Kikwete anapwaya, "he is not president enough"

Mzanaki

Member
Feb 25, 2011
20
11
Kwa mtu mwenye maono ya mbali na busara aliyefuatilia kwa makini uongozi wa JK tangu mwaka 2005 hata kama mtu huyo ni mkereketwa wa kutupwa wa CCM kama mzee Msekwa,Kingunge nk. atakuwa amejiridhisha kuwa kiongozi huyu anapwaya.Kwanza kwa kumlinganisha na aliyemtangulia yaani Mkapa na pia kwa kuwatazama mawaziri wake kama wakina Sophia Simba,Wiliam Ngeleja nk.., achilia mbali waliojiuzulu hapo awali kama wakina Karamagi na Lowasa.
Utendaji kazi wa raisi huyu kwanza haufuati itifaki,Rais atazungumzia ujenzi wa nyumba Gongo la Mboto wakati waziri wa makazi yupo,..Rais atazungumzia maandamano ya amani ya Chadema tena kwa kutetemeka wakati waziri wa utawala bora yupo achilia mbali Waziri mkuu na Makamu wa raisi...Waziri wa maji Mark Mwandosya atafungua tawi la benki ya CRDB huku waziri wa biashara yupo..nk..nk..Hizi ni dalili za serikali iliyochanganyikiwa kutokana kupwaya kwa raisi wake.Ukimtazama JK kwa makini wakati wa hotuba yake ya mwisho wa mwezi, kwanza utagundua hofu kuu ambayo inazidi ile iliyoonyeshwa na Mubaraq, Ben Ali na hata Qadaffi!...Wewe bado unashikilia dola sasa hofu kubwa kiasi hiki inatoka wapi kama sio dhamira yako inakushitaki kutokana na kupwaya kwako?.Kaza msuli Mr.President otherwise wananchi watakung'oa kweli!.
 
Muda umeisha bro kashapoteza, watu wameshamchoka kilichobaki ni kuandamana tu.
 
we ndio umeamka leo kuona kua kikwete hafai ulimpenda mwanzo si ndio tel us amekufanyaje mpk umegundua ukwel?
 
Mtu yeyote hajulikani uwezo wake wa kiuongozi kwenye nafasi kubwa kama ya uraisi mpaka amekuwa subjected kwenye "vital leadership tests".Haya ni matukio makubwa yanayosababisha hofu kwa kiongozi na hapa unaweza kutoa mfano wa maandamano ya CHADEMA, Mabomu ya Mbagala na Gongo la Mboto, Kukosekana umeme na issue ya Richmond, hali ngumu ya maisha kwa wananchi n.k..kwangu mimi mitihani yote hii JK amepata alama za chini kuliko wanafunzi wa shule za kata.Alipokuwa anajibu maandamano ya CHADEMA hapo ndiyo alipata sifuri kabisa.
 
vital leadership tests"
Hapo umesema kweli mkuu
Kipimo kimojawapo cha uongozi ni kuangalia jinsi anavyofikiri,anavyosema na anavyotenda wakati wa majaribu makuu
Nilikuwa najua tangu mwanzo kwamba sio mtu mwenye haiba ya kufanya maamuzi magumu na matokeo yake ndiyo hayo tumejiridhisha,kwamba hawezi,nafasi aliyopewa/jipatia ni kubwa kuliko uwezo wake.
 
Back
Top Bottom