Kikwete awalinda Mawaziri - Asisitiza waachwe, UPEPO HUU UTAPITA!

Hivi hii serikali kweli inatupeleka wapi kweli Rais haya ni maneno yake?Eti huu ni upepo tu utapita tu
 
Jamani vipi kuhusu huyu CAG manake nae tusimsahau kamati ya bunge iliyochunguza suala la Jairo ilisema hafai aondolewe sasa naona kama amesahaulika, jamani vipi kuhusu huyu CAG nae anawajibikaje kwa issue ile ya Jairo?
 
Uko sahihi kabisa, Kama kweli mh. Pinda anaamini kuwa hao mawaziri wanatakiwa kung'oka na rais anagoma, kwa heshima yake inabidi yeye ajiuzuru ili raisi alazimike kuvunja baraza la mawaziri. Itakuwa ni heshima kubwa kwake.
kujiuzuru anaweza akawa anatamani lakini akawa hawezi. Pinda sio kama Lowasa, Lowasa anavitega uchumi vingi ukiachilia mbali siasa. Pinda yeye anategemea hela ya serikali kuishi. Viongozi wengi wa tanzania wana hili tatizo, vipato vyao vinatoka serikalini tu na hawana njia nyingine za kueleweka ku-make money. Na hili litaendelea kutuumiza, Pinda hawezi hata kumshinikiza Rais kuwatendea haki wananchi. Pia Pinda akijiuzuru usalama wake kipindi cha serikali ya kikwete utakuwa matatani, tofauti na Lowasa Lowasa ni jeuri na ana network kubwa kutosha kumuhakikishia usalama wake.
 
Nyerere alisema haya kwenye kitabu chake kuwa, kiongozi kazi yake kubwa ni kufanya maamuzi, tena maamuzi magumu kwa ngazi ya uongozi kama rais, akasisitiza kuwa ni bora ukafanya maamuzi ukalaumiwa kuliko kutokufanya maamuzi! Kikwete si riziki!
 
Hii nchi si ya jk wala ccm ni ya wananchi ndio wamemwajiri jk. Wananchi walipata raha na faraja kusikia kuna mawaziri watajizuru kumbe jk anawalinda kwa maslai binafsi. Huu ni upepo kwake kwetu ni kipunga. Wabunge wazalendo zile kura ziwe za kutokuwa na imani na raisi imejionyesha kwa pinda kuzarauliwa kwa mara ya pili. Hata mawazi wakijiuzuru atatafuta maswaiba wake watakaoficha maovu yake. Hatari kwa CAG na ripoti yake kuvunjwa nguvu kabisa maana ndio chanzo cha tatizo.
 


• ASISITIZA WAACHWE, UPEPO HUU UTAPITA

na Mwandishi wetu
WAKATI taarifa ya Kamati ya wabunge wa CCM chini ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, juzi iliridhia mawaziri wote wanaokabiliwa na tuhuma za ubadhirifu kwenye wizara zao wajiuzulu, jana Rais Jakaya Kikwete aliwasili nchini akitokea Brazil akiwa na msimamo tofauti.

Taarifa zinasema kumekuwa na mazungumzo baina ya Rais Kikwete na Pinda yaliyolenga kunusuru serikali yao lakini walitofautiana kuhusu hatua inayopaswa kuchukuliwa dhidi ya mawaziri waliotakiwa kujiuzulu.

Msimamo wa Pinda inadaiwa kuwa anataka mawaziri wanaokabiliwa na tuhuma waondoke ili kuleta uwajibikaji serikalini, lakini Rais Kikwete amesema mawaziri hao waachwe waendelee na kazi zao, kwa kuwa suala hili ni la upepo tu, liachwe litapita.


Tanzania Daima Jumapili limeelezwa kuwa rais anakataa shinikizo hilo kwa madai serikali haipaswi kuyumbishwa yumbishwa.


Miongoni mwa mawaziri wanaopaswa kuondoka ni Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo; Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Cyril Chami na naibu wake, Lazaro Nyalandu; Waziri wa Tawala wa Mikoa na Serikali za Mitaa, George Mkuchika na naibu wake, Aggrey Mwanri; Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda na naibu wake, Lucy Nkya na Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu.


Wengine ni Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige.


Habari zinasema Rais Kikwete na Pinda walitofautiana juu ya hatua dhidi ya mawaziri hao, hivyo kuwafanya baadhi ya mawaziri kutamba mitaani kuwa hawang’oki madarakani kwa sababu tayari bosi wao ameonyesha kutounga mkono tuhuma zinazoelekezwa kwao na wabunge wa upinzani na CCM.


Habari hizi zinasema pia kwamba Pinda amekuwa hafurahishwi na msimamo wa ‘bosi’ wake, hasa katika kushindwa kutoa uamuzi mgumu.


Zinadai kuwa rais amekuwa na tabia ya kuacha upepo uchukue nafasi yake wakati Pinda anataka baadhi ya watu wawajibike bila kujali nyadhifa zao au ukaribu na kiongozi mkuu wa nchi ili kurejesha imani ya serikali kwa wananchi.


Pinda inadaiwa amekuwa akitaka maamuzi magumu yafanyike, kwakuwa yeye ndiye anayesulubiwa na maswali pamoja na hoja za wabunge wawapo bungeni.


Baadhi ya wabunge waliozungumza na Tanzania Daima Jumapili, wameweka wazi kuwa kama Rais Kikwete ataamua kuwalinda na kuwatetea mawaziri wake basi watawaondoa kwa mkakati tofauti utakaomlazimisha rais kukubaliana na hoja za wabunge.


Baadhi ya wajumbe waliozungumza na gazeti hili waliweka wazi hatua hiyo inahitaji muda na mipango madhubuti na wao wapo tayari kufanya hivyo, kwani nchi inazidi kudidimia kwenye umaskini huku watu wake wakikosa huduma muhimu za kijamii.


Walisema kwa muda mrefu wamekuwa wakiwalalamikia watendaji wa serikali na chama tawala lakini rais amekuwa mgumu wa kuyashughulikia matatizo hayo.


Wanasema rais ndiye kikwazo kikubwa cha maendeleo ya chama chao na serikali, hasa kwa kuwateua mawaziri, wakurugenzi na maofisa wengine bila kuangalia uwezo wao wa kiutendaji.


“Kaka kwenye Bunge la Februari kuna mbunge alitoa kauli kuwa kama tunaona mambo hayaendi serikalini tupige kura ya kutokuwa na imani na rais, watu walimshambulia. Sasa tunaona umuhimu wa kauli yake ile,” alisema mbunge mmoja.


Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa makada wa CCM wameanza kuingiwa na hofu ya kubomoka kwa chama chao hasa baada ya makada wenzao kuanza kujiunga na vyama vya upinzani.


Wanasema wakati makada wa chama hicho wakiendelea kukihama uongozi wa CCM hauonekani kuchukua hatua zinazostahiki dhidi ya viongozi wanaochangia wananchi wakose imani na chama tawala.


Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe, aliweka wazi kuwa wabunge wa CCM ni lazima wakemee ubadhirifu kwakuwa Tanzania si mali ya CCM.


Mbunge huyo alikwenda mbali kwa kumtaja Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo, kuwa ni mwizi, mwongo na mbadhirifu wa mali za umma.


Mawaziri wasuasua kuwasilisha barua

Hadi jana Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema hajapokea barua ya kujiuzulu kutoka kwa waziri yeyote huku akiweka wazi kuwa kesho atatoa taarifa kamili juu ya jambo hilo.

Juzi vyombo vya habari vilipata taarifa kutoka kwenye kikao cha wabunge wa CCM kuwa baada ya wabunge kuzituhumu baadhi ya wizara kukithiri kwa ubadhirifu mawaziri wake wameamua kujiuzulu.


Taarifa hizo zilidokeza kuwa mawaziri hao walishinikizwa kuachia nyadhifa zao ili kukinusuru chama na serikali dhidi ya hasira za wananchi wanaokerwa na ufisadi.


Chami atoboa siri

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami, amejitetea kuwa wizara yake haimlindi Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Charles Ekelege, kama alivyotuhumiwa na baadhi ya wabunge.

Alisema amesononeshwa na taarifa ya ukaguzi wa CAG juu ya TBS iliyotolewa kwa waheshimiwa wabunge bila yeye mwenyewe au wizara kupewa nakala kwa kipindi cha wiki nzima.


