Kikwete and Family: Nani ni Nani?

Kafamilia kanachukua majukumu ya chama kinyemela afu wametulia tuliiiiii...
Wakereketwa wao wakiwapa kura watakuwa na ulakini...
Afu wanafurahisha utaskia eti chama ni taasisi...sielewi-elewi
 
Akishinda:
Minister of Statehouse Coordination: Hon Mrs S.J.M. Kikwete(Special seats(NGO) MP)
Minister of Sports,Young Africans,Advocates,Dynasty Systems and Youth Bodies Controls: Most Honourable R.J.M. Kikwete QC (Nominated MP)
 
JK ameamua kuhusisha fammilia kwenye kampeni baada ya ma tycoon na watu mbali mbali ambao baada ya kutoswa au kuona mambo ya hayaendi vizuri ndio kusema wao ndio wamemuweka madarakani , yani bila wao JK asingekua raisi wa Tanzania, sasa Mheshimiwa ndipo akamamua kutumia fammilia ili kusiwe tena na mtu kulipwa fadhila .JK kaamua kipindi hiki cha mwisho anataka awafunge mdomo wote walio sema hajafanya kitu , ana kaza buti zaidi na kuhakikisha heshima yake ina rudi na ku enziwa kwa vizazi vijavyo.Kutakua hakuna tena undugu ,urafiki na ile nawe ule hapo, ni kazi kwa Ari zaidi na kasi zaidi , hakuna kuangaliana machoni tena.Ila huyu Ruge wa nini ?

Unauhakika na Ulichosema hapa? Nadhani hat akatika utekelezaji wake ataakaa kusimamia wajenzi barabara; Bandari n.k else agawe kazi hizi kwa familia, (Ufalme)
Wasi wasi wangu ni kwamba, kama raisi ana ahidi ujenzi wa bara bara, mashule nakadhalika, Ahadi wangetoa Madiwani and wabunge....anyway (si mbaya) But kwa level yake angetoa ahadi za maana na za kimsingi (POLICY WISE ) like you know a twist vipi Uwekezaji uwe bora, % ngapi ya kodi na Revenue za Madini zinufaisheje nnchi, Sidhani kama kutakuwa na mabadiliko, Kama ametumia miaka 5 kuzunguka kuomba omba, hata neti na visivyo na maana, Mh I doubt ,
 
Ni bahati mbaya sana wengi tumekuwa vipofu kutokana na njaa zetu, anachokifanya Mkulu ni jambo la ajabu sana, kijana anasomewa risala na wakuu wa wilaya, mama ndo usiseme anapokewa na Ma DC na RCs halafu bado watu hawaoni wanasema huo ni wivu. Come on let's be serious!
Nafikiri Kikwete anaweza kuwa ni Rais wa kwanza na wa mwisho nchini kuihusisha familia moja kwa moja katika masuala ya chama na nchi. Nawashangaa akina Chiligati, Makamba na Msekwa kuendelea kumpigia debe Kikwete huku wakijua kabisa kwamba makamu mwenyekiti wa chama hivi sasa ni Salma Kikwete na Katibu Mkuu ni Ridhiwani.

Alianza kuwatosa akina Chiligati, Makamba na Msekwa tangu kwenye kuomba wadhamini, akasema Urais ni jambo binafsi na la kifamilia na si la chama. Lakini tumeona Slaa akizunguka nchi nzima kutafuta wadhamini akiwa ameongozana na viongozi wote wa Chama, the same to Lipumba, Mutamwega na Rungwe. Kwanini kwa CCM pekee urais uwe ni wa kifamilia wakati vyama vingine vyote vimeufanya urais kuwa chini ya mamlaka ya Chama? Au Kikwete ni mgombea binafsi?

Na kudhihirisha kwamba Urais ni suala la kifamilia, hivi sasa ndo kaamua kuwatosa viongozi waandamizi wa chama na hata maraisi wastaafu, na kuwatumia mke wake na mtoto wake katika kampeni, wakitumia resources za chama na serikali. Huu ni uhujumu wa waziwazi. Kazi iliyopaswa kufanywa na viongozi wa Chama hivi sasa inafanywa na wanafamilia ya Kikwete. Why? Ndiyo maana kuna wakati nilipendekeza hiki chama Kifutwe. Hakina tena sifa ya kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi. Kuna haja ya kumuomba Tendwa abadili registration ya hiki chama.
 
Just curious!!! Hivi nani ni mgombea urais kati ya hawa? Mbona wote wana majukumu sawa ya kuinua mikono ya wagombea ubunge na kuwatambulisha kwa wapiga kura?
Sijaona Makamu mwenyekiti wa chama (Msekwa) akitambulisha wagombea, au makamba akifanya hivyo. Ina maana Mama salma na Ridhiwani wana vyeo vikubwa kushinda makamu mwenyekiti wa chama na Katibu mkuu?
Yaani mke wa rais anakushika kwa mkono wake wa kushoto anauinua Juu. Kwa utamaduni wangu mimi hilo ni tusi na laana
 
Ukiwa mgeni unayetakiwa, mwezi mmoja unakuwa ni mfupi lakini ukiwa hutakiwi masaa mawili ni mengi mno. Nadhani umenisoma. Hata hivyo huenda ni mtindo wa wimbo fulani wa kwaya ya Arusha usemao Baba awe askofu, Mama awe mchungaji na Watoto wawe Wainjilisti.
 
