Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,884
Rais Kikwete katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi, katika kuongelea tukio la machafuko huko Zanzibar, licha ya kusikitikia uchomwaji makanisa na kwamba wanauamsho wanafanya kinyume cha malengo ya kusajiliwa, amesema pia uwanja uko wazi kujadili Muungano kwa kupeleka mapendekezo kwa Tume ya Katiba.
Ikumbukwe wakati anatangaza kuanza mchakacho wa Katiba na pale alipotangaza Tume ya Katiba alitamka wazi kwamba Muungano usiongelewe. Rasimu ya awali ya sheria ya kupitiaji upya Katiba iliyopelekwa bungeni ilitoa tishio la adhabu kali kwa atakayekiuka maagizo na sheria ya marekebisho ya Katiba.