Kikwete amemgeuka lowasa vibaya kinyume na makubaliano yao, hii itatugharimu tz

Major

JF-Expert Member
Dec 20, 2007
1,865
2,439
Habari za uhakika, 100%, ni kwamba baaba ya mheshimiwa JK, Kuamua kumtosa waziwazi rafiki yake ambaye bila yeye urais wa awamu iliyopita angeusikia radioni, mshikaji Lowasa sasa ameamua, MWAGA MBOGA, NAMWAGA UGALI. Hali halisi ni kwamba sasa hivi mambo ni magumu sana serikalini, na kuna tetesi kuwa huyu Mkwere kuna hati hati ya kutokumaliza utawala wake vizuri, mliopo tanzania mtagundua hali mbaya ya uchumi kupita wakati wowote mliowahi kushuhudia.

Habari za kuaminika ni kwamba hata lile zengwe la Richmond Mkwere ndiye aliyelisuka, na hii hata Samweli analijua, na hata juzi wakati wa uteuzi wa mawaziri lile zengwe la kwamba mtoto wa lowasa alivuta mpunga mkubwa huko ughaibuni lilisukwa na mkwere kwa lengo la kumtoa nje kabisa.

Hivi sasa habari za ukweli ni kwamba mkwere atakumbana na hali ngumu kuliko zote tangu alipozaliwa.na hii imeanza kushuhudiwa Tanzania, kwa mfano. wakulima mwaka huu ruzuku wataisikia redion
 
Kweli mkwere ni mtoto wa mjini.
Mkuu vipi kuhusu source au we ndo lowassa nini?
 
Mbona walipokuwa wanafukiza uvumba kuwania kiti cha enzi walituambia watakula sahani moja? Kulikoni sasa kinachoendelea?
Kifo cha panzi furaha ya kunguru
 
Hali mbaya ya uchumi haina uhusuiano wowote wa moja kwa moja na Lowassa, inabidi tuwe wa kweli. Hali mbaya ya uchumi inatokana na
1. matumizi mabaya ya serikali ikiwa ni pamoja na kutumia vibaya pesa za hazina kwa ajili ya kampeni ambayo walijua kuwa watazirudisha kwa njia moja au nyingine,
2. lakini pia wahisani wamepunguza misaada kwa karibia asilimia 50 uki-compare na mwaka jana hii ni kutokana na hali yao mbaya kiuchumi.
3. Pia tukumbuke ya kuwa bajeti iliyotangazwa Bungeni ilikuwa 'massaged' na haikuonyesha makadirio halisi ya kiuchumi iliandikwa na 'rose tinted glasses' na walikadiria mapato makubwa zaidi na matumizi makubwa zaidi bila kufuata principles za kiuchumi.

Lowassa anaweza kuwa na bifu na mshikaji wake wa zamani na wakaumizana, lakini nadhani victims hawatakuwa watanzania bali ni wenyewe na familia zao na hilo wanalifahamu kwa hiyo sitaraji kuona mabadiliko makubwa. Kumbuka jinsi ambavyo Lowassa ana siri za Kikwete, vice versa is also true...
Ni maoni yangu tu ..nawasilisha....
 
Kumbe bila Lowassa kuwepo madarakani uchumi wa Tanzania unayumba!! Major vipi bana hebu tufafanulie... lol!
 
kuhusu ruzuku kuwa wakulima wataisikia redioni si kweli kwakuwa huko iringa watu wameshachukuwa mbolea na mbegu za ruzuku. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe!.
mimi simo !
 
Eti kuna watu wanataka tuamini kuwa tangu Edward Lowassa atoke serikalini badala ya kulazimishwa kujiuzulu kutokana na kashfa ya Richmond, basi nchi imekwama. Eti serikali ya Kikwete inayumba bila Lowassa na mambo yamekuwa mabaya kweli kweli. Nchi inamuhitaji Lowassa arudi madarakani. Tehe, tehe. Kichekesho kweli. Mbona alivyokuwepo yeye serikalini bado kulikuwa na madudu kibao, ikiwemo hayo ya Richmond na mengineyo mengi. Lowassa na Kikwete wote ni mzigo kwa taifa hili la Julius Nyerere.
 
Mie naona all is just fine, Nyumba za Polisi zinajengwa, nimetoka Tanga juzi nimeona kamaa wako Pale Chalinze wanamalizia Feasibility Study ya 12 lanes highway ya DAR-CHALINZE, Kigamboni Bridge nayo iko njiani, Mchikichini mini city nayo naona tayari watu washaanza kuhamishwa ili wajengewe makazi ya kueleweka, traffic lights zinafanya kazi, Mabomu tuliotishiwa na waingereza over the weekend hatujayasikia,

all is just fine na JK naamini keshaanza consultation na stake holder s wanao matter kuhusu katiba mpya na bila kusahau umeme wa upepo wa Singida nao huooooo


Its not perfect lakini tupo tunasurvive unless one in the cyberworld where he doesn't meet the real people
 
naisha ni kuchagua hivyo tuendelee kulalamika tu ukweli utabaki pale pale hali ya watanzania haijawahi kuwa nzuri na kamwe kwa uongozi uliopo sasa ni ndoto kujakujinasua katika mikono ya mafisadi.
 
Sioni uhusiano mkuu kati ya jk, lowassa na hali ngumu ya maisha. Labda ufafanue kidogo. Au wewe lowassa mwenyewe nini!!
 
Huyu jamaa anatumia vibaya hii forum, who is Lowasa mpaka alete hali ngumu? Lowasa mwenyewe ni Mwizi kuliko Kikwete na uwezo wake mdogo kuliko Kikwete hana uwezo wa kutusaidia, alitolewa kwa wizi siyo zengwe la Rais acha mambo ya Nurse school hapa; hali ngumu pia inachangiwa kwa kiasi kikubwa na watu wenye upeo mdogo kama mtoa mada hii (Maoni yangu Binafsi).
 
Back
Top Bottom