Kikwete anaongea na watanzania gani?

Mnyakatari

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
2,027
1,791
Hotuba ya raisi Kikwete imeacha maswali mengi.Anasema chadema wanaandamana kushinikiza mambo yaleyale walioyashupalia kipindi cha kampeni na watanzania hawajaridhika nao nandomana wamewanyima uongozi.Malipo ya dowans ni suala jipya,halikuwemo kwenye kamapeni!Kupanda kwa gharama za maisha hakujakoma baada ya ccm kushinda,kwa nini liachwe?Gharama za umeme pamoja na kupigiwa kelele lakini wameonekana wanahitaji nguvu zaidi ya shinikizo la maandamano.Anakwenda mbali zaidi na kuwaita chadema wapenda vurugu na machafuko na kwamba wanataka kumpokönya madaraka ambayo watanzania hawakuwapa!Hii nayo ni propaganda nyingine.Kazi za chadema kama chama cha siasa sio kushiriki uchaguzi pekee balh ni kuwapa elimu wananchi na kuwafumbua macho jinsi watawala waliowaamini wanavyoliangamiza taifa.Sasa chadema wanafanya kosa gani?Kama wanaenda kinyume na katiba kwa nini asiwafungulie mashtaka mbona yeye ndo amiri jeshi mkuu?Raisi anawambia watz wawapuuze chadema na mambo yao!Chadema ni akina nani?Ni wabunge na viongozi wote wa chadema au na ule umati unaofurika kwenye maandamano?Chadema sio watanzania?Anawaambia watanzania au anawambia CCM?Raisi anapoanza kuexclude kundi mojawapo kwakuwa tu eti linasema ukweli unaomuuma,anakaribisha machafuko.Raisi anatakiwa awe informed kuwa chadema si kundi dogo la watu bali ni kundi kubwa la watanzania.Yeye anaongea na watanzania gani?

Kaanza kusoma alama za nyakati na vuguvugu la mapinduzi ya nguvu za umma linamkosesha usingizi ndio maana kaanza kulalamika mapema ili ionekane ni CHADEMA ndio wanataka kumpokonya madaraka yake.

Hotuba ya raisi Kikwete imeacha maswali mengi.Anasema chadema wanaandamana kushinikiza mambo yaleyale walioyashupalia kipindi cha kampeni na watanzania hawajaridhika nao nandomana wamewanyima uongozi.Malipo ya dowans ni suala jipya,halikuwemo kwenye kamapeni!Kupanda kwa gharama za maisha hakujakoma baada ya ccm kushinda,kwa nini liachwe?Gharama za umeme pamoja na kupigiwa kelele lakini wameonekana wanahitaji nguvu zaidi ya shinikizo la maandamano.Anakwenda mbali zaidi na kuwaita chadema wapenda vurugu na machafuko na kwamba wanataka kumpokönya madaraka ambayo watanzania hawakuwapa!Hii nayo ni propaganda nyingine.Kazi za chadema kama chama cha siasa sio kushiriki uchaguzi pekee balh ni kuwapa elimu wananchi na kuwafumbua macho jinsi watawala waliowaamini wanavyoliangamiza taifa.Sasa chadema wanafanya kosa gani?Kama wanaenda kinyume na katiba kwa nini asiwafungulie mashtaka mbona yeye ndo amiri jeshi mkuu?Raisi anawambia watz wawapuuze chadema na mambo yao!Chadema ni akina nani?Ni wabunge na viongozi wote wa chadema au na ule umati unaofurika kwenye maandamano?Chadema sio watanzania?Anawaambia watanzania au anawambia CCM?Raisi anapoanza kuexclude kundi mojawapo kwakuwa tu eti linasema ukweli unaomuuma,anakaribisha machafuko.Raisi anatakiwa awe informed kuwa chadema si kundi dogo la watu bali ni kundi kubwa la watanzania.Yeye anaongea na watanzania gani?

Kikwete anataka Watanzania tujipuuze. Anahitaji kutuomba radhi

Well said mkuu...niliicheck ile hotuba, analia lia tu nothing more. Nani asiyeona hii hali ya maisha ilivyo kuwa mbaya ana bado wanacheka cheka tu ovyo they dont do anaything feasible. Umeme kila siku.. serikali gani hiyo. Aache kulalama afanye kazi.

anakuja na mbinu za kitoto kweli badala ya kuja na mbinu za kuweza kutukwamua kiuchumi na kuondoka na jinamizi la umeme na mfumko wa bei, acha kulia hovyo na CDM waache wazunguke na wewe kama una jeuri wajibu kwa vitendo kama vile mwisho wa mgao leo jioni, kuanzi kesho sukari, mafuta ya kula, pamoja na vingine bei chini wananchi watambue kweli sasa umedhamiria sio hotuba yote imejaa malalamishi ooooohhhh CHADEMA CHADEMA vuruguru ghasia tupe jipya

ni kweli ilitakiwa ajibu kwa vitendo zaidi! LAKINI HUYU JAMAA AMAFISADI ANAOWAKUMBATIA WATAMUUUA!

Huyu bwana hana jipya kabisa,hotuba ndeeefu isiyo hata na sentensi moja yenye kutia matumaini.Kulia lia tu,kwa taarifa yake moto ndo ushawashwa hii ni mpaka aikimbie nchi!

anaogopoa kufikishwa mahakama ya kimataifa na kunyimwa ruhusa ya kusafiri kama alivofanyiwa Ghadafi.

Hotuba ya raisi Kikwete imeacha maswali mengi.Anasema chadema wanaandamana kushinikiza mambo yaleyale walioyashupalia kipindi cha kampeni na watanzania hawajaridhika nao nandomana wamewanyima uongozi.Malipo ya dowans ni suala jipya,halikuwemo kwenye kamapeni!Kupanda kwa gharama za maisha hakujakoma baada ya ccm kushinda,kwa nini liachwe?Gharama za umeme pamoja na kupigiwa kelele lakini wameonekana wanahitaji nguvu zaidi ya shinikizo la maandamano.Anakwenda mbali zaidi na kuwaita chadema wapenda vurugu na machafuko na kwamba wanataka kumpokönya madaraka ambayo watanzania hawakuwapa!Hii nayo ni propaganda nyingine.Kazi za chadema kama chama cha siasa sio kushiriki uchaguzi pekee balh ni kuwapa elimu wananchi na kuwafumbua macho jinsi watawala waliowaamini wanavyoliangamiza taifa.Sasa chadema wanafanya kosa gani?Kama wanaenda kinyume na katiba kwa nini asiwafungulie mashtaka mbona yeye ndo amiri jeshi mkuu?Raisi anawambia watz wawapuuze chadema na mambo yao!Chadema ni akina nani?Ni wabunge na viongozi wote wa chadema au na ule umati unaofurika kwenye maandamano?Chadema sio watanzania?Anawaambia watanzania au anawambia CCM?Raisi anapoanza kuexclude kundi mojawapo kwakuwa tu eti linasema ukweli unaomuuma,anakaribisha machafuko.Raisi anatakiwa awe informed kuwa chadema si kundi dogo la watu bali ni kundi kubwa la watanzania.Yeye anaongea na watanzania gani?
kIKWETE anatakiwa atuombe radhi watanzania. Ametutukana. Hivi yote yanayotokea haya- mfumuko wa bei, matatizo ya umeme, ufisadi - wananchi hawana ufahamu ama uwezo wakuyajua mpaka wahamasishwe na Chadema?! ina maana sisi wananchi ni mambumbumbu kiasi hatuwezi kwa akili zetu wenyewe tukajua hili baya hili zuri? Ajue pia kuwa Chadema ni wananchi wa Tanzania na hayo magumu wanayolalamikia yanawapata na wao pia.

Nafikiri mheshimiwa Rais anasahau kwamba ni Rais wa watanzania wote ndani ya watanzania kuna wafuasi wa chadema,wafuasi wa CUF,kuna wafuasi wa CCM,wafuasi wa NCCR na hata UDP na TADEA. Kwa kutambua hilo hapaswi kuanza kuwabagua watanzania kwa itikadi zao bali anapaswa ku-address matatizo ya watanzania na kuwapatia majawabu ya matatizo mbali mbali wanayopitia.

Rais anapoanza kuhutubia taifa kama anahutubia mkutano wa chama chake anakuwa anaonyesha mapungufu makubwa.

Aachane na nini wanafanya Chadema kama chama bali ashughulikie matatizo ambayo wananchi wa nchi bila kujali vyama vyao wanayoyapitia toka alivyoingia madarakani miaka 6 iliyopita.

Suluhisho kwa viongozi wetu ni kuacha kumtumikia shetani na kumrudia mungu hapo ndipo majawabu ya matatizo yetu yatapatikana si kwa ushirikina wala kuwa na waganga wengi kutoka afrika magharibi au mlingotini.

