Elections 2010 Kikwete: Gharama hizi za nini?

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
7,510
7,534
nilitegemea JK kampeni zake za kipindi hiki kuwa za utulivu zaidi ya zile za 2005 kwa sababu tayari ameshakuwa madarakani na ametekeleza yale aliyoahidi. kwamba hana sababu ya kuwa na hofu kwa sababu waTZ ni waelewa na hawawezi kumlipa ubaya(kutomchagua) kwa wema wake aliowatendea(kutimiza ahadi) kwa sababu inafahamika mtenda wema hulipwa kwa wema(sidhani kama hili limabadilika) au waTZ ni wabaya kiasi hicho kwenda kinyume na hoja hiyo.lakini hali haiko hivyo gharama inayotumiwa ni kubwa zaidi( angalia wingi wa mabango, kama yanalipiwa lakini!),helcopter (kuna wakati mpaka tatu, imeripotiwa hii), machapisho ya fulana na vipeperushi vingine.kwa kweli naamini hii gharama itavunja rekodi ya matumizi katika kampeni za CCM.hoja yangu ni, je JK anahofu ya nini wakati yeye tayari ana mtaji wa utendaji wake kufahamika na wananchi? au wananchi hawa ni mbumbumbu kiasi kwamba wanasahau haraka sana mema waliyotendewa yaani wanadanganyika kirahisi zaidi?. mimi nadhani ambao wanastahili kufanya kampeni kwa nguvu zaidi ni wagombea ambao hawajawahi kuendesha nchi kwa sababu wao ndio wanastahili kuwashawishi wananchi zaidi ili wawaamini na sio ndugu JK. napata mashaka na hili.
 
Mkuu hapo umenena. Mimi naona hana haja ya kufanya kampeni kabisa. Arudi dar akapumzike asubili October 31, kisha aapishwe. kama anaendelea na kampeni na kuzidisha mabango na kuendelea kutumia helkopta 3 (12M kwa saa); anajua alilowfanyia watz kuwa si jema hivyo lazima atumie nguvu kuliko mgombea yeyote tangu Tz ipate Uhuru!!
 
Ukweli ni JK na CCM yake wananjijua vizuri kuliko tunavyowafahamu.

Wanajijua ya kuwa kiutendaji hawakidhi mahitaji ya taifa hili kwa hiyo inabidi watumie nguvu nyingi kubaki madarakani.............
 
Unajua hata mm najiuliza sana mgombea huyu tunayeambiwa ana rekodi ya mafanikio kuliko raisi yeyote aliyewahi kutokea Tz, mgombea aliyeleta maisha bora kwa kila mtanzania kwa ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya. Mgombea anayekubalika, mwenye upendo, asiye na makuu, mkulima kama sisi.................

Sasa ni kwa nini kampeni ya gharama kuliko nadhani yoyote iliyowahi kutokea Tanzania, Media polarization, media zote za serikali kwake.............

Doesn't this tell us otherwise kuhusu huyu mgombea????????
 
wa Tz tungekuwa ni watu wa kufanya analysis kama hii tusingekuwa huku tulikopelekwana hawa jamaa.Utashangaa hata watu wenye akili zao wapo katika kumshauri kuwa njia nzuri ni mabango.WATANZANIA AMKENI!!!!!!!!!!!!!!Huyu jamaa atatupeleka jehanamu kabla ya wakati wake ,kataeni.
 
nilitegemea JK kampeni zake za kipindi hiki kuwa za utulivu zaidi ya zile za 2005 kwa sababu tayari ameshakuwa madarakani na ametekeleza yale aliyoahidi. kwamba hana sababu ya kuwa na hofu kwa sababu waTZ ni waelewa na hawawezi kumlipa ubaya(kutomchagua) kwa wema wake aliowatendea(kutimiza ahadi) kwa sababu inafahamika mtenda wema hulipwa kwa wema(sidhani kama hili limabadilika) au waTZ ni wabaya kiasi hicho kwenda kinyume na hoja hiyo.lakini hali haiko hivyo gharama inayotumiwa ni kubwa zaidi( angalia wingi wa mabango, kama yanalipiwa lakini!),helcopter (kuna wakati mpaka tatu, imeripotiwa hii), machapisho ya fulana na vipeperushi vingine.kwa kweli naamini hii gharama itavunja rekodi ya matumizi katika kampeni za CCM.hoja yangu ni, je JK anahofu ya nini wakati yeye tayari ana mtaji wa utendaji wake kufahamika na wananchi? au wananchi hawa ni mbumbumbu kiasi kwamba wanasahau haraka sana mema waliyotendewa yaani wanadanganyika kirahisi zaidi?. mimi nadhani ambao wanastahili kufanya kampeni kwa nguvu zaidi ni wagombea ambao hawajawahi kuendesha nchi kwa sababu wao ndio wanastahili kuwashawishi wananchi zaidi ili wawaamini na sio ndugu JK. napata mashaka na hili.

