Kikwete azomewa Mbulu

Sir R

JF-Expert Member
Oct 23, 2009
2,175
298
Watu walihudhuria mkutano wa JK katika jimbo la Mbulu leo 17/09/2010, walimzomea mgombea huyu baada ya kuanza kuisemea Chadema vibaya. Walianza kwa kupiga miluzi huku wakiondoka katika mkutano huo wakati JK akihutubia. Polisi walijitahitahidi kuzui watu lakini hawakufanikiwa.

Hali hiyo ni mwendelezo wa wa zomea zomea inayoikumba mikutano ya CCM katika jimbo hilo la Mbulu. Akiwa Haydom Mgombea wa ccm Philip Marmo alizomewa na kuachwa huku DC akiamuru polisi kuzuia watu waliohudhuria wasiondoke lakini ilishindikana.
 
Watu walihudhuria mkutano wa JK katika jimbo la Mbulu, walimzomea mgombea huyu baada ya kuanza kuisemea Chadema vibaya. Walianza kwa kupiga miluzi huku wakiondoka katika mkutano huo wakati JK akihutubia. Polisi walijitahitahidi kuzui watu lakini hawakufanikiwa.

Hali hiyo ni mwendelezo wa wa zomea zomea inayoikumba mikutano ya CCM katika jimbo hilo la Mbulu. Akiwa Haydom Mgombea wa ccm Philip Marmo alizomewa na kuachwa huku DC akiamuru polisi kuzuia watu waliohudhuria wasiondoke lakini ilishindikana.

Hawakutafutwa watu wa kusombwa kwa mabasi, kupewa sh 5,000 kila mmoja na kuambiwa wasizomee?
 
Hawakutafutwa watu wa kusombwa kwa mabasi, kupewa sh 5,000 kila mmoja na kuambiwa wasizomee?

pesa wamekula na kuzomea wanazomea tu kama hawana akili. Hawa watanzania wa mwaka 2005-2010 wananifurahisha sana.

Watanzania wamegundua kuwa Kikwete na majambazi wenzake wanawayeyusha tu... na kuanzia kipindi kile cha zomea zomea ya Zitto. Siku hizi jamaa hawana simile.

VIDEO please kama kuna mtu anayo
 
Marmo ataondoka; confirm pls nahitaji hii faraja hili jama silitakiga kabisa ktk serikali lakini maamuzi yako kwa wananchi
 
Hawaampeni vizuri kutafutwa watu wa kusombwa kwa mabasi, kupewa sh 5,000 kila mmoja na kuambiwa wasizomee?

Wambulu ( Wairaque)wakishakugeuzia mgongo huwa ni vigumu kuwashawishi hata kwa fedha, Walishawahi kumfundisha Mwl Nyerere maana ya democracy. Enzi hizo Nyerere alimpenda chief Dodoo awe mgombea wa ubunge wa jimbo la Mbulu, akamkampeni vizuri, wakamwitikia ndio lakini alipoondoka, Wairaque hao wakamchagua chief Sarwat kuwa mbunge wao. Nyerere akasema hii ni demokrasia ya kweli. Ikabidhi akubaliane na maamuzi ya wairaque hao.

Hivyo pesa siyo kitu. Wazee wanafanya sala zao za asili kumwombea Dr Slaa.
 
Ama kwa hakika nafarijika sana kuona wananchi elimu ya uraia imewaingia vizuri. Watu wamechoka, watu wananjaa, watu wanahasira na maisha na umasikini wa kutupwa then nyie mwaleta mbwembwe za kutembea na msululu wa wasanii mamluki wanaoimba wasichokitenda. Nafarijika sana kuona wananchi wakiwa na kiu na shauku kubwa ya kufanya mabadiliko ya uongozi wa nchi. Hayaa shime watanzania wenzngu tufanye kweli mwaka huu tumpe shoka na sululu Dr. Slaa kung'oa mizizi yote ya ufisadi na ujangiri unaofanywa na hao wa kijani. Mzomeeni huyo kwa bidii zote, nyie ndiyo wapinzani wa kweli.
 
Watu walihudhuria mkutano wa JK katika jimbo la Mbulu leo 17/09/2010, walimzomea mgombea huyu baada ya kuanza kuisemea Chadema vibaya. Walianza kwa kupiga miluzi huku wakiondoka katika mkutano huo wakati JK akihutubia. Polisi walijitahitahidi kuzui watu lakini hawakufanikiwa.

