KadaMpinzani
JF-Expert Member
- Jan 31, 2007
- 3,715
- 86
ni vizuri ulivyopingana na mimi bila ya kuonyesha utoto, ni kweli uliyosema and i respect that, ila mimi ndo nilivyoona niliyosema !
asante !
asante !
Wewe mtoto wewe,
Haya mambo ndio nimekuwa nakuonya hapa. Wakati mwingine unafanya jambo unadhani kuwa ni sifa kumbe ni hatari kwa nchi. Mambo ya kijeshi yanaongelewa jeshini na ni ya usalama wa nchi. Hii habari inaweza kuwa ni ya kweli lakini sio vyema kuitoa wazi namna hii.
Wewe kwa nini hujiulizi kuwa kwa nini vyombo vya nyumbani bado haviongelei hii habari ya kambi ya kijeshi. Mambo mengine sana tunakaa kimya ila inabidi ifike wakati tuyakatae. Hutakiwi kabisa kuongelea mambo ya kijeshi hapa hadharani.
Utoto tu ndio unakusumbua!
ni vizuri ulivyopingana na mimi bila ya kuonyesha utoto, ni kweli uliyosema and i respect that, ila mimi ndo nilivyoona niliyosema !
asante !
uko right. nadhani keshamaliza mafuta sasa anataka kuivamia zenji akaibe karafuu za zenji.ha ha ha.(joke)Hii kali kweli hakuna lolote hapa kuna nchi nadhani inataka kupigwa mika aijayao ukanda wetu ndio maana umeweka hku kama ni sasa za kiusala wa marekani why Tanzania mbona kuna distance kubwa sana hii itakuwa ni war base yake hapa mbele atakapata kupigana na nchi za jirani.
Tutakuwa hatuna akili timamu tukiwakatalia Wamarekani kujenga kituo chao cha kijeshi...haiwezekani hata kidogo kuwakatalia Wamarekani
hata kama ni ukweli lakini mzee nyani naona watu wanaangalia nje nje, kwani marekani ndo kwanza wanaanza kujenga base yao tanzania ?
kwanza kujengwa kwa base tanzania haitotugarimu chochote
itaongeza usalama na kuepusha ugaidi kwa kiasi fulani
misaada itaongezeka
huduma zitaongezeka mfano:mafuriko, njaa n.k (kumbukeni tz ilitumia mabilioni ya mapesa wakati wa njaa kiasi nusu tu tuanze kutumia reserve ya taifa)
hivyo naamini kabisa kwamba hata kama wakijenga, hawajengi bure kuna faida zake zitaambatana !
Tutakuwa hatuna akili timamu tukiwakatalia Wamarekani kujenga kituo chao cha kijeshi...haiwezekani hata kidogo kuwakatalia Wamarekani
watu humu mawazo yao ovyo kweli kuanzia huyo mwanzilishi wa hii thread, nashangaa tena sana watu wanapoona ubaya wa kitu fulani na kukashifu tu bila ya uzuri wake kuonyeshwa !
tukiendelea hivyo tutajiweka katika wakati mgumu sana maana ukweli utabainika na uwongo utajitenga !
Basi kama ni hivyo walete na Rais na waziri mkuu kutoka USA
walete na viwanda, maWTC, nk
Maana nasikia hotel wameshaanza kujenga huko serengeti
Ndiyo maana Rais anataka kujenga international airport kule bwagamoyoooo!!
Vyanzo vyangu vya hapa USA vimethibitisha uvumi ambao kwa muda umekuwa unaendela Tanzania kuwa serikali ya marekani ina mpango wa kujenga kituo cha kijeshi cha kudumu (permanent base) nchini Tanzania.
Ingawa serikali ya Tanzania imekuwa inajaribu kuficha hizi habari kwa visingizio kuwa mambo ya kijeshi hayajadiliwi kwa vile yanahusu usalama wa taifa, nimeamua kuwaambia wanajeshi kuwa hili suala la kuwa na base ya wamarekani Tanzania ni kubwa na hivyo ni vyema wakaruhusu watanzania wakalijadili.
Siku za karibuni Kikwete amekuwa na vikao vya wazi na vya siri na wamarekani ambao wanatafuta nchi katika pwani na pembe ya afrika ili wajenge kambi ya kijeshi ya kudumu kama ile waliyo nayo kule KATARI (sijui namna ya kutamka hii nchi kwa kiswahili) kule mashariki ya kati.
Wazo la kuweka kambi Ethiopia limeonekana gumu kutokana na hali ya usalama, chaguo la pili la marekani lilikuwa Kenya ambayo hali ya ukabila inatishia usalama wa Kenya. Wamarekani wameamua kuchagua Tanzania ambao so far wanaona kama nchi yenye amani na utulivu.
Habari zinasema kuwa kimsingi Kikwete amekubali (nani angekataa pesa kibao wamarekani walizotoa) na Marekani imelipa pesa indirect kwa kuahidi kutoa mabilioni ya pesa za msaada. Yes, hizi pesa walizoahidi juzi za kuisaidia Tz zitaishia mfukoni mwa wachache na zitakazobaki zitasaidia kujenga base.
MY TAKE.
1. Mimi naunga mkono suala la wamarekani kuwa na base ya Tanzania maana ikiwepo au isiwepo sioni faida au hasara yoyote ukichukulia kuwa Kikwete na wenzake wanauza nchi kila siku.
2. Ni vizuri Kikwete aendeleze mchezo wa kula pande zote mbili za wa-Irani na wamarekani.
3. Kikwete awaambie ukweli wa-Tanzania wa kile kinachoendelea.
4. IMF na Benki ya dunia wakome kusifia Tanzania kuwa inaendelea wakati wakijua ni uongo ila wanatimiza moja ya masharti ya Tz kukubali ku-host base ya marekani.
5. Kikwete atimize ahadi yake kabla Raila hajashinda uchaguzi wa Kenya maana Raila naye amekubaliana na wamarekani katika hili.
Thanks!