Elections 2010 Kikwete awateua Meghji na Nahodha ubunge

Sasa huyu kumtoa kwenye taaluma ya ufundishaji na kumleta kwenye SIASA ni matumizi mazuri kweli ya Rasilimali watu?
Mkuu tazama list hii
1. Dkt Mwakyembe
2. Prof. Kapuya
3. Prof. Mwandosya
4. Prof. Maghembe
5. Prof. Msolla
5. Dkt. Burian
6. Dkt. Shein
7. Dkt Bilal
8. Prof. Lipumba
9. Dkt. Slaa
10. Prof. Mwakyusa
11. Prof. Mwalyosi
12. Prof. Tibaijuka
13. Dkt. Ishengoma
14. Dkt. Migiro
15. Dkt. Kawambwa
16. Dkt. Magufuli
17. Dkt. Mwinyi
18. Dkt. Wanyancha
19. Dkt. Lucy Nkya
20. Dkt. Chami
.........
.........
.........

HAWA BWANA WANAKIMBIA NJAA HUKO VYUONI WALIKOKUWA WANAFUNDISHA AU WANAKOSTAHILI KWENDA KUFUNDISHA KASORO WA 9. HUYU NI MTUMISHI WA KWELI WA WANANCHI
 
Ni vibaya sana kuzungumza bila kuwa na ufahamu mzuri, Labda watu wafahamu kwamba, Rais ana nafasi 10 za uteuzi. Katika hizo 7 ni Bara na 3 ni kwa visiwani. na tunafahamu kwa akili ya kawaida tu kwamba, huwezi kuteua Mkrito toka zanzibar, kwa hiyo hakuna udini kwa hapo. ni geographical and cultural reason ndio imekuwa hivyo. nafasi 7 za bara ndio tusubiri na ndio za kujadili kama kuna huo uwiano wa kujadili.

Kama tukitaka kujadili hivyo basi tujiulize, kwa nini Nafasi za viti maalum vya Chadema karibu vingi vinatoka North? vipi wao kuhusu Muungano? au na wao wapo agaist na uislamu na kwa hivyo huwezi kuona mzanzibari katika viti hivyo zaidi ya 20? lakini najua kutakuwa na sababu za msingi juu ya hilo. lakini nani kaliezea kwa ufasaha. Chadema ijipange vizuri watanzania wanahitaji mabadiliko lakini yasiyokuwa na shaka.

Nawasilisha
 
Nahodha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na mama mkwe "jikoni kumtayarishia babamkwe mahanjumati". Tehe-tehe-tehe!
 
Ni vibaya sana kuzungumza bila kuwa na ufahamu mzuri, Labda watu wafahamu kwamba, Rais ana nafasi 10 za uteuzi. Katika hizo 7 ni Bara na 3 ni kwa visiwani. na tunafahamu kwa akili ya kawaida tu kwamba, huwezi kuteua Mkrito toka zanzibar, kwa hiyo hakuna udini kwa hapo. ni geographical and cultural reason ndio imekuwa hivyo. nafasi 7 za bara ndio tusubiri na ndio za kujadili kama kuna huo uwiano wa kujadili.

Kama tukitaka kujadili hivyo basi tujiulize, kwa nini Nafasi za viti maalum vya Chadema karibu vingi vinatoka North? vipi wao kuhusu Muungano? au na wao wapo agaist na uislamu na kwa hivyo huwezi kuona mzanzibari katika viti hivyo zaidi ya 20? lakini najua kutakuwa na sababu za msingi juu ya hilo. lakini nani kaliezea kwa ufasaha. Chadema ijipange vizuri watanzania wanahitaji mabadiliko lakini yasiyokuwa na shaka.

