Kikwete amsafisha Chenge; Asema Hakuna Rushwa Kwenye Kashfa ya Rada

Georgia

You are right!

Rais Jakaya Kikwete ni mvivu kusoma ama his memory is very short. The bunch of Wahahariri wangemuliza ajibu kwa ufasaha ni sababu gani zilimfanya Andrew Chenge akajiuzulu uwaziri?

Kama sio rushwa what really transpired . RADA ilininuliwa kwenye awamu ya kwanza ya Ben Mkapa . What made the change kuchukua zaidi ya miaka kumi kurudisha if it was simply a typing error?

Jakaya hao washauri wanaokuzunguka hutaenda nao kaburini . Nakuahidi ukimaliza mwaka 2015 unatarajia kwenda kuishi wapi? I think it's better ukaboresha magareza for sure tutakuondolea hiyo immunity and jail will be your first choice wewe endelea kujifunika na net kuzuia mvua. Hata watoto wako wezi mtaungana wote in jail.

You have the chance then take it watu wote Deep Green, Kagoda, Meremeta na akina Richmond , na RADAR peleka jela wewe cheka tu ulisema mwenyewe akili ya kuambiwa changanya na ya kwako?

Leo nimepata mshangao wa mwaka,tangu lini typing error ikawa punishable?.Mimi nilizoea kuchukua correcting fluid na kurekebisha kasoro hiyo.Leo nimejifunza kitu

 
Hivi alijibu nini kuhusu swali la Kagoda iliyochota mahela ya uchaguzi 2005?au aliipotezea?

Jitahidi uwe unasoma taarifa nzima na sio kuishia kwenye heading tu.
Jibu la swali lako lipo kwenye paragraph ya pili kutoka mwisho ktk taarifa hii.
 
Naamini dr.slaa atakuwa ame-take note kwani hiyo ni kete kwa uchaguzi 2015 kwa kuwa ccm sasa nidhahiri haiwezi kutengwa na rushwa.kwa ccm rushwa is just 10% commission.

Ni kweli kabisa yaani CCM na rushwa ni kama uji na mgonjwa.
 
wote tumemsikilza rais alichojibu na kimeeleweka sasa hapa mnataka kupotosha,ushahidi wenu mtasema gazeti limeandika hovyooo....! wagala punguzeni chuki jamaa kafanikiwa sana ktk uongozi wake.Mbona hamsemi alichosema kuhusu sekta ya afya ilivyopiga hatua.Acheni kuropoka kama yule mwandishi aliyesema ct scan kwa bei ya shangingi

duh.! Kwenye msafara wa mamba kenge hakosekani.
 
nina hamu sana ya kumuona huyu mzee akiwa amestaafu urais...he is messing everywhere he is stepping his feets..aaagh
 
duh.! Kwenye msafara wa mamba kenge hakosekani.

Mkuu inaonyesha hujasikiliza hutuba....kikwete kasema wazi kabisa anayesema kwamba bei ya shangingi moja ni ni sawa na CT SCAN moja basi aende kwake watampa hela akanunue hiyo CT SCAN.....

Watu wasipotoshe kila kitu mwisho hapa JF patakuwa kama kijiwe cha Kahawa na sehemu ya Kijifurahisha tu...hizi habari za CT SCAN zilienea sana humu JF
 
Jamani tuache kumlaumu hakuandaa majibu ya swali kabla, alisahau kama hao sio wazee wa dsm, akashindwa kutoa uongo unaofanana na ukweli badala yake akatoa uongo kabisa
 
Mh! JK amefunga kweli? maana haya majibu yake mengine hayana ukweli
 
Ni wakati sasa wa Chenge kumshikia bango Nape ili aweze kutoa uthibitisho wa kumuita Fisadi na ni Gamba katika CCM kwani mwenyekiti wake kisha msafisha.
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya rais wa nchi na kiongozi wa nchi....huyu tuliye naye ni rais na hayuko pale kuongoza waTanzania. Ataendelea kuropoka hivihivi hadi atakapomaliza kipindi chake 2015. Tumeongozwa na marais 4 hadi sasa: Mwl JK.Nyerere (Safi), AH.Mwinyi (Ovyo), BW.Mkapa(Safi), na JM.Kikwete (Ovyo). Kila mtu anayo mapungufu yake lakini mapungufu yanapofunika mazuri basi mimi nasema huyo rais ni wa Ovyo. Siyo kusema sasa Nyerere na Mkapa hawana mapungufu; lakini mapungufu yao yalifunikwa na mazuri ya uongozi wao kwa taifa letu.
 
Ni jibu sahihi kisheria akinukuu kesi iliyoendeshwa ughaibuni (UK). Chenji ilirudishwa na BAE bila kukiri kosa la jinai (rushwa). Tatizo kwa rais ni kwamba, kwa dhamana yake kubwa, hatakiwi kujipa raha kwa maamuzi yaliyofanyika huko UK. Yeye na Serikali yake wana wajibu wa kuwathibitishia Watanzania usafi wao katika dili hilo na juhudi za dhati walizofanya kiuchunguzi na kisheria kuthibitisha rushwa na wizi uliotendeka.

Sisi si wajinga kiasi cha kuamini kuwa BAE wameturejeshea chenji nzito kiasi kile kwa kosa la kalamu kuteleza vibaya tu kwenye karatasi (mere accounting irregularity)! Hata Chenge alipojiuzulu uwaziri ilikuwa paniki ya kufikiri ukweli umeshamwagika hadharani. Muda tu umemsaidia kurejesha jeuri katika suala hili. Jibu la Kikwete ni ujumbe rasmi kwamba wao wataendelea kula tu ilhali sie Watanzania tunaendelea kuwachekea na kuwarejesha tena na tena madarakani. Raisi atajiridhishaje na hukumu/maamuzi ya nchi ya nje katika suala nyeti kwa nchi yake?
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya rais wa nchi na kiongozi wa nchi....huyu tuliye naye ni rais na hayuko pale kuongoza waTanzania. Ataendelea kuropoka hivihivi hadi atakapomaliza kipindi chake 2015. Tumeongozwa na marais 4 hadi sasa: Mwl JK.Nyerere (Safi), AH.Mwinyi (Ovyo), BW.Mkapa(Safi), na JM.Kikwete (Ovyo). Kila mtu anayo mapungufu yake lakini mapungufu yanapofunika mazuri basi mimi nasema huyo rais ni wa Ovyo. Siyo kusema sasa Nyerere na Mkapa hawana mapungufu; lakini mapungufu yao yalifunikwa na mazuri ya uongozi wao kwa taifa letu.

Ndugu yangu, huyo jamaa anazo sifa nyingine unazoweza kumpa - sio hiyo.
 
Kunatofauti kubwa sana kati ya JIBU(Answer) na Majawabu(Solution)..... Yeye amekuwa bingwa wa Majibu :wacko:

Haitoshi kusema kuwa hakukuwa na rushwa kwenye kashfa ya Rada........he should go further.....and tell the public what went wrong.......?and who did so? and how do we call/name that wrong?
 
Ndugu yangu, huyo jamaa anazo sifa nyingine unazoweza kumpa - sio hiyo.

Nimempa hiyo kwa tafsiri yangu hapo chini...wala sikujali matatizo ya Kiwira, mashamba ya miwa na Hotel Lushoto.....nakumbuka daraja kule Rufiji...inflation drop....stadium na mengineyo mengi
 
Takukuru ni taasisi ya kuzuia kupambana na rushwa na si vinginevyo.

Kuhusu kuikana rushwa ya rada kwanza kabisa kikwete haoni soo kudanganya kama mnabisha basi naamini kabisa kuwa kuna siku atakuja kukataa kuwa aliwahi kuwa rais wa tanzania na atatoa vielelezo.

Pili kikwete ni mwoga kama mkapa akikomaliwa na kutishwa na mtuhumiwa yeyote wa ufisadi anakubali yaishe kwani kwa kisingizio kuwa kila jambo ni upepo tu na utapita kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi.

Tatu, kikwete ni mla rushwa tangu aitwe fisadi nambari wani na chadema ameamua kufanya kweli hadharani kula mali ya umma bila kunawa mikono. Siku lowasa akiutema ukweli wote itakuwa ni zaidi ya milipuko ya mbagala.
 
Mkuu inaonyesha hujasikiliza hutuba....kikwete kasema wazi kabisa anayesema kwamba bei ya shangingi moja ni ni sawa na CT SCAN moja basi aende kwake watampa hela akanunue hiyo CT SCAN.....

Watu wasipotoshe kila kitu mwisho hapa JF patakuwa kama kijiwe cha Kahawa na sehemu ya Kijifurahisha tu...hizi habari za CT SCAN zilienea sana humu JF


Nadhani KITU cha msingi hapa ni KUpunguza Kama siyo kuachana Kabisa NA matumizi ya anasa serikali ni, hivi tukiacha HAYO mashangingi tutapata CT Scanners ngapi? Cha msingi ni tuache kuishi kifahari, hii Tanzania ni ya wote, siyo wengine milo mitatu, wengine lunch ZA uji, Mungu NA alegeze mioyo ya wote walafi
 
sasa kama hakuna rushwa ile pound million moja chenge aliyoifadhi kwenye bank kule uk aliitoa wapi?? maana mshahara wake sidhani kama ungeweza kumfanya apata one million pounds
 
Back
Top Bottom