Kikwete amteua Peter Noni Mkurugenzi mpya TIB!

Kwanza hii INATISHA sana. Lakini kuna mambo ya kuweka kumbukumbu sawa. Kwanza kubwa ni kuhusu kampuni ya Mirambo inayomilikiwa na familia ya Rostam, Noni hakuficha share zake Mirambo, bali ameuza kwa RA aliyeamua kuhamishia zile za Caspian katika Mirambo. Wanaweza kuwa wanajua wanachokifanya kwa kuwa kuna watu wengine wako nyuma yao (viongozi wa sasa na wa zamani). Inawezekana waliamua kufanya hivyo ili waweze kutekeleza ule mpango wao wa kuuza hisa zao South Africa na tayari walikwishakutumia hisa hizo kuchukua fedha kutoka benki ya NedBank ya Afrika Kusini. Tukumbuke madudu yote ya Meremeta na Tangold, NedBank inahusishwa na wakurugenzi wa benki hiyo ni wanahisa wa Deep Green (dudu jingine).

kwa hiyo, kwa Noni kufanywa shahidi, kwa Noni kuteuliwa kwends TIB, kwa Rostam (Kagoda) kutoshitakiwa, kwa Maregesi na wengine kutoshitakiwa (japo kwa sasa) na kwa RA kutetewa kwa nguvu zote na kwa TICTS kuendelea kupeta (Karamagi&RA) tunapata picha moja kubwa ya kutisha ambayo kwa maoni yangu (wengine watafikiri kivyao) ni kwamba:

Kuna SIRI NZITO itakayokuja KUTIKISA NCHI ikiwa WATANZANIA (kokote duniani katika nafasi zote) WATAAMUA kusema SASA INATOSHA.(Nitaeleza kwa kina kwa wakati mwafaka).

Hoja ya pili ni kuhusu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TIB,William Mlaki: Mlaki ni mmoja w awatuhumiwa wa kesi ya wizi wa fedha za CIS akiwa na Yussuf Manji na mwanamke mmoja anayetajwa kwa jina la Rehema. Hao watatu walikuwa tayari wameandaliwa mashitaka kwa DPP, tayari kupelekwa Kisutu, tokea mwaka 2007. Jambo la kusikitisha na kutisha zaidi ni pale kesi hiyo ilipoyeyuka, na huenda sasa inaweza kufikishwa mahakamani baada ya Mlaki kustaafu (kama alivyofanywa Mgonja). Kwa muhtsari nchi hii imekuwa ya KUSADIKIKA, maana hatuna uhakika wa kitakachotokea.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WALAANI MAFISADI, BABA UTULINDE TUJIKOMBOE
 
- Maneno mazito sana mkuu Halisi, kama kawaida yako na tupo pamoja sana hapo!

Respect.

FMEs!
 
baada ya kumsoma Halisi nimepata picha halisi....asante sana mkuu
 
Kikwete to announce stimulus for economy
Sawa Kuiga Stimulus au Bailout kama Marekani. Muiga tembo kunya ****** hupasuka!!!

Tumejiandaaje au ni kukurupuka hatimae pesa ziishie kwa makampuni mafisadi.

Jamani watuambie hizo pesa wamepata wapi?

Pia hiyo stimulus itainuaje uchumi.

Inatakiwa kama kuna pesa zipelekwe kwenye CRDB, NMB,NBC,TIB ili wajasiriamali wadogo wapate sio zikopeshwe kwa makampuni makubwa iwe kama EPA au Import Support Bil 216 ambazo hazilipiki.

Kwa nini NSSF,NPF inakopesha viongozi na watu wengine Lakini wafanyakazi wanaochangia Hawakopeshwi???

Wafanyakazi wanaochangia NSSF wanatakiwa wapewe nafasi ya kukopa hela zao.

Nafikiri Stimulus package ingepelekwa Kilimo, mbolea ya ruzuku ikaongezwa, mbegu, matrekta.

