Kikwete apokelewa kwa mabango na bendera za upinzani!

Si kweli, mtu hawezi kuvunjwa mkono na kulazimishwa kusaini matokeo.

Mkono kavunjwa, kasaini na mguu?

mkuu kwan yeye si ana mikono miwil au?

Katani A Katani. Alipigwa na polisi hadi kuvunjwa mkono akilazimishwa kusaini matokeo ambayo ni wazi yalibadilishwa.

Hiyo kesi ya Katani iko wapi? Kwanini asishtaki pia kwenye mashirika ya haki za binadamu? Kama ameifungua hiyo kesi locally most likely itapigwa dana dana; lakini it will help akiisema story yake kwa different NGO's, this issue needs to be in record itasaidia kwenye awareness raising wakati wa uchaguzi na pia ni ushahidi mzuri usio na chenga.

I believe there are some human rights NGO's who are working on documentary on these issues, his story needs to be heard.

Si kweli, mtu hawezi kuvunjwa mkono na kulazimishwa kusaini matokeo.

Mkono kavunjwa, kasaini na mguu?
mkuu kwani ana mkono mmoja? Acha ubishi bana.

Mkuu umenikumbusha mbali sana, wabunge wa CCM wanatakiwa kupimwa akili ndio maana wananchi wanawaita ndondocha yuko mbunge mmoja aliwahi kuomba bungeni kuwa mkoa wa Mtwara kuna uhaba wa Pingu na virungu.

Kweli tunawachukia na hata hiyo siku ya kutangaza matokeo Tandahimba nilikuwepo pia nilikuwa msimamizi kituo cha Mihambwe. Sio kwamba Katani Kachakachuliwa bali kanyang'anywa. Kwani kule ndani kulikuwa na ubishani kama atangazwe au La! aliyebadilisha mambo ni Mkuu wa wilaya ambaye alikuja kumlazimisha mkurugenzi wa H/w ambaye alikuwa anasimama kama kiongozi wa tume amtangaze Njwayo(CCM), Huku akisisitiza kuwa Rais atamuelewa vipi kama jimbo hilo litaenda kwa Wapinzani? (Huyu mama mkuu wa Wilaya ni yule aliyetimuliwa UWT)

Baada ya matokeo kutangazwa jambo la kwanza lilikuwa ni kuwapiga mabomu ya machozi mamia ya wananchi ambao walikuwa wanasubiri kushangilia ushindi huo wa Katani.

Kweli mimi ni Mwana CCM naapa kwa Mungu nilikuwa mwana CCM lakini kwa sasa sina imani tena na Chama hicho kwani walivuruga amani ya Tandahimba kiasi ambacho ilisababisha hata baadhi ya nyumba kuchomwa moto, siwezi kusema lile lililonikuta binafsi kwani nikifanya hivyo ni sawa na kutaja jina langu hapa jamvini kitu ambacho siko tayari kwa sasa! Yaani kama nitasema lililonikuta wana CCM wenzangu watajua kama ni nani anayetoa siri hii!

Pia siwezi kusahau kumtaja Makamba kuwa ndiye aliyekuwa anapiga simu mara kwa mara na kumlazimisha Mama Mwilima KUmtangaza mbunge wa CCM badala ya Yule mshindi!

Alivunjwa mkono baada ya kukataa kusaini matokeo, habari isiyo rasmi ni kuwa walikuwa na lengo la kummaliza. Alilazwa hospitali ya wilaya Tandahimba baadae akaletwa Muhimbili kwa Matibabu zaidi!

<br / halafu ikawaje alisain au walimsainia?? Shame on them

Si kweli, mtu hawezi kuvunjwa mkono na kulazimishwa kusaini matokeo.

Mkono kavunjwa, kasaini na mguu?

kama kavunjwa mkono anaweza kusaini,ila kama kavunjwa mikono ndo atasain kwa mguu

siku nyingine wasiandike mabango bali ikiwezakana wafunge barabara ili asimame maana mkuu wetu siku hizi hasikii tena bila kulazimishwa kwa maandamano..

