Kikwete: Anayeona CCM hakukaliki, ruksa kuhama!

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=1][/h]

6db9d786bc77dd73357197bb3040a188.jpg

Na Reginald Miruko - Imechapwa 16 May 2012

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amewataka wanachama wote wa chama hicho wanaoona hakikaliki, kuhama badala ya kubaki wakilalamika.

Kikwete ametoa kauli hiyo ndani ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kilichomalizika mjini Dodoma juzi usiku.

Kauli hiyo ya Rais Kikwete imekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kukaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa tatizo la CCM ni uongozi.

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara eneo la Mto wa Mbu ndani ya jimbo lake la Monduli, Lowassa alisema kuwa ingawa CCM ina misingi ya kutetea wanyonge, ina tatizo la uongozi na utendaji.

“Pamoja na uzuri wake, muundo wa chama chetu ni mzuri sana, imani ya chama chetu ni nzuri sana, misingi inayoongoza chama chetu ni mizuri sana, lakini tuna tatizo la utendaji na uongozi ndani ya chama chetu,” alisema Lowassa.

Mmoja wa wajumbe wa kikao hicho cha NEC ameiambia MwanaHALISI kwamba kauli hiyo ndiyo inaonekana ilimchochea Rais Kikwete kusema kuwa “kama kuna wanachama wanaoona viongozi wa chama hawafai, au chama hakitekelezi vema majukumu yake wana haki ya kuondoka”.

Kikwete amewataka wanachama hao, badala ya kubaki wanatishia kuhamia kwenye vyama vya upinzani, ni bora wakahama haraka kwenye chama hicho.

Katika mkutano wake, Lowassa alisisitiza, “Siku CCM inaacha kutetea wanyonge mimi si mmoja wao.”

Aliulaumu uongozi wa chama hicho kwa ama kuchelewa kufanya maamuzi, kufanya maamuzi yasiyo sahihi au kutochukua hatua kwa matatizo yanayowakabili wananchi kwa wakati muafaka.

Lowassa alieleza kuwa matatizo hayo ndiyo yanayowafanya watu wakichukie chama hicho na kukiona kuwa ni kero kwao hivyo kutafuta mbadala wake.

Lowassa ambaye amekuwa miongoni mwa wanachama wanaoshinikizwa kujiuzulu nyadhifa zake kutokana na jina lake kuhusishwa na tuhuma za ufisadi, alitaja misingi mitano ambayo inamfamnya aendelee kuwa mwana CCM.

  • Moja ni kwamba ni chama kinachotetea wanyonge. Umoja na mshikamano
  • Raia wa kawaida analindwa katika kupata na kufaidi rasilimali za nchi dhidi ya matajiri na wawekaji wa nje.
  • Kuna mfumo unaowezesha watu kujisahihisha... “Ndani ya CCM kuna vikao, kuna taratibu za vikao, kuna kufukuzana na kuonyana.
  • Pia ndani ya CCM kuna haki za msingi za mwanachama za kupiga kura au kupigiwa kura.

Lowassa alisema kitendo cha viongozi kushindwa kushughulikia kero ndiyo mwanzo wa chama hicho kuparaganyika kwa kuwa watu wanatafuta mbadala wa kero zao na matatizo yao.

Kauli hiyo ya Lowassa iliamsha hasira za Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama ambaye alimtaka azungumzie matatizo yanayolikabili jimbo lake badala ya kufanya mikutano ya hadhara kukiponda chama.

Mukama amesema si sahihi kwa Lowassa kutoa kauli hiyo kwenye mikutano ya hadhara wakati anajua bayana taratibu za chama hicho.

Amesema Lowassa alipaswa kuzungumzia matatizo ya jimbo lake yakiwemo migogoro ya ardhi, wawekezaji na wananchi, wakulima na wafugaji, maji na kero nyingine mbalimbali na si kukishambulia CCM.

Kwa mujibu wa Mukama, kama Lowassa amebaini matatizo ya uongozi ndani ya CCM, alipaswa kuyazungumzia ndani ya vikao vya chama kwa sababu ana mamlaka ya kukosoa au kurekebisha.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa CCM Monduli, Ruben Olekuney ameibuka na kusema kwamba Mukama amekurupuka kumjibu Lowassa.

Olekuney amesema Lowassa alikuwa akizungumzia uongozi wa chama hicho eneo la Mto wa Mbu na si wilaya, mkoa au taifa.

Amesema ni kweli kulikuwa na udhaifu kwenye uongozi wa kata na wamechukua hatua kwa kumpa onyo diwani wa eneo hilo kwa kutoa vibali vya ardhi bila ya kufuata taratibu zilizopo.

“Kwa kweli Mzee Mukama anatakiwa kwanza asome maudhui ya yale aliyosema Edward, siyo kukurupuka, huku,” amesisitiza.

Katika kikao hicho, pia matokeo ya uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki yalijadiliwa na kubainika kuwa kilichosababisha chama hicho kushindwa ni makunndi ndani ya chama.

