Kikwete: Foleni jijini Dar itakuwa historia

Bro hakuna research iliyofanyika kugundua chanzo cha 4leni DSM, Ni wameamka na kuja na mradi huu wa magari ya kasi. Tenda utaisikia kwa SIMON G**_P...Kisha jiulize yy na UDI? . Inawezekana solution sio magari yaendayo kasi bali ni ufinyu wa barabara tulizonazo na nyingi kua na shortcut kibao hivyo kua na msongamano hasa katika Junctions. Wataalam wapo tatizo ni kuchukua mamlaka ya katiba yanatumika sehemu yoyote. Hii ni sawa na Mkunga wa Jadi awe Neurosergion.

Kiongozi, utafiti umefanywa na wataalam wa chuo cha ardhi. Ukitaka details za findings wasiliana nao watakupa.
 
Ndugu wanajamvi jana mkuu wetu wa nchi alikuwa anazindua mradi wa ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi. Na katika hotuba yake nilivutiwa na kauli kutoka kwa mkuu wetu wa nchi kuwa hali ya foleni ktk jiji la dsm baada ya huu mradi kukamilika itabaki kuwa historia. Je kwa huo mradi peke yake inaweza kuondoa tatizo la kero ya foleni hapa dsm au kuna haja ya kuwa na projects nyingine za kusupport kupunguza hii kero? J e unadhani ilikuwa sahihi kwa kiongozi mkuu kutoa kauli kama hii kwa sasa? na vp kama haitakuwa kama alivyosema? nini kifanyike? nawasilisha

Aliwahi kutuambia kuwa foleni ni dalili ya maendeleo, sasa foleni ikiisha si tutakuwa tumerudi nyuma kimaendeleo?
 
...Na kwanini atake Foleni kuwa Historia wakati aliishasema Foleni ni Ishara ya Maendeleo?? Hataki Maendeleo?? :confused2:

Kuna utafiti ulifanyika na matokeo yake yalitolewa mwezi August,2010.Kila siku katika kipindi hicho foleni za Dar zilikuwa zinasababisha hasara ya 4 million. Je, hayo ndiyo maendeleo aliyoyasema mheshimiwa?
 
Kiungwana kabisa nampongeza mheshimiwa kwa kuelekea kutimiza ahadi yake hii moja!! Ila pia nimuombe asiupe mradi huu utukufu usiostahili,kusema kuwa huo ndio mwarobaini wa foleni jijini ni sawa na chupi kuiita suti,
 
Kiungwana kabisa nampongeza mheshimiwa kwa kuelekea kutimiza ahadi yake hii moja!! Ila pia nimuombe asiupe mradi huu utukufu usiostahili,kusema kuwa huo ndio mwarobaini wa foleni jijini ni sawa na ...

Aksante mkuu kwa kuliweka hili wazi. Sijui ni kwa nini hatujifunzi kutoka kwa jirani zetu! Walipokuwa wanaweka flyovers Nairobi walisema hayo hayo, lakin ukiangalia hali ya foleni ilivyo ni hatari.

Nadhan mkazo uwekwe kwenye barabara za pembezon pia. Na kisha kupunguza mrundikano wa maofisi city centre
 
Ama mradi wa DART Unaweza kuwa moja tu ya njia kujaribu kupunguza tatizo la foleni katika jiji la dar es salaam lakini nina uhakika si kwa kiwango cha kile kinachokusudiwa.
yapo mengi ambayo mengine haya hitaji fedha nyingi sana kuweza kusaidia kupunguza foleni ila akili na sheria za barabarani
mfano yafuatayo yanaweza kupunguza foleni

