Kikwete Atafanya Mabadiliko Karibuni

mwana siasa

Senior Member
Aug 28, 2007
119
6
[/B
Ndugu wana jf kuna TETESI kuwa baada ya kuona hali ya hewa hapa nchini kwetu haindi vizuri,muungwana atafanya mabadiliko makubwa sana katika baraza lake la mawaziri,na zoezi hili linasemekana kufanyika moda wowote kuanzia sasa na kabla ya bunge la octoba,hasahasa atakaporudi kutoka italy na france,na hatua hii inakuja baada na ccm kuona hali ya serikali na chama kwa ujumla si nzuri hususani baada ya kugundua kuwa viongozi wengi wa serikali wako kwa ajili ya matumbo yao,licha ya hivyo pia inasemekana kuwa baada ya muungwana kuwepo ndani ya mtandao huo wa maslahi ambao umemwezesha kufika hapo alipo inasemekana kuwa ccm halisi + wazee wa chama ili kunusuru jina la serikali na chama yataletwa majina mapya kabisa katika mabadiliko haya,na pia kuna tetesi el atabaki ila 2010 itakuwa mbinde kutokana na ccm hiyo halisi kumuona ni mtu anayependa mno maslahi yake binafsi kuliko kitu kingine duniani.Na hapo ndo tofauti kati ya jk na el itaanza kuonekana mara baada ya muungwana kuvutwa kutoka katika kundi hilo la mtandao mpaka kwenye kundi la ccm halisi,na sura hizi mpya ndo zitakuwa mapendekezo ya ccm halisi na muungwana kwa ujumla na licha ya hivyo pia baraza hili ndo litatoa picha halisi ya baraza kamili la 2010,

Swali,je kuna mwenye aliyepata tetesi kuhusiana na habari hii?
Na je ni nani atatoka na ni nani ataingia?
 
iliandikwa kitu kama hii over 3-4 times in a 2 week period consecutively ! i hope this time it turns out right !
 
Kwa hiyo apo yote hayo ni tetesi, itabidi nisubirinione kama ni kweli, kwani anarudi lini na October ndo hiyo inaishia?
 
Phillemon Mikael upo? Maana wewe ndie huwa unatuletea za uhakika kabisa kutoka jikoni. Tafadhali tuna hamu ya kuzisoma hizi.
 
alisema kuwa ziara hiyo itakuwa ya siku nane tu ambayo sawa na wiki moja tuu,so naamini kabisa kuwa yuko katika siku zake za ukingoni uko ughaibuni
 
akifanya mabadiliko ina maana kelele za wapinzani zinamsumbua, so ili kuwa consinstent hatafanya mabadiliko hivi sasa hadi sometime middle next year.. ila kama yatakuwepo ni yale ya shuffling of ministers.. siyo kuwatema. Na kuna dalili kuwa atafanya semina nyingi ya kutathmini miaka miwili iliyopita... na kuwapa wasaidizi wake nafasi ya mwisho to prove to him kwanini wasitemwe..
 
Na hadi semina ziishe itakuwa na 2010 imeshafika, maana kwa miaka 2 ndo umekuwa mwendo wa semina elekezi na warsha, which means kazi halisi itakuwa haijafanywa, na hivyo kuwa na justification ya miaka mingine 5 'ili kazi ifanyike' maana sasa hao mawaziri na watendaji 'wapya' watakuwa wameiva, no?
 
tupunguzeni mambo ya siasa wazee, tusubiri atakachofanya ni kwa ajili ya maendeleo ya taifa ! kelele nyingi saa nyingine hazisaidii !
 
