Kikwete apokelewa kwa mabango na bendera za upinzani!

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Rais wa Tanzania J.M. Kikwete alijikuta anapata wakati mgumu pale alipokuwa anakatisha katika vijiji mbalimbali vya wilaya ya Tandahimba. Mheshimiwa huyo alijikuta akipita kwa kasi katika baadhi ya vijiji bila kusimama na wala kupunga mkono kama ilivyo kawaida baada ya kukuta mabango ambayo wananchi walikuwa wanadai kurudishwa kwa mbunge wao aliyechakachuliwa. "TUNAMTAKA MBUNGE WETU ALIYECHAKACHULIWA", "HATUMTAKI NDONDOCHA WENU MLIETUWEKEA" "TUNATAKA KESI YA KATANI IISHE" Hivyo ndivyo yalivyosomeka baadhi ya mabango huku bendera za upinzani zikipamba bara bara za vijiji hivyo.

Bendera za vyama nilizobahatika kuziona ni CUF, CHADEMA, NCCR na TLP. Kikwete alipita maeneo hayo kwa lengo la kuwashukuru wananchi kwa kumpigia kura lakini hakufanya hivyo kutokana na mapokezi hayo ya aina yake!
 
Ni mbunge gani alichakachuliwa? Wengi hatujui hayo tusaidie !!!!
 
mkuu hebu tuwekee picha...maana nimeipenda hii ya bendera za TLP na NCCR.hakuna za DP?
 
Kwahiyo Katani A Katani ni CCM aliyeenguliwa... well alisha wahi kuwa Mbunge Miaka iliyopita kama sijasahau...
 
Daaah, kweli dhuluma mbaya. Unaona sasa hata raha ya uongozi jamaa haifaidi. Anashindwa hata kuwapungia mkono wananchi anaowaongoza!!!!! Kesho utamsikia m.k.w.e.r.e kageuza kibao anaenda zake ulaya kula bata ambako hakuna maandamano wala mabango.
 
mkuu hebu tuwekee picha...maana nimeipenda hii ya bendera za TLP na NCCR.hakuna za DP?
Nitajitahodi kwa matukio mengine kuweka picha, kule vyama vinavyofahamika zaidi ni hivyo vinne!
 
Kwahiyo Katani A Katani ni CCM aliyeenguliwa... well alisha wahi kuwa Mbunge Miaka iliyopita kama sijasahau...
Hapana siyo huyo katani unayemfahamu huyu ni kijana mdogo kama kina Mkosamali, huyo katani unayemsema ni mzee!
 
katani Ahmed katani mgombea wa cuf kweli wamemchakachua huyu kijana anakubalika sana na ukiongeza mtandao wa cuf kusini maana kila kona ni bendera za chama hiki.
 
Duuuh! aibu ilioje kwa Jk na tim yake nzima? natamani hii hali iendelee nchi nzima kwa maeneo ambako umefanyika uchakachuaji wa hali ya juu mfano Shinyanga mjini
 
Katani A Katani. Alipigwa na polisi hadi kuvunjwa mkono akilazimishwa kusaini matokeo ambayo ni wazi yalibadilishwa.

Si kweli, mtu hawezi kuvunjwa mkono na kulazimishwa kusaini matokeo.

Mkono kavunjwa, kasaini na mguu?
 
Si kweli, mtu hawezi kuvunjwa mkono na kulazimishwa kusaini matokeo.

Mkono kavunjwa, kasaini na mguu?

Alivunjwa mkono baada ya kukataa kusaini matokeo, habari isiyo rasmi ni kuwa walikuwa na lengo la kummaliza. Alilazwa hospitali ya wilaya Tandahimba baadae akaletwa Muhimbili kwa Matibabu zaidi!
 
Back
Top Bottom