Hakuna dili hapo, ni wizi tu

Connecting dots
 
TIB CEO si mteule wa Rais bali ilipaswa nafasi kuombwa na bodi kuteua mtu mwenye sifa. Alikosea kwa Mataka, akakosea kwa Ramadhani Khalfani wa BET na sasa TIB ambayo naona afadhali ya hao kina Mataka na Khalfan
 
Halisi asante sana. Nimepata picha nzuri sana, ni kama umenipa tochi ya mwanga mkali kama ile ya migodini.
 
TIB CEO si mteule wa Rais bali ilipaswa nafasi kuombwa na bodi kuteua mtu mwenye sifa. Alikosea kwa Mataka, akakosea kwa Ramadhani Khalfani wa BET na sasa TIB ambayo naona afadhali ya hao kina Mataka na Khalfan

Hizi huyu RAmadhani Khalfan siyo ndugu yake Mkulu kweli?ila Katika Nchi ya AMani kila jambo linawezekana na wakti mwingine inabidi tukubali..Je tukubali yaishe??
 
Fisadi papa RA ndiye RAis wa Tanzania?

Yaelekea huyu Noni anaenda kudhibiti pesa za EPA zilizopelekwa TIB. Lengo ni kuzitumia kifisadi kwa Uchaguzi 2010.

Mtimti ndiye mwenyewe Noni au?
 
Huu ni ushirika wa CHAMA tawala na waliomo wote wanajua nini kinaendelea, haishangazi sisiemeu wataendelea kushinda hadi tutakapojiuliza zile bakhshishi tunazohongwa wakati wa uchaguzi zinatoka wapi!
 
Ndugu zangu msisahau kwamba huu ndiyo utamaduni wetu.

Wakati watu wanalalamika kuhusu Zombe kwa mauaji na unyang'anyi; Mahita anampandisha cheo kuwa RPC Rukwa,

Wakati wana Shinyanga wanalalamika kuhusu mwenyekiti wao wa jumuiya ya wazazi kwa ubadhilifu, Mkapa anamteua kusafiri naye kwenye ziara za raisi,

Wakati watu wanalalamika kuhusu mzee wa vijisenti; CCM wanamteua kwenye kamati ya kuchunguza mkataba wa kifisadi wa UVCCM na jengo linaendelea kujengwa.

Wakati Hussein mwinyi alikacha JKT; anapewa kuingoza wizara ya Ulinzi na JKT!

Wakati mkuu wa wilaya ya Nyamagana anatetea uwanja usibinafsishwe na kubalishwa matumizi yake, mkulu anamstaafisha,

Wakati Mwakyembe anatetea NBC isiuzwe, wakubwa wanamuondoa kwenye bodi ya NBC,

Wakati Ibrahimu Katuma anatetea NMB isiuzwe; anaondolewa uenyekiti wa bodi,

Wakati TANESCO wanapinga kuletewa uongozi wa Net Group solution; Net group solution wanaingizwa kwa mtutu wa bunduki na virungu vya FFU

Wakati Mengi anataja majina ya mafisadi papa serikali inamjia juu na kutaka kubadilisha sera ya vyombo vya habari;

Wakati fisadi RA anataka kumtaja Mengi kama fisadi nyangumi na mkwepa kodi serikali unamruhusu kutumia TBC1.

La Jakaya kumpa ulaji Noni sio la ajabu jamani, ndiyo utamaduni wetu!