Alisema kuwa baada ya kusikia kuwa waheshimiwa wabunge wengi wanayo taarifa hiyo na hata naibu wake kukiri bungeni kwamba taarifa imetoka wakati yeye hana nakala, alikwenda kwa Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashillilah na kuiomba nakala ya taarifa hiyo.


Alibainisha kuwa baada ya kufanya ufuatiliaji katika ofisi ya CAG ilikiri kuigawa kwa wabunge na kusahau kuipeleka kwa wizara hiyo ambayo ndiyo inayohusika.


“Hapa wasomaji wapime wenyewe. Inawezekanaje taarifa ya CAG iliyoandikwa kutokana na takwimu zilizotolewa na wizara yangu, iwafikie wabunge huku wizara yangu itakayotakiwa kuifanyia kazi taarifa yenyewe haipewi nakala, eti kwa kughafilika?


“Ni ukweli ofisi ya CAG walighafilikiwa, au jambo hili limesukwa ili kuniaibisha mimi mbele ya Watanzania, rais aliyeniteua na hasa wapiga kura wangu wa Moshi Vijijini?” alihoji.


Nundu ajitetea

Naye Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, alisema tuhuma dhidi yake zilizoelekezwa na baadhi ya wabunge, hazina ukweli na zimelenga kumchafua.

Alisema kilichoelezwa na Kamati ya Miundombinu ni uongo na uzushi, kwani nyaraka walizozitumia kuorodhesha tuhuma dhidi yake si halali.


Kuhusu kuingilia utendaji wa Mamlaka ya Bandari kwa masilahi binafsi, alisema si kweli, akaongeza kuwa kinachomponza ni kuipinga kampuni inayotetewa na menejimenti isipewe zabuni ya kufanya upembuzi yakinifu peke yake na kwenda kukopa na baadaye iruhusiwe kujenga gati namba 13 na 14.


“Wanasema namtaka mwekezaji ambaye makubaliano yanaonyesha atamiliki gati hilo kwa miaka 45. Nachelea kusema ni uongo na uzushi,” alisema Nundu.


Mkuchika apata kigugumizi

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika, alipoulizwa juu ya suala hilo alishindwa kukubali wala kukataa iwapo ataandika barua ya kujiuzulu. Alimtaka mwandishi amuulize Katibu wa Kamati ya Uongozi

Kikwete has nothing too loose in 2015 but CCM has something to loose. Tunakushukuru JK, na endelea hivyo hivyo kutupa CHADEMA ajenda nyingine zakuing'oa ccm. Uligoma la madaktari, la kumvua Lema,nk.
 
inadhihirisha tatizo ni JK. Nadhan itakuwa busara kama zile sahihi 70 zitageuzwa kudeal naye bungeni. Tunataka UWAJIBIKAJI na si kulindana


Bunge laweza
kumshtaki Rais
Sheria ya 1992
Na.20 ib.8
Sheria ya 1995
Na.12 ib.4
4 6A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii,
Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani
endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa
mujibu wa masharti ya ibara hii.
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja
yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama
inadaiwa kwamba RaisSheria ya ….
(a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja
Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili
yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa
yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba, au
(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais
wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya
namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja
kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.
(3) Bunge halitapitisha hoja ya kumshtaki Rais isipokuwa tu
kama-
(a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa
mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya
Wabunge wote itawasilishwa kwa Spika siku
thelathini kabla ya kikao ambapo hoja hiyo
inakusudiwa kutolewa Bungeni, ikifafanua makosa
aliyoyatenda Rais, na ikipendekezwa kuwa Kamati
Maalum ya Uchunguzi iundwe ili ichunguze
mashataka yaliyowasilishwa dhidi ya Rais;
(b) wakati wowote baada ya Spika kupokea taarifa
iliyotiwa sahihi na Wabunge na kujiridhisha kuwa
masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja
yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja
kuiwasilisha hoja hiyo, na kisha Spika atalitaka
Bunge, bila ya kufanya majadiliano, lipige kura juu ya
hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi na
kama ikiungwa mkono na Wabunge waiopungua
theluthi mbili ya Wabunge wote atatangaza majina ya
wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi.
(4) Kamati Maalum ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya ibara
hii, itakuwa na wajumbe wafuatao, yaani-
 
Nyerere alisema haya kwenye kitabu chake kuwa, kiongozi kazi yake kubwa ni kufanya maamuzi, tena maamuzi magumu kwa ngazi ya uongozi kama rais, akasisitiza kuwa ni bora ukafanya maamuzi ukalaumiwa kuliko kutokufanya maamuzi! Kikwete si riziki!

mkuu, hata haya maamuzi aliyoyafanya ni magumu sana. kuwatetea wezi dhidi ya wananchi wa Tanzania, huu ni uamuzi mgumu na mzito haswaa.
 