Nawasilisha

Mizizi nakubalina na wewe katika aya yako ya kwanza ambayo umeeleza vizuri sana kuhusu uteuzi wa rais kwa wabunge watatu toka zanzibar na ninakubaliana nawe kabisa.
Hata hivyi paragraph ya pili mimi sikubalini na maelezo yako kwani yanapotosha hali halisi ya CHADEMA, na isingekuwa haki kufananisha uteuzi wa Kikwete na hali ya chadema

Kwanza chadema haina viti vingi maalum huko kanda ya kaskazini kama unavyotaka watu waamini, kama ilikuwa hivyo kwa miaka mitano iliypita ni tofauti na sasa, naomba upitie orodha ya CHADEMA special seats uone hao watu waligombea kupitia mikoa gani?
Kuhusu CHADEMA na muungano bado nafikiri huwatendei haki, tena mwaka huu CHADEMA waliweza hata kusimamisha wagombea ubunge zanzibar kwa bahati mbaya hawakuchaguliwa na hii inatokana na ukweli wa siaza za zanzibar hasa kutokana na historia ya vyama viwili vya CCM na CUF na kwa hiyo inakuwa vigumu sana kwa vyama vingine kupata nafasi huko,
Hata hivyo CHADEMA hawakuishia hapo kati ya viti 23 vya wabunge wananwake kuna viti si chini ya watatu wanatoka visiwani, kama ingekuwa kutojali Muungano CHADEMA si wangesema Zanzibar hawakuwapa kura na hivyo hakuna sababu ya kuteua toka huko? lakini wameteua ili kuimarisha Muungano na pia kuongeza ushawishi kwa wazanzibar? au ulitaka wafanye nini zaidi ya hivi walivyofanya?


Ingekuwa vema sana sana kabla hatujatupa lawama zetu tuwe tunafanya utafiti kidogo tu ili kujenga nchi yetu na si tu kutumia fikra zetu au hear say
 
Hao walochagulia ndo mawaziri watarajiwa.....:)
Hivi mbunge ambaye hakuchaguliwa na wananchi anaweza kuwa waziri .......... hii
si kupeana mlungula sasa. Ngoja tumsubirie Mramba basi arudi
 
CCM ya siku hizi nzuri sana;UKINUNA kidogo tu wanakupa ulaji ili usianzishe kundi lako,nawashauri na nyie akina Dr Mwakyembe na wenzenu ili muwe Mawaziri na nyie NUNENI na JK atawapeni nafasi!

Kwa mwaka 2010 alianza Dr Balal baada ya kutoswa kupata U-Rais wa ZNZ na CCM ya JK ikampa ulaji;Juzi katoswa Samwel Sitta kwenye U-Spika nina bashiri atapata ulaji;Dr Shein akamtosa Vuai Nahodha kwenye Baraza lake la juzi na kupoozwa kateuliwa UBUNGE na nabashiri tena anaweza pata Uwaziri!

Walioshindwa kura za maoni ndani ya CCM na hata walioshindwa Ubunge nao pia watapoozwa ili WASINUNE;wana CCM kama Raphael Chegeni au hata Lau Masha wanaweza rudi Bungeni au kuapata nyadhifa zingine;wanapewa nafasi ili WASINUNE!

KUNUNA ndiyo sifa kubwa hivi sasa kupata nafasi ndani ya CCM na wala sio utendaji wako;Mbunge wangu na wewe NUNA ili na sisi Kyela tupate WAZIRI!
 
Halisi,

Prof. Mbarawa aligombea kupitia chama kipi huko Mkanyageni? Nataka kujua kama ni CUF na hivyo kuwa matokeo ya muafaka.

Hi ni dalili kutokea Zanzibar hakuna wabunge wa maana
wa CCM wanaoweza kuwa mawaziri na hivyo kuanza
kuteua.

Pia kwa watu toka Zanzibar lazima tutegemee kwa asilimia karibu 100 watakuwa Waislam hivyo sidhani kama tunahitaji hata kujadili juu ya dini zao.