Jibaba umenena. Sasa tutumie Ballot Box kubadilisha haya madudu. Tuwaondoe RA a.k.a RAis wa Tanzania na wapambe wake wote kama JK na EL(anayesubiri kurudi kwenye uongozi baada ya 2010)
 
Jaquline Noni, mke wa Peter Noni, ndiye aliyekuwa akiandamana na Salma Kikwete wakat wa kampeni za 2005
 
Acha hizo wewe mkuu wangu, kuwa na elimu ya A kwenye vyeti si maana kuwa wewe ndiye mtendaji sana!!! Kwanza vipanga wengi huwa si watendaji wazuri. Kama kweli Peter Noni ni mtendaji au kiongozi mzuri mbona hakuweza kutumia elimu yake kuzuia wizi wa EPA. Yeye kuna watu aliwabariki pale wakapata fedha zile chafu. RA RA RA RA, oh oh oh, Noni anafahamu vema dili zake. Na kwa kuwa RA ni Rais kivuli wa Tz ni lazima atamteua Noni kupitia msemaji ceremonial!!!

Halafu wakuu, fahamu kuwa the so called TIB ndiko zile pesa za EPA zinapelekwa, zitatumika kwa uchaguzi!!! Wewe subiri!!! Kama kweli ni za kununulia au kusaidia kilimo, kwa nini zisitumike kununua na kusambaza ile Mbolea kule kiwanda cha Minjingu??? Oh Oh Oh. Kingine ni kuwa TIB itakuwa (natumaini kazi imeshamalizika year 2007/2008) a morgage bank, sasa niambie who will benefit with that??? Oh Oh mafisadi papa bwana.

Majuzi naye huyo Peter Noni, aliteuliwa tena kuwa bodi member wa taasisi fulani hivi????? Of course anayeteua bodi member kwa taasisi za serikali ni Waziri mwenye dhamana!!! Waziri alisema wazi kuwa bodi member wale waliteuliwa kwa baraka zake mwenye Nchi!!! I laughed!!!

aisee aliteuliwa bodi ya taasisi gani tena?
 
Jaquline Noni, mke wa Peter Noni, ndiye aliyekuwa akiandamana na Salma Kikwete wakat wa kampeni za 2005

Duh, kumbe mipango ilianza zamani ! - sasa picha kamili yaanza kuwa wazi hata kwa kipofu wa kutupwa.

1. Bhyidinka Michael Sanze, wakili katika kampuni ya mawakili ya Malegesi – Malegesi Law Chambers – ya Dar es Salaam, anaitwa ofisini kwa Bw. Rostam Aziz.
2.
Anapopofika anawakuta Bw. Rostam Aziz, Peter Noni na Bw. Malegesi na kupewa“documents" – nyaraka ambazo zimeshaandaliwa na kuombwa azi-sign.
3. Anaposita anathibitishiwa kuwa zina baraka zote za Rais Mkapa ambaye amemwagiza Gavana Balali kutoa fedha hizo kwa Rostam kugharamia uchaguzi wa CCM.

Hivi sasa Balali ni marehemu, Mwandosya ni mshtakiwa lakini Noni kaula TIB. Nina wasi wasi Noni amekuwa mshiriki toka hatua za mwanzo kabisa - yeye na Balali ni kama Anthony na Brutus. Lakini kwa kuwa mpaka sasa amecheza karata zake vizuri ndiyo maana anazawadiwa. Nakubali Noni ni kichwa kama anavyodai Mtimti -
was Balali stabbed in the back by Noni ?
 
Unajua,watu wanamuhusisha NONI na EPA kwa sababu idara yake ndio ilikuwa inashughulika imekalia hizi fedha na yeye ndio alikuwa anatoa mapendekezo kuwa walipwe,lakini ikumbukwe kuwa huu mchezo ulikuwa unaanzia kwa balali kisha anapeleka kwa katibu wa benki na katibu anampelekea noni ili atoe mapendekezo (sio idhini),idhini alikuwa anatoa mwenyewe balali,pia wengine walikuwa wanaanzia huku kwenye idara ya madeni na mikopo ambaayo ilikuwa inaongozwa na mwakosya na komu(washtakiwa wa EPA),hukun walikuwa wanakuja na nyaraka feki na kampuni za uongo na hii idara inapitisha madai yao kisha mkulu balali anaidhinisha noni atoe pesa,sasa hapo unaweza sema noni ni mwizi kwa kuwa kashuhudia uchafu?au utamweka awe shahidi ili aeleze jinsi uchafu ulivyokuwa unafanyika?

