Kikwete face to face with Drogba

ibrah,unajua lunch ya watu kama 80 ni kiasi.hivi mnadhani hao watu wakienda ulaya wataitangaza tZ yetu ?how ?taifa stars wakienda Nigeria na kula lunch na raisi wao wataenda mahali kuitangaza nigeria na sio Tz ?mimi nina wasiwasi na hayo mawazo ambayo watu wanayo.lets wait n see lkn lunch kwa watu 80 na hali kama ya njaa na mafuriko sehemu mbali mbali..it doesnt make sense to me..na subirini akishashinda kwa kishindo mwisho wa mwaka..hiyo miaka mitano inayokuja mtaipata
 
Acha mawazo mgando wewe,unataka hela za walipa kodi zitumike kufanya nini? Wewe nyumbani kwako ukijiwa na mgeni unafanya nini?

Hii ni nchi bwana.

Tuliza boli uwanja mdogo, utapaisha bure!!

Hizo hela za walipa kodi zingetumika kuwapa hawa watoto madawati na kuwajengea madarasa sio kwenda kuzitumbua, unafikiria hawa wanafunzi wanafaidika na ujio wa kina Drogba?

Talking about mawazo mgando wewe unategemea hao wachezajiwa Ivory Coast wataitangaza Tanzania kisa wamepewa lunch na Rais, Na nchi yao nani ataitangaza?
9534_179942535338_747855338_4355325_7952301_n.jpg

shulembuyuuuuu[1].jpg
 
lakini wazee hatutegemei jeikei akaja kununua madawati huku kigoma,ndio maana kunakuwa na uongozi katika kila ngazi.

kunakuwa na allocations of funds kwenye kila idara,tatizo ni viongozi wote.

mbona obama kila siku tunamwona yupoo bize na watoto/familia yake mara ice-cream mara nini mara hivi na U.S inasonga mbele?
 
What about those who die of hunger in different places in TZ? and their beloved prezo is having good time throwing parties for Drogbas, what a shame this is?
 
What about those who die of hunger in different places in TZ? and their beloved prezo is having good time throwing parties for Drogbas, what a shame this is?

Nah, the president is doing his job:eek:... afterall the lunch imelipiwa na wanaoitakia mema nchi yetu:D baada ya kugundua chochote kinachofanywa na mawaziri huwa hakipewi uzito... Labda yule anayetumia mda wake kuongea na simu kwenye ATM wakati watu wamepanga foleni wakitumia mda wa kazi
 
What about those who die of hunger in different places in TZ? and their beloved prezo is having good time throwing parties for Drogbas, what a shame this is?
mama lao naona hapa unamix vitu viwili tofauti!
hizi njaa na umaskini wetu visitufanye tushindwe ukimarisha uhusiano wa kimataifa na nchi nyingine!
.......unajua ishu ya ndrogba ni zaidi ya futiboli!...
 
lakini wazee hatutegemei jeikei akaja kununua madawati huku kigoma,ndio maana kunakuwa na uongozi katika kila ngazi.
Angewaachia TFF na waziri wa michezo wawaandalie hiyo lunch lakini sio rais wa nchi.

kunakuwa na allocations of funds kwenye kila idara,tatizo ni viongozi wote.
Hehehehe ndio maana tumetenga bilioni saba za kampeni za kombe la dunia wakati tuna matatizo chungu nzima. Kwa kifupi hatujui kuzimanage hizo funds, tunaunguza funds zetu kwenye mambo ya mpito.

mbona obama kila siku tunamwona yupoo bize na watoto/familia yake mara ice-cream mara nini mara hivi na U.S inasonga mbele?
Umeshasema familia yake, Obama alivyompeleka mkewe NY kwenye Broadway show wananchi walimpigia makelele kama hawana akili nzuri.
 
Angewaachia TFF na waziri wa michezo wawaandalie hiyo lunch lakini sio rais wa nchi.


Hehehehe ndio maana tumetenga bilioni saba za kampeni za kombe la dunia wakati tuna matatizo chungu nzima. Kwa kifupi hatujui kuzimanage hizo funds, tunaunguza funds zetu kwenye mambo ya mpito.


Umeshasema familia yake, Obama alivyompeleka mkewe NY kwenye Broadway show wananchi walimpigia makelele kama hawana akili nzuri.
mkuu,
unasahau kwamba kuna kipindi ambacho hizi mechi za kimataifa TENA ZA KIRAFIKI zinakuwa involved na mambo ya SIASA!

AKIWA NYUMBANI J.K ALIPASWA KUFANYA HIVYO!enewei......
 
Hata mimi sioni tatizo kwa hilo alilolifanya Mr. President. Naona Mi-Tanzania mingine inataka kuwa michoyo hata kwa chakula
 
kuhusu kuwaalika chakula cha mchana sio mbaya na kama watu wanavyodai tumefuja hela sio mbaya vile kwenye gharama ya chakula na wapishi si walipa kodi kwahio wamelipwa na pia mchele ,nyama na vitu vingine vimenunuliwa kwenye masoko yetu kama mtu aliongezea cha juu sasa hio ni udokozi na ni swla tofauti kabisa.


turudi sasa kwa muheshimiwa rais ambaye kila siku ya mungu lazima aje na mpya na saa nyingine huwa najiuliza je kweli rais wetu ana watu wakumshauri na kama anao je ni wanao qualify hio kazi au ndio kubebana bebana tu kama tulivyozoea?