  • kufwata kwa sheria zote za barabarani, namna ya utumiaji wa bara bara kwa mfano bara bara ya lanes 2 upande wa kulia unatakiwa itumiwe na magari madogo tu.(privates cars) malori ,daladala,mabasi,tractors , bajajs , piki piki zote na kama hayo yasikae kabisa upande wa kulia wa barabara.
  • sheria sasa zinaweza kutiwa nguvu na kuanza kutumia faida ya kuwa na smart driving licence. baada ya kutoa faini kwa kila kosa basi ni wakati wa kuweka mtindo wa kuweka driving points kwa madereva na points ziwe zinazidi kwa kila offence na ikifika points maalum basi licence inakuwa revoked for one year , nk
  • sehemu zote zenye bara bara za 4 ways basi vituo vya dala dala visiwekwe just uki kata kona tu, mfano pale ubungo na tazara, na sehemu nyengine kama mnazi mmoja pale . vituo hivyi wiwekwe mbali baada ya kukata kona hii inapunguza sana magari kublock gari nyengine pale inapokuwa zimeruhusiwa na taa za barabarani
  • vituo vyote vya dala dala viwekwe camera kuangalia dala dala zinazopakia nje ya kituo, na hawa faini yao iwe kubwa , hili litawafanya kutii sheia kwani hakuna rushwa ila kila dala dala itayofanya kosa itakuwa inapatiwa faini yao na Sumatra
  • kupunguza vituo vya dala dala ndani ya jiji
  • 3 lane ya lowasa ali hasan mwinyi road waongeze moja ziwe 4
  • speed limits katiak baadhi ya sehemu ziwe imposed
  • feeder roads ziongezwe
  • barabara zote ndani ya city center mfano kariakoo yote, upanga yote,ilala yote kuwekwa lami
  • kutoa barabara mpya kutoka muhimbili juu mpaka kinondoni upande wa makaburini , ni sehemu ndogo tu inaezekana
  • mashimo yote lazima yafukiwe na kutengenezwa. mtindo wa sasa wa vibali vya kupasua barabara kwa ajili ya kupitisha pipes za maji ama wire za umeme au simu una walakini lazima ubadilishwe na iwe ni jukumu la anaeomba kibali atengeneze bara bara hiyo kupitia contractors maalum na lazima iwe kwa muda maaalum na lazima pia waweke dhamana ya kutosha .
  • na mwisho lazima halmashauri ya jiji ivunjwe wameshindwa kuliendesha jiji hili, mtindo wa sasa wa kuliendesha kwa kutumia madiwani ambao uwezo wao ni mdogo sana kuliko matarajio na mahitaji ya jiji hakika haufai.inatakiwa jiji hili sasa liwe na wizara kamili ya Dar es salaam.
  • mwisho wa hoja uchaguzi wa mayor wa jiji sasa ufanywe kwa uchaguzi wa kura kwa jiji zima na sio achaguliwe na madiwani pekee na pia sio lazima atoke chama cha siasa,
 
Ndugu wanajamvi jana mkuu wetu wa nchi alikuwa anazindua mradi wa ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi. Na katika hotuba yake nilivutiwa na kauli kutoka kwa mkuu wetu wa nchi kuwa hali ya foleni ktk jiji la dsm baada ya huu mradi kukamilika itabaki kuwa historia. Je kwa huo mradi peke yake inaweza kuondoa tatizo la kero ya foleni hapa dsm au kuna haja ya kuwa na projects nyingine za kusupport kupunguza hii kero? J e unadhani ilikuwa sahihi kwa kiongozi mkuu kutoa kauli kama hii kwa sasa? na vp kama haitakuwa kama alivyosema? nini kifanyike? nawasilisha
Usanii mwingine!! Hebu tujikumbushe ahadi zilizotolewa hapo kabla na hazijatimizwa. 1. Maisha bora kwa kila Mtanzania badala yake yamekuwa Maisha ya mateso makubwa kwa wa-TZ. walio wengi, Maisha bora yamebaki kwa JK mwenyewe na maswaiba wake 2. Tatizo la maji Dar itakuwa historia, badala yake matatizo ya maji yameongezeka na kuwa makubwa kuliko hata mwaka 1961, tulipopewa uhuru na wakoloni!! 3. Tatizo la mgao wa umeme litakuwa historia, badala yake kila kukicha miungurumo ya majenereta kwa wenye nazo. Walala hoi tunalala gizani, au tunanunua mishumaa, ambayo ishasababisha maafa kadhaa!! Hiyo ni mifano michache, CONCLUSION, another babu kubwa la changa la macho!!!
 
Nimeamini kweli watu wana viwanda vya uongo, na aneongoza kuwa na kiwanda sophiticated cha uongo ni H.E. 5Dr. Mr. Sir DHAIFU.
 