Kuna mawili hapa,

Ama wewe ndie Peter Noni au una maslahi ya aina fulani in relation to Peter Noni. Mbona huko juu sana kumtetea huyu jamaa wakati wakili aliyekwenda kusaini makaratasi kwenye ofisi ya RA (Kagoda syndicate) anasema na Peter Noni alikuwepo? Mbona yeye hajawahi kukanusha dai hili?

Tafuta gear mpya hizo unazo kuja nazo ni za kitoto tu!!!!!

Tiba
 
nimegundua kuwa wengi hapa mnaandika ama mnashabikia tu kitu ambacho hamkijui,katika mabandiko yote sijaona hata moja lenye kumhusisha noni na ufisadi zaidi ya ushabiki tu ufisadi,ufisadi,ufisadi.
wengi humu ama hamjui au hamna history ya noni hivyo mnajaribu kuunganisha unganisha sentensi za uongo na ushabiki ili kumweka kwenye kundi la mafisadi,mmoja kasema kuhusu jaq noni kuwa swahiba na mama salma,hiyo ni kweli lakini haimfanyi kikwete kuchagua watu wabovu kwenye serikali yake.
kuna watu wamenichana sana kwenye mabandiko yao kuwa nanufaika na pesa za noni ama mimi ndio noni mwenyewe lakini nasema kwamba,kumjua na kumfahamu noni hakutonifanya nimfichie madhambi yake,namfahamu noni kuwa ni mtu mwadilifu,mwenye busara na heshima na mwenye kufuata maadili ya kazi,hivyo sintoacha kumtetea kwa nguvu zote pindi nnapoona watu ambao hawamjui wala hawajui lolote kuhusu noni wakileta ushabiki wao tu hapa wa kufuata mkumbo
nawasilisha
 
Jaquline Noni, mke wa Peter Noni, ndiye aliyekuwa akiandamana na Salma Kikwete wakat wa kampeni za 2005

Kuandamana na mtu wakati wa kampeni haimaanishi kwamba ni fisadi. Ina maana Mwl. Nyerere naye ni fisadi kwa kuandamana na Mkapa Tanzania nzima kumpigia debe mwaka 1995?
 
mwenye contacts za huyu jamaa chonde naomba mnipatie. Ningependa kuzungumza naye juu ya mikakati na mipango yake ya kuiboresha TIB!
 
mwenye contacts za huyu jamaa chonde naomba mnipatie. Ningependa kuzungumza naye juu ya mikakati na mipango yake ya kuiboresha TIB!

Sasa bushman kid hapa hueleweki. Mwenye contact tena kivipi wakat i swahiba wake Mtimti ameshajipambua kuwa yko karibu naye kuliko hata mkewe. Mwambie akupe contact ambazo anazo kwa kina.
 
Noni ni mchapa kazi mzuri sana. SIna shaka na uteuzi wake. Namfahamu vizuri na sina interest yeyote kwake. Ameenda shule vizuri na ni muwajibikaji.
 
Noni ni mchapa kazi mzuri sana. SIna shaka na uteuzi wake. Namfahamu vizuri na sina interest yeyote kwake. Ameenda shule vizuri na ni muwajibikaji.

Mko wengi mnaofaidika na wizi wake. Bahati nzuri kwenu na bahati mbaya kwa wanaharakati wa JF sheria za JF haziruhusu kuanikana hadharani lakini mnafahamika mlivyokuwa mnamganda huyo noni wakati wa vikao vya harusi vya mwizi mwingine noni type (mtoto wa jenerali mstaafu Mayunga)mwaka 2006.
 
Back
Top Bottom