Hivi jamani! huyu raisi ana akili kweli! au hii habari ni propaganda! sitaki kuamini kuwa raisi wa nchi anakuwa thick kama hivi! this is not real!
 
Huyu jamaa has nothing to loose (anamaliza kipindi chake) inabidi sasa wengine ambao wanadhani hiki chama bado kina future, wagundue kwamba this chap is part of the problem both kwa chama na nchi in general
 
Tutasema tutalala, kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji
JK mwongo, mwoga. Hivi ahadi alizodanganya nazo walalahoi wakati wa kampeni 2010 zimetekelezwa ngapi?!
Hapo ndio utakapojua uongo wa serikali yetu na udhaifu wa viongozi wetu
Nyumba dhaifu inasababishwa na msingi dhaifu, wa kung'oa ni JK sio baraza la mawaziri
 
Yup haya ndo mavuno tuliyotarajia wakati kila m2 back in 2005 tunamchagua huyu Baba Mwanasha eti ni handsome na mcheshi w2 walisahau product ya m2 yoyote mcheshi na mwenye mvuto is always hawapo serius coz all the time wao wapo kwenye sanaa. 2015 yanahitajika maaumzi magumu iwe ni kwa magamba na chama chao kuamua kujali maslahi ya wengi na kuusoma upepo au ama sivyo kwaupepo huu CDM njia nyeupe 2015.
 
Huyo ndiye JK. Mtajuta kumfahamu. Kumbuken riport ya RICHMOND, kuwaacha watuhumiwa huru ndiko kunaongeza chuki baana ya wapambanaji na watuhumiwa. na wote mnafaham; mpambanaji asipopewa silaha(ulinzi) obvious mtuhumiwa atafanya kila awezalo kuhakikisha anampoteza (hata ikibidi kumuua) kwenye huo ulingo. So, msishangae yatakayomkuta CAG. Suala sio CAG;je yaliyotajwa na CAG ni sahihi au? Hivi kinachowawajibisha ni riport za kifisadi au ni CAG? Na kama ataenda kinyume na mapendekezo ya Bunge Hivi tutarajie nini kiutendaji kati ya Pinda na Hao mawaziri.Nadhani pia kuna shida ya ki-mfumo (system). Hili liangaliwe upya katika katiba mpya. Kwa hali ilivyosasa Pinda hana tofauti na raia wa kawaida;Pinda analalamika; huku wananchi wanalalamika. Ningekuwa mimi ni Pinda, kwa gharama yeyote ile ningetoa Ultimatum that either mawaziri waliotajwa wajiuzuru or mimi najiuzuru that is it. Wapi Jairo,wapi richmond,wapi mauaji ya Arusha yaliyokudhalilisha Bungen. Huyo ndiyo ****** anakula bata.
 
Mh. Pinda,
Jiuzulu sio kwa kushindwa bali kwa kuilinda heshima yako. NAKUSIHI KAMA KWELI HAWAJAJIUZULU MAWAZIRI BASI JIUZULU MWENYEWE. Pia wabunge wa CCM onyesheni heshima kwa nchi yenu juu ya mambo mazito kama ufisadi unaotesa nchi hii.
Nitashangaa sana kama Mh. Pinda hutajiuzulu. Matumaini ya mwisho ya Watanzania hivi sasa yako kwako. Sio kwa kurejesha kile kilichokwishaliwa, sio kwa kumfanya JK abadili maamuzi yake, bali angalau kwa kuona kuwa huko pamoja naye, pamoja nao. Jiuzulu Mzee, Watanzania waone kama kweli wewe ni MTOTO WA MKULIMA kama ulijigamba ulipoingia madarakani.

