Kikwete chonde chonde.....waziri wa fedha....

Sirikali hii haiangalii CV ya mtu, ina angalia ushahiba. Usishangae kuona Vicky Kamata anapewa ukuu wa wilaya au naibu waziri!
 
Mr. Arnold B. S. Kilewo
Mr. Arnold Kilewo (67) has been in public service for 29 years in senior management position.

A lawyer by profession, Mr. Arnold B. S. Kilewo holds an LLB Degree from the University of London.

AMP (Harvard) 1981.

Fellow, Institute of Directors (London).

He is presently an Independent consultant.


His past employment has been in the following institutions and positions:
Executive Managing Director, Tanzania Breweries Limited (1991-2004); Chairman and Managing Director, National Development Corporation (1977-1991);
Chairman, East African Airways Corporation (now defunct East African Community) (1973-1977);
Assistant Attorney General, Government of the United Republic of Tanzania (1972-1973);
Commissioner for Lands and Registrar of Buildings, Government of the United Republic of Tanzania (1970-1972); Director of the Bureau of East African Affairs, Ministry of Finance (1970);
Secretary to the National Bank of Commerce, Legal and Trustee Manager, NBC (1967-1970);
State Attorney, Attorney General Chambers (1965-1967).
Other Interests include Chairman of the Darbrew Ltd, Fedha Fund Ltd (supported by CDC, DANIDA, FINFUND, E.I.B NORFUND and SWEDFUND), Confederation of Tanzania Industries (CTI) and Stanbic Bank (Tanzania) Ltd.
 
ARNOLD KILEO 'THE SILENT GOLD-STAR TECHNOCRAT' NILIEPATA KUMFAHAMU:
HAJUI SIASA, HAJUI SURA YA MTU, ANAJUA NA KUHESHIMU 'TASK' NA KUFANYA MAMBO MAKUBWA SANA AKIPEWA NAFASI


Aliiokota TBL ikielekea jalalani na akaichukua, kaipangusa uchafu wote, kaipulizia dawa ya kuua wadudu wote walioajiriwa bora watu kazini, na TBL ikapata kusimama kwa miguu yake tena bila ya ufadhili toka kwa serikali.

Chini yake Mh Arnold Kileo, mtu wenye ueledi na makini kazini, TBL kampuni ambayo wakati fulani ilikua ikipumulia mashine ICU, mg'ao wake ukaja ukavuka mipaka ya nchi yetu na ukaja ukazidi ule mg'ao wa almasi. Jambo ambalo hadi kinapobinafsishwa, wawekezaji walikua wanakigombania ile mbaya.

Kwa kifupi, huyu ndiye Baba yetu, Arnold Kileo, niliyepata kumfahomu. Hakika, anao uwezo wa kufanya WONDERS akipewa uhuru zaidi ya KUREKEBISHA MIFUMO YOTE ya uchumi wetu, na wanasiasa wakazuiliwa kando kumuingilia pindi aingiapo kazini. Ni mpole sana mitaani, ni zaidi ya pilipili kazini - hivyo ndivyo wanavyosema waliopata kuwa karibu naye. Mbali na huyu baba, kama Mzee Utou, the 'silent gold-star technocrats wapo wengi' tu nchini wenye GREAT SELFLESSNESS but are most often POLITICALLY IN-CORRECT!!!

Mapendekezo kama hayo hayaninyimi furaha, vijana huenda tukapata ajira tena miaka mingi ijayo. Hata hivyo, wewe mpendekezaji, ulifikiria nini hadi ukafikia hapo??? Chukua TANO zangu TASLIM sasa hivi.
 
Anord Kilewo ni mbunge wa wapi?

MAVUVUZELA KUSHIKA NAFASI ZA UMMA SASA BASI:

Tanzania Tufike mahala tukawatumia ipasavyo watu wanaoitwa Technocrats (Wanataalum waliobobea sio tu katika Nadharia za fani zao Vyuo Vikuu bali hasa kwenye Kutenda kwenye uhalisia) kuipumulia Uchumi wetu hewa safi na Ajira zaidi tukapate.

Najua enyi mlioko serikalini miaka yote huwa HASIKILIZI hata siku moja maneno ya Mpiganaji Mwanamuziki wa Bongo Flava Mhe 20 Percent na Mhe Prof J. Laiti mngekua mnawasikiliza kwa makini wenzetu hawa, yale yote wanayoyasema ndio hali halisi inayotukumba na Umasikini unavyotung'ata mpaka kuonekana KITUKO mbele za 'Waungwana Mafisadi' wachahe.

Uzoefu unaonyesha kwamba siku zote Technocrats ni watu ambao hawajui kitu Siasa. Hivyo inakua rahisi sana kushinwa ubunge hata na 'Prof' Maji Marefu aingie bungeni na dhahabu kama hiyo tukaitupa jalalani bila huruma. Hivyo, sala zangu zinasema kwamba siku za usoni viongozi waje wafikirie kutumia nafasi za UBUNGE VITI MAALUM na UBUNGE NAFASI KUMI za Raisi kuteua na kuingiza bungeni TECHNOCRATS na wao kushika UWAZIRI kwa misingi ya taaluma zao ZILIKOTUKUKIA huku uraiani kwetu.

Kwa jinsi hii nao Ma-Professora HAWATAENDELEA kutoroka ualimu VYUO VIKUU kukimbilia siasa tu!! Watajitahidi sana mitaani ili nao wapate kung'ara katika taaluma zao na kuchangia japo kidogo tu KUTUFANYIA ULIMWENGU kuwa mahali pazuri pa kuishi.

Hata hivyo msijali Ma-TECHNOCRATS wetu msiokua POLITICALLY CORRECT, si mbali sana hili tutaliingiza katika KATIBA MPYA na kuelekeza VIGEZO nani awe Waziri au nafasi gani na STRICTLY apatikane vipi kisha kuelekeza mle Jinsi na vipindi vya kuwafanyia PERFORMANCE APPRAISAL. UWAZIRI, Ukatibu Mkuu au nafasi nyinginezo nyeti kwa MAVUVUZELA SWAHIBA sasa basi!!!!
 
TBL si ili rekebishwa na makaburu?
by the way sera za Kileo na JK ziko sawa? labda wahisani wamtake ndio atapata,
 
40 kuunda baraza jipya la mawaziri
BARAZA jipya la mawaziri linalotarajiwa kutangazwa wiki hii na Rais Jakaya Kikwete linatarajiwa kuwa na mawaziri kati ya 40 na 45, kati yao 23 wakiwa ni mawaziri kamili.Kwa maana hiyo, baraza hilo litakuwa na wizara 23 tu, Mwananchi imedokezwa.Habari ambazo Mwananchin imezipata zinaeleza kuwa katika baraza hilo jipya, ambalo litakuwa la tatu kwa Rais Kikwete tangu alipoingia Ikulu mwaka 2005, waliokuwa manaibu waziri watano katika baraza lililopita, watapandishwa na kuwa mawaziri kamili.

Vyanzo vyetu vya kuaminika vimeeleza kuwa idadi ya mawaziri wanawake itaongezeka kulinganishwa na baraza lililopita na kwamba uteuzi umezingatia umri, uzoefu pamoja na uwiano wa mikoa.Pamoja na kuwepo kwa sura mpya, idadi kubwa ya waliotajwa katika baraza hilo ni wanasiasa wakongwe ambao wengi wao walikuwamo katika baraza lililopita.
Chanzo chetu kimeeleza kuwa Rais Kikwete amekataa kuwapa nafasi ya uwaziri wabunge waliopata ushindi kwa kura chache katika uchaguzi mkuu uliopita.
Miongoni mwa wabunge waliokuwa manaibu kwenye baraza lililopita ni Emmanuel Nchimbi (Songea Mjini) ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Adamu Malima (Mkuranga) aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini na Christopher Chiza (Buyungu) ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji.
Wengine ni Dk David Mathayo (Same Magharibi) aliyekuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Ushirika pamoja na Balozi Khamis Kagasheki (Bukoba Mjini) aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani.

Habari hizo zinasema kuwa Wizara ya Fedha na Uchumi itaendelea kuwa na manaibu waziri wawili kama ilivyokuwa katika ngwe ya kwanza ya miaka mitano ya serikali ya Rais Kikwete.
Mbali na wabunge 27 waliotajwa na gazeti hili jana wengine ambao wametajwa kuwemo kwenye serikali mpya ya Rais Kikwete ni Muhammed Seif Khatibu kutoka Jimbo la Uzini ambaye alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Stephen Wasira(Bunda) aliyekuwa Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, na Hawa Ghasia (Mtwara Vijijini) aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma.