Hali hiyo ni mwendelezo wa wa zomea zomea inayoikumba mikutano ya CCM katika jimbo hilo la Mbulu. Akiwa Haydom Mgombea wa ccm Philip Marmo alizomewa na kuachwa huku DC akiamuru polisi kuzuia watu waliohudhuria wasiondoke lakini ilishindikana.

Jamani tunaweza vipi pata hizo video clip tutengeneza TV ADVERT kuwaonesha wananchi hali halisi ya wazalendo wa kweli
 
Marmo ataondoka; confirm pls nahitaji hii faraja hili jama silitakiga kabisa ktk serikali lakini maamuzi yako kwa wananchi

Kwa kukuhakishia Marmo kuondoka Mbulu, wananchi wengi wana hasira naye kwani aliwambia hatawasipompigia kura atashinda, alisema hayo wakati wa kura za maoni, inasemakana Marmo alishindwa katika kura ya maoni na Ndg Lori lakini akafanya maarifa zake. Walikuwa wanamuunga mkono Lori (mshindwa) wameamua kumkampenia mgombea wa Chadema Ndg Mustapher Akonaay. Na juzi alipokuwa anazindua kampeni yake Mustapher alipata mapokezi makubwa ukilinganisha na Marmo.

Vile vile mijadala imeibuka katika maeneo mbalimbali kuwa mwaka huu Chadema wapewe nafasi kwani CCM na Marmo wamepewa muda wakutosha lakini hawakufanikiwa kuleta maendeleo.

Pia wairaque wanasema wenzao wa Karatu kama waliweza nao pia wanaweza kufanya mabadiliko ya uongozi ambao utaleta maendeleo.

Marmo hali yake ni mbaya kisiasa kwa vile Upepo wa Dr Slaa unavuma sana kiasi cha kuwavuta wengi katika maeneo ya Mbulu, kwani wengi wanamfahamu Dr Slaa vizuri.

Kitu kingine kinachomfanya Marmo kukosa mvuto wa kisiasa ni kwa vile amekaa kwenye nafasi hiyo muda mrefu ( miaka 25) Watu wanataka mabadiliko
 
Marmo pole - lakini huenda ukapewa UDC au nafasi nyingine ya namna hiyo kukupoza.
 
asante sana Sir R, kwa hii update

Ahsante Mkuu,

CCM hofu yao ni kubwa zaidi maeneo ya Dongobesh kwani maeneo hayo Marmo anakosa kabisa nguvu ya kufanya kampeni; Sababu kubwa Chadema imeshikilia maeneo hayo tangu 2005.
 
Hii ni dalili ya watu kuchoka, mishipa ya damu ya CCM inaendeshwa kwa nguvu ya pesa, uhai wa wanachama wake kwa miaka miwili ijayo utategemea pesa zaidi ya mapenzi. Tabia hii inakuzwa na viongozi wenyewe, siku hizi mwanachama hawezi kuhudhuria mkutano bila kupewa pesa na kuhakikishiwa usafiri wa kwenda na kurudi, chama hakiendeshwi hivyo hiyo ni dalili mbaya kwa uhai wa chama.

Hata kama chama kina uwezo kiasi gani ni vizuri mwanachama wa chini akashirikishwa kukichangia,tunaona kwenye mikutano ya Chadema huwa wanapita na vikofia kichangishana hiyo si kuwa wanatemea sana pesa hiyo ili waendeshe chama kwa vile sidhani kama huwa wanapata kiasi kikubwa lakini hata kama mtu atatoa sh.200 bado atajiona ni mmoja wao.

Tunaona hata vyama vya ulaya pamoja na utajiri wao kama Democrats, Reps, Conservative, Labor nk lakini bado huwa vinapitisha bakuli kwa wanachama wake. Nionavyo mimi CCM inajiua yenyewe, ninavyosema hivyo si kwamba itakufa mwaka huu lakini haina muda mrefu.
 
Jamani tunaomba picha na video. Pia nawashauri wananchi watumie hata hizi simu za kichina kurekodi matukio kama haya. Mungu awabariki ndugu zetu Wairaque, Mungu ibariki Tanzania!
BTW nasikia hawa wambulu walihamia Tanzania karne zilizopita kutoka eneo linalojulikana kama Ethiopia - enzi hizo ilikuwa Abyssinia, the land of His Majesty Haile Selassie. Kama ni hivyo basi hao kweli ni maJah people na hawataki ujinga... RESPECT :smile-big:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom