Kikwete amtema rasmi Lowassa

Niliwahi kusema kuwa hata "CCM imsimamishe NYAU" kugombea urais ni lazima atangazwe mshindi. Kwa hiyo sioni ajabu kwa mipangilio hii ya kurithishana vyeo. Ila JK angefanya kitu cha mbolea sana kama angemchagua Dr. Salim kumrithi
 
Hivi hili gazeti limespecialize kuandika habari za Lowassa tuu... hili ni toleo la nne in a row, heading ni Lowassa tuu, au ndio njia nyingine ya kumsafisha? Si wangeliita Mwanalowassa tujue moja
 
Hongera sana mzee wangu dr shein kwa kuwa jasiri kiasi hicho, nadhani hilo hata mimi mwanao nilikuwa nategemea ungelifanya, hakuna aliye na shaka juu ya uongozi wako utapokuwa smz, hiyo ndio karima aliyokupa m.mungu. Kila la kheri mzee shein
 
wasipopigiwa kura hawatatawala, ila ndio hivyo CCM bado inatutawala itakavyo na sie tunawaruhusu.
 
Unajua tatizo ni la wananchi wenyewe wanaiamini sana ccm hata kama wanamweka mtu yeyote ili mradi ni wa ccm basi anapewa kura kibao na ndio maana ccm ina jeuri ya kurithishana tu uongozi kadri wanavyotaka.
ni kweli mkuu
, tatizo wamelewa ''mvinyo chapa CCM'', hawaoni hawambiliki, wanaumizwa lakini hawasikii maumivu, wakilizwa kidogo tu, utasikia bwaaaa!! lakini kesho wamesahau tena

mtumiaji wa mvinyo huu, daima hana huruma, tena huwa mwizi wa mali za umma, ana ahadi za uongo, ni fisadi, mropokaji nk
 
Bla blah za kubenea na chuki zake kwa EL,RA na kujikomba kwake kwa Muungwana na Mengi
 
Nchi hii imekuwa ya holela kwelikweli. Wakuja wanachukuwa kutwaa ardhi, na biashara. Kwa mfano Wachina wanafanya 'umachinga' hapa as if wako kwao na sidhani iwapo wazalendo hapa watakubaliwakufanya biashara za kimachinga kwao. Serikali iko kimyaaaa. Halafu sasa urais wa holela -- wa kuachiana tu utafikiri usultani. Mwee jamani!!!!!

Hivi karibuni Gwangzhou (CANTONE) imeingiliwa na machinga weusi toka nchi mbali mbali za Afrika.
 
I have never read such nonsense as this one! Yaani yule ambaye hajatenda lolote la maana kwa watu wake katika miaka 10 iliyopita, yule 'Rais' ambaye huteremshwa kutoka kwenye majukwaa na wapambe kutokana na kuunyaka kisawasawa, yule kiongozi ambaye aka 'Chai Jaba' -- ndiye awe Rais wa Muungano? NO WAY!!!

Hivi hii nchi sasa imekuwa ni ya holela? Yaani any impostor can be President? MY GOD!!

Yawezekana tatizo ni wewe kukubali PROPAGANDA holela kama hizi bila hata kuchukua hatua za kujua undani na zaidi maslahi ya waendesha propaganda hii.

Omarilyas
 
Yawezekana tatizo ni wewe kukubali PROPAGANDA holela kama hizi bila hata kuchukua hatua za kujua undani na zaidi maslahi ya waendesha propaganda hii.

Omarilyas

Mkuu Omarilyas,
Utakuwa umewasaidia na wengine wasiojua ama wenye kukubali PROPAGANDA holela kwa kuwajuvya undani na maslahi ya waendesha propaganda.
 
hii si kweli, karume hawezi kuongoza Tanzania hata siku moja, ni mlegevu kama uyoga hapo ndo itakuwa dondoka ya ccm chali...hawezi hawezi yaani nasema hawezi. labda ungesema mtoto wa mwinyi yule kidogo ningefikiria kwamba pengine anaweza kuleta kaupinzani kwa ugombea urais hapa bara.

kwa habari ya rais wa mwaka 2015, atakuwa mkristo, si mwislam tena, tumechoka na makadhi na ma OIC. hivyo sahau kupeana urais kama pipi, iyo haipo na imepitwa na wakati. upo hapo?
 
Kikwete amtema rasmi Lowassa

Na Mwandishi wetu, Mwanahalisi

* Amwandaa Karume kumrithi 2015
* Dk. Shein ‘kupewa’ urais Zanzibar
* Lengo ni kumaliza makundi, fitina


RAIS Jakaya Kikwete na Rais Amani Abeid Karume watakabidhiana urais wa Jamhuri ya Muungano mwaka 2015, taarifa zimeeleza.

Taarifa zilizoenea Dar es Salaam na mjini Zanzibar zinasema mwaka huu, Rais Karume ndiye atateuliwa kuwa mgombea mwenza wa Kikwete ili kuhakikisha rais wa Muungano ajaye anatoka Zanzibar.

Kwa hatua hiyo, ndoto za Edward Lowassa, waziri mkuu aliyelazimshwa kujiuzulu kutokana na kashfa ya Richmond, za kujisafisha na kuwa rais baada ya Kikwete, zitakuwa zimezimwa.

Aidha, ndoto za Dk. Mohammed Gharib Billali kuwa rais wa Zanzibar baada ya uchaguzi mkuu mwaka huu, zitakuwa zimeyeyuka pia, kwani anayeandaliwa kwa nafasi hiyo ni makamu wa rais wa sasa wa Muungano, Dk. Ali Mohammed Shein.

Taarifa zinasema kwa mpangilio huo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitakuwa kimeondokana na ushindani wa “niue-nikuue” na makundi ambayo yanakaribia kukisambaratisha.

“Kuna hili la Shein kupitishwa na hilo likimalizika, tunataka Rais Kikwete amteue Karume kuwa mgombea mwenza. Hapa kila kitu kitakuwa kimefikia tamati na umoja na mshikamano ndani ya chama utakuwa umeimarika,” ameeleza mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu katika serikali na CCM.

“Mkakati wa kumpitisha Dk. Shein umelenga pia kumuinua Karume. Huyu ndiye tunayetaka awe mgombea mwenza wa Kikwete, lengo likiwa kumjenga kwa ajili ya 2015,” kimeeleza chanzo cha taarifa.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, mkakati umewekwa kuhakikisha jina la Dk. Shein ndilo pekee linalofikishwa katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho kwa ajili ya kupigiwa kura.

Kiongozi mmoja wa serikali aliye karibu na mpango wa kutaka Shein kuwa mgombea pekee, ameliambia MwanaHALISI kwamba tayari mikakati yote imekamilika.

“Mambo yote yanakwenda kama yalivyopangwa. Tunataka Dk. Shein ndiye pekee aingie katika kinyang’anyiro cha urais Zanzibar. Hili litasaidia kuondoa makundi na kumaliza fitina za kisiasa visiwani,” amesema akimnukuu kiongozi mmoja wa serikali na CCM.

Alisema kwamba ili kuhakikisha mpango huo unafanikiwa, “Mkakati unasukwa wa kuhakikisha jina la Dk. Shein ndilo linakuwa jina pekee linalofikishwa NEC kwa ajili ya kupigiwa kura.”

“Hili la Shein likimalizika, tunataka Rais Kikwete amteue Karume kuwa mgombea mwenza. Hapa kila kitu kitakuwa kimefikia tamati na umoja na mshikamano ndani ya chama utakuwa umeimarika,” alisema.

Habari zinasema lengo la kumuibua Karume kutoka Zanzibar na kumleta Bara ni kutaka kumrithisha urais wa Muungano, baada ya Kikwete kumaliza kipindi chake cha urais.

Habari zinasema mchakati huo utaepusha kile kinachoitwa, “misuguano ya urais 2015” kutoka kwa wanasiasa wa Bara.

Wanasiasa kadhaa, akiwamo Lowassa, waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye na waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, wanatajwa kutaka kumrithi Kikwete.

Mwingine anayetajwa na ambaye amekuwa akitajwa sana kuwa mwiba kwa kambi ya Lowassa na swahiba wake mkuu, Rostam Aziz, ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe.

Urais wa 2015 ndio unaotajwa kuwa kiini cha msuguano ndani ya bunge na katika chama ambapo Lowassa na mshirika wake, Rostam wanatajwa kujenga ngome ya kuwatetea kwa gharama yoyete ile.

Katika mchakato huu, mwanasiasa mmoja mwanammke ambaye ametangaza kugombea ubunge katika jimbo moja la Kanda ya Ziwa Victoria, ndiye anatajwa kuandaliwa nafasi ya waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa.

Hata hivyo, wachambuzi wa mambo ya siasa wanasema mkakati wa kumfanya Shein kuwa mgombea urais wa Zanzibar, utakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa wapambe wa Dk. Billali.

Taarifa zinaeleza, miongoni mwa sababu zitakazotumika kumwengua Dk. Billali ni pamoja na uamuzi wake wa kugombea urais Zanzibar mwaka 2005 kupingana na rais aliyepo madarakani.

“Unajua yule bwana alikosa subira. Chama chetu kimeweka utaratibu wa rais aliyepo kuachiwa kumaliza vipindi vyake viwili kwa mujibu wa katiba. Lakini yeye katikati ya shughuli alikuja kuanua majanvi na kumwaga ubwabwa,” kimeeleza chanzo cha taarifa.

Amesema, mbali na tuhuma za kuchukua fomu kumpinga Karume, Dk. Billali anakabiliwa na tuhuma nyingine ya “kuhujumu chama” siku chache kabla ya uchaguzi kutokana na hatua yake ya kumtuhumu Karume kuendesha nchi kifamilia.

Vilevile Dk. Billali anadaiwa kubeba watu waliowahi kuonywa na Kamati Kuu (CC) kuvuruga chama; kuleta mpasuko katika chama na kumdhalilisha rais wa Jamhuri.

Wanaotajwa kubebwa na Dk. Billali na ambao waliwahi kuonywa na CC, ni pamoja na aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM), Zahoro Mohammed na mwanachama wa Zanzibar, Mohammed Hija.

Tayari Rais Kikwete amechukua fomu za kugombea urais wa Muungano na mjini Zanzibar, juzi Jumatatu, Dk. Shein alichukua fomu za kugombea urais ikiwa ni hatua moja katika kufanikisha mchakato unaoripotiwa.

Hadi Jumatatu ni Jakaya Kikwete pekee aliyekuwa amechukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM kwa upande wa Tanzania Bara.

Mbali na Dk. Shein, waliochukua fomu kugombea urais Zanzibar ni pamoja na Billali, Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha, Naibu Waziri Kiongozi, Ali Juma Shamhuna, Naibu Waziri Afrika Mashariki Mohamed Abood, mdogo wake rais wa Zanzibar, Balozi Ali Karume na Kamishna wa wizara ya elimu na utamnadiuni, Hamza Bakari Mshindo.

Mohammed Seif Khatib, waziri katika ofisi ya waziri mkuu (Muungano), jana alitarajiwa kutoa msimamo wake iwapo atagombea urais Zanzibar.

Hata hivyo, mchakato huu wa kuandaa viongozi una dalili za kukumbana na upinzani mkali ndani ya vikao vya CCM kutokana na kuwepo mikakati ya awali kuwania uongozi miongoni mwa viongozi mbalimbali.

Kwa mchakato huu, wawaniaji urais waliokuwa wakitajwa, akina Lowassa, Sumaye, Mwandosya na Membe hawana upenyo labda kwa njia ya upinzani.

Huu ni udaku tu, mtu kaamua kutunga habari auze gazeti lake tu. Utupe evidence.

Mfumo hauko hivo. Rais wa Jamhuri ya Muungano Hawezi kuwa mzenji. Na wala Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano hawezi kuwa Rais wa Zenji.

Sikutarajia mwanahalisi liandike habari ya umbea kiasi hiki
 
Nawambia kuwa Karume mnae mkitaka msitake 2015 ,ni Raisi atakaetawala Tanzania kwa kipindi cha miaka kumi..niliwahi kusema as a TETESI ,je leo ukweli si umeanza kuchomoza :-


Karume Kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano



Kuna tetesi kuwa Rais wa Seikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Abeid Amaan Karume kuwa atapewa nafasi ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM 2015,habari zimezidi kuelezea kuwa yeye ndie atake kuwa mrithi wa Kikwete baaada ya Mheshimiwa Kikwete kumaliza ngwe yake 2015. Maandalizi ya kumuwezesha Mheshimiwa Karume kukubalika ifikapo mwaka 2015 yameanza na kufanya ziara za mara kwa mara katika mikoa ya Tanzania Bara ili kumjenga kwenye macho ya wananchi.

Hii inasemekana imetokana na utamaduni ambao kuna haja ya kuona unaendelezwa wa kupokezana nafasi ya kiti cha Urais wa Tanzania kwa upande wa bara na visiwani.Baada ya kokosekana wakati alipoondoka Mheshimiwa Benjamin Mkapa.

Pia habari zimezidi kutonya kuwa upo uwezekano wa mgombea huyo kupitia CCM kusimama katika kugombea kiti hicho kwa uchaguzi mkuu ujao 2010 endapo Rais Kikwete akiamua kupumzika, habari za wachunguzi wa mambo ya siasa wameona jitihada za Mheshimiwa Karume kuwekwa mstari wa mbele katika shughuli nyingi za Kichama hapa Tanzania Bara na Chama chake.
Embu rudieni hapa
https://www.jamiiforums.com/uchaguz...me-kugombea-urais-wa-jamhuri-ya-muungano.html
 
Back
Top Bottom