Mkuu Mtanzania habari za siku, Prof Mbarawa alikua mgombea wa CCM na alikua chaguo la Dr Bilal ambaye alitarajia angekua Makamu wa Pili wa Rais kama angekua Rais wa Zanzibar, na hivyo ni chaguo la Bilal ambaye sasa ni Makamu wa Rais wa Muungano. Mgombea wa CUF alikua Mohamed Habib Mnyaa.
 
- Well, kwa kweli kwenye siasa ni lazima ku-comment kwa chochote kinachotokea hasa wakati huu wa mwisho wa uchaguzi na hasa uchaguzi wa mwaka huu,

- However: my take ni kwamba huu uteuzi ni non-effect kwa taifa kwa sababu kwa wale mnaojua vizuri functions za wabunge na effect zao bungeni, Wabunge wa Viti Maalum na wabunge 10 wa kuteliwa na Rais huwa hawana nguvu kabisaa na hata Mawaziri huwa hawawasikilizi kabisaa.

- Otherwise, Mh. Nahodha akiwa Visiwani hakuharibu na amekua royal asiye na makundi, pia ni mchapa kazi kwa hiyo hapa naona akipewa u-Waziri wa Muungano. Mama Meghji, ameshiriki sana kwenye kampeni za majuzi na ni mtu wa karibu sana na "Kigogo" mmoja na yeye namuona akirudi Cabinet, huyo mwingine namuona akiwa mbunge tu!

- Ninaamini ni uteuzi wa kisiasa za Muungano zaidi kuliko 2015, ingawa kama Mama Meghji atarudi tena Cabinet, baada ya kuondoka kwa kashfa italeta maswali valid ya commitment ya uongozi wa hiii awamu kwa wananchi, hasa ukiheshimu matokeo ya uchaguzi ulioisha, siamini kwamba CCM watafanya makosa hayo, maana itakua ni kuanza kujichimbia mapema kaburi la 2015.

- CCM imefika mahali sasa ni lazima tuambiane ukweli tena bila kuogopana wala kuoneana haya hizi tabia za kuwazungusha viongozi wale wale na hasa walioharibu tayari na huku tukiacha vijana wengi waliochaguliwa majuzi tena wengi wao ni Ma-Doctors wa kweli, itakatisha tamaa sana, maana comes 2015 hawa vijana wataishia kuingia Upinzani kwa hili ninasema hivi iwapo tu huyu Mama atapewa tena U-Waziri, ni matumaini yangu kuwa Mwenyekiti wa CCM taifa ataheshimu matokeo ya uchaguzi wa majuzi na kumuacha huyu mama bungeni tu, au ikibidi kumpa nafasi hukooo kwenye mambo ya Muungano tu!

- Wananchi tumechoshwa na hawa viongozi walioharibu tayari, sasa wapewe wengine wapya, maana wapo wengi sana!



William.
 
JK kamchagua Zakhia Meghji....!!!!?? Mungu wangu..... as usual wanaoboronga wenye kashfa ndio CCM chaguo lao, imani yangu kwa JK is -ve 100%, JK what is up...? Zakhia, na kashfa zote juzi, juzi tu, alijiuzulu tena ww ukiwa Rais, eeeeeeeehhhh, aiseeeeeeeee, nangojea MADUDU ZAIDI, no dought, natabiri 100% i will be right, mwisho wa CCM 2015. Everyday watu tunashangaa vitu vya ajabu kabisa, DR Slaa ulisema na yanatimia kuichagua CCM ni MAAFA, mwenye, macho oneni, masikio sikieni, subirini MAAFA ZAIDI.
 
huyu mama aliniacha hoi bajeti yake ya kwanza,kama waziri wa fedha ikuwa mgogoro.......!
 
Kwanini mnamwita Meghji mama mkwe halafu hamsemi ukweli why you call her tht way? tujuzeni basi nasi tufahamu. Inamaana meghji ni mama yake salma kikwete?
 
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Wabunge watatu (3) kwa mujibu wa Ibara ya 66 (1) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, kama ilivyorekebishwa na kupewa mamlaka ya kuteua Wabunge 10.