Alishanyea kambi huyo!

Octoba Out!!
 
Hii analysis nimeipenda nilitegemea mabango kama hayo yawekwe na mgombea uraisi kupitia chama cha upinzani maana hakuna mtu anayekifahamu kwa utendaji wake hivyo walitakiwa ndo wawe na kazi ngumu ya kujitambulisha, hii inashangaza kwasababu kikwete anafahamika mpaka na watoto wa chekechea kuwawekea picha na matangazo kwenye mabango ni matumizi mabaya ya rasirimali finyu tulizo nazo.
 
ccm tunapesa bwana thus why! Upinzani hawana pesa! wananchi wanaipenda ccm na wamechangia saana chama chao!
 
ccm tunapesa bwana thus why! Upinzani hawana pesa! wananchi wanaipenda ccm na wamechangia saana chama chao!

I really likes JF!!!:becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky:
 
:mad2: Enzi za Mrema Bwana Mkapa (kipindi cha kwanza) aliingia ikule kwa asilimia 61(61%) na kipindi cha pili aliingia kwa asilimia 72 (72%) kuonyesha kwamba alipanda chati. Ndugu huyu (JKkikwete) aliingia kwa asilimia 86 (86%) kipindi cha kwanza anaogopa kupata chini ya hapo ambayo ni ishara ya utendaji mbaya. Pia wanaogopa kuja kuulizwa ufisadi walioufanya.
 
Alishasema kwamba aslimia 70 ya watanzania ni Bendera fuata upepo.. halafu mnataka atulie bila kuendelea na kampeni? Upepo huo wa WaTanzania utaelekea sehemu nyingine...Kwa setrikali mbadara (Wapinzani)
 
unajua hata mm najiuliza sana mgombea huyu tunayeambiwa ana rekodi ya mafanikio kuliko raisi yeyote aliyewahi kutokea tz, mgombea aliyeleta maisha bora kwa kila mtanzania kwa ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya. Mgombea anayekubalika, mwenye upendo, asiye na makuu, mkulima kama sisi.................

Sasa ni kwa nini kampeni ya gharama kuliko nadhani yoyote iliyowahi kutokea tanzania, media polarization, media zote za serikali kwake.............

Doesn't this tell us otherwise kuhusu huyu mgombea????????

debe tupu haliachi..................................?
 
Duniani kote marais wanaoomba ridhaa ya kipindi cha pili wanapiga kampeni za nguvu hata pale wanapokuwa wamewtekeleza ahadi. Ni kipindi cha kufanya muhtasari wa ahadi zilizotekelezwa, na kutoa ahadi mpya kwa kipindi kijacho. si vema kumkadria uzito mdogo mpinzani kwa kuwa wagombea wote wana lengo moja la kushoka dola kama ilivyo kwa rais anayemaliza kipindi cha kwanza.
 
ccm tunapesa bwana thus why! Upinzani hawana pesa! wananchi wanaipenda ccm na wamechangia saana chama chao!

Hivi unawajua wale Makamba aliowasema wanalala bila kula kariakoo, afu kumbe anajua wapo kwa nini msingewapelekea sehemu ya pesa yenu ili nao wajione kama wanadamu angalao kwa siku moja tuu?
 
ccm tunapesa bwana thus why! Upinzani hawana pesa! wananchi wanaipenda ccm na wamechangia saana chama chao!

CCM mna pesa au wana pesa??? Isijekuwa we mchovu tu unakula mlo mmoja halafu unadai ccm mna hela wakati kila mtu anajua kuwa ni hela za wahindi wanataka kuendelea kuitafuna nchi kwa kuwatumia vibaraka kama wewe na jk.... Kama mna hela wekeni vifaa ktk maabara za shule za kata na kuweka vitanda ktk zahanati ili mama zetu wasilale watatu watatu huko hospitalini hadi vitoto vinavyozaliwa vinajisikia vimezaliwa ktk chi ya laana vinawaza kuwa vifisadi tu badala ya kujenga taifa. Yote haya matatizo yameletwa na ccm yako wewe.
 
Back
Top Bottom