That is funny! Naona Kikwete ametekeleza hilo. Baba ni Rais, Mama makamu wa Rais na mtoto ni waziri mkuu!! Au siyo?!
 
kkwa kweli hali ya nchi hii inanishangaza sana,ikulu imefanywa kama mali ya familia ya mkuu
 
hawana imani na viongozi wote wa ccm maana wakati wowote wanaweza kuwageuka na kumnadi Dr. Slaa, familia imeungana na kuwa ccm, ndio uaminifu mkubwa wa JK ulipo kwa sasa. Maana wengi sana wamekwishamdanganya sasa hana imani nao kwa ajili ya kitumbua chake cha kumalizia ngwe yake hii ya mwisho kama akishinda. Familia itakuwa na nafasi kubwa sana kwenye serikali ijayo ikiwa JK atashinda. Ni hayo tu
 
Ni hivi,wanaowapokea na wapokewa(familia potofu ya jk) ni malimbukeni walioshuka toka kuzimu ooops sorry waliushuka toka kwa nabii shekhe yahya(hhahhaah tutarogwa mwaka huu)
 
JK ameamua kuhusisha fammilia kwenye kampeni baada ya ma tycoon na watu mbali mbali ambao baada ya kutoswa au kuona mambo ya hayaendi vizuri ndio kusema wao ndio wamemuweka madarakani , yani bila wao JK asingekua raisi wa Tanzania, sasa Mheshimiwa ndipo akamamua kutumia fammilia ili kusiwe tena na mtu kulipwa fadhila .JK kaamua kipindi hiki cha mwisho anataka awafunge mdomo wote walio sema hajafanya kitu , ana kaza buti zaidi na kuhakikisha heshima yake ina rudi na ku enziwa kwa vizazi vijavyo.Kutakua hakuna tena undugu ,urafiki na ile nawe ule hapo, ni kazi kwa Ari zaidi na kasi zaidi , hakuna kuangaliana machoni tena.Ila huyu Ruge wa nini ?

Acha ujinga wako. Kwani 2005 uliwaona hao "tycoons" unaowataja wakifutana na JK kwenye kampeni? Akili fupi mna taabu sana.

Hajafanya kitu na hayo yaliyofanyika yote umefanya wewe na mchungaji wako? :hand:
 
hahaha hahaha hahaha napata picha hapo

Lakini this is shame to our nation kuwa family imechukua hatamu za uongozi wa nchi kuanzia kwenye kampeni hadi nshaaa matumizi ya hovyo ya rasilimali za umma. .

Ni aibu hivi imekuwaje tukafikishwa hapo?
 
Mbona simuoni Miraji Kikwete akiisaidia familia ya kifalme kwenye kampeni au yeye karithi uchakachuaji wa mabinti kwa mfalme Jakaya 1.
 
JK ameamua kuhusisha fammilia kwenye kampeni baada ya ma tycoon na watu mbali mbali ambao baada ya kutoswa au kuona mambo ya hayaendi vizuri ndio kusema wao ndio wamemuweka madarakani , yani bila wao JK asingekua raisi wa Tanzania, sasa Mheshimiwa ndipo akamamua kutumia fammilia ili kusiwe tena na mtu kulipwa fadhila .JK kaamua kipindi hiki cha mwisho anataka awafunge mdomo wote walio sema hajafanya kitu , ana kaza buti zaidi na kuhakikisha heshima yake ina rudi na ku enziwa kwa vizazi vijavyo.Kutakua hakuna tena undugu ,urafiki na ile nawe ule hapo, ni kazi kwa Ari zaidi na kasi zaidi , hakuna kuangaliana machoni tena.Ila huyu Ruge wa nini ?

Nazani analysis yako inaweza ikawa ni kweli kabisa. Ila tu asije akampa mkewe uwaziri mkuu na Rizhi1 uwaziri wa mambo ya nje kama kuwalipa fadhira.
 
Nadhani kuna mabadiliko ya kiserikali to a Monarchy Government. Sidhani kama kutakuwa na uchaguzi tena baada ya huu kama sisiem ikishinda. Mrithi wa Kikwete in this coming Monarchy Gov. atakuwa Ridhi1.
 
JK alishasema URAIS ni jambo la kifamilia, nyie mlie tu yeye mwendo mdundo. Kikubwa tumkomeshe kupitia sanduku la kura ifikapo 31/10/2010.
 
wana jf naomba kupata ukweli wa hili suala maana dogo anatajwa sana,na amehusishwa ktk kashfa mbalimbali za kuwahujumu watu kwenye siaasa,who is this?
 
Prince Ridhiwan Kikwete, ni mwana wa Mfalme Jakaya Mrisho Kikwete I, wa Falme ya Danganyika
 
Back
Top Bottom