Wana jf kuna mtuanaye mfahamu anaye mwandalia jk hotoba ? Kwani ukiangalia
Hotuba za maraisi wa awamu zote sijapata kusikia hotuba ya uswaazi kama hii
Imekua kama mipasho vile ! Badala ya kuonyesha mwelekeo ana lalamika sas kama baba mwenyenyumba analia je watoto watafanyaje?

Pole sana JK, kwani washauri ulio nao ni vilaza ila wewe ni kilaza zaidi. Nasema hivyo kwa sababu ungekuwa una uwezo kuliko wao usingekubali hizi hotuba ambazo zina kushushia hadhi yako. Raisi ni mtu wa kutoa maamuzi na kuya simamia kwa maslahi ya taifa lake, siyo mtu wa kulala mika eti CDM wanavuruga taifa na kuomaba huruma ya wananchi wa wakatae. Eleza mikakati ya muda mfupi na mrefu ya kupunguza ugumu wa maisha na msimamo wa serikali kuhusu malipo ya DOWANS, watu tumechoka siasa ambazo matendo yake hayapo. wewe na wenzako serikalini mnatembelea magari ya mamilioni, posho kubwa, mishahara mizuri wakati wengine hatuna hata huduma ya afya au chakula na shule zetu hata waalimu hazina then unatuambia sisi tusubiri wakati wengine mnakula raha, ipo siku nyie mnaokula raha leo mtaonja machungu tunayo yapata.

Hotuba ya raisi Kikwete imeacha maswali mengi.Anasema chadema wanaandamana kushinikiza mambo yaleyale walioyashupalia kipindi cha kampeni na watanzania hawajaridhika nao nandomana wamewanyima uongozi.Malipo ya dowans ni suala jipya,halikuwemo kwenye kamapeni!Kupanda kwa gharama za maisha hakujakoma baada ya ccm kushinda,kwa nini liachwe?Gharama za umeme pamoja na kupigiwa kelele lakini wameonekana wanahitaji nguvu zaidi ya shinikizo la maandamano.Anakwenda mbali zaidi na kuwaita chadema wapenda vurugu na machafuko na kwamba wanataka kumpokönya madaraka ambayo watanzania hawakuwapa!Hii nayo ni propaganda nyingine.Kazi za chadema kama chama cha siasa sio kushiriki uchaguzi pekee balh ni kuwapa elimu wananchi na kuwafumbua macho jinsi watawala waliowaamini wanavyoliangamiza taifa.Sasa chadema wanafanya kosa gani?Kama wanaenda kinyume na katiba kwa nini asiwafungulie mashtaka mbona yeye ndo amiri jeshi mkuu?Raisi anawambia watz wawapuuze chadema na mambo yao!Chadema ni akina nani?Ni wabunge na viongozi wote wa chadema au na ule umati unaofurika kwenye maandamano?Chadema sio watanzania?Anawaambia watanzania au anawambia CCM?Raisi anapoanza kuexclude kundi mojawapo kwakuwa tu eti linasema ukweli unaomuuma,anakaribisha machafuko.Raisi anatakiwa awe informed kuwa chadema si kundi dogo la watu bali ni kundi kubwa la watanzania.Yeye anaongea na watanzania gani?

Mimi ninaona aibu. Amri jeshi gani muoga hivyo! analia lia tu oh:blah::blah::blah: badala ashughulikie matatizo yaliyopo..........ameonyesha udhaifu mkubwa sana kwa kweli. Mimi i doubt kama atamaliza kipindi yake ya miaka mitano. Juzi tu wameumbuka baada ya Gomz kulipuka mabomu. Hawakujifunza chochote kwa Mbagala. Sijui anataka mpaka watu wangapi wafe au mabomu yalipuke na kwingine. Suala ya Dowans sijui yeye anali rate vipi. Vitu vimepanda gosh! things are getting crazy. Let me break first.

Wana jf kuna mtuanaye mfahamu anaye mwandalia jk hotoba ? Kwani ukiangalia
Hotuba za maraisi wa awamu zote sijapata kusikia hotuba ya uswaazi kama hii
Imekua kama mipasho vile ! Badala ya kuonyesha mwelekeo ana lalamika sas kama baba mwenyenyumba analia je watoto watafanyaje?
January na Yusufu Makamba

Kazi kuu ya chama cha upinzani ni KUIONDOA MADARAKANI SEREKALI ILIYOPO NA KUCHUKUA NAFASI HIYO.. Na hicho ndicho wanachokifanya CHADEMA hivi sasa. Ubaya uko wapi?

Back
Top Bottom