Mkuu ni mpaka busara ya hivyo iwepo!Nafikiri mwenyekiti alitakiwa kuwaomba radhi ukumbini wawakilishi wa vyama vya upinzani ili kuset stage kwa makasuku walio chini wanaojua kuwa kushambulia upinzani ndiyo kupata ushindi na kujikomba zaidi kwa viongozi wa juu CCM ili baadae wapatiwe posts.
Mkuu Lady N,
Hapo ndipo nilipokasirika SANA na kusema TUJALI MASLAHI YA NCHI na tuache ushabiki wa kipumbavu ambao uko waziwazi. Huwezi kudai vyama vya upinzani ni mavuvuzela ilhali umewaalika; ni ukosefu wa busara mkubwa kwa viongozi wa CCM na kwa hili wanatakiwa kuwaomba radhi.
Inaudhi sana; kama siasa ni matusi namna hii basi mimi sitarajii kushiriki siasa za namna hii! Nchi inaangamia kwa mfumuko wa bei watu wanakaa kuitana mavuvuzela...
Wanafunzi wa vyuo vikuu wanaimba "CCM kiboko yao, na wapinzani wanajua". Wanasisitiza CUF wanajua...! Hahaha na TLP wanajua! Aibu kwa Mrema na Lipumba....
Maina Owino bwana...ha ha ha...anaangaika kweli kweli...ila ndo zake toka enzi zake UDSM....alikuwa DARUSO huyo...!Watu kwenye DIASPORA wanataka kurudi kuwa wanasiasa tu...hakuna kitu kipya...
Hawa Albino inakuwaje?Mwenyekiti aliyeongea ni wa-chama cha ma-albino wana-CCM ama?
Mpogoro ulikuwa hujui....Yule Mamluki wao
Mwimbaji mzuri ndio lakini..nashangaa badala ya kumuimbia Mungu, anamuimba Kikwete kwamba no one like him in this world.Sikujua kama dokii ni mwimabaji mzuri hivyo. Ila navyomwona jakaya lazima aombe namba hapo maana mtoto si mchezo
Kishatumbuiza Vick Kamata kisha wakatumbuiza wasanii wa TMK wakiongozwa na Juma Nature, wametinga mavazi ya CCM kwa raha zao.
Sasa anatumbuiza Flora Mbasha, anaimba "Kikwete Kiongozi bora, Ushindi ni LAZIMA".
Violeth Mzindakaya ndiye MC wa shughuli hii.
Wamehudhuria Lipumba, Mrema na viongozi wa Demokrasia Makini
Mwimbaji mzuri ndio lakini..nashangaa badala ya kumuimbia Mungu, anamuimba Kikwete kwamba no one like him in this world.
She is hopeless, anajaribu kuchumia tumbo. Hamna lolote. Nimemdharau sana na sintampenda kwa ujinga wake huu. Ukimuona mtu anajipendekeza kwa kikwete kwamba hakuna rais duniani mzuri kama kikwete ujue hamnazo. Nimuite libwege.
Well kwa kuwa ni mwana mama nisishangae sana maana huku kwetu kuna kamsemo kuwa mwanamke usifia kila mwanamme aliye naye kitandani kwamba yeye ndiye yeye hajawahi kukutana na mwingine kama yeye. Kumbe ulaghai.
ChapakaziSasa kwani walilazimishwa kuja hapo?
Kwenye siasa unahitaji ngozi ngumu mkuu! Sasa hawa mafala sijui wameenda hapo kufanya nini? Wewe umeshaona Obama anahudhuria mikutano ya Republican kwa madai kuwa kakaribishwa? Mimi hata nashindwa kuelewa wamekaribishwa kufanya nini! Huu ni mkutano wa CCM na hivyo CCM ina haki ya kufanya itakavyo!
Wapinzani wakiamua wanaweza kutumia hizo kashfa za CCM kuonyesha ujinga wa CCM.