Najisikia Kumpolomoshea Mitusi.
Mtukane tu. Nimeshamkodi Lusinde Mtukanaji kuja kutumbuiza - lol

kujiuzuru anaweza akawa anatamani lakini akawa hawezi. Pinda sio kama Lowasa, Lowasa anavitega uchumi vingi ukiachilia mbali siasa. Pinda yeye anategemea hela ya serikali kuishi. Viongozi wengi wa tanzania wana hili tatizo, vipato vyao vinatoka serikalini tu na hawana njia nyingine za kueleweka ku-make money. Na hili litaendelea kutuumiza, Pinda hawezi hata kumshinikiza Rais kuwatendea haki wananchi. Pia Pinda akijiuzuru usalama wake kipindi cha serikali ya kikwete utakuwa matatani, tofauti na Lowasa Lowasa ni jeuri na ana network kubwa kutosha kumuhakikishia usalama wake.
Unasema kweli Mkuu au unatania kufurahisha baraza? Kama Mh Pinda hatajiuzulu kwa sababu ullizozitaja, hapo ndio tutajua kuwa hayupo kuwatumikia Watanzania, hata hayupo kwa kulinda heshima yake bali kuganga njaa kama mtu asiyejali heshima yake. Kwani kwa mwenye heshima, huwa yuko tayari kufa njaa na kulala nje.
BARUA YA WAZI KWA MH. RaHisi

Mh. RaHisi, ninakupa ONYO LA BURE - upepo haupiti tu, usijidanganye, hasa upepo wenyewe ukiwa ni kimbunga, na hili la sasa ni kimbunga, ni tone la mwisho katika kikombe kilichokwishajaa. Unauita upepo wa kupita kama yalivopita ya WAZEE WA AFRIKA YA MASHARIKI, EPA, RICHMOND, RADAR, IPTL, KIWIRA, MABOMU YA G'LAMBOTO NA MBAGALA, MGOMO WA MADAKTARI, TUCTA, NDEGE YA RAIS, MFUMKO WA BEI, GIZA TOTORO....(Orodha itaishia wapi)
?

Mh. RaHisi, usijidanganye, huu unaouita upepo wa kutapita, ni kweli kwa maumbile ya upepo utapita, lakini njiani utaacha uharibifu mkubwa. Kwanza uharibifu wako, umewasaliti Watanzania. Pili, dhambi ulizozitenda kwa kuwatelekeza wananchi wako huu wanapokuhitaji, zitakuandama daima, usiku na mchana, macho na usingizini. Vilio, machungu na machozi ya Watanzania vitakutafuna, vitakuandama, utavisikia kichwani mwako saa zote. Ni vilio vya haki, na haki haipotei, "haipiti kama upepo". Nisingependa niwe mtabiri wa hatma yako, lakini ninakuhurumia Mh. RaHisi.

Ulipochaguliwa (ulipolazimisha kuchaguliwa) mara ya pili nilisema na ninarudia kusema, (na naomba niwe nimekosea) kuwa kwa mwendo huu hutakimaliza kipindi hiki salama kama hutatafakari SASA, sio halafu. Kiburi kinachokufanya useme hayo ni upole wa Watanzania lakini usijidanganye, Watanzania si wapole bali ni wastahamilivu, na kwa hili ustahamilivu wao umekwisha. HILI NI ONYO LA BURE Mh. RaHisi.

Huu unaouita upepo wa kupita, hautapita bure bure. NI UPEPO WA MABADILIKO.
Mungu akufumbue macho.
Mungu inusuru Tanzania!
 
Niliweka bandiko humu kuwa anayetakiwa kuwajibishwa ni JK na sio Pinda. Watu wakaniona pimbi. Sasa hapo mwenye afadhali nani kati ya hawa wawili? Tunataka mabadiliko halafu tunamuogopa mwenye nyumba? M4C ya kweli ni kuanza maandamano nchi nzima kuelekea ikulu moja kwa moja.

Hiyo ndio dawa,ni kwenda Mpaka Ikulu asituletee Upuuzi wake. Watoto hawana madawati harafu yeye kila kukicha anasafiri.
 
Kama haya ni ya kweli basi nchi imekwisha, hawa mawaziri ni vitega uchumi vya JK hizo pesa zinazofujwa si kwamba wanazichukua mawaziri ila ni kwamba wanazipeleka kwa JK, na hataki kuwafukuza kwakuwa mawaziri hao wanasiri nzito,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom