Kikwete analipanga jeshi kwa sababu ya mgogoro na Malawi; au majukumu ya Kimataifa pia?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
umetoa point nzuri sana na ambayo inahitaji kuangalia kwa karibu.

a. Je, yawezekana kuna wanajeshi wengi wa vyeo vya chini ambao walicheleweshwa kupanda vyao kwa wakati katika miaka hii sita? Au walirukwa vyeo?

b. Je, kuna wastaafu wengi wanakuja katika vyeo hivyo ndani ya miezi michache ijayo?

Jambo moja kubwa na la msingi ni kuwa hili si jambo dogo. Misri chini ya Morsi imewastaafisha baadhi ya majenerali kwa mkupuo na ikawa habari ya kimataifa; ilitokea pia Uturuki baada ya Chama cha Kiislamu kushika madaraka. Kwa Tanzania inabidi hili liangaliwe kwa karibu kwani ama ni udhaifu wa hali ya juu vinginevyo naliangalia kwa yale yaliyotokea kati ya Malawi na Tanzania.

Lakini vile vile tumesikia kuwa Tanzania imeombwa na sasa imekubali kuongoza kikosi cha kimataifa cha Africa huko Congo. Na wanaokumbuka tayari Marekani iliiomba Tanzania kupeleka wanajeshi Somalia (TZ ilikataa na kukubali kutoa mafunzo tu).

Mabadiliko haya si ya kawaida na hayawezi kuchukuliwa kwa kawaida na majirani zetu na taasisi za kimataifa za kiinteligensia. Ni makubwa mno kutokea kwa wakati mmoja.

Note:

Ukiangalia majina ya waliopandishwa vyeo utaona kuwa hatujaambiwa wanapangiwa majukumu gani mapya au wanapewa kazi gani mpya (ukiondoa ya Chief of Staff na yule wa JKT).

Maswali yamebakia.
 
kwani walioko sasa hawawezi mkuongoza vita ama yahusianayo na kijeshi mpaka achague wengine?

is that kind of strategic plan ?
 
... au huu ugawaji wa vyeo kama pipi dakika za ukingoni ni sehemu ya vijimotisha katika kupanga baadhi ya makada wa CCM jeshini ili waje wakalipigia chapuo la kiana hiki chama tawala mara baada ya kushindwa kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu 2015?????
 
1000xf.jpg


1000xx.jpg
 
MMM, A na B zote zinaweza kuwa jibu sahihi! Ila cha msingi, kwa hali jinsi ilivyo, binafsi naona ni busara zaidi kwa jeshi letu kushiriki mara kwa mara katika hizi operations ili kuimarisha jeshi na kuwapa tactics mpya za mapambano. Kuna habari moja inaelezea ugunduzi mkunbwa wa gesi na mafuta kiasi katika maziwa na bahari tunayoshare nayo mipaka, inaweza kuleta mtafaruku mkubwa sana na majirani. Ni vizuri kujiandaa kutokana na hali ilivyo sana.
 
MMM, A na B zote zinaweza kuwa jibu sahihi! Ila cha msingi, kwa hali jinsi ilivyo, binafsi naona ni busara zaidi kwa jeshi letu kushiriki mara kwa mara katika hizi operations ili kuimarisha jeshi na kuwapa tactics mpya za mapambano.

Kuna habari moja inaelezea ugunduzi mkubwa wa gesi na mafuta kiasi katika maziwa na bahari tunayoshare nayo mipaka, inaweza kuleta mtafaruku mkubwa sana na majirani. Ni vizuri kujiandaa kutokana na hali ilivyo sasa.
 
Mzee Mwanakijiji a greet you!

JWTZ is one of the few remaining institutions in the country that makes us feel proud as Tanzanians, lets respect whatever they are doing, and whoever is doing for them.
 
Mzee Mwanakijiji a greet you!
JWTZ is one of the few remaining institutions in the country that makes us feel proud as Tanzananians, lets respect whatever they are doing, and
whoever is doing for them.

Ooooooooooooh!!!! :doh:
 
Mzee Mwanakijiji a greet you!JWTZ is one of the few remaining institutions in the country that makes us feel proud as Tanzanians, lets respect whatever they are doing, and whoever is doing for them.
Waliofanya kuwa jeshi kuwa adilifu hawapo tena! Lijesh lisisile! Tuuachie muda uhukumu!
 
Back
Top Bottom