Kikwete anapoomba Msaada kutoka Ulaya kuwakamata wala rushwa, anamaanisha nini?

Huenda kama ni makengeza basi nafikiri hata masikio yangu pia yana makengeza; Kwani na mimi nimeisikia ITV jana saa mbili usiku. Nilibaki mdomo wazi, kwa mtu kama Raisi wa Tanzania, anayeelewa nchi yake na watu wake walivyo, anaomba nchi za Ulaya kusaidia kupambana na Rushwa katika nchi za Kiafrika.

TENA ALIKUWA ANACHEKA CHEKA WAKATI ANAONGEA KWA KUJUA KUWA ANACHONGEA SIYO ANACHOMAANISHA!!!!

PTYUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU!!!!!!!!!!!!!!!!

Kisha baadaye akawekwa BW. HOSEA WA TAKUKURU; ambaye alitudhihirishia kuwa KatikaSKENDO YA RADA HAKUNA MTANZANIA ALIYEHUSIKA, HIVYO NI UINGEREZA TU WALIHUSIKA KATIKA RSHWA YA RADA.

Nikabaki mdomo wazi, Iweje mtu wa nje ahusike katika rushwa inayohusu nchi yetu.

Je, huyo muingereza aliyehusika alikupewa Commission na nani??

Je, iweje achukue Rushwa mtu wa nje ili kutuuzia sisi Rada??

Je, kwanini bei iandikwe tofauti na bei halisia, kwani katika manunuzi lazima kulikuwa na Proforma Invoice, au Tender iliyotangazwa.

Jana niliangalia ITV mwisho niliamua kunyanyuka na kutoka nje kwani nilishindwa kuizima kwani kulikuwa na wengine wanaangalia.

KWA KWELI SERIKALI YA AWAMU YA NNE HAIJUI HATA INAFANYA NINI. Huenda waliomba madaraka lakini hawajui hata Job Description yao.

TANZANIA TULIKOTOKA NI KUBAYA NA TUNAKOKWENDA NI KUBAYA ZAIDI!!!!!!!!!!!

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!

Kwa kweli wana JF hata mimi nilisikia nikashangaa sana!!! kumbe hata wana JF wenzangu waliosikia wamebaki midomo wazi. kama uraisi ni huo wa JK, basi kila mtu anaweza kuwa rais wa TZ. Kuwaomba wazungu fedha za kukamata mafisadi aliowasamehe yeye mwenyewe na kuacha kuwapeleka mahakamani? SFO walimweleza kuhusu waziri wake mwenye MABILIONI , wakamtajia jina na hata mahali pesa hizo zilikowekwa bado hakuchukua hatua... Leo anawaomba wampe fedha? Kudadadeki!
 
JKSpeak(11).jpg

Rais Jakaya Kikwete

Rais Jakaya Kikwete, amesema kuna ushahidi wa mafanikio katika vita dhidi ya rushwa kubwa nchini lakini hata hivyo, amesema bado kuna kazi kubwa ya kufanya ambayo ipo mbele katika mapambano hayo.

Alisema hayo jana wakati akifungua mkutano wa Chama cha Kimataifa wa Mamlaka zinazopambana na Rushwa, uliofanyika jijini hapa jana.

Hata hivyo, Kikwete alisema hakuna sababu ya kufurahia mafanikio hayo kwa sababu, “hatujafikia hatua ya kuridhisha katika mapambano hayo.”

“Hii inamaanisha kwamba, tunahitaji kuongeza nguvu mara mbili na kunoa ujuzi wetu katika kupambana na rushwa wakati tunapotarajia kuingia hatua ya tatu ya Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Rushwa na Mpango Kazi (NACSAP),” alisema.

Kwa bahati nzuri alisema, “kuna utashi wa kisiasa kwa upande wangu na kwa upande wa wenzangu wengi serikalini.”
“Kuhusu hili, nina imani kubwa kwamba wakati tukiendelea na vita hii dhidi ya rushwa na hivyo kutuweka katika njia imara na sahihi ya kufikia malengo yetu,” alisema.

