Kikwete apunguza maofisa anaosafiri nao nje

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Imeandikwa na Stella Nyemenohi, Dodoma; Tarehe: 25th July 2011

RAIS Jakaya Kikwete ameridhia idadi ya maofisa katika ziara zake za nje ipunguzwe ikiwa ni hatua ya kupunguza gharama.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe aliliambia Bunge mwishoni mwa wiki wakati akijibu hoja ya kambi ya upinzani iliyoendelea kutaka safari za nje kwa viongozi zipunguzwe.

Membe alisema katika safari ya hivi karibuni ya Rais Kikwete nchini Shelisheli, idadi ya maofisa alioongozana nao ilikuwa 34 na kwa safari ya Afrika Kusini ilikuwa 34.

Hata hivyo, Waziri Membe alisema wakati mwingine, wingi wa maofisa huzingatia na aina ya ziara na nchi anakokwenda.

Alitoa mfano kwamba, endapo anakwenda nchi ambayo ulinzi wake upo shakani, idadi inaweza kuongezeka.

Alisema, zipo ziara nyingine kama vile za kibiashara inawezekana akalazimika kuongozana na ujumbe wa wafanyabiashara.

Awali, katika kuchangia hotuba ya makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yaliyopitishwa, kambi hiyo ya Upinzani kupitia kwa Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ezekia Wenje ilisema safari za viongozi wa juu zinatakiwa ziendane na hali ya uchumi.

Wenje alisema katika dhana ya kupunguza matumizi, baadhi ya safari za nje ambazo siyo lazima mkuu wa nchi kwenda, awaachie viongozi wengine washiriki kwa kuwa msafara wa Rais nje ya nchi una gharama kubwa ikilinganishwa na mawaziri au maofisa wengine wa Serikali.

“Kambi ya Upinzani inaitaka wizara ikishirikiana na ofisi ya Rais kuweka utaratibu wa safari za viongozi nje ya nchi, ili kupunguza matumizi makubwa ya Serikali na hatimaye fedha hizo zielekezwe katika miradi mbalimbali ya maendeleo,” alisema Wenje.

Hata hivyo, Serikali imekuwa ikisisitiza kwamba safari za Rais Kikwete nje ya nchi ni zenye manufaa na imekuwa ikitoa mafanikio ya ziara hizo katika nchi mbalimbali duniani.

Kwa mfano, Marekani ambako Rais Kikwete amekuwa na ziara tangu wakati wa utawala wa Rais George W. Bush na sasa Rais Barack Obama, Tanzania imenufaika kwa kupatiwa fedha nyingi katika miradi ya barabara, umeme, afya na maji.
 
kadege kadogo hako mnajazana 34 haya angepata Airforce One ndio angechukua Saigoni yote na wangefika 400
 
Tatizo siyo idadi ya maofisa anaokwenda nao, yeye mwenyewe aache kwenda nje ya nchi na badala yake awasiliane nao kwa njia ya simu au internet!
 
wapi vasco dagama!, mpaka 2015 atakuwa ametembelea hadi mars kuona kama kunauwezekano wa kupata umeme kutokea huko!
Teh teh teh, sina mbavu. Inaelekea mkuu wa kaya amedhamiria kumpiku Da Gama, Columbus,Livingstone na wavumbuzi wengine wa enzi hizo waliosafiri sana. Kwa nini rais na waziri wa nje ya nchi? Does Obama, Merkel, Sarkozi travel like this?
 
Kabla ya idadi hiyo ya 34 zamamni walikuwa wangapi? Bila ya hiyo takwimu hatuwezi kujua wamewapunguza kwa kiasi gani
Ni kweli bila kujua awali alikuwa na msafara mkubwa kiasi gani, hii habari itaishia kuwa 'publicity stunt' tu. Halafu, hivi nchi zisizo na usalama wa kutosha ni zipi-sudani ya kusini au Australia/jamaica kwenye bembea?
 
