expert Member
Jul 30, 2010
1,071
185
Jamani naona muda unakatika sasa JK alimteua yule Mwarabu-Msukuma kuwa RC wa Dar, jamaa HAJA-FIT kabisa kwenye cheo hicho....
Hivi JK bado anatafuta RC?
 
Kwani haukumbuki! DR wa ukweli Dr Slaa alisema hivyo vyeo havina kazi na yeye hawezi kuviweka, sasa si unajua yeye anachosema ni lazima kifanyiwe kazi. Bado wanalifanyia kazi na hii inaonyesha jinsi vyeo hivyo visivyo na umuhimu.
 
alishasema 'ukiona umeula ujue umeliwa'

hajapata mtu wa kumla.

hahaha!

mkwere jamani na viswahili vyake!?
 
ndiyo maana katika mabadiliko ya katiba tunataka Rais apunguziwe madaraka! maana ana issues nyingi mpaka anasahau! kumbuka makaimu wengi ktk taasisi za Serikali!
 
.....hatuhitaji RC,,,,wanamaliza fedha za umma wa watanzania bure bila kuwa na shughuli maalumu za kufanya! kuzururazurura tu!
 
Hata hakuna haja ya huyo RC..mbona mambo yanaenda tu...ila wakati mwingine jamaa anapo-delay mambo anasaidia kuhalalisha hoja zinazosemwa kila siku na kupingwa...kama hii ya ma-DC na ma-RC kutokuwepo...............
 
Nadhani hiyo nafasi ndio inamfaa yeye. Aachie ngazi awapishe wenye akili kuongoza nchi!!! Capacity yake nadhani kama tukimpendelea sana ni ukuu wa Mkoa. Vinginevyo arudi jeshini akaongoze kombania.
 
Back
Top Bottom