Katika hatua nyingine, Kikwete alitaja sababu muhimu inayochangia kuwa na mafanikio mazuri katika vita dhidi ya rushwa kuwa ni uwepo wa raslimali kama vile watu, fedha na vifaa.

Kuhusu rushwa ndogo ndogo, alisema haihitaji sana uwekezaji hasa kwa sababu kinachohitajika ni kuwa na polisi wachapa kazi, mahakama na utawala bora, tofauti na ilivyo kwa rushwa kubwa ambayo makali yake yameongezeka kutokana na kukua kwa teknolojia ya kisasa na hivyo kuwa changamoto kubwa kwa taasisi zinazopambana na rushwa.

CHANZO: NIPASHE
 
JKSpeak(11).jpg

Rais Jakaya Kikwete

Rais Jakaya Kikwete, amesema kuna ushahidi wa mafanikio katika vita dhidi ya rushwa kubwa nchini lakini hata hivyo, amesema bado kuna kazi kubwa ya kufanya ambayo ipo mbele katika mapambano hayo.

Alisema hayo jana wakati akifungua mkutano wa Chama cha Kimataifa wa Mamlaka zinazopambana na Rushwa, uliofanyika jijini hapa jana.

Hata hivyo, Kikwete alisema hakuna sababu ya kufurahia mafanikio hayo kwa sababu, "hatujafikia hatua ya kuridhisha katika mapambano hayo."

"Hii inamaanisha kwamba, tunahitaji kuongeza nguvu mara mbili na kunoa ujuzi wetu katika kupambana na rushwa wakati tunapotarajia kuingia hatua ya tatu ya Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Rushwa na Mpango Kazi (NACSAP)," alisema.

Kwa bahati nzuri alisema, "kuna utashi wa kisiasa kwa upande wangu na kwa upande wa wenzangu wengi serikalini."
"Kuhusu hili, nina imani kubwa kwamba wakati tukiendelea na vita hii dhidi ya rushwa na hivyo kutuweka katika njia imara na sahihi ya kufikia malengo yetu," alisema.

Katika hatua nyingine, Kikwete alitaja sababu muhimu inayochangia kuwa na mafanikio mazuri katika vita dhidi ya rushwa kuwa ni uwepo wa raslimali kama vile watu, fedha na vifaa.

Kuhusu rushwa ndogo ndogo, alisema haihitaji sana uwekezaji hasa kwa sababu kinachohitajika ni kuwa na polisi wachapa kazi, mahakama na utawala bora, tofauti na ilivyo kwa rushwa kubwa ambayo makali yake yameongezeka kutokana na kukua kwa teknolojia ya kisasa na hivyo kuwa changamoto kubwa kwa taasisi zinazopambana na rushwa.

CHANZO: NIPASHE

EMPTY SUIT PREZ. amebakia kupambana na rushwa kwenye seminars na makongamano tu. ilipokuja rushwa yenyewe kwnye kagoda, uuzwaji wa nyumba za serikali na EPA he was no where to be found. i agree with Mkurugenzi wa takukuru kuwa JK is not serious ktk kupambana na rushwa since he is a beneficiary of past corrupt regime.
 
Rais Jakaya Kikwete

Kwa bahati nzuri alisema, "kuna utashi wa kisiasa kwa upande wangu na kwa upande wa wenzangu wengi serikalini."
"Kuhusu hili, nina imani kubwa kwamba wakati tukiendelea na vita hii dhidi ya rushwa na hivyo kutuweka katika njia imara na sahihi ya kufikia malengo yetu," alisema.

Sisi wananchi wa kawaida tunawapima kwa matendo yao si maneno.
 
te anakubaliana kabisa na udhaifu wa serikali yake na taasisi zake ndio maana ameamua kutafuta huu msaada kwa wazungu
 
Back
Top Bottom