Tatizo mkuu wa kaya anaongea huku hajadhamiria,lakini kama angekuwa amedhamiria,angefikia baadhi ya malengo!Mbona visasi kwake ni rahisi kwa nini mengine yashindikane?
 
Kiongozi, utafiti umefanywa na wataalam wa chuo cha ardhi. Ukitaka details za findings wasiliana nao watakupa.

Then solution ni mabasi yaendayo kasi? Yanatumika nchi gani na ufanisi wake ni % ngapi? Nisaidie kwa hili coz kwa ufinyu wa barabara zetu hata wakiweka haya mabasi bado kuna gari za raia wema na misafara hadi ya wake zao bana.
 
Then solution ni mabasi yaendayo kasi? Yanatumika nchi gani na ufanisi wake ni % ngapi? Nisaidie kwa hili coz kwa ufinyu wa barabara zetu hata wakiweka haya mabasi bado kuna gari za raia wema na misafara hadi ya wake zao bana.

Nimewahi kutembelea jiji la Istanbul na kwa kweli jiji hilo ni mfano halisi wa jinsi mabasi yaendeayo kasi yanavyopunguza foleni. Houston Marekani kwa mfano kuna barabara zinaitwa HOV (High Occupancy Vehicles) ni maalam kwa magari yenye abiria zaidi ya mmoja, hii pia inasaidia kupunguza foleni. Kule Marekani wamefanya hivyo ili kuencourage watu wanaokaa karibu na kufanya kazzi karibu kushare a ride. Huna mfano pia wa Chile. Wataalam wa chuo cha ardhi walienda Indonesia. Kuna thread hapa ukitafuta utaikuta inazungumzia huo utafiti.
 
kweli kuna kila dalili za kuwa historia ya foleni dar es salaam. Itabidi wanazuoni tutunge vitabu vya Historia ya Foleni Dar es Salaam...
 
Macos,

Nakubaliana na wewe, hasa kwenye hivi vituo vya daladala ambavyo vingi vimejengwa kwenye maeneo yanayochochea foleni mfano karibu na kona. Na hawa Daladala hawaingii vituoni.

Kuna swala la Parking pia, ukiingia Kariakoo kule hawa jama wa kukusanya ushuru wa Parking wanaweka magari kushoto na kulia halafu katikati inabaki nafasi ya kupita gari mbili kwa taabu sana. Serikali itafute majengo makubwa ya ghorofa kwa ajili ya Parking Kariakoo na Posta ili watu wasiache magari barabarani kabisa na hawa wanaopakua na kupakiza mizigo wafanye kazi yao usiku.

Haya yote yanawezekana kama kutakuwa na utaratibu mzuri wa kuhakikisha hizo kanuni zinafuatwa.
 
Mabasi yenye njia maalum (sidhani kama yanaenda kasi kwa sababu kama kawaida yetu tutaweka matuta akigongwa mtu hata kwa kosa lake si unaona watu wanavuka katikati ya round about). yatapunguza foleni ila sio kumaliza. Tena ni kwa muda. Fly overs, ring roads, kuondoa malori yanayofia njiani na kuwa na satellite city zenye huduma zote muhimu ndio suluhisho la kudumu.
 
Nadhani kauli hiyo imetolewa ili kutia vionjo shamrashamra za ufunguzi kama wafanyavyo mara zote wanasiasa wetu kwa miundo mbinu ilivyo inaweza kusaidia kwa kiasi fulani kupunguza foleni na sina uhakika kama kuna ufafiti wa kitaalamu uliofanywa ili kubaini matatizo ya foleni na ufumbuzi wake yote wa yote nasikia kituo cha Ubungo kinahamishwa sina hakika kama hii itakuwa ni ufumbuzi wa msongamano wa mabasi yaendayo mikoani.Inawezekana ikawa ni kuhamisha tatizo kutoka sehemu moja na kulipeleka sehemu nyingine
 
Tatizo la mikopo kwa wanafunzi litakuwa historia...by KIKWETE SEPT 2005 ukumbi wa DAIMOND JUBILEE.
 
Back
Top Bottom