Kikwete ateua Wakurugenzi Wapya Wizara ya Mambo ya Nje

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Ni Uteuzi uliotangazwa dakika chache zilizopita

TAARIFAKWA VYOMBO VYA HABARI
Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameteuaWakurugenzi wapya tisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifaambao pia watakuwa na hadhi ya Balozi.

Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa mjini Dar es Salaam leo, Jumatano, Mei 30, 2012na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi huo umeanza Mei 2,mwaka huu, 2012.

Walioteuliwani Ndugu Vincent Kibwana ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Afrika; NduguNaimi Aziz ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda; NduguCelestine Mushy ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa; NduguYahya Simba ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Mashariki ya Kati, na NduguBertha Somi ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Diaspora.

Wengineni Ndugu Irene Kasyanju aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi, Kitengo cha Sheria; NduguDorah Msechu ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Ulaya na Amerika,Ndugu Mbelwa Kairuki ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Asia na Australia, naNdugu Silima Haji ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Mambo ya Nje,Zanzibar.

Kablaya uteuzi wake, Ndugu Kibwana alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu, Ndugu NaimiAziz alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ndugu Mushy alikuwa Kaimu Katibu wa WaziriMkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ndugu Simba alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu, naNdugu Somi alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu.

NayeNdugu Kasyanju alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ndugu Msechu alikuwa MkurugenziMsaidizi, Ndugu Kairuki alikuwa Msaidizi wa Rais (Hotuba), Ofisi ya Rais, Ikuluna Ndugu Haji alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu.

..……..Mwisho……….

Imetolewa na:
Kurugenziya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR ES SALAAM.
30Mei, 2012

MY Take; Wale wanaosubiri uteuzi endeleeni kuwa na subira bado kuna nafasi zaidi hadi 2015 mtakuwa mmepata
 
Waislam 3 wakristo 6 jamani waislam tuongeze juhudi ktk shule haswa dada zetu!
 
Waislam 3 wakristo 6 jamani waislam tuongeze juhudi ktk shule haswa dada zetu!

sidhani kama hili ndo lengo lako la kubadili mada tajwa!!!kweli wewe bongolala!umechoka na utulivu kila wakati kutafuta namna ya kutifua maji yaliyo tulia!!shame on you!
 
Sasa hizi ndio taarifa nusunusu; waliokuwa Wakurugenzi kwenye idara hizo wameenda wapi? wamefukuzwa, wameacha kazi, mikataba yao imekwisha...au wamehamishiwa kwingine au idara hizo hazikuwa na wakurugenzi kabisa kabla ya hawa "wapya"?

hapo ndio wale wanaosubiri uteuzi waendelee kupiga jaramba huenda wakakumbukwa, orodha ni ndefu bado ya wahitaji
 
Waislam 3 wakristo 6 jamani waislam tuongeze juhudi ktk shule haswa dada zetu!

Kwa mtizamo wangu sidhani kuwa Waislam hawana elimu ndiyo sababu hawajateuliwa, nafikiri selection kama hii imeangalia uwezo wa kazi na experience zaidi, wengi wao walishakuwa tayari ndani ya system au kazi similar na hizo. Yamkini wangekuwapo Waislamu 6 na wana vigezo vinavyotakiwa wangeteuliwa sidhani JK anaangalia sana udini zaidi ni wanaomshauri kama Waziri wa Mambo ya Nje.
 
jina langu limerukwa tena, loh! hakika JK akimaliza mda wake watalia watu wengi, kuna wanaotamani aongezewe mda wa urais kwa matarajio yakukutana na zali la kuteuliwa.
 
Waislam 3 wakristo 6 jamani waislam tuongeze juhudi ktk shule haswa dada zetu!

raisa anajaribu kuwabeba ndugu zake hawabebeki ..hawaendi shule wanaenda kwenye uamsho badae baada ya mitihani wanadai wasahihishaji wa mitihani ni wakristo ..WTF?!!!!!!
 
Kama ulikuwa unasubiri nafasi bora ukamate jembe ukalime maana jamaa kama hajaiona uvccm vile. Ha ha ha kama Le Mutuz
 
Waislam 3 wakristo 6 jamani waislam tuongeze juhudi ktk shule haswa dada zetu!

pole kwa kuwa na mawazo mgando ya udini,tabu yako wewe ni kushinda kwenye kahawa na ............., unaacha kufikiria maendeleo unawaza udini,shame on u
 
Nadhani tuwe tunaacha kabisa kumjibu mtoa hoja za kidini hapa jamvini.
Tuaonekana sawa tukiendelea kulijadili. Ni kuwaachia wahusika walione na kuliondoa/kulifuta maana ni uchafu!
 
Back
Top Bottom