Majibu ya kihuni unaende Nchi usalama uko mashakani ? Nani mwendawazimu wa kumvamia JK ambaye hana impact hata katika Nchi yake.Yaani usalama wa Rais nchi aendayo jukumu kumbe si serikali ya kule ila na la JK na ujumbe wake ?Duh haya
 
Ina maana hawa 34 wote wanagharamiwa na serikali? na hapa wamepunguzwa..
 
Imeandikwa na Stella Nyemenohi, Dodoma; Tarehe: 25th July 2011

Hata hivyo, Waziri Membe alisema wakati mwingine, wingi wa maofisa huzingatia na aina ya ziara na nchi anakokwenda.

Alitoa mfano kwamba,
endapo anakwenda nchi ambayo ulinzi wake upo shakani, idadi inaweza kuongezeka.

Genuinely ni nchi gani wanataka Kumdhuru JK zaidi ya majority ya
Watanzania tokana na hasira zilizolimbikizwa na matatizo yalo maradufu
ya siku zoote.... In other words ni kama vile anasafiri kuepusha kuvamiwa
na wananchi wake inchini kwake - wenye hasira kali juu yake!!
 
Imeandikwa na Stella Nyemenohi, Dodoma; Tarehe: 25th July 2011

RAIS Jakaya Kikwete ameridhia idadi ya maofisa katika ziara zake za nje ipunguzwe ikiwa ni hatua ya kupunguza gharama.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe aliliambia Bunge mwishoni mwa wiki wakati akijibu hoja ya kambi ya upinzani iliyoendelea kutaka safari za nje kwa viongozi zipunguzwe.

Membe alisema katika safari ya hivi karibuni ya Rais Kikwete nchini Shelisheli, idadi ya maofisa alioongozana nao ilikuwa 34 na kwa safari ya Afrika Kusini ilikuwa 34.

Hata hivyo, Waziri Membe alisema wakati mwingine, wingi wa maofisa huzingatia na aina ya ziara na nchi anakokwenda.

Alitoa mfano kwamba, endapo anakwenda nchi ambayo ulinzi wake upo shakani, idadi inaweza kuongezeka.

Alisema, zipo ziara nyingine kama vile za kibiashara inawezekana akalazimika kuongozana na ujumbe wa wafanyabiashara.

Awali, katika kuchangia hotuba ya makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yaliyopitishwa, kambi hiyo ya Upinzani kupitia kwa Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ezekia Wenje ilisema safari za viongozi wa juu zinatakiwa ziendane na hali ya uchumi.

Wenje alisema katika dhana ya kupunguza matumizi, baadhi ya safari za nje ambazo siyo lazima mkuu wa nchi kwenda, awaachie viongozi wengine washiriki kwa kuwa msafara wa Rais nje ya nchi una gharama kubwa ikilinganishwa na mawaziri au maofisa wengine wa Serikali.

"Kambi ya Upinzani inaitaka wizara ikishirikiana na ofisi ya Rais kuweka utaratibu wa safari za viongozi nje ya nchi, ili kupunguza matumizi makubwa ya Serikali na hatimaye fedha hizo zielekezwe katika miradi mbalimbali ya maendeleo," alisema Wenje.

Hata hivyo, Serikali imekuwa ikisisitiza kwamba safari za Rais Kikwete nje ya nchi ni zenye manufaa na imekuwa ikitoa mafanikio ya ziara hizo katika nchi mbalimbali duniani.

Kwa mfano, Marekani ambako Rais Kikwete amekuwa na ziara tangu wakati wa utawala wa Rais George W. Bush na sasa Rais Barack Obama, Tanzania imenufaika kwa kupatiwa fedha nyingi katika miradi ya barabara, umeme, afya na maji.

Itakuwa kawapunguza kwa visasi au wivu? Au yamemkuta yaliyomkuta Moi kwa Ouko alivyokwenda USA kwani inasemekana Ouko alionekana kuwa aliqualify for Presidency na si Moi? Wewe kwa picha kama hii unategemea Obama atasemaje?

Obama-kikwete.jpg
 
Back
Top Bottom