Rais Jakaya Kikwete leo amemgeukia mbogo waziri Magufuli kwa kumwambia waziwazi kuwa aache ubabe na mpango wake wa Bomoa Bomoa wakati wa ziara ya Rais alipotembelea wizara ya Ujenzi leo hii.
Huu unaonekana ni msumari mwingine kwa mpiganaji Magufuli, kufuatia msumari wa kwanza uliogongelewa na Pinda wakati akiwa Bukoba hivi karibuni.
Hapo awali magufuli aliwataka 'Wajenga Hovyo" kando kando ya hifadhi za barabara kuwa wanabomoa wenyewe kwa kipindi kifupi. Now Mheshimiwa JK amemuagiza kuwapa "Hata miaka miwili" na kuwalipa na fidia.
Kazi inaendelea.... Je, Magufuli kuamua kujiuzuru kama tetesi zilivyosambaa hapo awali?
Binafsi, sikubaliani na utaratibu huu wa kuendesha vikao na kufanya maamuzi hadharani. Masuala haya ya Pinda, JK na hata Magufuli mwenyewe wangeweza kuyafanya na kukubaiana katika vikao vya baraza la mawaziri badala ya kutengeneza sinema hadharani.
I striongly believe they are trying to create "storyboard" for winning public attention kwenye masuala yasiyo ya msingi na kusahau yanayogusa maisha yao moja kwa moja.
Kama kiranja mkuu ametenda hivyo unavyotulipotia,napata swali la kujiuuliza kwamba,hivi magufuli huwa anafanya kazi zake kwa kutumia ubabe au kwa kufuata sheria na taratibu za nchi? au ukisimamia sheria unakuwa mbabe? kama hili la pili ni ndio, namshauri jeyikkeyi nae awe mbabe kama magufuli ili ainusuru nchi hii toka mikononi mwa wakoloni weusi(mafisadi) Wanaoi -xploit nchi hii.ASIWAHADAE wananchi waaliokiuka sheria,akumbuke siku zote ukweli UTASIMAMA DAIMA!