Kikwete ateua Wakurugenzi Wapya Wizara ya Mambo ya Nje

Hongera sana Mbelwa Kairuki.....mwezi uliopita mama mkweo kateuliwa tume ya katiba kuwa mjumbe, ikafata mkeo akawa naibu waziri na leo wewe mkuru.....Mungu yu pamoja na nyie,wenye wivu wajinuyonge

Kweli Mungu yupo pamoja nao, pigeni kazi... sio ushwahiba tu. Ndio raha ya kusoma na kujuana.
 
Waislam 3 wakristo 6 jamani waislam tuongeze juhudi ktk shule haswa dada zetu!
<BR><BR>Government posts are for the interests of the nation and not for the interests of individual religion, party, tribe, colour etc. USE YOUR BRAIN WHEN ARGUING IN THE FORUM AND NOT YOUR ILL FEELINGS. Mwalimu Nyerere&nbsp;angekuwa na mawazo finyu kama ya wewe ndugu yangu taifa hili halingekuwepo leo. Kaburi lako litakuja kupigwa fimbo na vizazi vijavyo. Fikiria upya na kwa umakini na uwe na maono mapana. Uone miaka 200 ijayo Tanzania itakuwaje siyo leo kama kuku vile. Mzalendo<BR><BR>
 
bado kuna vijana wenye akili timamu ambao wanadhani wakifanya kazi serikalini wataweza kupandishwa vyeo??

Career foreign ni ku kupetezeana muda tuu na ushahidi upo.
btw
Malamula kwa nini asiingie kwenye private sector?

Mwe! kwenye Private Sector Mulamula afanye kazi gani inayohitaji ujuzi wa kibalozi?

Sana sana ajaribu kuwa mwalimu pale Kurasini kama ana vigezo, nilimuonna anahojiwa TBC1 nadhani ni mtu mwenye upeo mkubwa and very outgoing anafaa aendelee na kazi zake za kidiplomasia.
 
Mwe! kwenye Private Sector Mulamula afanye kazi gani inayohitaji ujuzi wa kibalozi?

Sana sana ajaribu kuwa mwalimu pale Kurasini kama ana vigezo, nilimuonna anahojiwa TBC1 nadhani ni mtu mwenye upeo mkubwa and very outgoing anafaa aendelee na kazi zake za kidiplomasia.

Da namimi nimeachwa tena.mbona ntapauka sana mtaani.Ngoja nisubili riport ya CAG ya 2011/2012 labda itawavua gamba wengine tena bunge lijalo
 
Waislam 3 wakristo 6 jamani waislam tuongeze juhudi ktk shule haswa dada zetu!

Na bado watu wote wanaotumia makalio kufikiri ndiyo zawadi yenu hiyo, watu wanasoma nyie mnaota kuonewa na kutaka Ndalichako ajiuzulu unadhani Joyce anasahihisha mitihani kwa mkono wake? fanyeni juhudi kwenda kwenye uamsho sijui mnaamshwa kumbe mlikuwa mmelala eti eeeeeeeeeeeeee Ndalichako akitoka atakuja alhaji lakini majibu yatakuwa ni yale yale naye mtasema amenunuliwa kwani hatuwajui nyie kazi kwenu. Mi naona hata jua linawabagua linawaka kwa hao msowapenda eti kaka bongolala?
 
Ilianza na Asha Mkwizu, ikafuata Angellah Kairuki, then Mbelwa Kairuki......who is next after mama, bintiye na mkwe? Tafakari!
 
Ilianza na Asha Mkwizu, ikafuata Angellah Kairuki, then Mbelwa Kairuki......who is next after mama, bintiye na mkwe? Tafakari!

Hiyo tafakari itusaidie nini?
Kuingia siasa hamtaki, kufanya serikalini mnaona pesa ndogo, mengi watu wanakimbia hata mkitaka chaguliwa hawawezi.

Acha wale bata wanajishughulisha.
 
Hiyo tafakari itusaidie nini?
Kuingia siasa hamtaki, kufanya serikalini mnaona pesa ndogo, mengi watu wanakimbia hata mkitaka chaguliwa hawawezi.

Acha wale bata wanajishughulisha.

Mzurimie, tunachohitaji ni fair play! Wenye uwezo wapo wengi, I mean wapo, tupo! Si lazima ku-sychronize kwenye familia moja.
 
......Sasa hizi ndio taarifa nusunusu; waliokuwa Wakurugenzi kwenye idara hizo wameenda wapi? wamefukuzwa, wameacha kazi, mikataba yao imekwisha...au wamehamishiwa kwingine au idara hizo hazikuwa na wakurugenzi kabisa kabla ya hawa "wapya"?......


NIMEPENDA MAELEZO HAYA. NATAMANI IKULU ITOE UFAFANUZI KWA MASWALI HAYO.
 
Ni Uteuzi uliotangazwa dakika chache zilizopita


TAARIFAKWA VYOMBO VYA HABARI

Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameteuaWakurugenzi wapya tisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifaambao pia watakuwa na hadhi ya Balozi.

Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa mjini Dar es Salaam leo, Jumatano, Mei 30, 2012na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi huo umeanza Mei 2,mwaka huu, 2012.

Walioteuliwani Ndugu Vincent Kibwana ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Afrika; NduguNaimi Aziz ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda; NduguCelestine Mushy ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa; NduguYahya Simba ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Mashariki ya Kati, na NduguBertha Somi ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Diaspora.

Wengineni Ndugu Irene Kasyanju aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi, Kitengo cha Sheria; NduguDorah Msechu ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Ulaya na Amerika,Ndugu Mbelwa Kairuki ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Asia na Australia, naNdugu Silima Haji ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Mambo ya Nje,Zanzibar.

Kablaya uteuzi wake, Ndugu Kibwana alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu, Ndugu NaimiAziz alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ndugu Mushy alikuwa Kaimu Katibu wa WaziriMkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ndugu Simba alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu, naNdugu Somi alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu.

NayeNdugu Kasyanju alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ndugu Msechu alikuwa MkurugenziMsaidizi, Ndugu Kairuki alikuwa Msaidizi wa Rais (Hotuba), Ofisi ya Rais, Ikuluna Ndugu Haji alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu.


..&#8230;&#8230;..Mwisho&#8230;&#8230;&#8230;.

Imetolewa na
:
Kurugenziya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR ES SALAAM.
30Mei, 2012


MY Take; Wale wanaosubiri uteuzi endeleeni kuwa na subira bado kuna nafasi zaidi hadi 2015 mtakuwa mmepata
Liberata Mulamula
 
Back
Top Bottom