Hizi ramuli tumezizoea sasa hapa JF, lakini je kuna haja kweli ya kupiga ramuli? Kilichowazi ni kuwa Rais ana uwezo na mamlaka ya kufanya mabadiliko na kwa hali ilivyo hakuna cha ajabu kama atafanya hayo mabadiliko. Actually it is long overdue! Tayari kwa kuchelewa kufanya mabadiliko katika serikali yake ameshaonyesha kuwa yeye ni lile jibwa linaonekana kuwa ni li kali lakini kumbe halina meno (kibogoyo) na hivyo haliwezi kufanya chochote zaidi ya kubwaka na kutoa mate mengi mdomoni!
 
ni bora kupiga kelele kuliko kukaa kimya, kwani hata walinda mpunga hupiga kelele hata kama ndege wako shamba la jirani!! Ukinipa uchaguzi kati ya kufumba macho na kutopiga kelele huku kuombea mambo yataenda vizuri, na kupiga kelele na kuhamaki ili mambo yaende sawa, uchaguzi huo ni rahisi!!
 
Hivi hata JK akifanya mabadiliko, hao watakaokuja kweli ni nani na wana uwezo kiasi gani?

CCM sasa ina matatizo mengi, lipo la uwezo na lingine la ufisadi.

Mimi naona japo wanaweza kutokomeza la ufisadi lakini uwezo wa viongozi wetu wengi ni mdogo hata kama wana Ph.D.

Creativity ina lack kwenye viongozi wa juu na matokeo yake wanasubiri mpaka JK au Lowasa awaambie cha kufanya.

Mfano mmoja ni wizara ya Miundo Mbinu, yaani hapo kuna mambo mengi mno ya kufanya ili kuongeza utendaji wa serikali lakini
sioni kama kuna mipango mathubuti, ni mwendo ule ule wa kila siku wa kusua sua.

Kuna mawaziri wachache sana ambao wana uwezo hata wa kuwa CEO wa kampuni ya watu 1000 mbali ya huo uwaziri.
 
Jamani mwenyezi Mungu anisamehe,hakuna waziri ambaye namchukia kama kapuya,kamuamisha mzee wa watu pale oysterbay kisha kampeleka katika nyumba za jumuia za shirika la bandari,nyumba hiyo ipo oysterbay sehemu inaitwa morogoro stores jirani kabisa na kona ya kuja hospital ya macho ya ccbrt,
 
Huh??????????????????????????
 
Nyumba ya yule mzee aliyekuwa naibu gavana?
 
Mtanzania

Mabadiliko ndiyo yanayotakiwa, kwani nani alifahamu kwamba JK angekuwa rais au Mkapa let alone Mwinyi. Kweli wengi hawana uwezo na kama JK anaweza kufanya kweli hao watakaochaguliwa itabidi wafanye competition huko wanakowekwa ili waonekane wanafaa. Tatizo wale wanaofaa wanaibuliwa mizengwe na mafisadi ili waendelee kula pesa za walipa kodi.

JK lazima awatose wote wale ambao wanafanya biashara ili waendeleze biashara zao vizuri na kuwaacha wachapa kazi,sioni kama kuna tatizo hapo.
 
JK atawapaje mawaziri wake semina elekezi wakati yeye mwenyewe anahitaji hiyo semina elekezi? Ameshindwa kazi yeye na mawaziri wake wote waondoke ili wawapishe watu wenye uwezo wa kufanya kazi...asitupotezee muda.
 
hii sawa na ile

"kuna jamaa alikuwa akimuomba mungu sana ampe mali, lkn kila siku akawa maskini, mwisho akaamua kutukana na kusema wewe mungu gani huna lolote hata huwezi kunipa millions dala huna jeuri hiyo,sasa kuna swahiba yake akamuuliza baada ya maombi yake mbona unakufuru, akajibu nnamchonga ukali mungu anipe".

sasa hii ni sawa na kumchonga ukali Jk abadilishe baraza sawa sie tunaangalia kitachofuata
 
Mifano yako ionaendana sana na unachofikiri wewe mtu mwenye majina mengi humu. JK ni raia tu tena asiyejiamini
 
Back
Top Bottom