Kuhusu uchaguzi huo, ilielezwa kuwa chama hicho kiliathiriwa na makundi na kusababisha kiti hicho kwenda kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Vyanzo vya habari zimeeleza kuwa iliamuliwa kwamba kamati kuu ikutane na makundi yaliyohusika kila moja kwa wakati wake ili kufatuta suluhu na kuyapatanisha.

Suala jingine lililojadiliwa ni ugumu wa hali ya maisha ambapo baada ya kupata ripoti za ahali ya uchumi, ilibainika tatizo ni bei ya mafuta ambayo ilielezwa kuwa chama hicho hakina uwezo nayo.

Kuhusu bei za vyakula, kikao hicho kilielezwa kuwa serikali itatoa chakula kutoka katika maghala yake na kukisambaza kwa lengo la kudhibiti bei ya nafaka.

Fall Out... Hapo nani hana shukrani? Nani kamsellout his friend? tulisikia bila Lowassa Kikwete asingeweza kuwa Rais, sasa

Nini kimetokea kimesababisha Kikwete kumchoka rafiki yake? Na Ninasikia kuwa Riz1 ataandika Kitabu kuhusu watu waliom

saliti baba yake, lakini Lowassa sacrifice Uwaziri kwa manufaa ya Kikwete... TZ politics!!!!

WHO OWNS CCM NOWADAYS? IT SEEMS IT BELONGS TO AN INDIVIDUAL
 
Hawezi na hata hawezi kufikiri kukihama CCM eti akautafute Urais ACT au kwingineko! Alikuwa na imani kubwa ndani ya ccm na sasa wamemwagaaaa! ametumia pesa nyingi na mbinu nyingi kuwashawishi wana CCM lakini wamemmwagaaaa! Akienda ACT au kwingineko napo ataangukia pua na hapo presha itampanda, aibu ya kuforce uongozi, na matusi ya wapinzani wake hakika havitamuacha salama. Atulie tu ale pensheni yake ya uwaziri mkuu basss!
 
Lowasa hata mimi sishauri ahame ccm ,zaidi ya kubaki ccm n akuiua kutokea ndani..Waswahili wlaishamuuza kutokea sehemu asiyoweza fika.
 
Hawezi na hata hawezi kufikiri kukihama CCM eti akautafute Urais ACT au kwingineko! Alikuwa na imani kubwa ndani ya ccm na sasa wamemwagaaaa! ametumia pesa nyingi na mbinu nyingi kuwashawishi wana CCM lakini wamemmwagaaaa! Akienda ACT au kwingineko napo ataangukia pua na hapo presha itampanda, aibu ya kuforce uongozi, na matusi ya wapinzani wake hakika havitamuacha salama. Atulie tu ale pensheni yake ya uwaziri mkuu basss!

Umenena mkuu. Akitaka kuhama amuone kwanza Mzee Augustino Mrema kwa ushauri. Apime experience ya Mrema halafu afanye maamuzi magumu.
 
watu hushiriki hufanya hujuma lkn sikuzote MUNGU huwapa watu uhai ili nao waweze kuonja ubaya wa hujuma wakiwa hai duniani,hiyo ndio tabia ya dhambi na matokeo yake.MUNGU atubariki sote daima tutende mema kwa Binadamu wenzetu.
 
Kumbe lowasa kaangushwa na mambo. mengi.
Na inavyoonekana bifu lilianza zamani.
Basi tena akachunge ng'ombe.
 
watu hushiriki hufanya hujuma lkn sikuzote MUNGU huwapa watu uhai ili nao waweze kuonja ubaya wa hujuma wakiwa hai duniani,hiyo ndio tabia ya dhambi na matokeo yake.MUNGU atubariki sote daima tutende mema kwa Binadamu wenzetu.

Sadaktaaa, wao walimuhujumu na kumzushia Salim Ahmed, sasa ni zamu yao kuhujumiana wenyewe.
 
Kwa mujibu wa katiba ya CCM ibara ya 13, ibara ndogo ya (f) Team Lowassa ina haki kikatiba kuhamia chama chochote.

13. (1) Uanachama wa mwanachamautakwisha kwa:-(a) Kufariki.(b) Kujiuzulu mwenyewe.(c) Kuachishwa kwa mujibu waKatiba.(d) Kufukuzwa kwa mujibu waKatiba.(e) Kutotimiza masharti yauanachama.KuondokakatikaChamaKatiba ya Chama Cha Mapinduzi (f) Kujiunga na Chama kinginechochote cha siasa.

source: http://demo.ccm.or.tz/wp-content/uploads/2014/07/katiba.pdf
 
sasa unalia nini?
 
mbona kolimba na malima hawakuwahi kujiunga na vyama vingine?ogopa ccm,ni kama mafia anapokuwa na bunduki mkononi halafu anakwambia ondoka,atakushoot kwa nyuma!!!
 
mbona kolimba na malima hawakuwahi kujiunga na vyama vingine?ogopa ccm,ni kama mafia anapokuwa na bunduki mkononi halafu anakwambia ondoka,atakushoot kwa nyuma!!!
Malima alihamia NRA na akapewa uenyekiti ila Mungu tu akamuwahi
 
Back
Top Bottom