Nasema haya yote kwani kitu kikubwa kilicho nishangaza kwenye tukio hili ni muheshimiwa rais kitendo chake cha kuwabagua wachezaji wengine wa Ivory Coast na kwenda kuwapa jezi Drogba, Kalou, K. Toure, Y. Toure na E. Eboue. Hili swala sidhani kama rais alifanya tendo hili kupitia washauri bali alikurupuka tu kiushabiki na kibinafsi na kuwapa wachezaji hawa 5 jezi kwa vile ndio anawaona kwe runinga akiwa amepumzika weekend na sio kwamba kawapa hizi jezi kwa niaba ya watanzania yeye kama rais.

Kama ingekuwa kwa niaba ya watanzania basi wachezaji wote wa ivory coast wangepewa jezi ya timu yetu ya taifa. kitendo hichi ni cha kusikitisha sana na nategemea wahusika watajirekebisha siku nyingine kwani wote wale wachezaji wanafanikio makubwa na wanastahili kuheshimiwa kama hao wengine hawakuja hapa kushinda au nani bora wamekuja hapa kitimu na walitakiwa kuwajibishwa kwenye lolote lile. Kama JK alikuwa ana waona hao wa 5 bora angetafuta mda wake binafsi baada chakula wangekutana awape hizo jezi aliowaandalia.



Kosa la mwisho ni jezi za taifa letu kuandika majina ya hao (vimburu) wachezaji. Muheshimiwa rais jezi za taifa ni tofauti na za club, jezi ya taifa ni sawa na bendera ya nchi na kitendo cha kuandika majina yao ni sawa na kuandika jila la {drogba} (Drog the bar) kwenye bendera ya nchi yetu. Nadhani washauri wako hawakufanya uchambuzi zaidi na nichawashauri kwa vile lengo letu kubwa kuitangaza nchi yetu siku nyingine itakapokuja timu kama hivi ni vizuri jezi hizo za taifa muandike majina ya vivutio vyetu vya utalii nyuma badala ya kuandika majina ya hao wachezaji maarufu.kwa mfano hapo tungewapa wahezaji wote wa ivory coast jezi za taifa yenye majina tofauti hili kila mmoja wao atangaze nchi yetu popte waendapo.Badala kuandika Drogba mngeandika tu Serengeti, mt. Kilimanjaro ma kadhalika, hii ingesaidia sana kutangaza nchi yetu na ingekuwa wachezaji 25 badala ya 5.


hayo nimaoni yangu binafsi na tafadhalini kama ivory coast wakifika fainali haina haja kuwasafirisha watu kwenda kuishangilia tuwashangilie majumbani kwetu au kama kuna watanzania angola waende lakini tunaomba tusisikie delegation imetumwa Angola.kombe wakiataka kulileta mlima kilimanjaro walete ndio kutangaza kwenye na ndio nia yetu kubwa.


Ukiona rangi nyeusi jua nimeongeza chumvi Khe khe khe .


Huyo aliyo Magogoni ni lord loafer. Tena hapo umegonga msumari kunakohitajiwa.
 
Wadau, mimi sioni tatizo lolote kuhusu chakula alichowaandalia Ivory Coast maana Kiafrika hilo ni jambo la kawaida kabisa ya kuwa mgeni anakaribishwa na kupewa chakula kizuri kabisa kinachioweza kupatikana kwa mwenyeji wake. Huo ndiyo ukarimu wa Kitanzania.

Pili, nampongeza Rais kwa alichofanya, amewaonyesha wageni ukarimu wa Kitanzania hasa ukizingatia wachezaji wengi wa Ivory Coast wanatoka na kuishi Ulaya kwenye maisha ya kibinafsi na kichoyo, tena hata watu wa huko Afrika Magharibi wana tabia za ubinafsi-ubinafsi kwa hiyo hilo ni somo tosha kwa wageni wetu.

Tatu, si kweli kuwa kuna mabilioni ya shilingi yameteketea kwa gharama za kuandaa mlo mmoja, naamini hata mapato yaliyopatikana siku ya mechi yenyewe badi ni makubwa kulinganisha na gharama za chakula walichoandaliwa.

Nne Wa-Ivory Coast, kwa kutambua ukarimu wetu wameahidi kuwa iwapo watatwaa kombe la CAN basi watalileta Tanzania. Kwa hiyo, tumeweza kuwa-impact.

Mwsiho, pamoja na mapungufu yake nimegundua kuwa JK anajua sana PR na ndo maana huwa anapata favor ya ahadi za misaada anapotembelea ughaibuni ingawa kwa kweli misaada haitaweza kutusaidia sana iwapo hatutakaza buti dhidi ya ufisadi na kuhakikisha kinachopatikana kinafanya kazi iliyokusudiwa.

Mkuu,

Mimi sina tatizo na ukarimu wa mkuu tatizo langu hapa ni priority. Tuna watu kule kilombero wako katika hali ngumu ya kimaisha baada ya mafuriko lakini JK hajatia mguu huko. Je anaweza kusema hana nafasi? Muda alioutumia kuangalia mechi juzi ulikuwa unatosha kwenda kilombero kuwapa pole raia wake kule!!!!

Chakula kwa wafukuza gozi la ng'ombe ndio kipaumbele chake. It is very amazing!!!

Tiba
 
Mabilioni mangapi yametumika katika mlo huo? Nani kaidhinisha matumizi hayo kama hayakutoka mfukoni kwa Kikwete? Mwalimu asingefanya upuuzi kama huu. Kweli Rais tunaye! Pia anajua kujikomba sana, timu nzima akawape uzi wa Stars Drogba, Kolo Toure, Emmanuel Eboue, Solomon Kalou na Yaya Toure tu!
Kula ni kula mbaya kukomba mboga!Hata wewe ukipata nafasi kama hiyo utakula tuu tusidanganyane!Thidanganyikiiiii!!!!!
 
Back
Top Bottom