Wabunge walioteuliwa ni Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa na Ndugu Zakia Hamdan Meghji.

Rais atateua wengine waliosalia siku zijazo.

Rais Kikwete ameshawasilisha majina ya wateule hao kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anne Semamba Makinda (Mb) kwa ajili ya hatua zipasazo.

MWISHO
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu.
Dodoma
17 Novemba, 2010
Kikwete anadhani watanzania ni wasahaulifu kiasi hiki? Huyu Zakia Meghji alihusika sana katika harakati za kumwingiza madarakani Kikwete mwaka 2005. Nakumbuka yeye na walioitwa "marafiki" zake walichangia kampeni za CCM mamilioni ya fedha. Pia alihusika kikamilifu katika kashfa ya EPA kwani wizi wote wa EPA ulifanikishwa yeye akiwa waziri wa fedha! Yaelekea sasa Kikwete anataka kulipa fadhila. Huu ni ushahidi kwamba CCM ya juzi ndiyo ya jana na kesho. Hakuna mabadiliko yoyote. Tunawaomba wanaharakati wenye uchungu wa kweli na nchi hii waliweke wazi hili ili wananchi wote wajue. Ikumbukwe kwamba ni huyuhuyu Zakia Meghji aliyepinga vikali uwepo wa wizi kule Benki kuu lakini ambayo baadae ilidhihirika wazi. Haiwezekani tuteuliwe waziri mwenye kila element za kifisadi tunyamaze tu.
 
Mama mkwe kaula au anakplipa fadhila cause hajatoa mahari!!!!!

Hahah imnamaana hujuhi wewe? MKWEWE WETU WAKWERE HUYO, kifupi mama MZAA CHEMA!
Bado tu hujahelewa?

Watu wazima mnakaa kwenye computer zenu kusema uongo...Zakia megji ana watoto wawili wa kike na wote wameshaolewa. Acheni uongo, udini na chuki bila msingi. Hongera Zakia, mchango wako bado unaitajika!!
 
Watu wazima mnakaa kwenye computer zenu kusema uongo...Zakia megji ana watoto wawili wa kike na wote wameshaolewa. Acheni uongo, udini na chuki bila msingi. Hongera Zakia, mchango wako bado unaitajika!!

Sipendi masuala ya imani yapewe kipaumbele katika kutathmini uongozi wa mtu, lakini kama mchango unaouongelea ndio ule uliopita, hapana ndugu, wengi wetu ulitukwaza....
 
Huu ni mwanzo wa kuwafahamu mawaziri wake wateule, ishu hapa ni kujua watapelekwa wizara gani, Mama mkwe wizara ya mali asili na Utalii.

Mama mkwe kaula au anakplipa fadhila cause hajatoa mahari!!!!!

ni mkwe wa rais

Hehehe mama mkwe! sasa JK atafanya lolote atakalo kwa shinikizo la mafisadi kwani hatarudi tena kwa wananchi kuwajibika after 5 years

Jamani, mwashangaa nini? Meghji ni "mama mkwe" wake JK? Au MUMESAHAU?

Ismase,

Ni Mama Mkwe wangu kwa yule mke wangu wa tatu

Weraaaaa weraaaaaa mama mkwe! Acha kodi za watanzania zilipe mahali!

Hahah imnamaana hujuhi wewe? MKWEWE WETU WAKWERE HUYO, kifupi mama MZAA CHEMA!
Bado tu hujahelewa?

Msijaribu kupotosha umma, huo ni uongo na ufisadi. Hivi mnapata raha gani mnaposema uongo?? Kwanini tunashindwa kujadidi issue na ukweli wenyewe. Tuwache udini na chiku zisizokua na msingi!!
 
Mke+mdogo+wa+Kikwete+2.jpg


:tape::tape::tape::tape::tape::tape::tape::tape::tape::tape::tape::tape::tape:
 
Back
Top Bottom