Mtumishi Wetu
JF-Expert Member
- Oct 12, 2010
- 5,714
- 1,906
Mkuu mzeelapa usiende mbali chunguza kinacho endelea Kenya wenzetu kwenye EAC, JUZI WAMEFUKUZA KAZI mAJAJI WA MAHAKAMA YA RUFAA WANNE, Sio kuwastafisha ni kuwafukuza kazi!!!! Bado huoni faida ya kuwa na mabadilko tuu, umelidhika na wizi unaoendelea chini hapa tuu?????Nimegundua watu hapa wana chuki binafsi na JK au na CCM sio siasa. Kuwa na vyama vya upinzani sio mwisho wa matatizo ya nchi yo yote ila ni aina fulani ya kichocheo cha kutimiza matakwa ya walio wengi. Bahati mbaya sana sijasikia katika nchi yo yote ya Kiafrika ambayo mabadiliko makubwa yamefanyika baada ya upinzani kushika madaraka. Ninachoona vyama vya upinzani ni mbinu za nchi za magharibi kutugawanya ili waweze kututawala kiuchumi na wakati mwingine kifikra. Tuko busy na kutumia muda mrefu kugombea madaraka badala ya kufanya shughuli za kiuchumi. Nashauri upinzani utumie sera zao kuwaendeleza wananchi katika maeneo ambayo hayategemei serikali badala ya kung'ang'ania kushika madaraka kwanza. Bahati mbaya sana Waafrika tuna ubinafsi fulani baada ya kupata madaraka. Chunguza kwa undani ni nini kinachoendelea huko Misri, Libya, Sudan na nchi za Afrika magharibi, baada ya mabadiliko ya watawala.