Kikwete: Foleni jijini Dar itakuwa historia

Mzalendo wa ukweli

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
559
149
Ndugu wanajamvi jana mkuu wetu wa nchi alikuwa anazindua mradi wa ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi.

Na katika hotuba yake nilivutiwa na kauli kutoka kwa mkuu wetu wa nchi kuwa hali ya foleni ktk jiji la Dar baada ya huu mradi kukamilika itabaki kuwa historia.

Je, kwa huo mradi peke yake inaweza kuondoa tatizo la kero ya foleni hapa dsm au kuna haja ya kuwa na projects nyingine za kusupport kupunguza hii kero?

Je, unadhani ilikuwa sahihi kwa kiongozi mkuu kutoa kauli kama hii kwa sasa?

Na vipi kama haitakuwa kama alivyosema nini kifanyike?
 
tatizo la maji litakuwa historia kufikia 2013

MCG imefikia wapi coz azimio hili la maji lilikua 2010, ila kwa stats ni less than 50% wans access ya maji safi. Kwa hesabu ya kawaida tunahitaji miaka 50 mingine kufikisha 80% of population with access to clean Water. Tafakari!!!!!!!!!!!!
 
Foleni itapungua lakini kuisha kabisa itetegemea na nauli ya hao DART na convenience.

Wanatakiwa watushawishi na hiyo DART tuache magari nyumbani, hapo ndio foleni itapungua.

Bro hakuna research iliyofanyika kugundua chanzo cha 4leni DSM, Ni wameamka na kuja na mradi huu wa magari ya kasi. Tenda utaisikia kwa SIMON G**_P...Kisha jiulize yy na UDI? . Inawezekana solution sio magari yaendayo kasi bali ni ufinyu wa barabara tulizonazo na nyingi kua na shortcut kibao hivyo kua na msongamano hasa katika Junctions. Wataalam wapo tatizo ni kuchukua mamlaka ya katiba yanatumika sehemu yoyote. Hii ni sawa na Mkunga wa Jadi awe Neurosergion.
 
Tatizo hili naliona sana bro na miaka inavyozidi kuongezeka na tatizo linakuwa kubwa.

Zile sehemu ambazo serikali wanaogopa kuvunja nyumba za chini soon zitakuwa magorofa sasa sijui 20 yrs from now kama wataweza kufanya maamuzi magumu.

Solution hapa ni kuamua kwamba hapa itapita barabara wananchi waanze kujiandaa kuhama hata kama 20 yrs later fidia italipwa ila wajue kwamba wataondoka. Itabidi tuamua tu kutengeneza barabara bila kujali kwamba kuna wakazi wameshajenga!
 
Siamini kabisa, huu mradi ni partial approach, with a lot of dead ends.
Ni kama sasa hivi kuna ngeleja huku nilipo wakati tuliambiwa itakuwa historia.
 
Tatizo wakijenga barabara na.kuboresha miundombinu mingine watu watazidi kuja.dsm hivyo.kusababisha misongamano mingi na kuongeza foleni.kwani watu wengi wataopt kutumia usafiri wao kuliko kutumia public
 
Bro hakuna research iliyofanyika kugundua chanzo cha 4leni DSM, Ni wameamka na kuja na mradi huu wa magari ya kasi. Tenda utaisikia kwa SIMON G**_P...Kisha jiulize yy na UDI? . Inawezekana solution sio magari yaendayo kasi bali ni ufinyu wa barabara tulizonazo na nyingi kua na shortcut kibao hivyo kua na msongamano hasa katika Junctions. Wataalam wapo tatizo ni kuchukua mamlaka ya katiba yanatumika sehemu yoyote. Hii ni sawa na Mkunga wa Jadi awe Neurosergion.

Nakubaliana na wewe kuwa wataalam wapo lakini tatizo ni kuchukua mamlaka na kuyatumia sehemu yeyote; inanikumbusha uongozi wa National Institute of Transport ulipoondolewa kwa shinikizo la Yusuf Makamba simply because chuo kilitaka kutekeleza mradi ambao mkwe wake Makamba nae alikuwa na interest!!True story, Makamba alitumia influence yake na uongozi ukaondolewa to protect personal interests badala ya National interests-- ilikuwa enzi ya Mkapa wakati huo yuko Uswisi kwa matibabu!!
 
Back
Top Bottom