Kikwete amteua wakili wa Lulu kuwa Jaji

Komba alikua anapiga na ndo ulikua mzigo wake, ila Kanumba alikua wa usiku wa manane tu na ndo maana hakuna udaku uliokuwepo juu ya Lulu na Kanumba hadi kifo kilipowaumbua. Kanumba alikua anaiba kwa Komba.........
Komba tumbotumbo? Ndiyo maana wanalilia kuongezewa posho.
 
http://www.mwananchi.co.tz/habari/5-habari-za-siasa/24043-rais-amteua-wakili-wa-lulu-kuwa-jaji

Yupi katika walioteuliwa unafikiri hana weredi?
Nashauri tuwe tunafuatilia kwanza weredi wao ndio tuseme huyu hafai huyu anafaa.
Hapo juu nimetoa link ambayo unaweza pata kwa kifupi weredi wa huyo tunaemjadili hapo na si tujadili sababu alikuwa wakili wa Lulu kama wengi wanavyoelezea hapo.

Pia kuteuliwa haimaanishi lazima uwe kibaraka wa aliyekuteua hata siku moja, hiyo ni hulka ya mtu binafsi kama ana dhana ya uoga hata asipoteuliwa akipewa nafasi fulani atakuwa hivyo tuu. Tunao watu wa namna hiyo wengi tu na sio wa nafasi za kuteuliwa, pia wapo wa nafasi za kuteuliwa ambao wanafanya kazi kwa kufuata
sheria misingi na Taratibu.

Naomba tumtumie huyu mama kama sample
Naomba utupe mchango wake katika Tasnia ya Sheria na Haki katika nchi yetu ama duniani kwa ujumla so far. Kuna sehemu imesemwa hapa kwamba amepata tuzo ya mwanamke jasiri wa mwaka 2012 ukitaka kutumia tuzo hii kama justification naomba utueleze hapa waliompa tuzo hiyo ni nani na walitumia basis gani kumpatia, sababu kuna vyuo mpaka sasa vinasubiri upepo utulie kidogo vimpe DR kikwere shahada ya Udaktari wa nini sijui.

Karibu.
 
224960_126471244096505_100002008907798_183410_2770049_n.jpg


Huyu mtoto kagonganisha na kuchanganya vichwa vya watu, hata akina Komba wamo sasa nani atabaki kuhusishwa katika sokomoko hili?

Komba nae na mkitambi wake? duh!
 
Hizi teuzi za huyu jamaa mie basi tena, hapo ukipigwa changa la macho utadhani una tija kwa taifa.....nyuma ya pazia
utakuta ni ndugu/jamaa za watu wale wale.

Hiki chombo kinayumba sana na mawimbi na upepo bado yanapiga sijui, lini tutafika nchi kavu
 
Kwani huyu mtu ana sifa au hana sifa?

Ina maana kumtetea Lulu iwe disqualification ya kuwa jaji?? teh teh teh


Kwa hiyo unataka kusema laisi alikuwa na bifu na mwigidhaji hadi amtetee anayetuhumiwa kumuua?

No wonder Diamond naye kawa fliimasoni baada ya kufanikiwa
 
Naomba tumtumie huyu mama kama sample
Naomba utupe mchango wake katika Tasnia ya Sheria na Haki katika nchi yetu ama duniani kwa ujumla so far. Kuna sehemu imesemwa hapa kwamba amepata tuzo ya mwanamke jasiri wa mwaka 2012 ukitaka kutumia tuzo hii kama justification naomba utueleze hapa waliompa tuzo hiyo ni nani na walitumia basis gani kumpatia, sababu kuna vyuo mpaka sasa vinasubiri upepo utulie kidogo vimpe DR kikwere Educational Backgroung yake.

Karibu.
As great thinker ongea kitu ulicho na uhakika usipende kusema .......sijui nini.
Amepewa Tuzo na sio Shahada kama unavyolinganisha hapa.
Kama hufahamu Educational Backgroung yake kwanini unaanza kum critisize mtu usiyejua?
Fuatilia Hiyo tuzo hutolewa kwa mtu wa namna gani, imetolewa na nani utafahamu tu.
 
224960_126471244096505_100002008907798_183410_2770049_n.jpg


Huyu mtoto kagonganisha na kuchanganya vichwa vya watu, hata akina Komba wamo sasa nani atabaki kuhusishwa katika sokomoko hili?

Haka katoto siku kakizaa mtoto atakayezaliwa litakuwa janga kuu,
maana hiyo kolabo inayofanyika si mchezo.
 
As great thinker ongea kitu ulicho na uhakika usipende kusema .......sijui nini.
Amepewa Tuzo na sio Shahada kama unavyolinganisha hapa.
Kama hufahamu Educational Backgroung yake kwanini unaanza kum critisize mtu usiyejua?
Fuatilia Hiyo tuzo hutolewa kwa mtu wa namna gani, imetolewa na nani utafahamu tu.
sizungumzii elimu yake, nazungumzia mchango wa elimu yake katika tasnia ya sheria na utoaji wa haki, unanifanya nianze kuhoji weledi wako sasa kama hauoni shahada za udakitari za Jakaya ni sawa na tuzo.