<br / halafu ikawaje alisain au walimsainia?? Shame on them
Kilichotokea ni kichekesho kwani hata aliyeshinda alikimbia na hakusaini, amekuja kusaini siku kadhaa baadae huyu wa upinzani mpaka leo hajasaini na kesi iko mahakamani inapigwa danadana tu!

Gazeti wewe si ni ccm pure? au nakosea ndugu yangu.. si ulishawahi kugombea ubunge wakakuletea fitna .

Gazeti, lile tukio la mbunge kuvunjwa mkono lilikuwa maarufu sana mkoa mzima lilikuwa linafahamika, hata jinsi ushindi ulivyonyang'anywa ni jambo linalofahamika. Ina maana zile habari hazikutoka kwenye vyombo vya habari?

Mbona naona kama kuna watu wanaiona kama habari ngeni kabisa?

Gazeti, lile tukio la mbunge kuvunjwa mkono lilikuwa maarufu sana mkoa mzima lilikuwa linafahamika, hata jinsi ushindi ulivyonyang'anywa ni jambo linalofahamika. Ina maana zile habari hazikutoka kwenye vyombo vya habari? Mbona naona kama kuna watu wanaiona kama habari ngeni kabisa?
Walikuwepo baadhi ya waandishi ambao tuliambiwa ni wa Uhuru na habari leo, Pia Rashidi Kanga yule wa Radio one, Aliripoti taarifa za Tandahimba wakati akiwa Masasi, Yule ndo alikuwa mpotoshaji mkubwa kabisa!

Kwani alieleza kuwa vijana wamefanya fujo baada ya kuona wamekosa ushindi kwani CCM ilichaguliwa zaidi vijijini kwa hiyo wale wa mjini hawakulitambua hilo. Kila Mwenyeji wa Tandahimba ameshangazwa na taarifa hiyo.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida Rais wa Tanzania J.M. Kikwete alijikuta anapata wakati mgumu pale alipokuwa anakatisha katika vijiji mbalimbali vya wilaya ya Tandahimba. Mheshimiwa huyo alijikuta akipita kwa kasi katika baadhi ya vijiji bila kusimama na wala kupunga mkono kama ilivyo kawaida baada ya kukuta mabango ambayo wananchi walikuwa wanadai kurudishwa kwa mbunge wao aliyechakachuliwa. "TUNAMTAKA MBUNGE WETU ALIYECHAKACHULIWA", "HATUMTAKI NDONDOCHA WENU MLIETUWEKEA" "TUNATAKA KESI YA KATANI IISHE" Hivyo ndivyo yalivyosomeka baadhi ya mabango huku bendera za upinzani zikipamba bara bara za vijiji hivyo.

Bendera za vyama nilizobahatika kuziona ni CUF, CHADEMA, NCCR na TLP. Kikwete alipita maeneo hayo kwa lengo la kuwashukuru wananchi kwa kumpigia kura lakini hakufanya hivyo kutokana na mapokezi hayo ya aina yake!

Hii habari umeileta mahala husika maana hapa ndipo itakuwa hot cake.

Yule Rashidi Kanga mara kwa mara anapewa posho pale Halmashauri we unafikiri atatoa taarifa gani? Nashangaa mwandishi gani una shindwa kwenda eneo la tukio badala yake unaenda kuchukua taarifa ofisi ya CCM! Hapo lazima uwabebe wanaokupa ugali tu.

Safi kama wanaMtwara wameanza kuonyesha mabadiliko

AFADHALI WAMELIONA HILO,..MAANA HAWA WATU WA NTWALA WANAKUWAGA KAMA WALI CHEMSHIWA BENDERA YA JEMBE NA NYUNDO WAKANYWA MAJI YAKE. KHAAAAA!NA WANAVYOICHAKAKA CHULIWAGA KOROSHO ZAO WALA HAWAJIELEWAGI!!! NTU ANA HEKA KADHAA ZA SHAMBA LA KOROSHO LAKINI UTAKUTA NI MASKINI WA KUTUPWA

13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom