Kikwete ameteleza kushinikiza gas kupelekwa Dar es Salaam


Ni kuhakikisha mwana wa mfalme anapelekwa china kukatwa kichwa. Deal limevurumbuka, bwawa limeingia luba.

Tunabahati kuwa na watu wanaoona mbali, lakini dharau na kujiamini ndiko kunakokuja kusababisha kudhalilika.
 
Mungu simjinga kuielekeza gesi Mtwara..Anataka nafuu kwa watu wa kusini maana mda mrefu wana ugulia matumboni mwao bila ya wanadamu wenye shibe kuwasikiliza na sasa iki ndio kipindi chao
 
  • Ahadi ya Kikwete kipindi cha kampeni ni kuijenga bandari ya Mtwara na kujenga kinu cha kufua umeme kutokana na gas Mtwara

KAULI HII YA VIONGOZI WA DINI KWA WENYE UELEWA SERIKALI IFIKIRIE UPYA

  1. Mtwara ina Bandari yenye kina kirefu katika Afrika ya mashariki yote lakini mpaka sasa mipango ya kuiendeleza imekuwa ni kizungurumkuti. Wananchi wana taarifa kuwa mipango ya kuiendeleza Bandari ya Mtwara imepindishwa na kupelekwa Bagamoyo.
  2. Wananchi wanakumbuka kwa uchungu zao lao la biashara la muhogo ambalo serikali ya Tanzania huru imeliacha linakufa kuwa zao la biashara.
  3. Wakulima wengi wanalima mihogo mingi na wanaishia kuitupa tu baada ya kuoza maana si tu kwamba haina soko bali hata teknolojia ya kulitunza kwa muda mrefu hawana. Mashamba wanayo na wanalima kwa bidii wanavuna mihogo mingi lakini wa kumuuzia tayari serikali ilishampoteza na haina mpango wa kulifufua zao hili kama zao la biashara.
  4. Wananchi wa Mtwara na kusini kwa ujumla wana kilio cha muda mrefu cha zao la korosho na mpaka sasa serikali inababaisha tu haina mpango wowote wa kuboresha soko la zao hili. Wananchi sasa wanapomaliza kuvuna korosho zao wanaambulia vikaratasi tu na kutakiwa wasubiri pesa zao kwa muda mrefu bila kuzipata. Ingawa ni jambo liliowazi kuwa zao la korosho linachangia kiasi kikubwa tu cha fedha katika serikali. Kwa mfano, kuna takwimu zinaonesha kuwa Katika Mwaka wa Uchumi unaoishia Novemba 2012, Korosho imeliingizia Taifa jumla ya dola za Kimarekani 151 milioni sawa na shingi billion mia mbili arobaini na moja na million mia sita (TZsh241,600,000,000). Katika mwaka 2011 zao hili liliingiza dola 130 milioni sawa na bilioni mia mbili na nane (208,000,000,000) wakati Pamba iliingiza dola 53 milioni tu sawa na shingi billion themanini na nne na milioni mia nane (84,800,000,000).


  • Wananchi wa Mtwara na kusini kwa ujumla wanazidi kulia tu na kusuasua kwa ujenzi wa Barabara ya Mtwara-Lindi-Dar es Salaam. Wanazidi kuumia wanapoona ile mikoa inoyoheshimiwa na serikali ikiwa na Barabara nzuri zinazopitika tena ujenzi wake umekamilika kwa muda mfupi sana.
  • Miaka minane ya Mh. Rais Kikwete zile kilomita 60 za barabara kutoka Ndundu mpaka Somanga hazijaisha lakini gesi anataka kuiwekea bomba na mradi ukamilike kwa miezi 18.
  • Wananchi wameshuudia reli ya kusini iking'olewa bila sababu za msingi na huku ikijulikana kuwa reli ni moja ya miundombinu muhimu katika kuchochea uchumi na maendeleo ya jamii kwa ujumla. Reli haikung'olewa katika mikoa ambayo serikali inaiheshimu.
  • Wananchi wa Mtwara wameshuhudi mashine ya maji kitangali Newala ikiondolewa na kupelekwa Dodoma ambayo ilikuwa msaada kutoka Finland.
  • Wananchi wa Mtwara wameshuhudia kiwanda cha samaki Mtwara kikiondolewa na kupelekwa Dar es Salaam.

  • Wananchi wa Mtwara wameshuhudia taa za mwanga mkali za uwanja wa ndege Mtwara ziking'olewa na kupelekwa Arusha.
  • Wananchi wa Mtwara wameshuhudia mkataba wa kutumika bandari ya Mtwara na Malawi kibiashara ukipindishwa na kupelekwa Bagamoyo.
  • Wananchi wa Mtwara wamekaa na giza kwa muda mrefu na giza hilo limechangia kutokuwepo kwa kichocheo cha uchumi kwa kukosekana umeme wenye uhakika.
  • Ni hivi karibuni tu baada ya kugunduliwa gesi na kumekuwepo na nishati ya umeme ambao hautoshi kwa maana ya kumfanya mjasriamali mwenye mtaji kuweza kuwekeza Mtwara katika sekta ya viwanda. Mwenyezi Mungu anasema:-
"Kwa hakika MwenyeziMungu anaamrisha uadilifu,na kufanya ihsani,na kuwapa jamaa(na wengineo),na anakataza uchafu na uovu,na dhuluma.Anakunasihini ili mpate kufahamu(mfuate)"(Qur'an 16:90)

"Na timizeni ahadi mnazozitoa kwa jina la MwenyeziMungu mnapoahidi;wala msivunje hizo ahadi baada ya kuzithubutisha,hali mmekwisha mfanya MwenyeziMungu kuwa shahidi wenu.Hakika MwenyeziMungu anayajua yote mnayoyayafanya"(Qur'an 16:91)

Sasa ghafla, wanakutana na mpango wa kustukiza wa serikali kutaka kusafirisha gesi hiyo kwenda Dar es Salaam bila kueleza kwa nini kituo cha kufulia umeme unaotokana na gesi asilia inakopatikana gesi hiyo kisijengwe Mtwara?. Wanapojaribu kuihoji serikali wanaambulia matusi, kejeli na kupuuzwa kutoka kwa viongozi wao waliowategemea kuwatetea. Kwao wanaona ni hujuma tu wanataka kufanyiwa kama walivyofanyiwa huko nyuma na ndio maana wameamua KUFA na GESI indepo na mara hii serikali itawapuuza. Serikali imefikia upeo wa juu wa kuwapuuza wana Mtwara na WanaMtwara nao wamefikia upeo wa juu wa uvumilivu na ndio maana wanasema GESI KWANZA UHAI BAADAYE. Haya ndio mazingira halisi ambayo ndiyo KIINI cha mgogoro wa gesi Mtwara. Sio wanasiasa bali ni historia ya kudharauliwa ndio yaliyoibua mgogoro huu wa gesi kama tulivyoeleza hapo juu. WanaMtwara wana mfano wa gesi ya Songosongo inayopelekwa Dar es Salaam. Zipo taarifa zinazoelezea kwamba kodi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa asilimi 0.3 (0.3%) ilikuwa inalipwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na kampuni ya Pan Africa Energy. Ni baada ya juhudi za mbunge wa Kilwa Kaskazini Murtaza Mangungu kuingilia kati ndio kodi ikaanza kulipwa Kilwa.

TAMKO
SHURA YA MAIMAM INAUNGANA NA WANANCHI WA MIKOA YA KUSINI KUITAKA SERIKALI ISITISHE MPANGO WA KUSAFIRISHA GESI ASILIAYA MTWARA KUPELEKWA DARES-SALAAM NA BADALA YAKE MTAMBO WA KUFUA UMEME WA MEGAWATT 300 UJENGWE MTWARA KAMA ULIVYOKUSUDIWA AWALI KABLA YA USHAURI MBAYA WA TPDC KWA SERIKALI. NA KWA KUWA TUNAAMINI KUWA SERIKALI YETU NI SIKIVU ITATUSIKILIZA WANANCHI WA MIKOA HII YA KUSINI kama ilivyowasikiliza wananchi wote wa Tanzania tulipoitaka serikali kuwa na mjadala kuhusu kuandikwa kwa KATIBA MPYA ingawa msimamo wa serikali mwanzo ulisema katiba iliyopo inakidhi haja za wakati huu.
Ee ALLAH shuhudia kuwa tumefikisha na tumetekeleza wajibu wetu
.
 
Back
Top Bottom