Wengine ni Mustapha Mkulo (Kilosa) aliyekuwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Mathias Chikawe (Nachingwea) aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria pamoja na Aggrey Mwanri (Siha) aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, (Tamisemi).
Wengine ni Bernard Membe (Mtama) ambaye katika serikali iliyopita alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Kimataifa na Emmanuel Nchimbi (Songea Mjini) ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Mawaziri wengine waliokuwa katika Serikali iliyopita wanaotajwa kurejeshwa katika kipindi hiki cha mwisho cha utawala wa Kikwete ni Ezikeil Maige (Msalala) ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, William Ngeleja (Sengerema) aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, na Celina Kombani (Ulanga Mashariki) ambaye alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi),
Wengine ni Profesa Juma Kapuya (Urambo Magharibi), aliyekuwa Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana, Profesa Mark Mwandosya (Rungwe Mashariki), ambaye alikuwa Waziri Maji na Umwagiliaji, Dk Hussein Mwinyi (Kwahani), aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Shukuru Kawambwa (Bagamoyo), aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na John Magufuli (Chato) ambaye alikuwa Waziri wa Maendeleo Mifugo na Uvuvi.

Wabunge wanaotajwa kuingia katika baraza la mawaziri kwa mara ya kwanza ni Anna Tibaijuka (Muleba Kusini), Samuel Sitta (Urambo Mashariki) na ambaye alikuwa spika wa Bunge la Tisa, Dk Harrison Mwakyembe (Kyela), Anne Kilango (Same Mashariki).
Wengine ni Januari Makamba (Bumbuli) ambaye alikuwa msaidizi wa rais katika awamu ya kwanza ya utawala wa Rais Kikwete, Salehe Pamba (Pangani), Steven Masele (Shinyanga Mjini), Gerson Lwenge (Njombe Magharibi) na Nyambari Nyangwine (Tarime).

Wengine ni Shamsi Vuai Nahodha (mbunge kuteuliwa) na alikuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Angela Mkwizu (Viti Maalum) na Amos Makala (Mvomelo) ambaye ni Mweka Hazina wa CCM, Said Bwanamdogo (Chalinze), Lazaro Nyarandu (Singinda Kaskazini) na Zakia Meghji (wa kuteuliwa).
Chanzo hicho kimebainisha kuwa Rais Kikwete amedhamiria kuunda baraza dogo la mawaziri litakalo kuwa na tija ikilinganishwa na alilounda wakati akiingia madarakani mwaka 2005, ambalo lilikuwa na mawaziri wapatao 60 na ambalo alilivunja Februari 2008 baada ya Edward Lowassa kujiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu.

Lowassa alijiuzulu kutokana na kashfa ya zabuni tata ya ufuaji umeme wa dharura iliyotolewa kwa kampuni ya Richmond.
Hata hivyo, baraza jipya aliloliunda baadaye chini ya Waziri Mkuu mpya, Mizengo Pinda lilikuwa na mawaziri 27 na manaibu mawaziri 21.
Kati ya mawaziri ambao hawatarajiwi kurejea kwenye baraza jipya ni wale walioanguka katika mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM na wengine waliangushwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31, mwaka huu.
Akilihutubia Bunge Alhamisi iliyopita, Kikwete alidokeza kuunda serikali itakayokuwa na watu waadilifu, makini na wachapakazi hodari.
Pia alisema ataunda serikali ya watu wachache ambao wataondoa urasimu watakaokuwa karibu na wananchi na kushirikiana vizuri na wabunge wote bila kujali vyama vya siasa wanavyotoka.

Kuna habari zinasema Membe kupewa Wizara wa Fedha na nafasi yake kuchukuliwa na Mbunge wa Bumbuli January Makamba. Pia Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa zamani Mh Edward Lowassa kurudi katika baraza jipya na kushika Wizara Ya serikali za mitaa.
 
Mh! Huyu mzee waliwahi kuwa pale NDC tena akiwa Managing Director na Chairman wa Board, hana jipya alilofanya zaidi ya kuajiri wachaga tu, alipelekwa TBL ilifanya vizuri kulikuwa na damu mbili za watanzania na kaburu, hana jipya
 
Hivi ni mbunge wa wapi?Lengo ni kuona kama anaweza kuteuliwa kuwa mbunge katika zile nafasi kumi za rais ili baadae amchague kwenye baraza lake,
 
Nafamu Kikwete ana watu wake anaowapenda....
na nafahamu ninachojaribu kukisema hapa probably hakitamfikia....

but kama kuna watu humu mnaweza mfikia Kikwete nawaombeni chonde chonde
kwa maslahi ya nchi mshaurini amchague ARNOLD KILEO kuwa waziri wa fedha na uchumi................


wale ambao hamjui cv ya arnold kileo tafadhalini muitafute

Tanzania hii hakuna mtu better na more qualified to run the economy zaidi ya ARNOLD KILEO


Mtoa maoni hapo umekosea hata kama ni mawazo yako,
watu wako tena vijana, tatizo ni mfumo mbovu uliokuwepo nchini,
Mtu ambaye anafaa katika position fulan hapewi nafasi, wanapewa watu fulani ili waweze kuruburuzwa.
 
TBL ni ya makaburu period. msipoteze muda kudhani kuwa kuna Mtanzania kasaidia ipate maendeleo
 
Hacheni utani kwa mambo ya msingi. Hakuna jambo Ninavyofahamu mimi Mzee wa watu yeye fani yake ni sheria na ametumia mda wake mwingikwenye mashika ya kibiashara. Historia hiyo haimpi uhalali wowote wakufikiriwa ya kuwa anaweza akawa waziri wa fedha mzuri kuliko vijana wanao chipukia.
 
Mwacheni huyu mzee apumzike sasa tutamwua bure. Najua yuko principled na ndiyo maana TBL mpaka sasa haijatetereka.
 
Mbona unampigia chepuo hivyo huyo kileo! Mchaga ni mchaga tu ukimpa pesa unategemea nini. Ndo yaleyale ya mramba kutenga mabilioni ya shilingi kujenga barabara ya Tarakea-Rombo na kuacha barabara muhimu zilizokua na tija kwa uchumi wa taifa.. Isitoshe kikwete alishashe uwaziri hausomewi mahali popote pale na hakuna chuo kinachofundisha uwaziri.
 
Nafamu Kikwete ana watu wake anaowapenda....
na nafahamu ninachojaribu kukisema hapa probably hakitamfikia....

but kama kuna watu humu mnaweza mfikia Kikwete nawaombeni chonde chonde
kwa maslahi ya nchi mshaurini amchague ARNOLD KILEO kuwa waziri wa fedha na uchumi................


wale ambao hamjui cv ya arnold kileo tafadhalini muitafute

Tanzania hii hakuna mtu better na more qualified to run the economy zaidi ya ARNOLD KILEO

Hivi mwanafunzi anaweza kupima uwezo wa juu wa mwalimu wake???? wewe kama nani uweze kum muevaluate mtu alafu nawe mwenyewe usiwe na sifa hizo. kakutuma??????? Mwacheni Kikwete ajichagulie watu wake. Msubilini sraa ili mumshauri. Tena ni ajabu iliyoje, wewe kutwa unamtukana kikwete kwa maneno kunya alafu unaleta ushauri leo, umerogwa!!!!!!!!!!!!11 teheeeeeee
 
Hahaahah, ni kweli ni mzuri. je ulimuandalia mazingira? sio watu wengine wapigie sisi emu halafu wewe upendekeze mtu wako. je waliompigia wakiacha nao kuipigia kwa sababu watu wao hawakuchaguliwa. nyumba ni msingi ndugu yangu. ninaamini siasa iko ivyo dunia nzima, ila ninamkubali sana Kileo isipokuwa haukumjengea mazingira tujifunze kukubali ukweli
 
Nafamu Kikwete ana watu wake anaowapenda....
na nafahamu ninachojaribu kukisema hapa probably hakitamfikia....

but kama kuna watu humu mnaweza mfikia Kikwete nawaombeni chonde chonde
kwa maslahi ya nchi mshaurini amchague ARNOLD KILEO kuwa waziri wa fedha na uchumi................


wale ambao hamjui cv ya arnold kileo tafadhalini muitafute

Tanzania hii hakuna mtu better na more qualified to run the economy zaidi ya ARNOLD KILEO

Baraza si kuchagua tu bali je unaweza kuli handle?, nafikiri kila mtu anaangalia mtu ambaye anaweza kumgeuzageuza na kumbinua atakavyo kwa jinsi anavyoona inafaa. JK nae ana vigezo vyake ikiwemo kufukia na kuficha uoza wake. So ni lazima amchague mshikaji.
 
Kwani naye yumo kwenye mtandao? Kama hayupo usipoteze muda kuota
Tena asipoteze muda kwani yeye sio Mbunge wa Kuchaguliwa wala la katika wale wanaochaguliwa na Rais. hata hivyo baraza limeshatangazwa ingwawa ha pa JF wanaweza endelea kujadili hii thread.
 
Back
Top Bottom