Kikwete amenitukana....

fAIZA UNATUTUKANA PIA.Hivi hotuba yote ya Rais ndio hii? Mengi alikuwa akiyaongezea akijaribu kudadavua/kuchanganua alichoandikiwa.Mbona suala la Katiba alilolirudia mara mbilimbili halipo hapa? Acha zako.Acha kumtetea kilaza huyu....tutakuhesabu nawe ni muasi muda si mrefu
Inabidi tunaofatilia hotuba za Kikwete tukuone wewe kama ulivyoandika mwenyewe hapo juu. Hii hapa ni hotuba ya Kikwete ilippongelea Sukari ni wapi umeyatowa hayo unayosema wewe? au ndi unanihii wenyewe huo?:

Hali ya Uchumi
Ndugu Wananchi;
Katika kuelezea hali uchumi nchini, naomba nianze kwa kuelezea hali ya uchumi duniani kwani yanayotokea nchini yana uhusiano mkubwa na yanayotokea duniani. Hali ya uchumi duniani siyo shwari. Ukweli ni kwamba hali katika uchumi wa mataifa ya Marekani, Ulaya Magharibi na Japan haijatengemaa kufuatia machafuko ya masoko ya fedha na mdororo wa uchumi wa miaka miwili iliyopita. Hivi sasa uchumi wa mataifa tajiri ya Ulaya , wanachama wa Umoja wa Ulaya na hasa wanachama wa Umoja wa Sarafu ya Euro unapita katika kipindi kigumu na mashaka. Thamani ya sarafu hiyo inashuka na hata kuaminika kwake ni kwa mashaka. Mfumuko wa bei umepanda, ukosefu wa ajira umeongezeka na ipo hofu kubwa ya uchumi wa nchi hizo kudorora tena. Lakini nchi hizi ndiyo masoko makubwa ya bidhaa zetu, watalii na bidhaa za viwandani. Hivyo, athari zao zinatugusa na sisi. Kuongezeka kwa mfumuko wa bei kunaongeza bei ya bidhaa tunazonunua kutoka kwao. Aidha, kutetereka kwa uchumi wao nako kumepunguza masoko ya bidhaa zetu.
Lakini kulegalega kwa sarafu ya Euro kumesaidia kuimarika kwa sarafu ya dola ambayo kabla ya hapo ilikuwa imepungua nguvu. Kwa sababu hiyo thamani ya sarafu ya dola imepanda duniani ikilinganishwa karibu na sarafu nyingine zote pamoja na yetu. Wakati huo huo bei ya mafuta imeendelea kupanda duniani kutoka dola 76.1 kwa pipa Septemba,, 2010 hadi dola 100.5 Septemba, 2011. Jumla ya yote haya ni kuongezeka kwa mfumuko wa bei kutoka asilimia 4.2 Oktoba, 2010 hadi asilimia 17.9 Oktoba, 2011.
Ndugu Wananchi;
Serikali na vyombo husika vimekuwa vinachukua hatua mbalimbali kukabiliana na matatizo ya kushuka kwa thamani ya shilingi, bei ya mafuta, bei ya sukari na matatizo ya umeme. Kuhusu kushuka kwa thamani ya shilingi Benki Kuu imeendelea kuchukua hatua zilizopo ndani ya mamlaka yake hususan kubana ulanguzi wa fedha za kigeni, kudhibiti matumizi ya fedha kigeni kufanyia malipo hapa nchini na kuongeza fedha za kigeni katika masoko ya fedha. Kwa kweli uwezo wao una ukomo. Jawabu la uhakika lipo kwenye uchumi wa mataifa makubwa kuchukua hatua thabiti kuimarisha uchumi wao ili thamani ya dola irejee mahali pake stahiki na bidhaa zetu zipate masoko ya uhakika na bei nzuri ili mapato yetu ya fedha za kigeni yaongezeke.
Kwa upande wa mfumuko wa bei, ni vyema tukatambua kuwa Asilimia 75 ya ongezeko hili imetokana na kupanda kwa bei ya chakula na mafuta. Asilimia 25 iliyobaki imechangiwa na sera za fedha. Kwa upande wa mafuta, tunaamini utaratibu wa kuagiza mafuta kwa pamoja utasaidia kudhibiti bei za ndani za bidhaa hiyo. Aidha, itsaidia kupunguza makali ya athari ya bei za dunia zinazopanda. Kwa upande wa bei za vyakula, tatizo kubwa ni uhaba wa chakula katika nchi jirani unaosababisha wote kututegema sisi na hivyo kupandisha bei nchini. Tunaendelea kudhibiti magendo ya chakula na wakati huo kutengeneza taratibu rasmi za kuziuzia chakula nchi jirani.
Kwa upande wa sukari tumeamua kuruhusu tani 120,000 ziagizwe ili kupunguza uhaba wa bidhaa hiyo na kushusha bei yake.


Hatuko Peke Yetu

Ndugu Wananchi;
Ni vizuri tukafahamu kuwa, matatizo ya mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya fedha yetu siyo yetu peke yetu. Nchi zote za Afrika Mashariki zinakabiliana na matatizo haya. Kwa mfano, mfumuko wa bei kwetu ni asilimia 17.9, Kenya wako asilimia 18.9 na Uganda asilimia 30.5. Wakati mwaka wa jana sote tulikuwa kwa wastani karibu asilimia 5. Kwa upande wa kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola sote tumeathirika. Shilingi ya Tanzania imeshuka kwa asilimia 9.4, Kenya kwa asilimia 6.8 na Uganda kwa asilimia 17.4. Randi ya Afrika Kusini kwa asilimia 18.7, Rupia ya India kwa asilimia 9.8, Pauni ya Uingereza kwa asilimia 6.6. na Euro kwa asilimia 9.7.
 
fAIZA UNATUTUKANA PIA.Hivi hotuba yote ya Rais ndio hii? Mengi alikuwa akiyaongezea akijaribu kudadavua/kuchanganua alichoandikiwa.Mbona suala la Katiba alilolirudia mara mbilimbili halipo hapa? Acha zako.Acha kumtetea kilaza huyu....tutakuhesabu nawe ni muasi muda si mrefu

Sikuwa na haja ya kuibandika hotuba yote kamili, kwenye nyuzi hii hapa kilichoongelewa ni sukari, na sukari iliongelewa kipande hicho, sasa mleta mada au kama wewe unacho kipande kama anavyosema mleta mada kiweke hapa. Msitake kutujaza ujinga usiokuwepo.
 
hivi wazee wa Dar ndo wazee wa Tanzania??
Hawa wanawaza ubwabwa tu hakuna kingine, hata hawajui JK alikuwa anaongea porojo gani. unafanya mchezo na posho ya buku 5?

379135_291077990931762_100000886912967_831391_1156534665_n.jpg
 
Faiza,hotuba haikuwa ya kuandikwa tu.Mengi aliyaongezea pia.Sukari aliitaja alipozungumzia mfumuko wa bei.Nikupe mfano:hakuna mahala kwenye hotuba iliyoandikwa ambapo Kikwete alisema walisema eti hapatatosha..sisi tunataka patoshe..Hakuna! Lakini kwenye ile iliyosikika maneno hayo yapo.Faiza,don stick to written..look for audio pia.
Sikuwa na haja ya kuibandika hotuba yote kamili, kwenye nyuzi hii hapa kilichoongelewa ni sukari, na sukari iliongelewa kipande hicho, sasa mleta mada au kama wewe uanchokipande kama anavyosema mleta mada kiweka hapa. Msitake kutujaza ujinga usiokuwepo.
 
Na wewe mrudishie hivyo hivyo, si unakumbuka hata Mzeee Makamba anasema alitukanwa na kijana mmoja akiwa kwenye mkutano na askari wakataka wamkamate yule kijana ili wamshikikishe adabu, Mzee Makamba akawaambia wamuachie tu maana ameshamtukana na yeye pia, (yaani Makamba alimrudishia lile tusi) Mfano, Mjinga wewe (sijui kama mjina ni tusi ni mfano tu) kwahio na wewe unasema mjinga mwenyewe....hahahaaa hebu apply haka ka-formula toka kwa Mzee Makamba maana ukubwa dawa bhana si unaona hata Rahisi alitumia wazee
 
Wazee waliekwa kama maboya na wale akina mama kushangilia tu. Wkati ule waliambia mshahara hautapanda wakashangilia. hao ndiyo wazee tunaowategemea wamuulize Rais swali kweli?
 
Inabidi tunaofatilia hotuba za Kikwete tukuone wewe kama ulivyoandika mwenyewe hapo juu. Hii hapa ni hotuba ya Kikwete ilippongelea Sukari ni wapi umeyatowa hayo unayosema wewe? au ndi unanihii wenyewe huo?:

Hali ya Uchumi
Ndugu Wananchi;
Katika kuelezea hali uchumi nc......

Mweh!Ovyo!
 
Memo! Memory yako ni ndogo sana umechukua kipande tu cha hotuba,
Wakati akihutubia kuna kipindi alisema kuwa nchi zilizotuzunguka zinatumia chakula kutoka kwetu; alitoa mfano wa Kenya kwamba kuna waziri mmoja (hakumtaja jina) alifanya research kwenye supermarket nyingi kenya na kugundua kuwa sukari iliyoko huko ni ya kilombelo / kagera sugar n.k
Kwa sababu memory yako haiwezi kuchukua data kubwa ndo maana kuna mengine hujayachukua. Kwa nyongeza ya hapo nilikubali kuwa JK hafai pale aliposema kuwa serikali inafanya mpango wa ku-import sukari kutoka nje.... Hivi kweli hiyo ni akili? badala ya kuzuia iliyopo isitoke, serikali yake inaagiza sukari nje kwa gharama kubwa, anaendelea kuongeza matatizo mengine wakati tuliyo nayo yametuhelemea. Ikiagizwa sukari toka nje ni kero mizigo bandalini.
 
aaaahh FaizaFoxy, napenda maoni yako jinsi unavyo yaweka. Huwa najiuliza huyu mama/bibie kama kweli ww ni m/mke umelishwa nini, samahani nikuulize: MS ni mwalimu wako?
bibie unakaclaim maandishi sio--wenzako to read between the lines kisha tunachanganya na audio-hiyo ndiyo maana ya kwenda shule. Hivi dada ni lini utaachana na hako katabia eti watu wanamsema Rais Kikwete na sio serikali. Hivi nyumbani kwako ww kunajulikana kwa jina la nani? la mumeo, la kwako au la watoto wako? majibu unayo.

Mr.Kikwete is the Head of the State/GVT/Nation oooor you name it whatever.

Kwa hiyo mambo yakienda vizuri sifa zitamwendea yeye, ana yakiwa hovyo hovyo atasemwa yeye...umenisoma mpaka hapo bibie.

Hebu turudi kwenye hoja ya katiba: Katiba inayopigiwa kelele ni kwa ajili ya nani? kama sio WaTZ, kwanini tunanyimwa fursa ya kushiriki ktk mchakato kuanzia mwanzoni, ok, tunauhakika gani kuwa sasa maoni ya wananchi yatazingatiwa kama hapa mwanzoni tu tumepuuzwa
 
Aliongea na wazee wa Dar es salaam! Ajaribu kusema atakwenda kuongea na wanafunzi wa vyuo vikuu aone ni nini kitatokea!
 
Asante kwa ufafanuzi wako.Nadhani FaizaFoxy atakuwa ameelewa vyema.Ubarikiwe!
Memo! Memory yako ni ndogo sana umechukua kipande tu cha hotuba,
Wakati akihutubia kuna kipindi alisema kuwa nchi zilizotuzunguka zinatumia chakula kutoka kwetu; alitoa mfano wa Kenya kwamba kuna waziri mmoja (hakumtaja jina) alifanya research kwenye supermarket nyingi kenya na kugundua kuwa sukari iliyoko huko ni ya kilombelo / kagera sugar n.k
Kwa sababu memory yako haiwezi kuchukua data kubwa ndo maana kuna mengine hujayachukua. Kwa nyongeza ya hapo nilikubali kuwa JK hafai pale aliposema kuwa serikali inafanya mpango wa ku-import sukari kutoka nje.... Hivi kweli hiyo ni akili? badala ya kuzuia iliyopo isitoke, serikali yake inaagiza sukari nje kwa gharama kubwa, anaendelea kuongeza matatizo mengine wakati tuliyo nayo yametuhelemea. Ikiagizwa sukari toka nje ni kero mizigo bandalini.
 
hahaahahah.....yaan kwenye huu uzi wote waliochangia wewe ndo umevunja record.. te he tehe tehe
UOTE=Memo;2856680]
avatar39905_1.gif
hawa nao wamepanda bei sana hawa....kilo buku saba>!!![/QUOTE]
 
Nasikitika kusema kwamba Rais wangu wa iTanzania amenitusi.Hii imetokea siku ya Ijumaa alipokuwa akihutubia Wazee wa Dar es Salaam.Alinitusi kwa kuniambia uongo huku akiwa anaujua ukweli.Aliniona mimi zuzu.Alidai kuwa eti mimi nanunua sukari kwa bei chee baada ya Serikali sikivu. kushusha bei ya bidhaa hiyo.Ukweli ni kwamba kila uchwao,bei ya sukari inazidi kupaa.Niishipo mimi,kilo moja ni shilingi 2300.Je,matusi haya kwangu ni kwakuwa amepotoshwa na wasaidizi wake? Je,amewatukana pia na Wazee waliokuwa wakimsiliza?

Kwani ni lazima ule sukari. Wenzio tunakula asali!
 
Back
Top Bottom