Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 233
Katika gazeti la MwanaHalisi la leo habri kuu ya ukurasa wa mbele ilikuwa na kichwa cha Habari "Rostam azimwa." Hii kutokana na ruling ya Mahakama y rufaa ya rufani ya gazeti hilo dhidi ya Rostam. Lakini Habari ya kusimumua zaidi kutokana na stori hiyo inatokana na kibwagizo "Kikwete ‘amkacha (Rostam) Afrika ya kusini", Habari ambayo iko mwishoni mwa stori hiyo na ninairudia hapa kuwarahisishia wana JF wenzangu:
…..Wachunguzi wa masuala ya vyombo vya Habari na haki ya uhuru wa kujileleza wanasema hukumu ya Mahakama Kuu ililenga kuzima uhuru wa Habari na kulinda mtu mmoja dhidi ya masilahi ya taifa.
Wamesema mahusiano ya kibiashara na kisiasa kati ya Rostam na wanasiasa na wafanyabiashara wengine, ambayo sharti yafahamike kwa kuwa yeye yuko katika nafasi ya kiongozi wa umma, yangezimwa moja kwa moja.
Kwa mfano, uhusiano wa Rostam na Rais Jakaya Kikwete, unaotajwa kutota hivi sasa, usingepata nafasi ya kuripotiwa katika chombo hiki na vingine.
Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya serikali zinasema, Kikwete ameamua kujiweka kando na Rostam. Imefahamika kuwa kuna wakati amekataa kukutana naye ana kwa ana.
Tukio la karibuni linalosimuliwa na maofisa wengi serikalini ni lile la nchini Afrika ya Kusini ambako Rais amedaiwa kukataa kukutana na Rostam katika Hoteli ya Hilton mjini Pretoria.
Kikwete alikuwa nchini Afrika ya Kusini kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma.
Kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa ngazi ya juu ndani ya CCM ambaye alikuwa nchini humo kuhudhuria sherehe hizo, Kikwete alikataa ombi la Rostam la kutaka kukutana naye lililowasilishwa kwake na wasaidizi wake.
"Ni kweli kwamba Rostam alifika katika Hoteli ya Hilton aliyofikia Kikwete kwa lengo la kutaka kumuona. Lakini hakufanikiwa kutokana na Kikwete kukataa kuonana naye," mtoa taarifa ameeleza.
Taarifa zinasema kuwa Rostam alikuwa amejifungia kwenye chumba kimoja hotelini humo akijaribu kusubiri jibu kutoka kwa wasaidizi wa Kikwete, lakini hakufaulu.
Aliamua kujaribu tena kuwasiliana na wasaidizi wa Rais Kikwete wakati wa sherehe fupi ya chakula cha usiku, lakini wasaidizi waliobeba ujumbe walianza kutupiana mpira wa kuwasilisha ombi la Rostam na ndiyo ikawa tamati ya juhudi za mbunge huyo wa Igunga, Tabora.
Haijaeleweka iwapo tangu hapo amefanya juhudi zozote tena za kukutana naye. Kama ada, simu ya Rostam ama haipatikani na ikiita haijibiwi.

Last edited by a moderator: