Kikwete chonde: Usitie sahihi mswada wa mfuko wa Jimbo

Huo mfuko hautakuwa na maana yoyote kwenye maendeleo na badala yake utatumika kuendeleza rushwa.

Pia nimeambiwa ni milioni 16 kwa mwaka ( sina uhakika asilimia 100) ambazo kwenye jimbo haziwezi kufanya mambo ya maana lakini zikipangiwa kazi nyingine kitaifa zinaweza kusaidia.

Itakuwa vizuri JK akikataa kuweka sahihi yake. Pamoja na credit crunch hii wao wanaendelea kuongeza gharama kwenye serikali.

Ni kweli kabisa tupo pamoja. Huu mfuko ni sawa na kubariki rushwa kwa style nyingine na isitoshe wabunge ambao mfuko huu utawakuta kwa maana utakuwa chini yao ndio utawazidisha ukiburi na ubabe na kuwabariki waendeleea kuwepo kwenye ubunge huo milele hata kama ni vilaza.

PLEASE IM BEGGING YOU DONT SIGN THIS, LET THEM BE CREATIVE WITHOUT THIS
 
Wabunge wanapata kiburi zaidi wanapoteuliwa kuwa MAWAZIRI. Piganieni KATIBA iwaondoe kwenye TEUZI hizi. Mfuko huu ni KITANZI kwa Wabunge watakaoufakamia.
 
Wanataka kupata ulaji mwingine,wanapitisha mambo ya ajabu kabla ya uchaguzi then baada ya uchaguzi wanayafuta. Mankumbuka mambo ya takrima? Wanataka kupitisha pesa iwasaidie uchaguzi. Taifa hili litajengwa na wenye moyo na litabomolewa na wenye..........................
 
Wakuu bado nasubiri kujua zaidi kuhusu huu muswada..
Mzee Mwanakjiji, mbona waniangusha mkuu wangu.. unajua tena mimi sina makubwa, sina ubishi ikiwa sifahamu kinachohusika zaidi.

Ila kuna moja tu, hivi mnataka utaratibu gani wa mgao wa fedha za maendeleo ya nchi yetu ufuatwe?..Kwa sababu kila napoangalia WATU tuliokuwa nao hakuna njia hata moja watu hawashindwa ktk ULAJI..Nadhani tatizo haswa ni utaratibu utakao tumika na kusema kweli mimi sifahamu ndio maana nimebakia mtazamaji jukwaani.
 
Hapa tunasubiri Kamati Teule au Tume za kufuatilia matumizi mabaya ya mfuko huu! Sasa sijui ile kazi ya kuisimamia Serikali itafanywa na nani kwa kuwa Bunge ndio linageuka kuwa chombo cha utendaji!
 
Hapa tunasubiri Kamati Teule au Tume za kufuatilia matumizi mabaya ya mfuko huu! Sasa sijui ile kazi ya kuisimamia Serikali itafanywa na nani kwa kuwa Bunge ndio linageuka kuwa chombo cha utendaji!
Sasa mkuu wangu bila mbunge kujihusisha na utendaji tutaweza vipi kusema mbunge fulani kaleta maendeleo, Hivi mbunge si ndiye mwakilisho wa matatizo yetu iweje yeye asiwe na nguvu ktk utekelezaji wa mahitaji yenu..Sii ndio yale ya Pinda kudai maendeleo ya Kigoma (barabara) imejengwa na CCM au kusema Mwakyembe hajapeleka maendeleo Kyela!

Kisha, ebu tujiuliza nchi nyingine hufanya vipi hivi?..Hivi kweli bado mnataka serikali kuu (Central Government) kuendesha utekelezaji wa maendeleo ya kila kata, wilaya, mkoa na hata jimbo zima..
 
Back
Top Bottom