Alafu acha kunipiga chenga, nieleze hiyo tuzo imetolewa na nani na basis ya utoaji wake ni nini, kama na wewe haufahamu achia watu wanaojua waje watueleze, sio unaandika andika tu mambo yasiyo na msaada,
 
Acha kujishaua, Kama ujaji ni profession, ni profession inayowajibika kwa UMA, unaposema hapa kwamba iko corrupted hauwezi kujustify kwamba ongezeko la majaji litapunguza corruption.

Kama kuna incompetence yoyote ambayo inajikita kwenye mahakama zetu kutokana na appointment za namna hii, utegemee Rushwa kuongezeka zaidi.

Labda niende kwenye Point sasa.
Rais Kikwete ni maarufu sana kwa kufanya teuzi za watu dhaifu kwenye utendaji wao, tunaendelea kuliona hili kutoka kwenye baraza lake la mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya, na wakurugenzi wa mashirika ya UMA na hata kwenye Chama, analalamikiwa kwamba anafanya teuzi hizi kwa misingi ya ulafiki na mahusiano ya kifamilia mpaka mahusiano ya Kingono, sasa kwa namna tunavyoelewa umuhimu wa majaji katika mahakama zetu au Taifa kwa ujumla unategemea ni kwa nini nisiwe na wasi wasi kwamba uteuzi wa namna ile ile unatumika kutupatia majaji. Unanihakikishia vipi professionalism katika mazingira kama haya?
acha kujamba jamba maputo ndugu..wewe unajua nikisema proffession namaanisha nini?? Maana yangu ya kusema proffession ni Legal Proffession, ambayo hata hao majaji wamo...the legal proffession is not only confined to lawyers but did cut across all the other learned fellow Judges being among them..Ndio namfahamu De mello and she is good Kikwete Hakukosea..inawezekana hata humfahamu lakini napiga kelele tu kuwa hafai bila kuujua utendaji wake...Unaposema dhaifu hiki kipimo umekitoa wapi kwa mtu ambaye hata humfahamu?? sembuse kufanya nae kazi...be realistic..
 
Tupo hapa tulipo kwa sababu ya UDHAIFU wa Rais Kikwete, Bunge legelege na upuuzi wa CCM- J J Mnyika - Mbunge Ubungo
 
Jamani huyu mwanamke ni NOUMER na anadiserve that cheo ni kati ya wanawake wachache wasomu...ila ukimuona physicaly ni balaa SHEPU HILOOO...kiuno kama nyigu HIPS;WOWOOO uwiiii....enzi za ujana sijui ilikuaje maana me nilimjulia st joseph aalikua anasali sana misa za asubuhi miaka hiyooo ya mkapa
 
224960_126471244096505_100002008907798_183410_2770049_n.jpg
images


Rais amteua wakili wa Lulu kuwa Jaji

RAIS Jakaya Kikwete amemwapisha kuwa Jaji wakili wa kujitegemea, Joaquine De-Mello ambaye alikuwa akimtetea msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) anayetuhumiwa kwa mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba.

Wakili huyo, ambaye ni mshindi wa tuzo ya Mwanamke Jasiri Tanzania ya Martin Luther King ya mwaka 2012 na ambaye alikuwa pia alikuwa mmoja wa makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) ni miongoni mwa majaji 10 walioapishwa jana na Rais Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
De-Mello ni miongoni mwa mawakili wanne waliojitokeza Aprili mwaka huu kumtetea Lulu katika kesi hiyo ya mauaji inayomtuhumu kumuua usiku wa kuamkia Aprili 7, mwaka huu.

Mawakili wengine wanaomtetea Lulu ambaye umri wake umekuwa na utata ni Kennedy Fungamtama, Peter Kibatala na Fulgence Massawe.

Akizungumza kwenye viwanja vya Ikulu, De-Mello alisema baada ya kuteuliwa kuwa Jaji, sasa atafanya kazi hiyo na moja ya mikakati yake ni kukabiliana na changamoto za wingi wa kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

Hii habari inahusiana vp na hili jukwaa la siasa??
 
Majaji hawatoshi...nyie ambao mpo nje ya proffession hamjui kero zilizomo...basi kama hamjui uchache wa majaji ndio mojawapo ya sababu kubwa za rushwa katika mahakama maana kuahirishwa kwa kesi mara kwa mara kutokana na wingi wamashauri na uchache wa majaji na mahikimu..wafanyakazi wengine wa mahakama hutumia mwanya huo kufanya michezo michafu kwa minajili ya kujipatia kipato..ila kama mashauri yanasikilizwa kwa wakati basi hata mianya ya rushwa itapungua

Umeongea ukweli mkuu, watu walio nje ya taaluma ya sheria hawaelewi hili suala wanabaki kulaumu tu.
 
Back
Top Bottom