Kikwete, bilioni 50 za uchaguzi zingenunua vitanda vya wazazi vingapi?

Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,359
692
Miaka zaidi ya 40 ya uhuru bado wagonjwa na akina mama waliojifungua wanakaa chini kwa ukosefu wa vitanda. CCM mnajivunia nini ktk hali kama hii?? Hamuoni aibu mnapokwenda kutibiwa nchi za watu na mkaketi na kulala kwenye vitanda vya maana???

Mwananyamala.jpg
Picha hii ni akina mama waliojifungua wakiwa wamekaa chini kutokana na ukosefu wa vitanda hospitalini hapo.

Huu ni mwaka wa kutoipigia kura CCM na tuchague vyama vingine.....hasa CHADEMA inaonekana kuwa na mwelekeo.
 
Wapinzani wana hoja nyingi na nzuri tu za kuiondoa CCM madarakani. Wakitengeneza documentaries za mambo kama haya wakayatolea maelezo mazuri Watanzania watawaelewa kuliko kila kukicha wanaanzisha vyama vipya. Zipo shule za msingi mbavu za mbwa, mahakama za mwanzo magofu, vituo vya polisi majalala, barabara za vijijini mahandaki, mazao ya wakulima yasiyo na soko, ukosefu mkubwa wa ajira, uhaba wa walimu mashuleni, sekondari zisizo na maabara wala maktaba,........
 
Wapinzani wana hoja nyingi na nzuri tu za kuiondoa CCM madarakani. Wakitengeneza documentaries za mambo kama haya wakayatolea maelezo mazuri Watanzania watawaelewa kuliko kila kukicha wanaanzisha vyama vipya. Zipo shule za msingi mbavu za mbwa, mahakama za mwanzo magofu, vituo vya polisi majalala, barabara za vijijini mahandaki, mazao ya wakulima yasiyo na soko, ukosefu mkubwa wa ajira, uhaba wa walimu mashuleni, sekondari zisizo na maabara wala maktaba,........

Mkuu mimi pia nashangaa kwa nini vyama hivi watengeneze documentaries ambazo zinaonyesha hali halisi ya mambo yalivyo na kuzitumia ktk mikutano yao?? Na nakumbuka tumewashauri sana kuhusu hilo lakini haliwaingii akilini.
 
Halafu wanachangishana mabilioni kwa ajili ya ulaji wa uchaguzi. Kwanini tuwachangue watu kama hawa? Hivi hizi picha wanaziona? Hivi JK hajui haya? Huko kwenye NEC yao hawaongei hoja za wananchi? Na bado wanakuja na slogans kama za 'Maisha Bora kwa Kila Mtanzania' na bado tunawapa kura. This time lets say NO to CCM by all means.
 
Kweli una magezi (akili), bandugu ndio tujue ya kwamba CCM ipo kwa maslahi yao tu. Hivi hawakuona umuhimu wa kuita harambee ya vitu kama:

1. Ununuaji wa vitanda mahospitalini.
2. Uboreshaji wa zahanati hasa za vijijini.

* Wao wameona umuhimu ni kuita harambee ya kuchangia CCM ishinde lakini vitu vingine muhimu zaidi ya hio billioni 50 hawaoni ??

HII INA MAANISHA CCM YA HIVI SASA KIPAUMBELE NI HELA TU HAMNA KINGINE, ACHA WATU WAFE KWA NJAA, MONEY IS EVERYTHING. ''THIS IS TOO BAD'' NA MWALIMU SAID '' OGOPENI MASKINI AKISHA KATA TAMAA''....... THIS IS HOW AND WHERE WE ARE NOW.
 
Ndio mafanikio yenyewe hayo wanayoanza kuytapigia debe mawaziri kaika ziara zao wanazotaka kuzianza. Mweeeee nji hiii!!!!!!!
 
Magezi uko sahihi kabisa lakini tufanyeje au tupitie njia gani tuweze kufanikiwa wako watu ambao kwao hilo hawalioni kama tatatizo na ndio wengi wa wapiga kura.
 
May be i am crazy lakini jamani hizi hela wanachanga wanachama na wapenzi wa ccm kwa madhumuni maalum. Hizi siyo pesa za kikwete hivyo kuhusisha mambo ya vitanda haina mantiki
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom