Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,884
- 6,885
- Thread starter
- #21
Mtwara Nadhani imelaaniwa toka kitambo!!! Nipo Mtwara kwa shughuli zangu kwa zaidi ya miaka mitatu sasa but yanayoendelea ni aibu kuyasema, Kabla ya Hili la GAS Nilitaka wananchi wa Mtwara waungane na Kumng'oa KANJI BAI ambae ndo mbunge wao, hana msaada zaidi ya kutumia fulsa ya yeye kuwa mbunge kuilinda Diplomatic Passport yake, pia Kama vila la Mbunge halitoshi wakachagua KANJI BAI mwingine kuwa Mwenyekiti wa Mkoa CCM, najua nitaibua hisia za watu wasioipenda CCM hapa lakini kama unafuatilia mambo mengi ya kisiasa hapa nchi basi maamuzi mengi ya Serikali yetu hufanywa na SISIEMU kwenye vikao vyao vya NEC na Kutekelezwa na SERIKALI yake, hivyo kuwa na watu wawili ambao nathubutu kusema kuwa sio watanzania potelea mbali nikiitwa MBAGUZI lakini sio watu amabao wanaweza kuwatetea WANAMTWARA kwenye shida zao. HIVYO UKOMBOZI WA MTWARA UANZIA HAPO KWANZA NA WAKIWA NA WAWAKILISHI MAKINI BASI NAFASI YA MADAI YA MSINGI HASA HILI LA GAS BASI LIOTAWEZEKANA. INATOSHA SASA KUTAWALIWA NA WAGENI
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Mataifa Mheshimiwa Bernard Membe,
Waziri wa Katiba na Sheria Mathias Chikawe, kuna wengine wengi mashuhuri kama akina Anna Abdalah, na mwingine mbunge wa siku nyingi alisimamia uchaguzi wa Speaker kule Dodoma.
Wapo akina Mkapa na wengineo lakini hakuna jitihada za kukumbuka kutetea ukanda wao si kwa upendeleo bali kutetea wananchi wanufaike na malighafi zipatikanazo huko.
Kinachoendelea ni sawa na wazungu wanavyokazania kukomba madini nchini na kutoroshea kwao sisi tumelala usingizi tu.
Wabunge wa huko kusini wajue Charity begins at home.
Filikunjombe amepigania Ludewa yake madini yachimbuliwe na viwanda vya kuyafinyanga vyuma vijengwe huko sambamba na plant ya umeme itakayoendeshwa na makaa ya mawe, kwa nini isiwe hivyo Mtwara?